Hatimaye tumekutana tena. Alinifaa kwa Jua lake leo nimemfaa kwa mvua yangu

Hatimaye tumekutana tena. Alinifaa kwa Jua lake leo nimemfaa kwa mvua yangu

Right Way In Light

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2024
Posts
1,322
Reaction score
3,461
Huyu jamaa alishawah nisaidia nikaipata bag ya laptop niliyoibiwa nikiwa nimepaki gar ofisin na laptop nimeacha ndani ya gari.

Hanijui simjui ila alikua mpangaji mwenzagu kwenye hizo frame.

Alinisaidia baada ya kuitafuta sana kuambulia patupu nikakata tamaa. (Ni story ndefu sana).

Ila mwisho wa siku nikaipata na tukaachana na hatukuwahi onana tena miaka maana hata ofisi nikaamua kuhamisha.

Sasa juzi kati nikakutana nae TRA anafuatilia Tax clearance. Biashara yake imekua sasa na anaifanya kwa mfumo wa kampuni.

Ila ni mgeni kabisa kwenye masuala ya mahesabu na uandaaji wa taarifa kwaajil ya kodi akanielezaaa na mwisho wa siku akanambia kila anapogusa, tax consultant wa chini kabisa kamtoza 2M na hiyo pesa hana na ana haraka na hiyo certificate.

Tukabadilishana namba kisha nikapiga simu kadhaa kwa mtu wangu wa karibu tunae heshimiana nikamuomba amsaidie jamaa angu, kisha nikawaunganisha.

Baada ya siku 1 akanipigia jamaa anashukuru mnooo, maana yule mdau wangu wa hesabu alimfanyia kaz yake sawa na bure kabisa akamtoza hela ya maji tu 300k kutokana na mahusiano baina yanfu na yake.

Jamaa akafurah sana.
Nami pia nikafurahi.
Maana alishanisaidiaga kwanza before!!!.

Dunia Duara...
Malipo hapa hapa
 
Thats super mkuu,Hakuna mtu ambaye hakufai hata siku moja,heshimu sana watu sio kwa sababu wana kitu,hapana bali kwa sababu ndio ustaarabu wenyewe na palipo na nafasi ipo siku mtu atakufaa mpaka utashangaa mwenyewe.
 
Sahihi sana, huyu bwana alinisaidia sana. Na nimekuja kugundua kuwa unapomsaudia mtu kwa moyo bila kutegemea chochote, unajisikia raha sana moyoni
 
Isije ikawa aliiba mwenyewe akaamua akurudishie tu.
Ila wema ni akiba mkuu... Mbarikiwe wote
Hapana, tukiwakamata jamaa walioiba, na ndio maana nikasema ni story ndefu maana kwenye ile laptop bag pia kulikua na wife device ambayo ilikua connected na simu yangu so ilituongoza kupata muafaka japo jamaa ali play part kwa 95% maana jamaa nafikiri ana uhusiano na polisi yale maeneo niliokuwepo
 
Thats super mkuu,Hakuna mtu ambaye hakufai hata siku moja,heshimu sana watu sio kwa sababu wana kitu,hapana bali kwa sababu ndio ustaarabu wenyewe na palipo na nafasi ipo siku mtu atakufaa mpaka utashangaa mwenyewe.
Ni sahihi na hii ndio kanuni yangu ya maisha, kuheshimu na kumsaidia kila mtu pale niwezapo japo kuna wengine wanatujeruhi na kutaka kutufundisha Roho mbaya na ukatili.
 
Ni sahihi na hii ndio kanuni yangu ya maisha, kuheshimu na kumsaidia kila mtu pale niwezapo japo kuna wengine wanatujeruhi na kutaka kutufundisha Roho mbaya na ukatili.
Ni kwel, sio wote wanakua waungwana ,japo ndio hivyo unafanya tu kwakua iko ndani ya uwezo kama usemavyo
 
Dr hyperkid nimekuwekea screenshot ya chat fupi ili uamini kuwa am not intending anything else.
Screenshot_20241022_084332_Messages.jpg
 
Isije ikawa aliiba mwenyewe akaamua akurudishie tu.
Ila wema ni akiba mkuu... Mbarikiwe wote
Dada 😀😀
Ni kweli wema ni akiba ila Mimi kila nilipoyatinyanga wale niliowatesa uwa nakutana nao wakiwa na uwezo kuliko Mimi naishia kujichekesha tu 🤔 japo uwa wananivungia maisha yanaendelea .

Dada mbona wikiendi hukunistua nitende wema ili kesho unifae kwa dhiki .?
 
Mimi kama roho nzuri ni maradhi basi itaniua sisubiri kuambiwa nna roho safi sana hua nautenda wema unarudi mara 10 zaidi na ukihitaji kufurahia ihsan basi fanya kwa siri inafungua sana njia hio
Ni kwel chief. Hata katika mafundisha ya baadhi ya dini, inasisitizwa kuwa fanya msaada pasipokujionyesha. Fanya kwa dhati ya moyo..
Binafsi nimeleta kisa hiki kwa lengonla kujifunza tu na kutiana moyo kuwa it feels good to do good
 
Dada 😀😀
Ni kweli wema ni akiba ila Mimi kila nilipoyatinyanga wale niliowatesa uwa nakutana nao wakiwa na uwezo kuliko Mimi naishia kujichekesha tu 🤔 japo uwa wananivungia maisha yanaendelea .

Dada mbona wikiendi hukunistua nitende wema ili kesho unifae kwa dhiki .?
Ahahahahahahahqhqh...
Umenichekesha sana mkuuu..
Wanasemaga kuwa "shida zina tabia ya kukupeleka kwa wale uliowazingua ndio wakusaidie " 🤣🤣🤣
Sasa hapo lazima tu uwe fund wa kujichekesha ili mambo yaende 😆😆
 
  • Thanks
Reactions: apk
Je ingekuwa hajawahi kukusaidia usingemsaidia? Je unatenda wema kama malipo?

Tukiishi na nadharia ya kutenda wema, kila mtu akawa na roho nzuri, dunia invekuwa sehemu salama zaidi.

Usimtendee mtu wema kisa alikusaidia, tenda wema kwa kila mtu kwa kuwa, kufanya mema inakiwa furaha na amani ya moyo.

Rushwana upuuzi mwingine vipo sababu hatutendeani mema.
 
Back
Top Bottom