Hatimaye! Unaweza kufanya malipo mtandaoni kwa M-Pesa

So Mkuu naweza kufanya manunuzi kwa ebay ambao wanatumia sana paypal?
 
Hii ishu imerahisisha sana maisha. Nimejiunga mchana. Jioni hii nimelipa dollar 25 google play kwa kuitumia. Voda wametisha. wafanye tu kuitangaza.
Mwamba pale kwenye card no, tunaingiza zoteee hadii zile CVV
 
Hapana, CVV ni namba 3 unazopewa, kwenye card halisi zipo nyuma ya kadi yako. Ukijaza kwenye platform utaoneshwa sehemu ya kujaza card number, CVV na expiry date
Mwamba pale kwenye card no, tunaingiza zoteee hadii zile CVV
 
Ni jambo zuri pls rate ya kubadili fedha isiwe kinyongeo cha kunyonga wateja wenu.
 
Card yangu ya Master Card imekataa kufanya kazi aliexpress kwingine inafanya now natumia Visa Card
 
Wakuu kama kuna mtu amefanikiwa kuitumia huduma hii naomba msaada,Sehemu ya cardholder name tunaingiza jina gan? Nimejaribu kuingiza jina lilipo kwenye account ya mpesa but sijafanikiwa. Nahisi kuna specific predefine name kwa ajili ya card zote. Msaada tafadhali. Nimejaribu kuwacheck vodacom lakini naona menu ya kuongea na huduma kwa wateja imetolewa.
 
Kuna kitu Nataka kuagiza nimecreate card wamenipa namba ya card na cvv lakini kila nikijaza wanasema payment decline
 
Hivi ikiexpire card na kukiwa kuna mkwanja inakuaje kuhusu pesa?
 
Je, ni Lazima uwe na akaunti katika BankABC ilikukamilisha huduma hii?
 
Je, ni Lazima uwe na akaunti katika BankABC ilikukamilisha huduma hii?
Ukijisajili na M-Pesa Master Card ni rahisi tu mkuu.

Ingia M-pesa chagua number 4, Pay by Mpesa. Kicha chagua number 6 Mpesa Master Card halafu chagua number 1 Create Card.

Your Mpesa Master Card now is ready.

Utatumiwa Card number na pia CVV number.

Sasa weka pesa na uanze kufanya manunuzi mtandaoni.

Nimetumia Mpesa Master Card kununua bidhaa AliExpress.

Kulipia Shopify Pan, kununua domain name kwaajili ya website yangu nk.

It works just fine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…