SAHIHI
Jamii na Wanajamii wanapokuwa hawako tayari kutoa hesabu ya utayari wa maisha na maendeleo yao daima watakuwa wahanga wa 'maamuzi ya watu wengine'...
Hata lawama na vipakazio, havitowasaidia kwa lolote khasa bali kuwa muktadha akilifu wa kujiziuka, kujizima data, kujipumbaza akilini labda ni serikali na wataalam wake wanaokosea pahala...
Kiufundi, haya ni matatizo ya kijamii yatokanayo na 'Tabia na Mazoea'.
Ni tabia na mazoea, viwili vinavyohusiana moja kwa moja na sifa na hadhi ya Kielimu ya Wanajamii; katika jamii Elimu muafaka si 'visomo vya cheti na madarasa' bali mambo ya 'Nuru ya Ufahamu' na 'Uono Fasaha' wa mambo/utamaduni...
Watalaam na mchango wao 20% hauna pumzi ya kuwarekebisha wanajamii wengi ambao 'Hawajitambui'--labda sana sana na wao wanaweza kujikita kwenye lile jambo lao, mambo yao kipenzi ya mapendekezo ya hatua zakuchukuliwa: 'Jamii ipewe Elimu' ama 'Jamii ijengewe Uwezo' ama 'Fedha zaidi zitolewe kwa ajili Elimu na Mafunzo kwa umma na Watendaji'...
Daima kinachofuatia kwa sura na utendaji wa namna hii ni 'ujenzi/uimarishi wa daraja la kati' la wanajamii, mambo ya vipato na privileji kwa makundi fulani ya utendaji, utumishi na biashara.
Hii ndiyo adha ya Elimu na Utumishi badala ya 'Elimu ya Mwangaza kwa Jamii'; Suala la Elimu ya Mwangaza kwa jamii ndiyo khasa kusudi la dhana ya '
Mwenge wa Uhuru'...
Watu wasio na Elimu ya Mwangaza wa Maisha, mwangaza wa mbali kupita mapana ya maandalizi yao ya kimifumo ya maisha ya kileo 2024, daima si 'watu huru' khasa--tena huenda hawa si watu wa nasibu ya kutambua ama/na kujitambua kuhusu 'Uhuru Binafsi' na 'Heshima ya Kweli' ya Utu wao.
Ni watu miongoni mwetu wanaoamka na katafuta kujua ilivyobora ndiyo wanayonasibu ya kuwa chumvi na nuru ya utamaduni wa jamii pana--tuseme jamii ya Watanzania.
Watu hawa wanaweza kuchipuka kokote, kutoka kwenye kada za utumishi wa Umma, Elimu, Biashara, Sayansi, Ujasiriamali n.k--hili linataka tu nia na dhamiri ya kujiongeza.
Wakati mmoja siku za mbele, tena wakati tumefanikiwa katika shughuli ya
Mwenge wa Uhuru, Ilimu na Elimu jumuishi ya mambo itageuza sura na maendeleo ya jamii kuwa jambo tutakalolibayanisha kana 'Ujasiriamali wa Kijamii'; kwa leo kuzungumzia Ujasiriamali wa Kijamii si ajabu hata wanaojiita 'Wataalam wa Uchumi na Maendekeo ya Jamii' watang'aa ng'aa macho ama kujikuna akili--ndiyo 'mashikolo' gani?
Kuna jambo ni Dosari katika dhana na ufikirifu wa mwelekeo wa utaasisi wa 'PPP'; hili ni kwa kuwa PPP ni jambo linalodhihiri kwa namna ya ufikirifu unaojizima data kwa mengi sana kwenye jamii ambayo hayapaswi kufumbiwa macho. Ukiwa na jamii ambayo inamapungufu ya Mwenendo wa Tabia na Mazoea yake katika Maisha na Uisho basi hata PPP hujakuutumia huo mwanya hata kwa mabaya zaidi--mahodhi na ulimbikizaji wa mali kwa watu binafsi/mashirika hata ikibidi kubadili sura nzima ya Utaifa/Dola na Uzalendo; Maendeleo si Vitu--Maendeleo ni Watu...
Ukiwa na watu wanaochekelea 'Mitaji' na 'Ukoloni Mamboleo' ni sawa sawa na jambo la 'kupenda njia ya mkato' ili 'Kupata na Kuwahi'--mambo ya kupenda majibu mepesi kwa maswali magumu... Katika mapelekeo ya mwenendo wa namna hii upo muktadha akilifu wa kudhani 'umepata' na kumbe 'umepatikana'...
Tujitahidi kuwa macho juu ya yote, tuwe na uono na ufikirifu mifumo, kwa kuwa namna yoyote ya 'upembuzi yakinifu' inaweza kuwa ni 'maarifa ya kukosa' na kuhalalisha mabovu ya kijamii. Mengi ya machagua ya kitaasisi, hata muktadha wenyewe wa PPP yanaweza kusahihishwa kwa kuzingatia hesabu muafaka za udhamirifu wa 'Maendeleo ya Watu'; si kwa vigezo mushkeli vya 'fedha, mitaji, ajira na masoko' zaidi...
Jamii yetu inahitaji 'Mwangaza' na '
Wadau wa Utu na Maendeleo' katika Kweli khasa na si 'Usahihi wa Kisiasa za Mambo'...