Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Hakuna maendeleo yameletwa na CCM miradi yote mikubwa imejaa ufisadi mkubwa kuna 10% ununuzi wa Ndege, SGR bwawa la umeme flyover na miradi yote mikubwa, Dr Slaa hakuondoka chadema kwa kupenda alinunuliwa kwa dola milion 2 na kupewa nyumba canada hana mfano wa kuigwa hata mmoja ni mwizi kama wezi wengine huko CCM,
Mfano wa kuigwa ni wewe tu minyoo
 
Wabunge Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza mchakato wa kusajiliwa Jijini Dodoma.

Majina yao yamewasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA

ORODHA YA WABUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA 2020.
1. Halima Mdee
2. Grace Tendega
3. Ester Matiko
4. Cecilia Pareso
5. Ester Bulaya
6. Agnesta Kaiza
7. Nusrat Hanje
8. Jesca Kishoa
9. Hawa Mwaifunga
10. Tunza Malapo
11. Felister Njau
12. Naghenjwa Kaboyoka
13. Sophia Mwakagenda
14. Kunti Majala
15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest
17. Salome Makamba
18. Conchesta Rwamlaza
19. Asia Mohammed

HOTUBA FUPI YA HALIMA MDEE KWA NIABA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA

Mheshimiwa spika, nitazungumza kwa niaba ya wenzangu wote kwa hiyo nitazungumza peke yangu. La kwanza nikushkuru kwa amabo umepelekea kiapo kikafanyika

Pili nikishkuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kwasababu kupitia wao ndio sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu ambacho kwa mujibu wa matakwa ya sheria za nchi kimekidhi vigezo vya kupata viti maalum, kwa hiyo viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata.

Nikuhakikishie mheshimiwa spika na mimi unanifahamu vizuri, tumefanya kazi wote kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10, tutafanya kazi kwa uaminifu kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile ambavyo tumekuwa tukivifanya.

Lakini mwisho lakini sio kwa umuhimu, tuwahakikishie vile vile watumishi wa Bunge, kuna vijana wapya hapa wameingia, sisi kama dada zao tutahakikisha wanafanya kazi bora na nzuri kwa ajili ya Taifa hili.

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana. Baada ya kusema maneno hayo Mh Spika nirudie kukushkuru wewe, katibu wa Bunge na timu yake wewe na nikishkuru chama chetu kwa sababu kupitia

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu ndio tumepata fursa hii ya kuwakilisha watu wengi ambao wana imani na sisi.

SPIKA NDUGAI: Muongezeeni makofi Halima, ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wapya na kwa niaba yenu wote ningeomba tuwapigie makofi.

Kwa mujibu wa ibara ya 78, ibara ndogo ya kwanza ikisomwa na ibara ya 66, ibara ndogo ya 1(B) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Vyama vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge vitapendekeza kwa tume ya Taifa ya uchaguzi majina ya wanawake kwa kuzingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa wabunge ili hao waliopendekezwa wawe wabunge wa viti maalum kupitia vyama hivyo.

Tarehe 20 Novemba 2020 nimepokea barua kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi yenye maelezo kuwa imefanya uteuzi wa wabunge wanawake 19 wa viti maalum wa CHADEMA kwa mwaka 2020 ambao ni kama tulivyowaapisha hapa.

Mimi kama spika nawaahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano, najua kambi yenu itakuwa ni ya wabunge wachache, wajibu mmojawapo wa spika ni kuwalinda wale walio wachache, nitajitahidi sana kuwalinda, nitajitahidi kuwapa haki, nitajitahidi kuhakikisha kwamba mnatekeleza majukumu yenu kikamilifu katika kuwatetea watanzania, kuwasemea watanzania na kufanya kila lile ambalo linawapasa katika kazi za kibunge ili muweze kufanikisha jukumu hili la kikatiba.

