Hatimaye Uingereza yaipiga marufuku Huawei kuweka mitambo ya 5G nchini humo

Huawei sio sim tu ndiyo kampuni kubwa inayotengeneza equipment za 5G networks pamoja na software duniani. Shida ni kwamba inasemekana inakua backed up na Chinese army,wazungu wanaogopa uwezekana wa China/ Huawei kuweka backdoors kwenye systems na kuiba Tech na information.

Pia wanaogopa kuwa tegemezi kwa tech ya mchina make itabidi wacheze mziki wake,wangependa huawei at least iwe kampuni huru isiokua na uhusiano wowote Na CCP, Govt lakini kwa China haiwezekani.

Sio kwamba Huawei yuko peke yake kwenye 5G,kuna Nokia ya Finland, Ericsson ya Sweden, Qualcomm ya USA. Tofauti ya hizi na Huawei ni kwamba ni 100% private owned companies bila mkono wa serikali yoyote,Ila bei za kit zao ziko juu kuliko Huawei.

Ukiangalia hata sim zao huawei data centres kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za wateja wa Africa ziko Hongkong kwa sababu mainland China hakuaminiki,taarifa za ulaya zinahifadhiwa pale pale,marekani hauzi sim. Hongkong new security law imevuruga kila kitu.
 
Kitu kingine ambacho nahisi kitaweatesa Huawei ni kwamba chips za 5G Zina disainiwa na kampuni za marekani,wamepewa ban saiz inabidi waje na chips zao wenyewe from the ground bila kukopi.
 
Sidhani ni kwa sababu hiyo,,, huawei equipment zitakua phased out kwa awamu ili kuto disturb mfumo wa mawasiliano na pia kupunguza stress za gharama kwa makampuni ya sim. BT, Vodacom walishanunua na kusimika kit za kutosha za 5G toka huawei kwa pesa nyingi,hawawezi zitoa kwa pamoja kwa wakati mmoja.
 
Masuala yamigogoro yamipaka yalikuwepo tu kabla lahili saga la HUAWEI je hakukua naushirikiano wakibiashara baina yao ukiwemo huu wa HUAWEI ?!
yalikuapo ila kadri China inavyokua kiuchumi na toka Xi alivoingia madarakani amekua akiwaburuza wote anaokua na migogoro nao. Hao majirani wanaona China is not to be trusted especially kwenye issue za usalama wa mataifa yao.
 
yalikuapo ila kadri China inavyokua kiuchumi na toka Xi alivoingia madarakani amekua akiwaburuza wote anaokua na migogoro nao. Hao majirani wanaona China is not to be trusted especially kwenye issue za usalama wa mataifa yao.
Kuhusu uwepo wa Xi nakuwaburuza ambao wanamigogoro nao sina neno hapa sababu inaweza ikawa kweli

Ila kuhusiana na UCHINA nakuaminika juu yamasuala ya Usalama wa mataifa Mengine nikwamba linapokuja suala la usalama wataifa lako hutakiwi kumuamini hata unaemuona nirafiki yako nandio maana kuna kipindi Kansela wa Ujerumani Angela Markel Ilisemekana amefanyiwa Udukuzi na US nandio maana hata linapokuja suala lamaelewano kwa US na GERMAN nishida kidogo tofaut na ULAYA wengine wakimagharibi...
 

Nikwambie kitu, BT haitangoa chochote wala nini sijui - wanacho fanya ni kuchota akili akina Trump na genge lake, Waingereza wanajua fika kwamba ni suala la muda saga yote hii ita sublime into thin air na mwisho wa siku America itabaki helpless like a beetle on its back - mtu uwezi ukawa na roho mbaya/uchoyo halafu ukategemea kwamba unaweza ku-thrive kwenye mazingira ya ajabu kama hayo ya kwa nini? Sadly Uncle SAM never saw it coming, lakini as days goes by watajifunza the hard way, kwamba uwezi ku-fool watu wote muda wote.
 
At least wazungu wanaweza kaa kwenye round table na kuzungumza,hawawezi fanya hivo kwa mchina. Best option ni kumuondolea mwanae mpendwa ambae ni Huawei. Tafakari bila vikwazo vya USA mwaka huu Huawei alikua awe smartphone maker no 1 duniani,ameshindwa kufikia lengo,na type kwa kutumia sim ya huawei.

Soko la ulaya ameporomoka , USA hajawahi kuruhusiwa kuuza sim, India amepigwa ban na hayo ndo masoko yenye faida .Huku Africa ni watu wangapi watanunua p40 pro out of the box dukani? Nazipenda sana sim zao lakini bahati mbaya vita ya tembo huwaei ni nyasi ndiye anaeumia, mipango ya kuliteka soko la dunia wasahau kwa sasa.
 
