Hatimaye nimetimiza miaka 30 ila sina mbele wala nyuma naombeni ushauri

Kuna nafasi ya kusomea uganga WA kienyeji Handeni mwaka mmoja ukimaliza hapo naamini utapata ajira na bila shaka nyuma na mbele utupata
 
Maisha hayana formula, unavyoyatengeneza ndivyo yanavyokua.
Usiwe na tamaa ya kujifananisha na matajiri ambao hujui historia za maisha yao.
Jifunze kupangilia na kubana matumizi kwa kipato chako unachokipata.
Usipende kujitanua ili watu wakuone unazo wakati unajua uwezo wako. Jichanganye na watu, tumia kipato chako kujiongezea miradi mingine.
Mafanikio hayaji kwa kukaa na kuyasubiri bali hutafutwa kwa udi na uvumba
 
Mambo matatu yatakusaidia dunia hii
1.Ujuzi/maarifa
2.Nani unamjua
3.Nani anakujua

Ukitaka maendeleo jiweke karibu na watu wenye maendeleo.ukitaka kujua kupika kuwa karibu na wapishi.Kama wewe ni maskini l, rafikizo na kampani yako wote wako na hali kama yako basi hutakaa usogee abadan.

Jitahidi kuongeza maarifa mapya kila siku.siju isipite hujajifunza kitu kipya chenye maslahi.be resourceful.ukifuata ushauri huu,mwakani muda kama huu utakuwa mtu mwengine kabisa.
 
Duu namimi nilieneza miaka 30
29 /9/2017 hongera sana mkuu safari bado nindefu ndoo tuko robo ya mugabe [emoji23][emoji23]
 
Kaka asante nimeupenda sana
Ushauli ulionipa
 
Ushauri wangu 2020 usiwapigie kura CCM
 
Jamani leo ni birthday yangu

Nimetimiza miaka 30 lakini sina mbele wala nyumaa

Vyuma vimekaza hadi sasa sina mbele wala nyuma

Naombeni ushaurii

Sasa unajisaidia vipi haja kubwa na ndogo Ikiwa huna mbele wala nyuma!!?
 
Hili bandiko lina hisia kali sana...kwa kijana yeyote anayejitegemea na mwenye malengo ya kimaisha hawezi kuleta maskhara hapa!pole sana chief inabidi tu kuzidisha juhudi kwa unachokifanya huku ukitafuta namna nyengine ya kujinasua.
 
Kwanza ijue hali yako
Pili zitambue sababu za uwepo wa hali hiyo. Tatu tafuta alternative tatu za kuondokana na hali hiyo bila uoga.
Mfano umesoma ajira hakuna angalia uwezekano wa kuingia ktk kilimo kwa mtaji mdogo tu hata laki mbili ukibase ktk mazao yasiyo na purukushani nyingi kama mahindi, maharage na karanga. Tumia zaidi nguvu yako siyo vibarua.
Fanya kazi zozote usichague lenga kupata mtaji kusanya pesa usiidharau usiwe na silika ya kumaliza hata kama umepata kidogo tunza kidogo.
Jiepushe na kazi za magendo kupata pesa kubwa.
Kama kulima huwezi tafuta biashara za kuzungusha hasa matunda mtaji laki mbili unatoboa tu.
Usiwe mvivu na mwenye dharau kwenye pesa Mungu hapendi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…