Hatimaye tumeletewa Shumileta Part 3, Kiu ya mashabiki inaenda kukatika

Watoe na kinyamkela, ilijua kunitishaa hii.. nsyuka nilijuaga ni mrisho mpotoπŸ˜†πŸ˜† kulala ilikuwa kasheshe enzi hizo..
Mack aliteseka sana kwenye Kinyamkela ili akubali kurithishwa mkoba wa kiganga

Kinyamkela mwishoni Mack anafariki kama unakumbuka.

Mack alifariki baada ya kuchoma moto ule mkoba wa uganga .

Kama unakumbuka alianza kuugua kwanza uchizi baada ya kuukojolea ule mkoba aliokabidhiwa na marehemu mama yake ,

Alikataa aliona kama anashusha hadhi yake maana yeye kitaaluma ni daktari sasa kuwa tena mganga akaona weeeee usinitanie,
 
Hahaha nakumbuka kiasi chake! Ila ilikuwa na balaa duhh zilituogopesha sana
 
Watoe na kinyamkela, ilijua kunitishaa hii.. nsyuka nilijuaga ni mrisho mpotoπŸ˜†πŸ˜† kulala ilikuwa kasheshe enzi hizo..
Nsyuka ameahidi kuitoa kulingana na maoni ya wadau ila naona haina haja.

Maana main character (Doreen) alifariki kwenye ile Insyuka part 3 na Nsyuka akakaa muda mrefu kisha akarudi kwenye maisha ya Sanjo na kuanza kumsumbua.

Mwishoni kabisa Nsyuka anapata kiboko yake, mganga mmoja mashuhuri sana na kumuonesha umwamba aliyeyuka na kutokea mgongoni kwa Nsyuka kisha akagonga msumari kwenye mti mkubwa kumdhibiti Nsyuka.
 
Kwelii..

Vipi na mama mwenye nyumba unaikumbuka?
 
Nilikuwa nauimba sana huo wimbo wa chite chite ukaeeπŸ˜†πŸ˜† hivi hiyo ndio alikuwa anamtokea mtu anamuita fettyyyyyyπŸ™†πŸ½β€β™€οΈ.. siku hizi hakuna muvi za mizimu sjui kwannπŸ˜€
Doreen kwenye Chite Ukae hakutumia jina la Fetty na hakuwahi kutumia kwenye filamu yoyote ile, jina alilotumia kwenye Chite Ukae limenitoka kidogo.

Yule bibi alijua kumuhangaisha sana Doreen miksa kumuulia kila bwana anayempata πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mwisho wa siku Doreen naye anatakiwa arudi nyumbani yani Chite (Rudi) Ukae (nyumbani) na kurudi nyumbani kwenyewe ndio kufa .

Alipata Shida sana, tatizo lake mpaka mganga mashuhuri mzee Kigwasi (Chili) alishindwa kufua dafu ila akabahatika kupata mganga mwingine wa kizaramo huyo kiboko mbaya zaidi ndio alikuwa amebakisha siku moja tu afe na ile anatoka tu kwa mganga njiani anakutana na kundi kubwa sana la wachawi .
 
Nahisi hata sahivi na ukubwa huu naweza kuogopa, hadi kulala ilikuwa mtiti
Sikuhizi hata kwenye jamii mambo ya wachawi wachawi yamepungua kwa kiasi kikubwa ndio maana hata filamu unaweza usiogope tofauti na miaka ya nyuma uchawi unaona live na kwenye TV pia unaona.

Ila jamaa kaahidi kuja vitu adimu sana
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Una kumbukumbu kali!

Umenikumbusha mzee msisiri mpk nilihisi ni mwanga yule mzee.. anaigiza kama kweli!
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Una kumbukumbu kali!

Umenikumbusha mzee msisiri mpk nilihisi ni mwanga yule mzee.. anaigiza kama kweli!
Kuna vibibi ambavyo havina hata majina Mussa Banzi sijui alikuwa anaviokotea wapi.

Yani achilia mbali kuigiza, wale bila shaka ni wachawi kweli au wanajua sana mambo ya kishirikina.
 
Hapana kuna moja inaitwa mama mwenye nyumba aliwatesa sana wapangaji kwa ushirikina, mpangaji alikuwa ana mtoto anaitwa moyo, mwenye nyumba akamuua yule mtoto
Hiyo siikumbuki kumbuki.
 


Nyie wadada wakazi. Mnaandika kitu kama sisi sote tunafahamu. Mi nlidhani issue ya kwetu wanaume. Kumbe mambo yenu mabeki tatu na wamama wa nyumbani. Haya hayo mambo tuwaachie wenyewe mnajuana na lugha zenu.
 
Kuna vibibi ambavyo havina hata majina Mussa Banzi sijui alikuwa anaviokotea wapi.

Yani achilia mbali kuigiza, wale bila shaka ni wachawi kweli au wanajua sana mambo ya kishirikina.
Wale mussa kuna sehemu anawakusanya sio siri! vile vikao vyao jamn uwii! Yani ulikuwa ukisikia tu mussa banzi likaaanza kuoneshwa giza unakaa chonjo kukimbilia chumbaniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wale mussa kuna sehemu anawakusanya sio siri! vile vikao vyao jamn uwii! Yani ulikuwa ukisikia tu mussa banzi likaaanza kuoneshwa giza unakaa chonjo kukimbilia chumbaniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna wengine kwenye maisha halisia walipata changamoto za kiroho kulingana na filamu walizoigiza mfano yule Doreen wa Insyuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…