Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
- Thread starter
-
- #81
Ubarikiwe sana. Kuhusu uchawi babu aliniacha vizuri hivyo namna watakavyokuwa wanakuja ndivyo watakavyopokelewa. Ahsante sanaNi kweli kabisa.,.
Kina samike ndio moja ya watu wa kwanza kwanza kuuza chumvi huko
Miaka ya nyuma mpanda ilikuwa kama kisiwa yaani bidhaa zilikuwa chache uhitaji mwingi.
Na mpka sasa najua Bado uhitaji ni mwingi huko wa bidhaa mbalimbali angalia kitu kimoja Fanya.
Nilikuchunia kuhusu kunipm sababu najua tu utafanya utafiti na kujua cha kufanya.....
Hata upande wa madini wako vizuri Fanya utafiti dhahabu IPO nyingi.
Unaweza kusogea pia hapo sumbawanga ukafanya utafiti kidogo maana pia hapo ni pazuri sana kibiashara.
Angalizo mdogo wangu..... Hiyo Kanda uchawi wao mkubwa ni chuma ulete kuanzia shambani mpka kwenye biashara kuwa makini.
Asubuhi njema.
Mkuu umenikumbusha mbali sana! Hizi sehemu zote nimepita na baadhi ya uliowataja hapo nilibahatika kuonana nao ana kwa ana!Kutoka Tabora unakwenda Sikonge then Ipole. Hapo kuna game reserve. Ukitoka Ipole unapiga pori hadi Mto koga. Hapo ndio Mpaka wa Tabora na Katavi.
Pori la Mlele Game reseve kuna ufugaji sana wa Nyuki na kuna Umoja wa wafugaji nyuki Inyonga (IBA) japo sasa hauna nguvu rena kama kipindi wakiwa chini ya akina Bro. Kamaka.
Ukiingia Hapo Inyonga kuna Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Ilikuwa moto sana kipindi cha DC Lubinga na DED Benne.
Fursa zipo sana Hapo Inyonga kwenye Kilimo cha tumbaku, Mpunga, Mahindi, Karanga na kuweka viwanda vya kubangua na kuchakata Karanga. Nilijaribu Kilimo cha Tumbaku, hahahah shuruba alafu unakuja kutapeliwa na viongozi wa UKONONGO AMCOS. 😂😂😂
Kutoka hapo unapiga pori hadi Urwira kuna kambi ya Wakimbizi Hapo na wanafursa ya Kilimo cha Mbogamboga pia dili haramu za Wanyamapori bila kusahau Tumbaku a.k.a Sunko.
Mpanda mjini pamechangamka sana na kuna fursa kwenye viwanda vya kuchakata mazao. Msalimie sana Said Kafirika pamoja na wale vijana wa Mzee Zozi(Sasa naamini ni wazee wenzangu)
Kabla ya kufika mwese, kuna sehemu panaitwa Kapanga. Hapo ndio nilinusurika kuuawa wasukuma tulipoenda kupora ardhi. Yule diwani aliwahamasisha wasukuma kutukata mapanga pamoja na kumuhonga Powertiller.
Msalimie Choef Kapongo chief wa Wabende wa Hapo Mwese. Atakusaidia sana kwenye mashamba japo nina ekari 60 zangu Hapo mwese nilizitelekeza. Mtafute na msalimie Bwana Shamba mstaafu mzee Mwakilema mzee wa Kahawa. 😂😂
Mizinga umetengeneza ta kisasa mkuu?Mkuu umenikumbusha mbali sana! Hizi sehemu zote nimepita na baadhi ya uliowataja hapo nilibahatika kuonana nao ana kwa ana!
Mimi nilibahatika kupata mashamba kule Manga kati ile njia ya kwenda mto Ugala...nikamegewa ardhi ya kutosha ni nimeshaweka mizinga 200!! Najipanga nirudi huko mwakani nikaangalie mambo yangu yanaendaje! Niuzie hizo ekari ulizozitelekeza mkuu
skimu za umwagiliaji bado zinafanya kaz ila mashine za mwampuli zilishajifia kutokana na matajiri wengi kuweka mitambo ya kisasa hapa mji wa majimoto.Hivi ile mashine ya kuchakata mpunga ya Mwamapuli inafanya kazi pamoja na skimu za Kilida na Mwamapuli?
Tulipigaga pesa ya ufisadi pale.
