Hatimaye TEC yapoteza imani katika jamii

Huyu naye sijui anaandika ujinga gani huu
 
Hapo awali wadau mbalimbali walifafanua kuwa ule haukuwa mkataba Bali maafikiano tu ya ushirikiano wa kibiashata.
Kwa hiyo na wewe unaendelea na msimamo kuwa ule sio mkataba bali ni maafikiano tu ya ushirikiano wa kibiashara? Tangu lini 'maafikiano tu' yakaenda kujadiliwa na kupigiwa kura bungeni ili kuyapitisha?
 
Kwa hiyo na wewe unaendelea na msimamo kuwa ule sio mkataba bali ni maafikiano tu ya ushirikiano wa kibiashara? Tangu lini 'maafikiano tu' yakaenda kujadiliwa na kupigiwa kura bungeni ili kuyapitisha?
Think it differently, ingekuwa mkataba ingewaje tena uakaeditiwa? Mkataba ni final hasa ukishasainiwa
 
TEC walituandikia waraka wakidai wamebaini MAPUNGUFU kwenye mkataba wa bandari, waraka ukasomwa kwenye nyumba za ibada kuishinikiza serikali IUFUTE MARA MOJA.

tumeshuhudia zawadi ya Milioni 100,kanisani na kikao cha Kadinali na serikali baada ya hapo tumeona MCHANA KWEUPE TEC inatuma wawakilishi kwenye hafla ya kusaini mkataba!!!?

Je TEC walishindwa kutupa taarifa ya nini kinachoendelea? Kitima amekosa uungwana wa kutuambia kwanini wanakubali kuhudhuria na kuubariki mkataba? Je kuna muendelezo wa kuishinikiza serikali iufute au ilikuwa ni DANGANYA TOTO

KITIMA njoo hapa useme unatuonaje watanzania?
 
Kawaulize hao mapadri wako kama wameuona huo mkataba uliosainiwa jana, na yale makubaliano ya mwanzo uliza kama yamefutwa usiwe unaropoka tu
 
Kitima anasema aliitwa bila kujua anaenda kufanya nini
 
Kama wamebadilisha vipengele basi Dr Slaa, Mudude, Mwabukukusi na Tundu Lissu wachukue maua yao.
 
Think it differently, ingekuwa mkataba ingewaje tena uakaeditiwa? Mkataba ni final hasa ukishasainiwa
Kwani hukuona ule umeenda bungeni ukiwa tayari umeshasainiwa? Watu walipokuwa na mashaka, usifikiri ni wajinga. Mojawapo ya mambo yaliyoleta mashaka ni kuwa ulishasainiwa.

Majaji wa Mahakama kule Mbeya wameuita kuwa ni mkataba, wewe sijajua ni nani unasema sio mkataba!

 
Kwani, wewe unajua ni kwa kiwango gani maoni yao yamesababisha mabadiliko kwenye mkataba wa sasa?
Ucjal.
Haya yote tukipata muda, tutayajadili kwenye kitabu changu kipya kiitwacho, 'Arch-@ngels Entertained!'.
 
Marekebisho yamefanyika kwa % kubwa, hakuna ambaye anapinga uwekezaji watu walikuwa wanapinga aina ya mkaaba maboresho yamefanyika
 
Kwani, wewe unajua ni kwa kiwango gani maoni yao yamesababisha mabadiliko kwenye mkataba wa sasa?
Mabadiliko gani Mkuu kwani hayo mambo kuwa DPW watapewa gati no 4-7 na ukomo wa muda utakuwepo kati ya DPW na TPA si ndio mambo Serikali ilikuwa inasema kila siku mpaka wakatumwa kina Kitila,Wasira nk kuja mikoani kutufafanulia mambo hayohayo?

Hata Mwandishi mkongwe Pascal Mayalla kila siku alikuwa anatoa elimu kuhusu mambo hayo hayo? Wote tulivimbisha vichwa na kudai Serikali ni waongo IGA ndio Mkataba wenyewe sasa Leo Kiko wapi?

Yale yale waliosena Serikali ndio yaliofanyika kama leo tunaipongeza Serikali kwa kitu tusichokiona kwa nini tusingewaamini toka mwanzo mpaka tukataka kufanya maandamano?

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa hili sakata je leo nani ni mkweli kati ya Serikali na Wanaharakati na wanasiasa wetu hawa? Ukweli lazima usemwe inaonekana dhahiri kuna baadhi yetu tulikuwa tunapinga kwa kuufuata mkumbo au chuki tu za kidini kwa sababu tu wawekezaji ni Waarabu
 
Tena maboresho makubwa sn yamefanyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…