Hatimaye tumeletewa Shumileta Part 3, Kiu ya mashabiki inaenda kukatika

Hatimaye tumeletewa Shumileta Part 3, Kiu ya mashabiki inaenda kukatika

Watoe na kinyamkela, ilijua kunitishaa hii.. nsyuka nilijuaga ni mrisho mpoto😆😆 kulala ilikuwa kasheshe enzi hizo..
Mack aliteseka sana kwenye Kinyamkela ili akubali kurithishwa mkoba wa kiganga

Kinyamkela mwishoni Mack anafariki kama unakumbuka.

Mack alifariki baada ya kuchoma moto ule mkoba wa uganga .

Kama unakumbuka alianza kuugua kwanza uchizi baada ya kuukojolea ule mkoba aliokabidhiwa na marehemu mama yake ,

Alikataa aliona kama anashusha hadhi yake maana yeye kitaaluma ni daktari sasa kuwa tena mganga akaona weeeee usinitanie,
 
Hahaha nakumbuka kiasi chake! Ila ilikuwa na balaa duhh zilituogopesha sana
 
Watoe na kinyamkela, ilijua kunitishaa hii.. nsyuka nilijuaga ni mrisho mpoto😆😆 kulala ilikuwa kasheshe enzi hizo..
Nsyuka ameahidi kuitoa kulingana na maoni ya wadau ila naona haina haja.

Maana main character (Doreen) alifariki kwenye ile Insyuka part 3 na Nsyuka akakaa muda mrefu kisha akarudi kwenye maisha ya Sanjo na kuanza kumsumbua.

Mwishoni kabisa Nsyuka anapata kiboko yake, mganga mmoja mashuhuri sana na kumuonesha umwamba aliyeyuka na kutokea mgongoni kwa Nsyuka kisha akagonga msumari kwenye mti mkubwa kumdhibiti Nsyuka.
 
Kwelii..

Vipi na mama mwenye nyumba unaikumbuka?
 
Nilikuwa nauimba sana huo wimbo wa chite chite ukaee😆😆 hivi hiyo ndio alikuwa anamtokea mtu anamuita fettyyyyyy🙆🏽‍♀️.. siku hizi hakuna muvi za mizimu sjui kwann😀
Doreen kwenye Chite Ukae hakutumia jina la Fetty na hakuwahi kutumia kwenye filamu yoyote ile, jina alilotumia kwenye Chite Ukae limenitoka kidogo.

Yule bibi alijua kumuhangaisha sana Doreen miksa kumuulia kila bwana anayempata 😂😂😂😂 mwisho wa siku Doreen naye anatakiwa arudi nyumbani yani Chite (Rudi) Ukae (nyumbani) na kurudi nyumbani kwenyewe ndio kufa .

Alipata Shida sana, tatizo lake mpaka mganga mashuhuri mzee Kigwasi (Chili) alishindwa kufua dafu ila akabahatika kupata mganga mwingine wa kizaramo huyo kiboko mbaya zaidi ndio alikuwa amebakisha siku moja tu afe na ile anatoka tu kwa mganga njiani anakutana na kundi kubwa sana la wachawi .
 
Nahisi hata sahivi na ukubwa huu naweza kuogopa, hadi kulala ilikuwa mtiti
Sikuhizi hata kwenye jamii mambo ya wachawi wachawi yamepungua kwa kiasi kikubwa ndio maana hata filamu unaweza usiogope tofauti na miaka ya nyuma uchawi unaona live na kwenye TV pia unaona.

Ila jamaa kaahidi kuja vitu adimu sana
 
Doreen kwenye Chite Ukae hakutumia jina la Fetty na hakuwahi kutumia kwenye filamu yoyote ile, jina alilotumia kwenye Chite Ukae limenitoka kidogo.

Yule bibi alijua kumuhangaisha sana Doreen miksa kumuulia kila bwana anayempata 😂😂😂😂 mwisho wa siku Doreen naye anatakiwa arudi nyumbani yani Chite (Rudi) Ukae (nyumbani) na kurudi nyumbani kwenyewe ndio kufa .

Alipata Shida sana, tatizo lake mpaka mganga mashuhuri mzee Kigwasi (Chili) alishindwa kufua dafu zaidi ila akabahatika kupata mganga mwingine wa kizaramo huyo kiboko mbaya zaidi ndio alikuwa amebakisha siku moja tu afe na ile anatoka tu kwa mganga njiani anakutana na kundi kubwa sana la wachawi .
😆😆😆😆
Una kumbukumbu kali!

Umenikumbusha mzee msisiri mpk nilihisi ni mwanga yule mzee.. anaigiza kama kweli!
 
