Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.
Mara nyingi IMANI haifunziki hata kwa milango yote 5 ya fahamu, ndio maana baadhi wana IMANI kwamba hajafa ingawa wana ELEWA amekufa. Hivyo basi hata wakiona mwili wake bado IMANI yao kwamba hajafa itajazwa na visingizio ili kulazimisha MACHO yao yakatae kwenda kinyume na IMANI.
 
Mjane ni kweli anayo nguvu kubwa kwa sababu hii ni ndoa iliyofanyika majuu, na unajua majuu ni kina mama ndio wanaokuwa -favored na sheria, na besides ndoa za majuu ni mke na mume tu, ndugu baadaye sana, ndio maana unaona kuwa mama anaonekana kuwa na nguvu sana ni sheria mkuu za huko majuu.

FMES;

Hiyo argument ina matundu. Nguvu ya Mjane kufanya maamuzi ya misiba/mazishi ni mambo ya Kifamilia, sio 'sheria za majuu'. Hata Tanzania kwenye mfumo dume Serikali haiwezi kushurutisha mjane akazike mfu wake pale Serikali inapotaka. Hakuna sheria kama hizo hata Bongo. Uchambuzi wako wa tofauti za sheria za ndoa hapa hauhusiki. Umekosea!

Na hata tunge assume kwamba uko sahihi, kwamba ni "Sheria za Majuu" zinampendelea Mwanamke, kina Ballali wangebanwa na Sheria ya nchi walipooana, kama ulivyo sema. Lakini kina Ballali hawakuoana Marekani, ila Europe. Sheria za Ufaransa hazifanyi kazi Marekani. Unanielewa?
 
Kweli jMushi1 hii ishu si ndogo, ila watafanikiwa kuizima? maana tumeshupaliwa kama vile tumekula shumili ama pilipili, hatuelewi hatusikii,invisible naye mitini, Dooooo!!! hii si mchezo,

Tego kama kaulimbo, kamewanasa weengi.
Zogo piaa vikumbo, mithiri vijibepari
amini hizo za tumbo,tabainika ukweli
Mola bainisha haya tusiumizane vichwa

Invisible njoo na data ndugu yetu, sisi vinyapori bado twakusubili, sije zikwa mzee tukakosa la kusema, ikawa limekwisha, wa mbili akavaa moja,
 
Kweli jMushi1 hii ishu si ndogo, ila watafanikiwa kuizima? maana tumeshupaliwa kama vile tumekula shumili ama pilipili, hatuelewi hatusikii,invisible naye mitini, Dooooo!!! hii si mchezo,

Tego kama kaulimbo, kamewanasa wengi.
Zogo piaa vikumbo, mithiri vijibepari
amini hizo za tumbo,tabainika ukweli
Mola bainisha haya tusiumize vichwa

Invisible njoo na data baba, sisi vinyapori bado twakusubili, sije zikwa mzee tukakosa la kusema, ikawa limekwisha, wa mbili akavaa moja,

Hapana!
Hatutakubali na ndio maana tunasubiri hayo maziko!
Kama kafa hapa NI LAZIMA KUNA UCHUNGUZI BINAFSI WA WAMAREKANI..May be FBI!
Tutademand kauli za uchunguzi wao!
Kwasababu wale makachero hawawezi kuja tu kufanya uchunguzi bila ya kuwashirikisha FBI kwasababu ya sovereignity issue!
Hakuna raia wa nchi nyingine anayeweza kuja hapa kufanya uchunguzi bila ya local authorirties kujulishwa!
Hivyo sisi na wananchi wa hapa marekani tutahitaji FBI watueleze nini hasa kilifanyika kwenye nchi yao huru!
 
Jmushi.. nani alikuambia makachero wametumwa na serikali wakati serikali ilikuambia na ilionesha kuwa haimfatufi? You need to pause and think......

1 + 2 + 3 + 4 = 1234
 
1
. Hiyo argument ina matundu. Nguvu ya Mjane kufanya maamuzi ya misiba/mazishi ni mambo ya Kifamilia, sio 'sheria za majuu'.

Mkuu saa nyingine jaribu kufikiri angalau kidogo kabla ya kuandika, sheria za US ziko wazi ni mke na mume tu, sasa mume hayupo amekufa sheria iko wazi hapa kuwa mke ndiye bosi, kwa sababu ingekuwa bongo kaka wa marehemu au baba yake ndiye angeshika usukani, huko majuu sheria inamtambua mjane mkuu sio ndugu wa familia kama bongo, kwa hiyo hata kama familia ya mume/marehemu wangetaka ku-take charge wasingeweza unless labda wapewe hiyo nafasi na mjane, lakini otherwise ni lazima mjane a take-charge kwa sababu ni sheria kwanza na familia ya marehemu baadaye!