Lazima waitoe kwa sababu hata wabunge wa chama tawala conservative wanataka huwei isihusike kabisa kwanye kutoa huduma ya 5G network nchini mwao.

Check hii link toka kwenye gazeti la the Guardian,

UK's expected U-turn on Huawei fails to satisfy Tory rebels
 
Kwenye masuala mazima yakiuchumi linaangaliwa maslahi yataifa husika kwanza kabla yajambo jengine

Nahisi ushawahi kuupitia vyema kabisa mradi mkubwa kabisa wa NORD STREAM 2 wa RUSSIA na GERMAN ?!

unahisi kati ya RUSSIA na GERMA na GERMAN na US wapi wapo vyema kisiasa (USHIRIKIANO) ila GERMAN alipitisha ama anapitisha Bomba lagesi kutokea MOSCOW to BERLIN

wakati huo huo US alimuoffer German kumpatia GESI ila kikubwa alichokiangalia GERMAN ni maslahi yataifa lake kwanza nahakujali kelele za US

Bukyanagandi kuna sehemu huko juu alikwambia kama US hawez kudanganya watu kila siku kuna wakati GERMAN alikua hawez kupingana na kauli za US ila kwasasa anapingana nao tu kuhusiana na NATO kuhusiana na Gesi yaani GERMAN anampinga tu basi uelewe hili vugu vugu lakuipinga US lipo ulaya nzika ijapokua wanaolionesha kama GERMAN bado hawajawa wengi

Kuna kipindi MACRON alisema kama NATO imekufa Ubongo

Watu wanaangalia maslahi kwanza MKUU mengine baadae nakuhusiana nasuala hili GERMAN kalithibitisha kupitia Mega Project ya NORD STREAM.
 
[emoji24][emoji24]
 

Please revisit hiyo link isome kwa umakini zaidi - may be my command of Queen“s English is a bit rusty - nilicho kiona pale ni siasa tu na maoni/mapendekezo ya wabunge kumbuka sio lazima Serikali ya Uingereza ikubaliane na mapendekezo ya wabunge - Serikali inacho jali ni maslahi mapana kwa ajili ya Taifa lake na sio mambo ya siasa na ugomvi wa kiuchumi kutaka kuondoa Huawei kwenye soko ili wamfurahishe Trump na wenzake, Waingereza hawako hivyo hata kidogo hawawezi kukubali wabaki nyuma katika suala la matumizi ya 5G huku wakusuburi Ericsson na Nokia wa roll out 5G ya kweli ambayo ni improvised 4G LTE waingereza si wajinga kiasi hicho. They will always stick by Chinese Huawei kwa kuwa wanajua hao ndio magwiji wa tejnilojia ya 5G, Hauwei ndio wanamiliki asilimia karibu 80 za patents za teknolojia ya 5G si rahisi kuchukulia Huawei kimzaa mzaa - Waigereza na Mataifa mengine yenye hekima na busara wanajua ukweli huo.
 
Serikali imeamua tayari hakuna namna tena,pressure ya kuachana na Huawei imetoka nje na ndani ya UK. Uingereza serikali ni Bunge na the moment wenye hoja wakiwa na majority bungeni huwa haina ujanja.

Kuna kitu kingine ambachi kinafanya compaign dhidi ya Huawei kuwa effective, kuna ushirikiano wa kijasusi na kiuchumi kwa mataifa ya magharibi. The five eyes ni alliance kati ya USA, UK, Australia, Canada na New Zealand kwenye Mambo ya ujasusi. USA ilitahadharisha nchi ambayo itakua inaendela kutumia kits za 5G toka Huawei itakua excluded kwenye intelligence sharing by mid of next decade.

So muingereza hana ujanja wa kutembea peke yake wakati washirika wake wamechukua njia nyingine. Alliances za wazungu zimetoka mbali toka first world war, WW2,cold war mpaka leo. So hata mfaransa,mjerumani atakaa kwenye mstari tu. China haina alliance na nchi yoyote kubwa hata ndugu zao wa rangi 1 huko Asia wanaitazama kwa jicho la mashaka.

Uchumi huu wa kisasa bila alliances hata kama nchi ina nguvu kubwa za kiuchumi kulinda maslahi yake effectively inakua ngumu. Huawei inahitaji masoko ya nchi za magharibi, Asia kwenye nchi zenye uchumi mkubwa ili iendelee kuwa kinara. Huko kote imepigwa kufuli ,soko la africa huku ni dogo sana.
 

Habari hii imekuwa ikitolewa na media zote kubwa duniani: BBC, sky news, Reuters, RT, AFP, etc.

Halafu mtu ukipuuza CNN na Reuters, ni media zipi za maana kwako kimataifa?
 
jamani mwenye hadithu ya kusisimua kuhusu 5G atusimulie tafadhali...

5G ni nini na ina uwezo gani mbona kwenye 3G na 4G hakukua na kelele ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…