ha ha mkuu, cha kwanza kukushauri kabisa ni kusali kwa imani yako, kuna nguvu kubwa sana katika maombi, na siku zote unapotaka kitu all the universe conspire for you to achieve it
Pili ni kukata aina ya marafiki ulionao, na pia mambo unayoyafanya kwa mda huu yasiyo na tija kama kukaa kijiweni, bar, ku bet n.k
"Cut all the grass, so that all snakes around you run away"
Pili, tafuta marafiki wapya, shughuli mpya ya kufanya hata kama ni ya kujitolea, hata kama ni banda nyumbani tengeneza, usikae tuu fanya kitu
***kuna dogo nilikuwa ninakaa naye home (kwa mzee kipindi icho) akawa mvivu sana na nikirudi anaomba hela, hamna kitu anafanya, nilimpa changamoto, leo hii ana kampuni yake ya landscaping, mimi nilimuambia tuu kwenye maua pale home lisizidi ua wala jani, kusikauke ua, wala uchafu wowote nisione, nitampa hela anapohitaji, leo hii ana kwake na anafanya shughuli zake na anaendelea kukua****
Acha dharau, tafiti zinaonyesha biashara ndogo zikiwa multiplied zinatengeneza faida kuliko kawaida, fungua biashara ndogo kabisa utakayoweza ku afford, then multiply it
zaidi ya yote, kukata tamaa ndio uchawi unaendelea kukuloga, leo huna nyuma wala mbele, kesho utakuwa na nini?acha kukata tamaa
Mwisho kabisa nikutakie Happy birthday, 30 years mzee si michache, mimi nitatimiza mwakani Mungu akijalia