2.
Hata Tanzania kwenye mfumo dume Serikali haiwezi kushurutisha mjane akazike mfu wake pale Serikali inapotaka. Hakuna sheria kama hizo hata Bongo. Uchambuzi wako wa tofauti za sheria za ndoa hapa hauhusiki. Umekosea!

Hapana mkuu wewe ndiye hujui kitu, kinachomfanya mjane wa Balali avimbe na kuikatalia serikali yetu ni sheria kuwa upande wake huko US na sio anything else, serikali ya Tanzania haiwezi kumlazimisha kwa nguvu ati mwili urudishwe bongo, mkuu hiyo haijawahi kutokea huko US, swali la msingi lililoulizwa ni kwa nini mjane anavimba sana, sio haya uliyoyasema kwa jazba mkuu ni out of line!

3.
Na hata tunge assume kwamba uko sahihi, kwamba ni "Sheria za Majuu" zinampendelea Mwanamke, kina Ballali wangebanwa na Sheria ya nchi walipooana, kama ulivyo sema. Lakini kina Ballali hawakuoana Marekani, ila Europe. Sheria za Ufaransa hazifanyi kazi Marekani. Unanielewa?

Kwa hiyo alipokuwa hai, wangegombana na kwenda mahakamani je sheria ingeshindwa kuumika wangeambiwa waende Italy waliko oana? Je wabongo walioko huko US walioo oana bongo sheria za huko hazitambui ndoa zao kuwa officially ni ndoa rasmi, na kisheria?

Wewe ndiye unahitaji kunielewa kuwa huelewi unachosema, ndoa hata kama imefungwa Mkuranga, mkienda US ni ndoa kisheria za huko mkuu, sijawahi kuskia kuwa watu walioko kwenye ndoa iliyofungwa nje ya US hwathaminiwi kisheria za huko eti kwa sababu walifungia ndoa nje ya US, mkuu unapaswa kuelewa better than this, damn!

Mkuu please sina mpango wa kuiharibu hii topic na majadiliano yasiyokuwa educative kwa wengine kuhusiana na the topic, labda uanzishe nyingine huko porini!
 
wasee,

hamna kitu kibaya kama kuwa na pupa!! hapa kuna kulishana sumu kuliko kithiri, tena ni zile zisokuwa na antidotes......subirini wazike, then polepole and naturally habari tamu tamu zitaanza kutiririka bila kutumia misuli!!.

Ijumaa njema, y'all.
 
Daaaaa!!!! Mwanakjj, hizi arama za kujumlisha zina maana gani mkuu? wale ngumbaru nasi tunase zetu nyeti, sijebaki patupu akaambulia mpita njia,

Mwanakjj una mkonga mrefu, lindima tusikie, mitima yetu itulie kwa wako udadisi, marekani si chalinze eti mtanzania atafika, kama ni kututega hakika wametunasa,twabakia mijineno wala hatujiwezi.

Sisi hatutoki hapa hadi hapo invisible atakaporejea,mimi amani itarejea,kwa wake ushaidi, Marekani si Chalinze hadi mtanzania afike
 
Jmushi.. nani alikuambia makachero wametumwa na serikali wakati serikali ilikuambia na ilionesha kuwa haimfatufi? You need to pause and think......

1 + 2 + 3 + 4 = 1234

Nadhani mantiki inaweza kutuambia hivyo. Walio kuja, kama walikuja, si ajabu walitumwa na Serikali kisiri siri.

Serikali ilisema haimtafuti Ballali lakini uchunguzi wa Ubadhilifu EPA bado unaendelea (na leo wamerudia tena). Mkubwa wa BOT wakati wa ubadhilifu ni Ballali. Kwa hiyo uchunguzi unaweza, tena unatakiwa, kuhusisha juhudi za kumfikia Ballali kumhoji. Walio ripotiwa wamekuja sio tume ya Rais, bali makachero. Uchunguzi mara nyingi unafanyika kisirisiri. Kwa hiyo haikuwa kushindwa ku 'pose and think' kwa JMUSHI kwamba waliokuja ni watu wa Serikali katika uchunguzi unaoendeshwa kisiri siri. Kitu kilichopelekea kuripotiwa kama ni makachero. Hizo ndio pieces of the puzzle ambazo watu wanajaribu kuziweka pamoja.

Nisaidie kama hayo niliyo yasema, ambayo yanawiana na hoja ya Mushi, ni 1 + 2 + 3 + 4 = 1234.

Halafu hata kama hawakuja kama Makachero Kamata Kamata au Chunguza Chunguza, inawezekana walikuja baada ya kupata habari za Msiba. Tumeambiwa Ikulu ilipata habari wiki iliyopita. Na FMES akauliza kwani Makachero walikuja lini, na ukakubali hilo swali ni poignantly relevant. Makachero wali ripotiwa wamekuja kipindi kile kile tunacho ambiwa Ballali alikuwa kesha kufa. Yawezekana walitumwa na Ikulu baada ya kuambiwa Msiba.

