Serikali inaweza kuchangia au isichangie kabisa kutegemea mradi husika.
Sheria inaruhusu kitu inaitwa viability Gap funding ( VGF) ambapo serikali inaruhusiwa kuchangia kiasi cha mtaji kufanya kampun binafsi itekeleze hasa kama mradi ni muhimu kiuchumi lkn haulipi kibiashara / hauna commercial viability .
Lkn kama mradi ni viable economically & commercially then serikali haina sababu ya kuchangia mraji asilimia yoyote labda tu kama serikali inataka pengine kutoa ruzuku ili kupunguza bei/ userfee.
Kwa upande wa dhamana/govt guarantee ni kwajili ya kuikinga kampuni binafsi dhidi ya baadhi ya viahatarishi na wakati mwingine hutolewa kama Comfort letter.
Kwa mfano mwekezaji analeta mabasi lkn mkusanyaji ni mamlaka ya serikali kama DART, Mwekezaji anaweza kuomba dhamana ya serikali ili endapo DART atashindwa kumlipa basi hazina imlipe/ payment guarantee.
Haya yote yako kwenye Sheria ya PPP
Nadhani nimekusaidia