Hatimaye Uingereza yaipiga marufuku Huawei kuweka mitambo ya 5G nchini humo

Hatimaye Uingereza yaipiga marufuku Huawei kuweka mitambo ya 5G nchini humo

Wachina walikuwa wanapata ajira nyingi sana kwenye makampuni makubwa ya IT na hata Serikalini. Sasa hivi washanyea kambi makampuni mengi yatawaangalia kwa macho manne manne na Serikalini ndiyo wasahau. Tuone sasa watakavyoendelea na wizi wao wa Technology na hiyo HUAWEI ndiyo inapigwa vita katika Nchi nyingi za magharibi kwa kuhofia kuendeleza wizi wa aina mbali mbali.

Ukimsoma aliekua MKUU wa CIA wa US mike pompeo utaelewa hili halafu utajua kama wizi ni uzalendo ama laa katika mifumo yao.....
 
Uzalendo wa kuiba mali za watu? [emoji15][emoji15][emoji15]
sijawahi kusikia Wazalendo wakihamasishwa kuiba mali za watu.
Umenichekesha sana mkuu
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Wachina walikuwa wanapata ajira nyingi sana kwenye makampuni makubwa ya IT na hata Serikalini. Sasa hivi washanyea kambi makampuni mengi yatawaangalia kwa macho manne manne na Serikalini ndiyo wasahau. Tuone sasa watakavyoendelea na wizi wao wa Technology na hiyo HUAWEI ndiyo inapigwa vita katika Nchi nyingi za magharibi kwa kuhofia kuendeleza wizi wa aina mbali mbali.
Wachina wataendelea kupata ajira MKUU labda huko umagharibini ila sio ASIA nakwengineko.....
 
Nasemea Nchi za magharibi ambapo maelfu wameajiriwa, sikuandika chochote kuhusu nchi za Asia.


Wachina wataendelea kupata ajira MKUU labda huko umagharibini ila sio ASIA nakwengineko.....
 
Kabisa inaonyesha angeacha game iwe fair mpaka 2025 Huawei ingekuwa na nguvu kuliko Kampuni nyingine yeyote ya technolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
Duniani hapa hakuna mchezo msafi, hasa kwa haya mataifa makubwa. Marekani anapambana kwa nguvu sana na Uchina kwasasababu anachofanya Uchina kwasasa ndicho kilekile ambacho Marekani alikuwa anakifanya dhidi ya Uingereza mnamo karne za 19 na 20.
 
Huu mchezo China mwenyewe ndio aliuanza,anachofanya Marekani ni kupita mule mule kwa China.
United States of America is second to none when it comes to the art of corporate/industrial espionage: Everything American was stolen from Europe, starting with Water-Powered Textile Mills to the Nuclear Bomb. History will remember America as the greatest technological pirate of all times.

NB: When it comes to corporate espionage China is just a kindergarten baby compared to the United States.
 
Jibu maswali yangu acha kuruka ruka! Kwani nimeandika Kichina!? 😳😳😳
Nimekuuliza swali rahisi sana na umeshindwa kujibu:
Unadhani teknolojia ya nyuklia ilianzia nchini Marekani ???
 
Why should I answer your question while you’re avoiding to answer my question? 😳😳😳 Do you find my question too difficult to answer?

Nimekuuliza swali rahisi sana na umeshindwa kujibu:
Unadhani teknolojia ya nyuklia ilianzia nchini Marekani ???
 
Hili linadhihirisha kwamba Marekani ameshikwa pabaya sana na Uchina. Muingereza ajipange tu maana ameamua kuingilia hii vita wakati hali yake siyo nzuri sana!
USA kaisha sema mimi ni nani nikataee?!! Mbona ni nchi nyingi sana zimesha ungana naye, INDIA, ITALY, FRANCE, UK!!! akishakuwekea fitina ni ngumu kupenya!!!
 
USA katika ujasusi wa kiuchumi hata sio wa kuwa tetea ndugu ...wameshawahi kucheza michezo michafu mingi tu
Mkuu Hearly mwanahistoria nguli wa Kiyahudi Doron Ben-Atar anasema maneno haya kuhusu Marekani kwenye kitabu chake kiitwacho "Trade Secrets" : "the United States emerged as the world's industrial leader by illicitly appropriating mechanical and scientific innovations from Europe"...........

Huu mchezo mchafu wa Ujasusi wa mambo ya nje Wamarekani walifundhishwa na Raisi George Washington ambapo unaambiwa aliliomba bunge la Marekani lipitishe bajeti ya ujasusi wa mambo ya nje ambayo hadi leo haijawahi kupitishwa na Marekani. Raisi Washington alipoona kwamba wako nyuma sana ya mataifa ya Ulaya aliomba wapitishe bajeti ya kijasusi ambayo ilikuwa ni asilimia 12% ya GDP ya Marekani (Hizi namba siyo mzaha) kwa kipindi hicho.

Miaka ilivyoenda ndiyo wakina Francis Cabot Lowell walikamatwa mwaka 1812 wakiwa wameiba mipango ya teknolojia mpya kutoka Uingereza ya kushonea (Power Loom) ambayo iligunduliwa na Muingereza Edmund Cartwright. Miaka ya 1939-1943 Marekani akaiba teknolojia ya nyuklia kutoka Ujerumani pamoja na wanasayansi wa Ujerumani. Mwaka 1945 akaanzisha Operation Paperclip ambapo alichukua maelfu ya wanasayansi wa Ujerumani na teknolojia yao huku akiwaambia kwamba atawalinda ili wasishitakiwe kwenye mahakama ya Nuremberg.

Wernher Magnus Maximilian Freiherr von Braun ambaye alikuwa Mjerumani ndiye aliyewapa Marekani siri za kutengeneza roketi ambazo ziliwasaidia NASA kupeleka hadi watu mwezini. Kama wasingekuwa hawa watu sidhani kama Marekani angefika hata mwaka 1970 kwenye vita baridi dhidi ya Umoja wa Kisovieti.
 
Ni Wamarekani wangapi waliokamatwa wakiiba technology ya Taifa jingine? Ni Taifa lipi hilo ambalo waliibiwa na wamarekani!?
Kwani MKUU unapo uongelea wizi lazima uwe wakiteknolojia ?!

Na kama ukiwa wakiteknolojia lazma wakamatwe ndio ujue kama wameiba ?!

POMPEO aliweka wazi hili kama wanadanganya nawanaiba sasa usichotaka kuamini naunakibishia kipi MKUU ?!
Nasemea Nchi za magharibi ambapo maelfu wameajiriwa, sikuandika chochote kuhusu nchi za Asia.
Naam najua hujataja chochote kuhusu ASIA namie sikutaja kuhusu WESTERN sababu hata dunia yenyewe kwakiasi kikubwa imeelemea ASIA kwasasa sababu ndio wahitaji wamekua wengi zaidi kuliko sehemu yeyote ile ULIMWENGUNI
 
Back
Top Bottom