Kwa hiyo nadhani kulikuwa na upungufu wa ku 'pose and think' kusema waliokuja walitumwa na Serikali kisiri siri, aidha ni Makachero au Wachunguzi wa Msiba au Ubadhilifu.
 
Jmushi.. nani alikuambia makachero wametumwa na serikali wakati serikali ilikuambia na ilionesha kuwa haimfatufi? You need to pause and think......

1 + 2 + 3 + 4 = 1234

Kama hawamtafuti hiyo inapingana na kauli yao waliyoitoa ambayo walidai wametuma makachero 7 hapa marekani kum comb Ballali!
Tatizo lako MKJJ unasahahu mapema mno!
Wewe ambaye ulianza kuja na rumours za kifo cha Balllali halafu bado wewe ndio mwenye ukaribu wa kupata taarifa ambazo untaka tuziamini bila maswali!
Mkjj ANGALIA USIJE UKATUMIKA VIBAYA KWENYE HII SCANDAL!
 
Kwanini ulikuja na taarifa kwamba anaweza akawa amekufa,halafu kuwa amekufa tarehe 16 then 18 then tu pause and think?
Pause and think yangu ni kuwa hata nyie mna utata mpaka hapo mtakapojisafisha ama kugundulika vingine!
Mmekuwa wakali wakati watu wakijaribu kutafuta ukweli na kufanya uchunguzi wa Ballali's personal life!
Umekuwa wa kwanza kututangazia kuwa Ballali alikufa akiwa huru hivyo technically hakuna tena kesi!
Umekuwa wa kwanza kukataa Zitto asifwatilie habari za Ballali alipokuwa huku!
Na kuna taarifa kwenye Tanzania Daima kuwa wale ndugu wa Ballali maisha yao yatakuwa hatarini kama wakipeleka taarifa kwa waandishi wa habari badala ya mtandaoni!
Sasa kweli kama unaiheshimu JF na watu wake kama madai yako..Then unaweza uongea haya mambo halafu watu wasiulize?
KWANINI MNATAKA MUMANIPULATE HIZI NYUUZ!
KWA NINI WALE NDUGU ZA BALLALI WATISHIWE KUTOA TAARIFA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA BADALA YAKE WAJE KUZITOA HUKU MTANDAONI?
HAPO NI ILI MUENDELEE KUTOA HABARI VILE MNATAKA?
HAWA WAKINA DADA WAMETOKA BONGO NA WANA HAKI YA KUPELEKA TAARIFA HIZO BONGO!
TATIZO KAMA NILIVYOSEMA BEFORE NA WAO PIA WATAWEKWA SAWA KWASABABU TAYARI WAKO KWENYE MAZISHI!
 
Jmushi.. nani alikuambia makachero wametumwa na serikali wakati serikali ilikuambia na ilionesha kuwa haimfatufi? You need to pause and think......

1 + 2 + 3 + 4 = 1234

John Forbes aliwahi kutueleza kwamba - nam-quote - "Education's purpose is to replace an empty mind with an open one".

Sirikali yetu nafikiri inadhani watanzania wote ni wajingajinga... Maana nafikiri spidi yao ya kuchezea wananchi akili inazidi kuongezeka, tena kwa kasi kubwa.
 
Kama hawamtafuti hiyo inapingana na kauli yao waliyoitoa ambayo walidai wametuma makachero 7 hapa marekani kum comb Ballali!Tatizo lako MKJJ unasahahu mapema mno!
Wewe ambaye ulianza kuja na rumours za kifo cha Balllali halafu bado wewe ndio mwenye ukaribu wa kupata taarifa ambazo untaka tuziamini bila maswali!
Mkjj ANGALIA USIJE UKATUMIKA VIBAYA KWENYE HII SCANDAL!

wrong... hakuna chombo chochote cha serikali kilichotoa kauli hiyo na kikasikika. Kauli ya mwisho yenye mamlaka bila kukosea ilitolewa na Ikulu kusema kuwa Balali ni mtu huru na kwa wakati huu (ule) walikuwa hawamtafuta Ballali na kama wakitaka kumtafuta wanamkono mrefu. Tatizo ni kuwa nadhani kuna baadhi kwa kueneza tetesi zisizo na msingi ndio wanatumiwa vibaya kweli bila ya wao kujua. Watu wakikaa chini kufikiria kama mchezo wa chess wataona kuwa goli halikufungwa jana au miezi iliyopita... goli lilifungwa ....... mnachoshuhudia ni nyavu kutikisika huku mnashangaa mpira umeenda wapi.

Ukitaka kuelewa rewind your tape!!!
 