Fursa hiyoMpanda huo mji vitu expensive sana
Miaka yote nilikuwa najua Mpanda ni mkoa 🤔Katavi ndo Mkoa.
Mpanda ni wilaya...like Moshi wilaya,mkoa Kilimanjaro.
So Mpanda ni maarufu kama Moshi.
Ni mizinga ya kisasa mkuu,nimeweka mwaka huu! Kuanzia mwakani ndio nitaanza kuvuna asaliMizinga umetengeneza ta kisasa mkuu?
Maana maeneo hayo kuna mizinga ya kienyeji tupu.
Vipi uzalishaji wa asali maeneo hayo upoje? Niliuliza Lita 20 za asali nikaambiwa 90k nikashangaa sana. Huku tuna Lita ya asali 13k hadi 15k
Maana yake Lita 20 ni zaidi ya 260k!
Nimesikia humu uchawi wa story nyingi za chuma ulete, tupe story maana halisi/how it worksNi kweli kabisa.,.
Kina samike ndio moja ya watu wa kwanza kwanza kuuza chumvi huko
Miaka ya nyuma mpanda ilikuwa kama kisiwa yaani bidhaa zilikuwa chache uhitaji mwingi.
Na mpka sasa najua Bado uhitaji ni mwingi huko wa bidhaa mbalimbali angalia kitu kimoja Fanya.
Nilikuchunia kuhusu kunipm sababu najua tu utafanya utafiti na kujua cha kufanya.....
Hata upande wa madini wako vizuri Fanya utafiti dhahabu IPO nyingi.
Unaweza kusogea pia hapo sumbawanga ukafanya utafiti kidogo maana pia hapo ni pazuri sana kibiashara.
Angalizo mdogo wangu..... Hiyo Kanda uchawi wao mkubwa ni chuma ulete kuanzia shambani mpka kwenye biashara kuwa makini.
Asubuhi njema.
Kama mwakani nitakuwa huko!Ni mizinga ya kisasa mkuu,nimeweka mwaka huu! Kuanzia mwakani ndio nitaanza kuvuna asali
Nililazimika kuwa mwanakijiji wa pale japo siishi pale! Michango ya maendeleo n.k nashiriki kwa ukubwa kama wanakijiji wa pale! Bahati nzuri nilienda kule kwa shughuli flani za utafiti wa kilimo ambao in the end uliwanufaisha wanakijiji kwahiyo ikawa rahisi mimi kupewa eneo (japo nilinunua pesa ndefu kiaina) na wao ndio walinisaidia kunitafutia mafundi wa mizinga n.k...mbao nilinunua mkuu,hawaruhusu kukata miti hovyoKama mwakani nitakuwa huko!
Japo sisalama lakini nijuze mkuu. ki Geography maeneo ya huko yana miti mingi chaguo lako au utakavyo hiyo mizinga si ulichongea hukohuko shambani? kumaanisha kwamba ulivuna miti humohumo na kuleta fundi ama sivyo?
Moja ya fursa zisizo na gharama ni hiyo na pia huhitaji nyuki kuwahudumia kama maji nk maana mito maji ni bwelele siku zote
Vyema kabisa. Mimi katika kuuliza niliambiwa sehemu kubwa ya ardhi ya kule ni hifadhi hivyo unaweza kushikishwa na wahuni waliozeeka nikweli hili?Nililazimika kuwa mwanakijiji wa pale japo siishi pale! Michango ya maendeleo n.k nashiriki kwa ukubwa kama wanakijiji wa pale! Bahati nzuri nilienda kule kwa shughuli flani za utafiti wa kilimo ambao in the end uliwanufaisha wanakijiji kwahiyo ikawa rahisi mimi kupewa eneo (japo nilinunua pesa ndefu kiaina) na wao ndio walinisaidia kunitafutia mafundi wa mizinga n.k...mbao nilinunua mkuu,hawaruhusu kukata miti hovyo
Ni kweli sehemu kubwa ya ule mkoa ni hifadhi so uwe makini! Ila kuna baadhi ya maeneo mengi tu makubwa kabisa tena ardhi yake ni very arable unaweza kufanya shughuli zako vizuri tu! Mfano Mwese ulikoenda,kuna sehemu kunaitwa namba 1 ni mbali kishenzi ila kuko poa kabisa na ardhi inapatikana kwa urahisi kabisa! Ukitaka kutoboa ukubali kukaa chaka na kukomaa na wasukuma! We si umeona hao wasukuma uliowatembelea life yao? Na wana hela kishenzi! Ukubali maisha hayo umatoboa vizuri tuVyema kabisa. Mimi katika kuuliza niliambiwa sehemu kubwa ya ardhi ya kule ni hifadhi hivyo unaweza kushikishwa na wahuni waliozeeka nikweli hili?
