Hatimaye tumekutana tena. Alinifaa kwa Jua lake leo nimemfaa kwa mvua yangu

Hatimaye tumekutana tena. Alinifaa kwa Jua lake leo nimemfaa kwa mvua yangu

Huyu jamaa alishawah nisaidia nikaipata bag ya laptop niliyoibiwa nikiwa nimepaki gar ofisin na laptop nimeacha ndani ya gari.

Hanijui simjui ila alikua mpangaji mwenzagu kwenye hizo frame.

Alinisaidia baada ya kuitafuta sana kuambulia patupu nikakata tamaa. (Ni story ndefu sana).

Ila mwisho wa siku nikaipata na tukaachana na hatukuwahi onana tena miaka maana hata ofisi nikaamua kuhamisha.

Sasa juzi kati nikakutana nae TRA anafuatilia Tax clearance. Biashara yake imekua sasa na anaifanya kwa mfumo wa kampuni.

Ila ni mgeni kabisa kwenye masuala ya mahesabu na uandaaji wa taarifa kwaajil ya kodi akanielezaaa na mwisho wa siku akanambia kila anapogusa, tax consultant wa chini kabisa kamtoza 2M na hiyo pesa hana na ana haraka na hiyo certificate.

Tukabadilishana namba kisha nikapiga simu kadhaa kwa mtu wangu wa karibu tunae heshimiana nikamuomba amsaidie jamaa angu, kisha nikawaunganisha.

Baada ya siku 1 akanipigia jamaa anashukuru mnooo, maana yule mdau wangu wa hesabu alimfanyia kaz yake sawa na bure kabisa akamtoza hela ya maji tu 300k kutokana na mahusiano baina yanfu na yake.

Jamaa akafurah sana.
Nami pia nikafurahi.
Maana alishanisaidiaga kwanza before!!!.

Dunia Duara...
Malipo hapa hapa
Reciprocation at work
 
Kuna kipindi fulani nilikuwa na pesa nikawa mtu wa kumsaidia Kila mtu mwenye shida ilimradi nina uwezo wa kumsaidia, leo sina kitu na wale niliokuwa nawasaidia ndio wanaonicheka. Wameshasahau jinsi walivyokuwa Wananijia usiku huku wakibisha hodi hadi mlango ukalegea kwa sauti zao zilizokuwa zinatia huruma. Sasa hivi nina roho ngumu hailezeki sitaki shobo na mtoto wa mwanamke.
 
Back
Top Bottom