Wakuu,

Mnaoenda kumzika Ballali (gogo) basi mazishi mema, kwa wale tusioamini kwenye hili tuendelea kufungua vichwa.

Wacha mimi nianze weekend na kupata moja moto moja baridi ili kunipunguza ukichaa wa Ballali.

Wengine tuna long weekend hapa, kazini mpaka Jumanne, kwahiyo Libeneke litakolea mno. Maneno ya Michuzi hayo, wala hata sijui Libeneke ndio nini.

Weekend njema kwa wote! Muhimu hapa sisi ni binadamu, tujitahidi kutenda mema na kupunguza uroho uliokithiri. Isingelikuwa ufisadi leo hii tungekuwa tunasherehekea maisha
ya msomi wetu Ballali na achievements kibao alizopata katika maisha yake. Watu kama hao wanatakiwa kuwa role models wetu na sio kuishia kukashifiwa kila sehemu.

Usione watu tunaandika hapa, lakini hii habari inasikitisha sana. Ni balaa kwa familia ya Ballali hasa wale walioko Iringa. Binafsi nawaombea wapate nguvu na kuweza kushinda haya majaribu yote na juu ya ndugu yao na kumwachia mungu maana hata wao ni victims tu kwenye hili sawa na Watanzania wengine.
 
There is no reliable source than JF even magazeti ya leo yanadai habari walizonazo ni kutoka kwenye mtandao (JF) Big UP
 