😆😆😆😆
Una kumbukumbu kali!

Umenikumbusha mzee msisiri mpk nilihisi ni mwanga yule mzee.. anaigiza kama kweli!
Kuna vibibi ambavyo havina hata majina Mussa Banzi sijui alikuwa anaviokotea wapi.

Yani achilia mbali kuigiza, wale bila shaka ni wachawi kweli au wanajua sana mambo ya kishirikina.
 
Kwa upande wa filamu bora zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania,basi kwenye hiyo listi Shumileta haiwezi kukosa hata iweje.

Stori ya filamu inasisimua sana na iliishia sehemu ya pili, na baada ya mashabiki kuomba muendelezo wake hatimaye gwiji Mussa Banzi anachia rasmi sehemu ya 3 ya filamu hii na habari zilizo njema zaidi wameshaanza ku shoot hii filamu na panapo majaaliwa huenda hata mwezi wa 4 usifike filamu itakuwa tayari imeshaachiwa.

Mussa Banzi ameyathibitisha hayo na uzuri ni kwamba wale main characters wote wapo,Shumileta mwenyewe yupo, Mack yupo, Monte (Jennifer Kyaka/Odama) yupo mama wa Shumileta naye pia yumo.

Mussa amezungumza kwamba wale wasanii wa zamani watakuwepo pia atachanganya na waigizaji wapya nao wapate nafasi ya kuigiza kwenye hii filamu.

Tujikumbushe kidogo filamu ilipoishia..........

Baada ya Shumi kumpenda Mack na kumpeleka ujinini kwa wazazi wake na kufunga naye ndoa ya kijini, huku duniani Monte alihangaika kwenye vilinge na vilinge kumkomboa Mack mikononi mwa Shumileta na hatimaye Chili aliifanya hiyo kazi vizuri sana kumrudisha Mack duniani ila kwa bahati iliyo mbaya mdogo wa Shumileta aitwaye Soya aliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kumtupia kombola la kijini hatimaye Mack akafariki dunia.
Lakini ikumbukwe kipindi hicho Shumileta alikuwa ametiwa nguvuni na mganga Chili na kufungiwa kwenye guduria .

Ila baada ya Shumileta kuweza kutoka kwenye hiyo guduria alikuwa na nguvu za ajabu zaidi kwa kuanza kuwahi makaburini kabla Mack hajazikwa , alifanikiwa kumfufua na kumrudisha tena ujinini.

Kimbembe huko ujinini Soya alikuwa anamtaka kimapenzi shemeji yake ambaye ni Mack na akamrubuni wamtoroke Shumileta na iwapo atamkubalia basi atamsaidia kumrudisha duniani wakaishi wote.

Hii ilipelekea vita kubwa sana huko ujinini na wazazi wa Shumileta wakaamuru Shumileta aachane na Mack na kama kuolewa basi ataolewa na majini wenzake.

Kwa upande wa Monte huku duniani alikuwa ameshajikatia tamaa kuhusu Mack maana amezunguka vilinge vingi kumpambania lakini wapi anajikuta tu anajitia matatizoni.

Ila baada ya vita kule ujinini kuwa kubwa na Mack kuachiwa kwa shinikizo la wazazi wa Shumileta, Mack alirejea duniani na kukutana na Monte lakini huko ujinini kaacha vita kubwa sana inaendelea na Shumileta hakuwa tayari kuachana na Mack.
.
.
.
.
.

Nyie wadada wakazi. Mnaandika kitu kama sisi sote tunafahamu. Mi nlidhani issue ya kwetu wanaume. Kumbe mambo yenu mabeki tatu na wamama wa nyumbani. Haya hayo mambo tuwaachie wenyewe mnajuana na lugha zenu.
 
Kuna vibibi ambavyo havina hata majina Mussa Banzi sijui alikuwa anaviokotea wapi.

Yani achilia mbali kuigiza, wale bila shaka ni wachawi kweli au wanajua sana mambo ya kishirikina.
Wale mussa kuna sehemu anawakusanya sio siri! vile vikao vyao jamn uwii! Yani ulikuwa ukisikia tu mussa banzi likaaanza kuoneshwa giza unakaa chonjo kukimbilia chumbani😂😂😂
 
Wale mussa kuna sehemu anawakusanya sio siri! vile vikao vyao jamn uwii! Yani ulikuwa ukisikia tu mussa banzi likaaanza kuoneshwa giza unakaa chonjo kukimbilia chumbani😂😂😂
Kuna wengine kwenye maisha halisia walipata changamoto za kiroho kulingana na filamu walizoigiza mfano yule Doreen wa Insyuka.
 
Back
Top Bottom