Kina Mwalimu Nyerere walijitahidi sana kuandaa vijana kukua katika maadili ya "UZALENDO WA TAIFA NA AFRIKA", na walifanikiwa kupandikiza uzalendo ndani ya damu zao.
Sishangai kwanini Mwalimu Nyerere alimchagua Hayati Mkapa visa Kikwete kugombea nafasi ya urais. Hakika, aliona mbali sana.
Ila tanzania ya sasa, inayo ongozwa na damu ambazo hazijazalishwa na kina Mw. Nyerere, inazalisha vijana wenye sumu katika damu zao za tamaa ya Madaraka/Vyeo/Pesa.
"KAMA TAIFA, SERIKALI INAZALISHA VIONGOZI WA KESHO (VIJANA) WASALITI NA SIO WAZALENDO".
Kamwe, serikali isije kulalamika kwamba taifa letu lina watu sio wazalendo wa nchi yetu. Kwasababu wao ndio "WAMEFUNDISHA WATU KUWA WASALITI" na kuwa "WENYE TAMAA YA MADARAKA/VYEO/PESA", sambamba na kuwaaminisha vijana wa kesho kwamba "SIASA NI BIASHARA", hasa kwa vijana wa kesho.
Na inazalisha raia wasiokua na "IMANI" kwa viongozi wao pamoja na wanasiasa wote.
Vijana wanaozalishwa na #teamMagufuli ndio watakaokuja kuliangamiza taifa uchaguzi ujao 2025 (pengine hata uchaguzi ujao tusifike).