Nduguze Ballali waonywa

na Mwandishi Wetu

DADA wawili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), waliokuwa wamepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki ijayo, wameonywa kuhusu uamuzi wao huo.
Onyo hilo limetolewa kwao kwa njia ya simu na watu mbalimbali waliowasiliana nao wakiwa Washington, Marekani, uliko msiba wa Ballali ambaye anatarajiwa kuzikwa leo.
Aidha, onyo hilo pia lilitolewa jana kwa njia ya simu na watu waliojitambulisha kuwa ni wasomaji wa Tanzania Daima, ambao walieleza wasiwasi wao wa wazi kuhusu uamuzi wa ndugu hao wa Ballali ambao taarifa za wao kuja kuzungumza na waandishi wa habari ziliandikwa jana na gazeti hili pekee.
“Mhariri, mimi ni msomaji mzuri wa gazeti lako. Ninapenda kukuomba uwafikishie salamu zangu hao dada wawili wa marehemu Ballali. Wasije wakajikuta wakifikwa na matatizo, kwa sababu ya uamuzi wao wa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kama mlivyoandika,” alisema mwanamke mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Alipoulizwa ni kwa nini alikuwa akifikiria kuwa ni jambo la hatari kwa kina dada hao kuzungumza na Watanzania kuhusu kile kilichomfika ndugu yao Ballali, msomaji huyo alisema hali ya hewa kisiasa imechafuka, hivyo kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa wao kudhurika, hata kabla hawajafanikiwa kuzungumza kile walichokipanga.
Watu wengine wawili waliozungumza na Tanzania Daima nao walieleza wasiwasi kama huo, na mmoja wao akafikia hatua ya kuwataka wanawake hao ambao hivi sasa wako Washington wakiomboleza msiba wa kaka yao, wafikishe kila wanalofahamu kuhusu mazingira ya kifo hicho cha Ballali kupitia mtandao wa intaneti.
“Mhariri naomba uwataarifu dada zake Ballali kutothubutu kuzungumza na waandishi wa habari hapa Dar es Salaam. Kama wana lolote la kusema kuhusu mazingira ya kifo cha ndugu yao, hawana budi kufanya hivyo kwa njia ya mtandao ambao katika siku za karibuni, imekuwa njia muafaka zaidi na salama kuitumia kufikisha ujumbe,” alisema muonyaji mmoja.
Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na ndugu mmoja wa Ballali aliyeko Washington katika msiba wa gavana huyo wa zamani wa BoT na kumweleza kuhusu wasiwasi huo, naye alikiri kupokea simu kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali waliosoma gazeti hili hapa nchini au kwa njia ya mtandao wa intaneti.
“Hata sisi hapa tumepokea simu nyingi zikitutahadharisha kuhusu hatua hiyo ya kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa hiyo suala hilo bado linajadiliwa na uamuzi wa kuzungumza au kutozungumza na waandishi wa habari utaangaliwa na ikibidi unaweza ukabadilishwa,” alisema.
Kuhusu uamuzi wa Ballali kuzikwa Washington, ndugu huyo wa Ballali alisema hata wao walifikia hatua ya kukubaliana na uamuzi wa yeye mwenyewe kutaka akifa azikwe huko kutokana na kuchafuka kwa jina lake, kutokana na kuhusishwa kwake na tuhuma mbalimbali za ufisadi.
Mwanafamilia huyo juzi aliieleza Tanzania Daima kwamba, Ballali alifikia uamuzi huo wa kuzikwa Marekani, kutokana na kufadhaishwa na namna jina lake lilivyokuwa likihusishwa na tuhuma nzito za ufisadi.
“Yeye mwenyewe ndiye aliyeamua azikwe huku Washington. Siku zote amekuwa akitueleza namna alivyokuwa akifadhaishwa sana kutokana na kuchafuliwa kwa jina lake, hata baada ya kuitumikia nchi yake kwa juhudi kubwa, moyo mkunjufu na kwa uadilifu wa hali ya juu.
“Alitueleza hapa kwamba hajapata kuiibia nchi yake hata senti moja. Hapo ndipo aliposema akifa angetaka azikwe huku huku Washington na si nyumbani, ambako alihusishwa na kila aina ya tuhuma,” alisema mwanafamilia huyo juzi, kauli ambayo jana aliendelea kuisisitiza.
Akizungumza jana, alisema alimuona Ballali kwa mara ya mwisho akiwa hai, Alhamisi ya wiki iliyopita, ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufikwa na mauti.
“Nilipomuona Alhamisi iliyopita nilimkuta akiwa amewekewa ‘drip’ nyumbani kwake, ikiwa ni kama siku moja au mbili tangu alipotolewa hospitalini, baada ya madaktari kumweleza kuwa walikuwa hawana lolote la kufanya,” alisema ndugu huyo.
Aidha, jamaa huyo wa Ballali alikanusha taarifa kwamba, Ballali alikufa baada ya mashine za kumsaidia kuishi kuzimwa kutokana na uamuzi uliofikiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na madaktari.
“Hapana, hakuwa katika mashine wakati akifariki. Alifia nyumbani kwake Washington na si Boston kama ilivyotangazwa na BoT,” alisema.
Mbali ya hayo, ndugu huyo wa Ballali aliieleza Tanzania Daima kwamba, mke wa Ballali, Anna Muganda, alikuwa ameomba msiba wa mumewe ufanywe kwa faragha, ukiwahusisha ndugu, marafiki na jamaa zao wa karibu.
Alisema kutokana na hali hiyo, shughuli hizo za msiba zilikuwa zikifanyika pasipo kuwapo kwa shughuli zozote za wazi kama vile kuchukua picha za video au kupiga picha nyingine za kawaida.
Aliieleza Tanzania Daima kwamba, kwa muda wote huo wa msiba, Anna alikuwa mtulivu na alikuwa amezima simu zake zote na hakuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya kumzika mumewe leo hii.
Alisema pia kwamba, mama mzazi wa Ballali ambaye hivi sasa anaishi Boko, jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 94 alikuwa ameshindwa kusafiri kutokana na uzee.
Pamoja na hilo, aliieleza Tanzania Daima kwamba, taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Katibu wa Gavana wa Benki Kuu, jana alikuwa amekwenda Boko kuhani, ikiwa ni pamoja na kutoa ubani kwa ajili ya msiba huo.
Habari kutoka Boston na Washington ambazo Tanzania Daima imeshapata kuziandika, zinaeleza kwamba, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisema kwamba, Ballali alikuwa akisumbuliwa na aina moja ya saratani kwa muda mrefu. Hata hivyo wakati kukiwa na taarifa hizo, baadhi ya ndugu, marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba, Ballali alilishwa aina fulani ya sumu isiyojulikana, siku kadhaa kabla hajakimbizwa Marekani kwa matibabu. Taarifa hizi za kulishwa sumu zimekuwa zikienea kwa haraka katika maeneo tofauti na baadhi ya watu tayari wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kujua ni kitu gani hasa kilikuwa kimempata
 