View attachment 1633801
View attachment 1633976
Wabunge wa Viti Maalum(CHADEMA) wakiwa na Spika Ndugai​

Suala hili lilizungumziwa na mwanaJF hapa > Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na wanawake wa CHADEMA

CHADEMA yakanusha kupeleka majina > John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum, tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua
Koma kabisa we Halima kututaja wanachadema nchi nzima koma , mtaje Jiwe aliyekupora hela na vitisho ukasalimu amri .
 
Dah sijui Lissu atawaambia nini Amsterdam na mabeberu wake.

Kitendo cha CDM kuteua wabunge ina maana uongozi aina communication na Lissu ambaye jana tu kadai wao wamesusia bunge na hawatambui matokeo ya uraisi.

In other words CDM wanatuambia tuache kumsikiliza anayoongea ni yake sio ya chama wala sio mtu anaeshirikishwa katika maamuzi
Lisu anadai yake kama mbowe kaamua kumsaliti yeye atasonga kivyake
 
Mhutu mtu wa ajabu sana , katumia nguvu kubwa Sana kuzuia wapinzani wasipate ubunge , leo huyohuyo katumia pesa , vitisho na masharti kwa baadhi ya viti maalum kuwatoa rumande ili waingie bungeni .Ningekuwa simjui Mhutu ningeshangaa kwa haya , ila kwa kuwa namfahamu sishangai mtu anayetenda kwanza halafu anafikiri baada ya kutenda , badala ya kufikiri kabla ya kutenda.
Umeshanyooshwa wewe! Pole!
 
Shikamooooooo CCM.
Wewe ni gwiji la siasa.
Kila siku unatupa kazi ya kuanzisha vyama vipya tu, wakati wewe ukiendelea kujidhatiti.

Mimi sishindani na wewe mpaka pale itakapo patikana katiba mpya, ila kwa sasa sikuwezi.

Kama uliweza kuisambaratisha NCCR ya mlema, ukakiuwa CUF ya Maalim & Lipumba, na leo umenithibitishia kua wewe sio mtu mzuri, kwa kukichinjilia mbali CDM, nasema wewe ni kiboko.

Kwambaali namuona ACT akipasha kuchukua nafasi ya walio tangulia.

Shikamooooooohhhhh Chanzo Cha Matatizo.
 
huwezi amini nimecheka sana kwa nikakumbuka yule aliyesema mwanasiasa akikwambia saa hizi mchana toka na tochi!
🤣🤣🤣

Mh.Mbowe alituambia "ninakwenda kuwa WAZIRI MKUU ndani ya masaa 72".

Hilarious 🤣
 
Leo ndio nimeamini Tanzania si lolote si chochote mbele ya hao mnaowaita mabeberu.Yaani nguvu iliyoyumika kuwaaminisha eti hali ni shwari ni dhahiri kibano cha mameberu ndio sababu ya haya yote,si kwa nguvu ile iliyotumika.
Mbuzi jike anahaha kumtuliza Beberu kwa kuingia gharama kuleta wapinzani Bungeni kwa njia haramu za kishetani angalau Beberu amuone mbuzi jike ana demokrasia
 
Shikamooooooo CCM.
Wewe ni gwiji la siasa.
Kila siku unatupa kazi ya kuanzisha vyama vipya tu, wakati wewe ukiendelea kujidhatiti.

Mimi sishindani na wewe mpaka pale itakapo patikana katiba mpya, ila kwa sasa sikuwezi.

Kama uliweza kuisambaratisha NCCR ya mlema, ukakiuwa CUF ya Maalim & Lipumba, na leo umenithibitishia kua wewe sio mtu mzuri, kwa kukichinjilia mbali CDM, nasema wewe ni kiboko.

Kwambaali namuona ACT akipasha kuchukua nafasi ya walio tangulia.

Shikamooooooohhhhh Chanzo Cha Matatizo.
🤣🤣🤣🤣

Kitoabu mzee wa KIMWEKUMWEKU....

CCM hairogeki...
CCM haichapiki Ahlul Badr...

Mlima wa CCM ni mrefu....WATAKAOFIKA JUU insh'Allah labda VIZAZI VIJAVYO sanaaa.....🤣🤣
 
Back
Top Bottom