Kama ndugu wanavyogombana wakati wa misiba, wengine kudai wana haki zaidi kuamua Marehemu azikwe wapi, nani awe "mrithi" wa kutunza familia, nani agawiwe mali na majukumu mingine ambayo ni kawaida ya binadamu, Jumuiya yetu nayo iko katika mvutano huo huo.
Najiuliza je ni kawaida yetu binaadamu kuwa na mvutano kuhusiana na kifo na hasa wakati wa msiba? je hii ni ni kawaida wakati wa maombolezo?
Nimejiuliza ya fuatayo na maoni yangu binafsi na imani yangu pamoja na maswali haya ni kuwa Ballali hayupo nasi tena. I believe Daudi Ballali is dead and I pray that his sould rest in peace.
Maswali ni haya;
- Je Ballali amekufa?
- Ni nani ananufaika kwa kifo chake
- Kama bado yupo hai na taarifa ya kifo ni ulaghai, ni kwa faida ya nani?
- Je tuna haki gani kutaka kuingilia mambo ya binafsi ya familia?
- Je kwa nini familia haitaki Ballali agwe na wananchi na kufanya msiba wake uwe jambo la familia tuu? ni wapi ule mshikamano wa kiafrika na utamaduni wetu?
- Je ni kwa nini kumekuwa na usiri mkubwa kuhusu kuugua kwake na hata kifo chake? je mimi nina haki gani au wajibu gani kujua kuhusu Ballali? kwa nini kuna utata mkubwa katika kila kitu kuhusu Ballali?
- Kifo chake ni pigo kwa nani?
- Kama sababu za kifo chake ni kuuwawa kama wengi wetutunavyokisia, kudhania au kuzusha, je ni nani aliyetaka Ballali afe? Ni lini aliuawa? na ni nini kilitumika kumuua?
- Ni siri gani ambayo amekufa nayo au kawapa familia, marafiki na wengine waitangaze?
- Je kifo chake kina sehemu gani au mahusiano gani kuhusiana/katika uchunguzi wa tuhuma za ufujaji mali, uhujumu na ufisadi wa pesa za Taifa Benki Kuu?
- Je kufa kwa Ballali kuna maafa gani katika vita ya ufisadi?
- Je familia yake inaungana vipi wakati kuna mgawanyiko kati yao kuhusiana na mazingira mazima ya yeye kutuhumiwa, kuugua na sasa kufa?
- Ni nani hao ambao wanatoa vitisho au wametoa vitisho na kutaka kila kitu kinachohusiana na Ballali kiendelee kuwa ama usiri, utata au mara nyingine kuwa ni uzushi? kwa faida gani? na ya nani?
- Je alikufa lini na wapi?lipi ni kweli na lipi si sahihi?
- La mwisho, kwa nini Familia ilitaka iwasiliane na Serikali kwanza kutangaza kifo cha mpendwa wao? kwa manufaa gani kama Ballali alishapoteza kazi yake na Serikali kudai haina taarifa au haijui Ballali yupo wapi? je kuna ukweli gani katika hili?
Kama nilivyosema awali, nimesikitishwa (saddened)na taarifa na kifo cha Ballali. naheshimu uamuzi wa familia na nawapa pole. Naheshimu uchu wa Watanzania kutaka kujua ukweli.
Nasikitika (disappointed) kuwa Ballai kaondoka na siri kubwa na hakuchuka fursa yeyote wakati akiwa hai (kama hakuwa anaishi katika vitisho na "kutekwa nyara") kutoa ushuhuda kuhusiana na kilichosababisha aidhinishe malipo makubwa ya EPA, CIS, Meremeta, Tangold ambayo yamegundulika kuwa yalikuwa ni batili na kwa makusudi ya kuhujumu uchumi na Taifa letu.
Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele, tugange kwa ya mbele. Katika sakata la EPA na BOT kutumika kuhujumu nchi, Ballali hakuwa Alpha na Omega, kifo chake hakijafunga au kusitisha uchunguzi.
Wale walio hai, Gray Mgonja, Basil Mramba na Ben Mkapa waje mbele na kutupa taarifa, ni vipi kulikuwa na upotevu, ufujaji na uhujumu mkubwa uliofanyika wakati wao wakiwa katika madaraka na kushikilia hazina ya Taifa? Ilikuwaje Ballali akaruhusiwa kuidhinisha malipo makubwa kiasi hicho bila kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mkubwa wake wa kazi?
Rest in Peace Ballali. You will forever be remembered.