"Mhariri, mimi ni msomaji mzuri wa gazeti lako. Ninapenda kukuomba uwafikishie salamu zangu hao dada wawili wa marehemu Ballali. Wasije wakajikuta wakifikwa na matatizo, kwa sababu ya uamuzi wao wa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kama mlivyoandika," alisema mwanamke mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Alipoulizwa ni kwa nini alikuwa akifikiria kuwa ni jambo la hatari kwa kina dada hao kuzungumza na Watanzania kuhusu kile kilichomfika ndugu yao Ballali, msomaji huyo alisema hali ya hewa kisiasa imechafuka, hivyo kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa wao kudhurika, hata kabla hawajafanikiwa kuzungumza kile walichokipanga.
Watu wengine wawili waliozungumza na Tanzania Daima nao walieleza wasiwasi kama huo, na mmoja wao akafikia hatua ya kuwataka wanawake hao ambao hivi sasa wako Washington wakiomboleza msiba wa kaka yao, wafikishe kila wanalofahamu kuhusu mazingira ya kifo hicho cha Ballali kupitia mtandao wa intaneti.
"Mhariri naomba uwataarifu dada zake Ballali kutothubutu kuzungumza na waandishi wa habari hapa Dar es Salaam. Kama wana lolote la kusema kuhusu mazingira ya kifo cha ndugu yao, hawana budi kufanya hivyo kwa njia ya mtandao ambao katika siku za karibuni, imekuwa njia muafaka zaidi na salama kuitumia kufikisha ujumbe," alisema muonyaji mmoja.
Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na ndugu mmoja wa Ballali aliyeko Washington katika msiba wa gavana huyo wa zamani wa BoT na kumweleza kuhusu wasiwasi huo, naye alikiri kupokea simu kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali waliosoma gazeti hili hapa nchini au kwa njia ya mtandao wa intaneti.
"Hata sisi hapa tumepokea simu nyingi zikitutahadharisha kuhusu hatua hiyo ya kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa hiyo suala hilo bado linajadiliwa na uamuzi wa kuzungumza au kutozungumza na waandishi wa habari utaangaliwa na ikibidi unaweza ukabadilishwa," alisema.
Kuhusu uamuzi wa Ballali kuzikwa Washington, ndugu huyo wa Ballali alisema hata wao walifikia hatua ya kukubaliana na uamuzi wa yeye mwenyewe kutaka akifa azikwe huko kutokana na kuchafuka kwa jina lake, kutokana na kuhusishwa kwake na tuhuma mbalimbali za ufisadi.
Mwanafamilia huyo juzi aliieleza Tanzania Daima kwamba, Ballali alifikia uamuzi huo wa kuzikwa Marekani, kutokana na kufadhaishwa na namna jina lake lilivyokuwa likihusishwa na tuhuma nzito za ufisadi.
"Yeye mwenyewe ndiye aliyeamua azikwe huku Washington. Siku zote amekuwa akitueleza namna alivyokuwa akifadhaishwa sana kutokana na kuchafuliwa kwa jina lake, hata baada ya kuitumikia nchi yake kwa juhudi kubwa, moyo mkunjufu na kwa uadilifu wa hali ya juu.
"Alitueleza hapa kwamba hajapata kuiibia nchi yake hata senti moja. Hapo ndipo aliposema akifa angetaka azikwe huku huku Washington na si nyumbani, ambako alihusishwa na kila aina ya tuhuma," alisema mwanafamilia huyo juzi, kauli ambayo jana aliendelea kuisisitiza.
Akizungumza jana, alisema alimuona Ballali kwa mara ya mwisho akiwa hai, Alhamisi ya wiki iliyopita, ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufikwa na mauti.
"Nilipomuona Alhamisi iliyopita nilimkuta akiwa amewekewa ‘drip' nyumbani kwake, ikiwa ni kama siku moja au mbili tangu alipotolewa hospitalini, baada ya madaktari kumweleza kuwa walikuwa hawana lolote la kufanya," alisema ndugu huyo.
Aidha, jamaa huyo wa Ballali alikanusha taarifa kwamba, Ballali alikufa baada ya mashine za kumsaidia kuishi kuzimwa kutokana na uamuzi uliofikiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na madaktari.
"Hapana, hakuwa katika mashine wakati akifariki. Alifia nyumbani kwake Washington na si Boston kama ilivyotangazwa na BoT," alisema.
Mbali ya hayo, ndugu huyo wa Ballali aliieleza Tanzania Daima kwamba, mke wa Ballali, Anna Muganda, alikuwa ameomba msiba wa mumewe ufanywe kwa faragha, ukiwahusisha ndugu, marafiki na jamaa zao wa karibu.
Alisema kutokana na hali hiyo, shughuli hizo za msiba zilikuwa zikifanyika pasipo kuwapo kwa shughuli zozote za wazi kama vile kuchukua picha za video au kupiga picha nyingine za kawaida.
Aliieleza Tanzania Daima kwamba, kwa muda wote huo wa msiba, Anna alikuwa mtulivu na alikuwa amezima simu zake zote na hakuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya kumzika mumewe leo hii.
Alisema pia kwamba, mama mzazi wa Ballali ambaye hivi sasa anaishi Boko, jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 94 alikuwa ameshindwa kusafiri kutokana na uzee.
Pamoja na hilo, aliieleza Tanzania Daima kwamba, taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Katibu wa Gavana wa Benki Kuu, jana alikuwa amekwenda Boko kuhani, ikiwa ni pamoja na kutoa ubani kwa ajili ya msiba huo.
Habari kutoka Boston na Washington ambazo Tanzania Daima imeshapata kuziandika, zinaeleza kwamba, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisema kwamba, Ballali alikuwa akisumbuliwa na aina moja ya saratani kwa muda mrefu. Hata hivyo wakati kukiwa na taarifa hizo, baadhi ya ndugu, marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba, Ballali alilishwa aina fulani ya sumu isiyojulikana, siku kadhaa kabla hajakimbizwa Marekani kwa matibabu. Taarifa hizi za kulishwa sumu zimekuwa zikienea kwa haraka katika maeneo tofauti na baadhi ya watu tayari wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kujua ni kitu gani hasa kilikuwa kimempata

