Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Leo naenda kuchoma kadi yangu ya CHADEMA na kujiunga rasmi na ACT-Wazalendo!
Kuna dalili zote Mkuu ulikuwa mfuasi wa Antipasu na si mwanachama halali Chadema. Mwanachadema halali anafikiria mapana ya kuimarisha nchi ya Tanzania achana na wale waliotunga Ilani ya uchaguzi ya mwaka huu!
 
Misimamo yangu ni dhabiti bila kujali udhaifu wa baadhi ya watu. Mimi ni mmoja ya watu wenye imani na cdm lakini nilipinga waziwazi ujio wa Lowassa ndani ya cdm. Na pia ni mtu ambaye nilipinga waziwazi Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm zaidi ya miaka 15. Sasa napata aibu ya nini kwenye changamoto za hivi labda? Sasa kama sikuogopa wakati huo na nilibaki kuwa mpinzani, hili la leo ninaogopa nini labda?
Mkuu mm pia nilikuwa si mwana chama lakin nilikuwa naiamin sana cdm kama mkombozi atayetetea ba kuleta mabadiliko nchini lakin pindi walivyomteua lowassa kugombea urais 2015.

Wanaonifahamu kazin niliwaambia kwanzia leo mm nimsikilizaji tu na sina imani na hawa viongozi wa chama hata kidogo kwan hawana uzalendo bali ni wametanguliza maslahi yao binafsi kuliko ya wengi.

2020 ndio imedhihirisha wazi chama kinaenda kufa kwa tamaa na ubinafsi wa viongizi, hawakuwa makin tangu mchakato wa kumsimamisha mgombea urais.

Sasa taifa bila chama pinzani chenye mikakati na uzalendo madhubuti tunaelekea wapi?
 
licha ya Mh Halima mdee kutoa maneno yenye ukakasi juu ya kura zilizopigwa. Nilitegeme spika kama nimjuavyo angetoa kauli ya angalau kumjibu Mh Halima mdee, kinyume chake amekuwa mpole na muungwana sana. Sasa najiuliza huu urafiki
Kuna jambo, si bure
 
Mabeberu si watu wazuri, inaonekana wametishia kukaza nati.
 
Swali liwe hivi: ni lini wabunge wa upinzani wameanza kujiweka karibu na speaker despite manyanyaso yake kwenye Bunge lililopita?

Maslahi yanalevya. Maslahi makubwa yanalevya zaidi. Penye udhia penyeza rupia!
 
Spika amewaambia CCM wenzake piga makofi mengi kwa Mdee!

Nikasema kweli, maisha hapa duniani mafupi sana.
 
Alafu nikuambie kitu Minyoo, sio wote tunao furahia hili swala ni wana CCM, hapana.
Wengine hatuna vyama, hii ni kutokana kushindwa kuelewa tuende wapi.
Yanayo fanywa na CCM (baadhi) hatuyapendi, lakini hata kwa hao wanaojiita wapinzani hatupati kile tukitakacho.

Binafs mimi naangalia harakati zangu zinaendaje, hayo maswala ya siasa nawaachia wenyewe wana siasa.

Ninacho waomba mimi wailinde nchi na maadui zetu, Kiufupi nataka nife bila kuiona vita, hilo tu.

Hayo maswala sijui ajira, kila mtu apambane na hali yake.
Mkuu mawazo yako na yangu yamepatana kwa asilimia zote, uzalendo ndo huo mkuu kwani tuna damu zetu katika ardhi hii hivyo lazima tuilinde kwa kutanguliza taifa kwanza.
 
Kama wangekumbuka Ile siku kule magereza tulivyo pambana na Askari ama Kama wangekumbuka tulivyo changa pesa kuwatoa gerezani wakati Madhinji alilipiwa na serikali wasingefanya hivi.
Umenikumbusha riwaya moja inaitwa Takadini (Sisi tumefanya nini?).

Akina Halima wamepambana kwenye uchaguzi mpaka anakamata kura feki,sisi tumefanya nini. Hawa wamama wameplay part yao. Labda bado hatujawa tayari.

Uganda wanajitahidi,vyombo vya habari angalau vinaonyesha msimamo, wananchi wanajitahidi.Sisi bado sana.
 
Mfalme Ndugai kama King Muswati!
3A317B31-2A12-4BA1-AEDC-2A516CD1D27B.jpeg
 
Leo naenda kuchoma kadi yangu ya CHADEMA na kujiunga rasmi na ACT-Wazalendo!
Nenda kaichome TU MKUU....kwani NI yako....ila KWANGU NITABAKI KUWA MWANACHAMA MTIIFU WA CHADEMA,MAANA TOKA BOB MAKANI,MPAKA LEO MNYIKA CDM IKO MOYONI KWANGU....MILIMA NA MABONDE TULOPITIA HILI SI KITU...CDM FOR LIFE
 
Watanzania na mashabiki wa CDM tusiwalaumu wakinahalima na kuwaita wasaliti. Kama waliitisha maandamano tukawagomea manayake tuliwasaliti sasa acha wafate katiba na tuwasapoti. Mambo ya kusema wamesaliti ni unafiki kabisa. Wacho tuonje chungu ya usaliti wetu ili tujifunze na sikunyingine tukiambiwa tuwasapoti kwa maandamano hatutasaliti tena.

Kwani nani kawashikilia mbona walishaachwa labda kama kilichobaki ni kufukuziliwa mbali.

Hicho tu ndicho tunachokisubiri. Ila kuachwa mbona kipindi tu?
 
Back
Top Bottom