Alafu nikuambie kitu Minyoo, sio wote tunao furahia hili swala ni wana CCM, hapana.
Wengine hatuna vyama, hii ni kutokana kushindwa kuelewa tuende wapi.
Yanayo fanywa na CCM (baadhi) hatuyapendi, lakini hata kwa hao wanaojiita wapinzani hatupati kile tukitakacho.
Binafs mimi naangalia harakati zangu zinaendaje, hayo maswala ya siasa nawaachia wenyewe wana siasa.
Ninacho waomba mimi wailinde nchi na maadui zetu, Kiufupi nataka nife bila kuiona vita, hilo tu.
Hayo maswala sijui ajira, kila mtu apambane na hali yake.