Ni nani huyo mwenye kuwaonya ndugu zake Ballali wazilete habari mtandaoni badala ya bongo?
Kama watu wa mtandaoni wana news zote then kwanini wanawashika shati na kuwatisha hao kina dada wazilete hizo habari huku?
 
wrong... hakuna chombo chochote cha serikali kilichotoa kauli hiyo na kikasikika. Kauli ya mwisho yenye mamlaka bila kukosea ilitolewa na Ikulu kusema kuwa Balali ni mtu huru na kwa wakati huu (ule) walikuwa hawamtafuta Ballali na kama wakitaka kumtafuta wanamkono mrefu. Tatizo ni kuwa nadhani kuna baadhi kwa kueneza tetesi zisizo na msingi ndio wanatumiwa vibaya kweli bila ya wao kujua. Watu wakikaa chini kufikiria kama mchezo wa chess wataona kuwa goli halikufungwa jana au miezi iliyopita... goli lilifungwa ....... mnachoshuhudia ni nyavu kutikisika huku mnashangaa mpira umeenda wapi.

Ukitaka kuelewa rewind your tape!!!

Unapingana na Slaa aliyesema the same thing kuwa serikali ilidai kutuma watu!
Hivi MKJJ seriously do you know where you stand? ama unabisha tu kwasababu umepewa kazi ya kutetea na kulinda maslahi ya kihabari?
Narudia tena ni heri uwe neutral utasamehewa!
 
