Hatimaye wachumi nguli waungana na David Kafulila

Mwangaza wenyewe ndio hii PPP na mengine mazuri ya kuijenga jamii yetu
UNACHEKESHA SANA...

Unaweza kuibayanisha/kuichambua fremukazi ya PPP kitalaam hapa ili tuoneshane njia moja kwa moja?

Kama unaweza...

ANZA!
 
Asante kwa kuongeza nyama, mimi naandika kitabu cha ujasiriamali fikirishi siyo tu jinsi ya kuanzisha na kuendeleza biashara bali nimeangaza kwanini biashara zinakufa na nini kifanyike.

Darasani tulifundishwa kidogo sana kuhusu mjasiriamali na yanayo mzunguka kumbe kuna mengi yaliyo jificha ambayo kumbe jamii ndiyo inaweza, (ina nguvu), kuweza kuyapigia kelele hasa kuhusu changamoto, (uncertainty), changamoto husababishwa na 1. Majanga asili, 2. Binadamu ambaye huwasababishia wengine changamoto kwa makusudi ama bila kujua, pia hujisabanishia Changamoto kwa uzembe uvivu ujinga na ushamba

Tunakazi kubwa ya kuelimisha jamii ambayo walio pewa dhamana kuahirisha kufikiri kizalendo a.k.a kujizima data
 
NI KWELI; NA MCHANGO UNAANGAZIA UKWELI WA MAMBO

Baraka Sana kwa Kazi yako!

Ndiyo, hayo unayoyataja yanafahamika na kiuono na ufikirifu mifumo kama 'Mazingira'--mazingira ya mtendaji ama na chombo; daima kuna (1) mazingira ya ndani, na (2) mazingira ya nje; mtu makini daima anatakiwa awe na jitihada ya macho ya kuyaona ya ndani na ya nje kwa ufasaha na upeo wa kumaizi anawajibika vipi kuilinda shughuli yake na kuihakikisha usalama wake wa kiuhai/pumzi...

Wanajamii wasipo jifahamu kuwa wawo ni 'rasilimali' katika mchakato wowote, mchakato wowote wa maendeleo ya kijamii na taifa, daima hawa wanageuka kuwa 'zigo la lawama'...



Kutoka kwenye maarifa rahisi ya menejimenti; liko hitaji la kuwaleta wanajamii katika elimu na ujuzi wa uono na ufikirifu mifumo:


Hmmm
 
Jamii kwasasa ukiielimisha ina elimika na wanauelewa mkubwa japo hawajabahatika kupata elimu.

Changamoto nyingine iliyoko kwenye jamii zetu ni wale wa bendera fuata upepo hawa wanapokea chanya na hasi, na wale wanaopotosha jamii kwa ushabiki ama kukosa maarifa ya kuelewa lakini jamii inadhani ndiyo kioo cha jamii husika, hawa hupotosha jamii hawa ukiwa bananisha kuhusu ufahamu wa alichokiongea anabaki kushangaa utadhani mjusi kabanwa na mlango
 
UNACHEKESHA SANA...

Unaweza kuibayanisha/kuichambua fremukazi ya PPP kitalaam hapa ili tuoneshane njia moja kwa moja?

Kama unaweza...

ANZA!
Public-private partnerships are arrangements between the public and private sectors that undertake and deliver projects to serve the public interest. They aim to leverage the strengths and expertise of both sectors to achieve mutual benefits, combining public resources and the efficiency of the private sector. These partnerships can vary, but they typically involve the financing, construction, operation, and maintenance of public infrastructure or the delivery of public services.
The public sector retains the responsibility for setting the policy objectives and ensuring the project's compliance with public interest considerations. The private sector partner brings its specialized skills, technological capabilities, and financial resources to design, build, and manage the project. The risks and rewards of the project are shared between the two parties, often through a long-term contractual agreement.
PPPs can be applied to various types of projects. Some examples are transportation infrastructure, utilities, social infrastructure such as schools and prisons, and information technology systems. PPP projects are contingent upon many factors that include the need for the expertise of the private sector, cost savings, potential revenue generation, and the complexity of the project.
The duration of PPP contracts can vary significantly and is contingent upon the nature of the project. Projects can be as short as two years but can span as long as several decades. The lengthy contract periods are necessary because they provide the private sector partner with the opportunity to recoup their investments and generate reasonable returns. The duration also allows the public sector to benefit from the private sector's expertise over an extended period and ensure the quality and sustainability of the infrastructure or services provided.
 
