Hatimaye nimemaliza salama miaka mitano JF bila Ban

Hatimaye nimemaliza salama miaka mitano JF bila Ban

Tarehe 24.9.2014 nilijiunga rasmi Jamii Forum baada ya kuwa naingia nakucheck kama mwaka hivi.

Kilichonifanya nijoin ni kujibu comments za watu tu.
KuNa muda naona comment imenifurahisha ila nashindwa kuijibu mpaka siku nilipokata shauri la kujiunga uanachama.

Kwa kweli kumaliza miaka mitano bila BAN wala kufungua ID ya pili sio jambo dogo.
Wengi huku wana maID manne matano ila mie hii moja tu na imedumu.

Kuna siku nilinusurika Ban naona ni Mungu alikua nami maana wenzangu karibu wote walipigwa ban ila mimi naona mods walinisahau.

Nilichojifunza kuepuka ban ni kuvumilia upumbavu wa kila mtu anaekukwaza na ukishindwa mjibu kistaarabu.
Nakumbuka hiyo siku aisee watu tulikula bani we ukapona hafi nikahisi

Kuna modi ni shemu etu
 
Nilikua naingia kwa blog ya Sinta.. kuna sehemu kunakua na list blogs nyingine, katika kufungua na kufungua nikakutana na JF. Nikawa naingia tu nasoma. Kwahiyo nikiangaza kublog naanza na Sinta, U-turn, JF na zingine
Swali linakuja kwako sasa...

Uliijuaje JF??
 
Ukizoea jukwaa la siasa ban lazima zikuhusu. Kule naingiaga kwa adabu aisee.
Ban ile nilinusurika pekee nahisi [emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3]hongera sana miye ban ya kwanza na mdada anaitwa Kimberly sijui yuko wapi siku hizi kisa Ali Kiba na Daimond mwaka 2016 ya wiki,ya pili nilijichanganya siasani nkawekwa dentetion siku moja,ya tatu ndo zile za mkumbooo uleee wewe ukanusurika siku hizi jf sijui kwa nini sio sana kuingia maana wala siko busy!kivile
 
Inawezekana kuna ukweli hapo mkuu
Hizi ID pia zina-reflect umri wa watu walio wengi wenye ID kongwe zenye zaidi ya miaka mitano asilimia kubwa ni watu wazima umri wao umevuka miaka 25, kwa hiyo sio rahisi kupata ban maana mtu anabehave kiheshima zaidi. Huwa nahamaki sana mtu mwenye ID kongwe aki-misbehave.
 
Nilikua naingia kwa blog ya Sinta.. kuna sehemu kunakua na list blogs nyingine, katika kufungua na kufungua nikakutana na JF. Nikawa naingia tu nasoma. Kwahiyo nikiangaza kublog naanza na Sinta, U-turn, JF na zingine

Hivi blog ya Sintah bado ipo? Nina kama miaka 7 hivi sijaingia kule.

Huu uzi nadhani haunihusu, maana nina ID kama 7 zote zina ban.
 
Back
Top Bottom