Nduguze Ballali waonywa

na Mwandishi Wetu

DADA wawili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), waliokuwa wamepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki ijayo, wameonywa kuhusu uamuzi wao huo.
Onyo hilo limetolewa kwao kwa njia ya simu na watu mbalimbali waliowasiliana nao wakiwa Washington, Marekani, uliko msiba wa Ballali ambaye anatarajiwa kuzikwa leo.
Aidha, onyo hilo pia lilitolewa jana kwa njia ya simu na watu waliojitambulisha kuwa ni wasomaji wa Tanzania Daima, ambao walieleza wasiwasi wao wa wazi kuhusu uamuzi wa ndugu hao wa Ballali ambao taarifa za wao kuja kuzungumza na waandishi wa habari ziliandikwa jana na gazeti hili pekee.
“Mhariri, mimi ni msomaji mzuri wa gazeti lako. Ninapenda kukuomba uwafikishie salamu zangu hao dada wawili wa marehemu Ballali. Wasije wakajikuta wakifikwa na matatizo, kwa sababu ya uamuzi wao wa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kama mlivyoandika,” alisema mwanamke mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Alipoulizwa ni kwa nini alikuwa akifikiria kuwa ni jambo la hatari kwa kina dada hao kuzungumza na Watanzania kuhusu kile kilichomfika ndugu yao Ballali, msomaji huyo alisema hali ya hewa kisiasa imechafuka, hivyo kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa wao kudhurika, hata kabla hawajafanikiwa kuzungumza kile walichokipanga.
Watu wengine wawili waliozungumza na Tanzania Daima nao walieleza wasiwasi kama huo, na mmoja wao akafikia hatua ya kuwataka wanawake hao ambao hivi sasa wako Washington wakiomboleza msiba wa kaka yao, wafikishe kila wanalofahamu kuhusu mazingira ya kifo hicho cha Ballali kupitia mtandao wa intaneti.
“Mhariri naomba uwataarifu dada zake Ballali kutothubutu kuzungumza na waandishi wa habari hapa Dar es Salaam. Kama wana lolote la kusema kuhusu mazingira ya kifo cha ndugu yao, hawana budi kufanya hivyo kwa njia ya mtandao ambao katika siku za karibuni, imekuwa njia muafaka zaidi na salama kuitumia kufikisha ujumbe,” alisema muonyaji mmoja.
Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na ndugu mmoja wa Ballali aliyeko Washington katika msiba wa gavana huyo wa zamani wa BoT na kumweleza kuhusu wasiwasi huo, naye alikiri kupokea simu kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali waliosoma gazeti hili hapa nchini au kwa njia ya mtandao wa intaneti.
“Hata sisi hapa tumepokea simu nyingi zikitutahadharisha kuhusu hatua hiyo ya kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa hiyo suala hilo bado linajadiliwa na uamuzi wa kuzungumza au kutozungumza na waandishi wa habari utaangaliwa na ikibidi unaweza ukabadilishwa,” alisema.
Kuhusu uamuzi wa Ballali kuzikwa Washington, ndugu huyo wa Ballali alisema hata wao walifikia hatua ya kukubaliana na uamuzi wa yeye mwenyewe kutaka akifa azikwe huko kutokana na kuchafuka kwa jina lake, kutokana na kuhusishwa kwake na tuhuma mbalimbali za ufisadi.
Mwanafamilia huyo juzi aliieleza Tanzania Daima kwamba, Ballali alifikia uamuzi huo wa kuzikwa Marekani, kutokana na kufadhaishwa na namna jina lake lilivyokuwa likihusishwa na tuhuma nzito za ufisadi.
“Yeye mwenyewe ndiye aliyeamua azikwe huku Washington. Siku zote amekuwa akitueleza namna alivyokuwa akifadhaishwa sana kutokana na kuchafuliwa kwa jina lake, hata baada ya kuitumikia nchi yake kwa juhudi kubwa, moyo mkunjufu na kwa uadilifu wa hali ya juu.
“Alitueleza hapa kwamba hajapata kuiibia nchi yake hata senti moja. Hapo ndipo aliposema akifa angetaka azikwe huku huku Washington na si nyumbani, ambako alihusishwa na kila aina ya tuhuma,” alisema mwanafamilia huyo juzi, kauli ambayo jana aliendelea kuisisitiza.
Akizungumza jana, alisema alimuona Ballali kwa mara ya mwisho akiwa hai, Alhamisi ya wiki iliyopita, ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufikwa na mauti.
“Nilipomuona Alhamisi iliyopita nilimkuta akiwa amewekewa ‘drip’ nyumbani kwake, ikiwa ni kama siku moja au mbili tangu alipotolewa hospitalini, baada ya madaktari kumweleza kuwa walikuwa hawana lolote la kufanya,” alisema ndugu huyo.
Aidha, jamaa huyo wa Ballali alikanusha taarifa kwamba, Ballali alikufa baada ya mashine za kumsaidia kuishi kuzimwa kutokana na uamuzi uliofikiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na madaktari.
“Hapana, hakuwa katika mashine wakati akifariki. Alifia nyumbani kwake Washington na si Boston kama ilivyotangazwa na BoT,” alisema.
Mbali ya hayo, ndugu huyo wa Ballali aliieleza Tanzania Daima kwamba, mke wa Ballali, Anna Muganda, alikuwa ameomba msiba wa mumewe ufanywe kwa faragha, ukiwahusisha ndugu, marafiki na jamaa zao wa karibu.
Alisema kutokana na hali hiyo, shughuli hizo za msiba zilikuwa zikifanyika pasipo kuwapo kwa shughuli zozote za wazi kama vile kuchukua picha za video au kupiga picha nyingine za kawaida.
Aliieleza Tanzania Daima kwamba, kwa muda wote huo wa msiba, Anna alikuwa mtulivu na alikuwa amezima simu zake zote na hakuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya kumzika mumewe leo hii.
Alisema pia kwamba, mama mzazi wa Ballali ambaye hivi sasa anaishi Boko, jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 94 alikuwa ameshindwa kusafiri kutokana na uzee.
Pamoja na hilo, aliieleza Tanzania Daima kwamba, taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Katibu wa Gavana wa Benki Kuu, jana alikuwa amekwenda Boko kuhani, ikiwa ni pamoja na kutoa ubani kwa ajili ya msiba huo.
Habari kutoka Boston na Washington ambazo Tanzania Daima imeshapata kuziandika, zinaeleza kwamba, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisema kwamba, Ballali alikuwa akisumbuliwa na aina moja ya saratani kwa muda mrefu. Hata hivyo wakati kukiwa na taarifa hizo, baadhi ya ndugu, marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba, Ballali alilishwa aina fulani ya sumu isiyojulikana, siku kadhaa kabla hajakimbizwa Marekani kwa matibabu. Taarifa hizi za kulishwa sumu zimekuwa zikienea kwa haraka katika maeneo tofauti na baadhi ya watu tayari wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kujua ni kitu gani hasa kilikuwa kimempata

Talking about wanamtandao!
Mtandao haswa haswa...
 
jmushi1,
Mbona haumulizii invisible, hawa jamaa wanafanya zile mbio za vijiti, unazifahamu? mmoja akipumzika anakamata mwingine, sasa ni zamu ya Mwkjj, akienda kula mara utamuona Invisible kaibuka , jmushi1,hadi tutachemsha, ni lazima washinde, wao ndiyo wanazijua habari hizi kwa kina, ila tunaomba kama wakifanikiwa kupata picha za babayetu Balali wakati akizikwa watuwekee hapa itatutia faraja sisi tulio mbingu ya saba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom