Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Kwa upande wa filamu bora zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania,basi kwenye hiyo listi Shumileta haiwezi kukosa hata iweje.
Stori ya filamu inasisimua sana na iliishia sehemu ya pili, na baada ya mashabiki kuomba muendelezo wake hatimaye gwiji Mussa Banzi anachia rasmi sehemu ya 3 ya filamu hii na habari zilizo njema zaidi wameshaanza ku shoot hii filamu na panapo majaaliwa huenda hata mwezi wa 4 usifike filamu itakuwa tayari imeshaachiwa.
Mussa Banzi ameyathibitisha hayo na uzuri ni kwamba wale main characters wote wapo,Shumileta mwenyewe yupo, Mack yupo, Monte (Jennifer Kyaka/Odama) yupo mama wa Shumileta naye pia yumo.
Mussa amezungumza kwamba wale wasanii wa zamani watakuwepo pia atachanganya na waigizaji wapya nao wapate nafasi ya kuigiza kwenye hii filamu.
Tujikumbushe kidogo filamu ilipoishia..........
Baada ya Shumi kumpenda Mack na kumpeleka ujinini kwa wazazi wake na kufunga naye ndoa ya kijini, huku duniani Monte alihangaika kwenye vilinge na vilinge kumkomboa Mack mikononi mwa Shumileta na hatimaye Chili aliifanya hiyo kazi vizuri sana kumrudisha Mack duniani ila kwa bahati iliyo mbaya mdogo wa Shumileta aitwaye Soya aliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kumtupia kombola la kijini hatimaye Mack akafariki dunia.
Lakini ikumbukwe kipindi hicho Shumileta alikuwa ametiwa nguvuni na mganga Chili na kufungiwa kwenye guduria .
Ila baada ya Shumileta kuweza kutoka kwenye hiyo guduria alikuwa na nguvu za ajabu zaidi kwa kuanza kuwahi makaburini kabla Mack hajazikwa , alifanikiwa kumfufua na kumrudisha tena ujinini.
Kimbembe huko ujinini Soya alikuwa anamtaka kimapenzi shemeji yake ambaye ni Mack na akamrubuni wamtoroke Shumileta na iwapo atamkubalia basi atamsaidia kumrudisha duniani wakaishi wote.
Hii ilipelekea vita kubwa sana huko ujinini na wazazi wa Shumileta wakaamuru Shumileta aachane na Mack na kama kuolewa basi ataolewa na majini wenzake.
Kwa upande wa Monte huku duniani alikuwa ameshajikatia tamaa kuhusu Mack maana amezunguka vilinge vingi kumpambania lakini wapi anajikuta tu anajitia matatizoni.
Ila baada ya vita kule ujinini kuwa kubwa na Mack kuachiwa kwa shinikizo la wazazi wa Shumileta, Mack alirejea duniani na kukutana na Monte lakini huko ujinini kaacha vita kubwa sana inaendelea na Shumileta hakuwa tayari kuachana na Mack.
.
Sasa je nini kitaendelea baada ya hapo?