Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Shubaamiti zenu WanaUfipa nilikuwa nawasapoti kumbe wote ni wachumia matumbo mavi mavi.
Kwa hasira naenda UDOM kuchukua degree in Political science and leadership.Nikirudi huko taanzisha chama langu.[emoji57][emoji19]
Safi mm nitakua wakwanza kukuunga mno
 
twende mbele turudi nyuma, ili kuikabli vzr CCM kidemokrasia ni lazima nguvu ya wananchi ihusike...
chdema wao kama wao kuitoa madarakano CCM awawezi pasipo wananchi kushiriki....
 
Wabunge Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza mchakato wa kusajiliwa Jijini Dodoma.

Majina yao yamewasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA

ORODHA YA WABUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA 2020.
1. Halima Mdee
2. Grace Tendega
3. Ester Matiko
4. Cecilia Pareso
5. Ester Bulaya
6. Agnesta Kaiza
7. Nusrat Hanje
8. Jesca Kishoa
9. Hawa Mwaifunga
10. Tunza Malapo
11. Felister Njau
12. Naghenjwa Kaboyoka
13. Sophia Mwakagenda
14. Kunti Majala
15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest
17. Salome Makamba
18. Conchesta Rwamlaza
19. Asia Mohammed

HOTUBA FUPI YA HALIMA MDEE KWA NIABA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA

Nikishukuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata

"Mh. Spika tumefanya kazi wote kwa miaka zaidi ya 10, tutafanya kazi kwa uaminifu kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa uadilifu mkubwa, tuna vijana wapya sisi kama dada zao tutahakikisha wanafanya kazi nzuri kwa ajili ya Taifa hili

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu"

SPIKA NDUGAI: Muongezeeni makofi Halima, ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wapya na kwa niaba yenu wote ningeomba tuwapigie makofi.

Kwa mujibu wa ibara ya 78, ibara ndogo ya kwanza ikisomwa na ibara ya 66, ibara ndogo ya 1(B)


Suala hili lilizungumziwa na mwanaJF hapa > Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na wanawake wa CHADEMA

CHADEMA yakanusha kupeleka majina > John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum, tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua
Siyo usaliti wache wakatuwakilishe ili at least wakalete changamoto.Mm kea kipekee nilikuwa nawamisi Sana halima mdee,esther bulaya na matiko.Ninauhakika watafanya kitu.Aluta Continua .Viva Chadema Viva.
 
Meseji kwa Amsrterdam na western Countries na USA Siasa za Tanzania ni pasua kichwa wakae nazo mbali

Tanzania ni peculiar country Africa kama ilivyo China

Ni nchi mbili tu duniani zilizo peculiar kwenye politics China na Tanzania tu

Leave Tanzania alone

nadhan wamekuskia loud and clear
 
ACT Wazalendo wapeleke jina la Maalum Seif Sharrif Hamad kwa Mheshimiwa MWINYI ili awe Makamu wa kwanza wa Rais.
Ruzuku na michango ya wabunge ni muhimu sana katika kujenga Chama.
 
Back
Top Bottom