Wewe mchakarikaji nimekukubali, hadi gongo, twende!Palinifungulia fursa......
2011 Niliweza kupata ardhi ya kilimo na kufanya biashara muda ambao wengi hawakuwa wakipafikiria. Hapo mpanda mjini wajomba zangu ambao ni wafanyabiashara walinipa gepu la kuuza chumvi.
Huko Kuna msimu wa kuuza madumu ya mafuta ya lita 20 na lita 5.
Kuna msimu wa gongo wa kuuza mapipa.
Vyombo vya plastic na masufuria tuliuzia ndani ya fuso tandamu wanazengo wanapanga mstari ni siku mbili tu vimeisha.
Tanzania Ina utajiri mkubwa sana
Huyo hapo juu kakupotosha, wewe wawezakuwa ulikuwa sahihi.Miaka yote nilikuwa najua Mpanda ni mkoa 🤔
Hahahaha ni zamani sana bosi. Toka 2011 hadi leo sijazifuatilia.Mkuu umenikumbusha mbali sana! Hizi sehemu zote nimepita na baadhi ya uliowataja hapo nilibahatika kuonana nao ana kwa ana!
Mimi nilibahatika kupata mashamba kule Manga kati ile njia ya kwenda mto Ugala...nikamegewa ardhi ya kutosha ni nimeshaweka mizinga 200!! Najipanga nirudi huko mwakani nikaangalie mambo yangu yanaendaje! Niuzie hizo ekari ulizozitelekeza mkuu
Mkuu hapa mwenye ni msukuma lakini daah jamaa zangu wanaishi kijima mnoo mtu ana ng'ombe 200 kasoro lakini wanalalia ngozi habari za godoro kwao ni anasa!Ni kweli sehemu kubwa ya ule mkoa ni hifadhi so uwe makini! Ila kuna baadhi ya maeneo mengi tu makubwa kabisa tena ardhi yake ni very arable unaweza kufanya shughuli zako vizuri tu! Mfano Mwese ulikoenda,kuna sehemu kunaitwa namba 1 ni mbali kishenzi ila kuko poa kabisa na ardhi inapatikana kwa urahisi kabisa! Ukitaka kutoboa ukubali kukaa chaka na kukomaa na wasukuma! We si umeona hao wasukuma uliowatembelea life yao? Na wana hela kishenzi! Ukubali maisha hayo umatoboa vizuri tu
Sahihi. Maana hakuna katavi bila MpandaHuyo hapo juu kakupotosha, wewe wawezakuwa ulikuwa sahihi.
Ilitakiwa akutolee mfano wa Mkoa wa Mara, Kagera, Simiyu, Kilimanjaro na Mikoa mingine ambayo majina yake ya Mikoa yametofautiana na majina ya miji ya makao makuu ya Mikoa hiyo.
Hapo Mpanda, kabla Mkoa wa Katavi haujaundwa ilikuwa ni makao makuu ya Wilaya ya Mpanda, Wilaya mojawapo iliyokuwa ikiunda Mkoa wa Rukwa.
Lakini hivi sasa Mpanda ndiyo makao makuu ya Mkoa wa Katavi.
Mtu anaposema: 'ninaenda Mkoani' elewa kuwa anamaanisha anaenda Mpanda makao makuu ya Mkoa.
Kwahiyo kuna uwezekano wanazengo wameshajipimiaHahahaha ni zamani sana bosi. Toka 2011 hadi leo sijazifuatilia.
Umamfahamu nani kati ya hao niliowataja? Chief Kapongo au?
Niliwaachia mkuu. Niliacha zingine 100.Kwahiyo kuna uwezekano wanazengo wameshajipimia
Sawa mkuu.Niliwaachia mkuu. Niliacha zingine 100.
Nitafungua ID yangu kwa baadhi ya wadau humu ila Siwezi kurogwa kwa ajili ya ardhi bosi. Hapa........ wasukuma walivamia eneo langu baada ya kufukuzwa hifadhini wakati wa operesheni ya "TOKOMEZA UJANGILI YA MWAKA 2013".