Niwe mkweli kabisa ,kada mwenzangu Kafulila nae bado hajui dhana ya PPP kwa undani wake .Kwa kuwa nawe upo humo naomba unijibu swali moja tu la kuanzia ,je ni kweli PPP Project serikali haiwekezi hela zake ? na kama haiwekeze hela zake ni kwa nini miradi mingi ya PPP duniani haswa ile ambayo siyo Project financed inabidi serikali kudhamini mwekezaji?
Ukituliza akili vizuri na kuweka ushabiki pembeni nitaungana nawe.
Hapa ninakuona leo kwa mara ya kwanza ukiweka ushabiki wa kichama pembeni. Hilo ni jambo jema.
Sijaona popote kwenye mada hii, na hata toka kwa huyo Kafulila mwenyewe akieleza kinaga ubaga hiyo PPP ni nini hasa; lakini wachangiaji humu hawaachi kupiga makofi kwa kule kutamka tu 'PPP".
Watu wanasema huu mpango wa PPP ndio unao tumika duniani kote, lakini hata mfano mmoja tu hawatoi na kuueleza.
Hii PPP ni mpango wa hizi taasisi za Bretton wood wanao upigia upatu sana siku hizi ili utumike kwa nchi hizi maskini. Kiufupi, ni njia ya kuwaneemesha wafanya biashara wa dunia kwa mgongo wa jasho la walipa kodi wa nchi maskini.
Jiulize kwa nini lazima pawepo ushiriki wa serikali katika mpango huo, bila ya hivyo hao wawekezaji hawaitaki miradi hiyo?
Hizi PPP sasa ndiko vichaka vya rushwa na uchafu tele utahamishiwa; hasa kwa serikali dhaifu kama hii yetu hapa.
Halafu watu wanashangilia tu bila hata kujiridhisha juu ya uelewa wa mpango huo.
Hawa akina Kafulila ni vyombo/vifaa tu vinavyo tumika kulaza akili za watu; na hasa watu kama waTanzania wasiokuwa na utashi wa kuhoji lolote.