Umenikumbusha kuhusu mradi wa mabasi yaendayo kasi hivi ule uko kwenye mfumo wa PPP maana siuelewi kabisa, kama upo kwenye mfumo huo wa PPP na ndivyo picha, (taswira), ya miradi ya PPP, inatakiwa iwe, basi naweka alama ya kuuliza ?, Kwenye maana halisi ya PPP
 

The public sector retains the responsibility for setting the policy objectives and ensuring the project's compliance with public interest considerations. The private sector partner brings its specialized skills, technological capabilities, and financial resources to design, build, and manage the project. The risks and rewards of the project are shared between the two parties, often through a long-term contractual agreement.
PPPs can be applied to various types of projects

Hio ndo sababu kwanini nchi za western viwanda viliota mbawa kwa sababu ya kuwa na mawazo mfu kama haya kazi ya serekali ni zaidi ya kutengeneza sera
 
SI MWANZO MZURI

Kwanza, ni vema ungelianza kwa maneno yako mwenyewe--si lazima uwe unajua sana ya PPP kwa mfano; kwa kuwa hili linaweza kuwa shauri la kuelimishana na kujengeana uwezo wa kubayanisha mambo.

Halafu hakuna haja ya matumizi ya lugha ya Kiingereza; haya yote uliyoyaweka hapo, na mengine ambayo hujawakilisha, yanaweza kuzungumzwa kwa Kiswahili--tutumie Kiswahili... Ama tutafsiri mengine yote kutoka kwenye lugha ya Kiingereza.

Kwa Uzoefu wa Utaasisi wa PPP kwa Tanzania; mahala pazuri pa kuanzia ni vyanzo vya habari vya taasisi zenyewe za Kiserikali: >KWA MFANO UKURASA HUU WA TOVUTI<--kufanya hili ili lau kuotea fremukazi ya Utaasisi wa PPP inafananiaje...

Fremukazi maana yake ni SURA YA MUONGOZO WA KIUTENDAJI ambavyo ndiyo husadifu miundo ya kiutendaji, dhamira zake za kiutendaji, usuli wa mashauri ya 'Kuhalalisha' makusudi ya utendaji wake -- ndilo hupata uhalali na kukubalika kupitia Sera na Sheria.

Kwa hivyo fremukazi inakuwa na mashauri ya Fikra, Maono na Kujichagulia kiserikali kama chombo ya Maslahi ya Umma na Itaainisha dhamira, miongozo na taratibu ya kuliendea jambo Kimipango na Utumishi wa Umma kama chimbuko za jitihada zenyewe.

Kinabaki siku zote kuwa 'Ukurusa wa Wazi' kwenye fremukazi yeyote ni 'Uwezo wa Jamii' ama 'Vyombo/Taasisi' za Serikali katika kutekeleza malengo ya Utaasisi wa Shughuli fulani--tuseme labda Shughuli ya Kutengeneza Uwepesi wa Makusudi ya PPP... Jambo linaloamuliwa na umahiri wa utendaji wenyewe na dhamira ya kujiimarisha kitaasisi na uwezo.

Fremukazi ni mambo ya Kujichagulia, Kujipangilia na Kujenga Ushawishi kwa kitu ambacho kwenye uono na ufikirifu mifumo hutajwa kama 'Koherensia ya Utaasisi--Institutional Coherence'--hili ni kwa ajili ya Maslahi fulani ya Jamii/Taifa/Dola--kwa hivyo daima huwa kuna 'mbigiri' za upeo, uwezo, utayari wa wanajamii wenyewe na watendaji... Si kila mwanajamii ama mtendaji analingana ama kufanana na mwenzake katika kutambua na kuyabayanisha 'maslahi ya Taifa/Jamii'--hapa ndipo kuna 'donda dungu'...

Kiufundi, tatizo lililo kwa sasa kiutendaji ni kuathirisha 'Koherensia ya Utaasisi' kwa mambo mengi yanayochukuliwa/kufanyika kwa ajili ya maendeleo ya jamii--uchanganuzi wa wakati mmoja wa sera mbalimbali ama sheria huwa na azma ya kulizingatia hili...

Hili lina namna yake 'kushughulika nalo' na daima huwa ni 'mchakato endelevu'... Ugumu ama wepesi wa mchakato wenyewe unategemea 'uzito' wa wanajamii wenyewe na watendaji katika 'kujifunza kutokana na makosa' ama 'kuwa na uwezo wa kubaini utendaji wa ari ya chini/duni/hafifu wa 'Watendaji Wote Husika'...​
 
kujifunza kutokana na makosa' ama 'kuwa na uwezo wa kubaini utendaji wa ari ya chini/duni/hafifu wa 'Watendaji Wote Husika'...๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘
 
Duuuh nchi ngumu sana hii aisee
 
Nitarudi...
 
Hii inahusikaje hapa?
 
Kuna hekima kubwa sana hapa
 
Hao wachumia nguli wameonesha wapi unguli wao? Ni wapuuzi fulani tu wenye. Vikaratasi vinavyoonesha wamehudhuria shuleni. Wachumia tumbo tu.

Watu mliofeli shule kwa kukosa akili huwa mnahasira sana na wasomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