Hatimaye tumekutana tena. Alinifaa kwa Jua lake leo nimemfaa kwa mvua yangu

Ahahahahahahahqhqh...
Umenichekesha sana mkuuu..
Wanasemaga kuwa "shida zina tabia ya kukupeleka kwa wale uliowazingua ndio wakusaidie " 🤣🤣🤣
Sasa hapo lazima tu uwe fund wa kujichekesha ili mambo yaende 😆😆
Kaka acha tu hamna muda mgumu Kama wakati unakutana na uliyemtesa alafu muda huo yamekubali ,utatabasamu Mara ujichekeshe mpaka unajionea aibu wewe
 
Je ingekuwa hajawahi kukusaidia usingemsaidia? Je unatenda wema kama malipo?
Angekua hakunisaidia maana yake tusingekua na ukaribu wa yeye kunifungukia ishu zake..
Ile siku kanisaidia ndio uhusiano wetu ulianza rasmi naweza sema maana before hapo ilikua tu kupeana hi kawaida sana.

Ila sasa kama tulivyo wanaume, licha ya kubadilishana namba ila hatukuwah wasiliana hata mara moja zaid ya mwaka mpka tumekutana hii juz kati ndio haya yakatokea
 
natural law pays
 
Mimi kama roho nzuri ni maradhi basi itaniua sisubiri kuambiwa nna roho safi sana hua nautenda wema unarudi mara 10 zaidi na ukihitaji kufurahia ihsan basi fanya kwa siri inafungua sana njia hio
Waliosema wema hauozi hawakukosea aisee. Wakati mwingine unafanya wema halafu unasahau baada ya muda fulani unakutana na surprise ya kulipwa mara 10 ya ulichotoa.
 
Sawa mkuu, mbarikiwe Sana...huo ndiyo ubinadamu
 
Sawa mkuu, mbarikiwe Sana...huo ndiyo ubinadamu
Amen..hakika japo ubinadam kazi maana sio wote binadam. Umakini pia ni muhim usije ukanyongwa kwa kamba yako mwenyewe au ukaponzwa na wema wako mwenyewe. Si unaelewa tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…