Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,780
Habari za usiku wadau. Natumaini wengi wenu mmejikunyata kitandani huku mkiendelea kutafakari hali iliyojitokeza jana jioni.
Taarifa iliyo rasmi ni kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba leo Jumanne tarehe 18 Machi 2014. Mtakumbuka kuwa jana jioni bunge maalum liliahirishwa baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na wabunge wa vyama vya upinzani kuzomea wakati Warioba akijiandaa kutoa hotuba ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba. Wabunge hao wa upinzani ambao wamejiunga pamoja katika umoja wao ujulikanao kama UKAWA wanadai kuwa Mwenyekiti wa Bunge Sammuel Sitta amevunja kanuni ya saba kwa kuruhusu Warioba kuwasilisha Rasimu ya Katiba kabla ya Rais hajazindua Bunge. Pia wabunge hao wa upinzani walikuwa wanalalamika kitendo cha Warioba kupewa dakika 120 tu kuzungumza muda ambao walisema kuwa hautoshi.
Kutokana na hali hiyo, ile Kamati ya mashauriano iliketi baada ya bunge kuvunjika jana jioni. Katika kikao hicho, imebainika na wabunge wa upinzani wamekiri kwamba Mwenyekiti Sitta hajavunja kanuni yoyote kwa vile kanuni hiyo ilitenguliwa kihalali jana asubuhi na bunge kwa kutumia kanuni ya 85. Kwa maana hiyo, hoja imebaki pale pale kwamba Warioba ataanza kuwasilisha na Rais atakuja kuhutubia siku ya Ijumaa kama wasaa utamruhusu
Kuhusu hoja ya Warioba kupewa muda kiduchu, Kamati ya Mashauriano imefikia muafaka wa jambo hilo kwa kumruhusu Warioba kuwasilisha hotuba yake kwa ukamilifu wake. Kwamba mara baada ya kiapo cha wabunge leo asubuhi, Warioba atawasilisha hotuba yake kuanzia saa tatu na nusu hadi saa saba mchana.
Hata hivyo, ingawa wabunge wa upinzani wamekubali kuwa kanuni ya saba haijavunjwa, hali huenda ikaendelea kama ya jana hasa ikiwa wabunge wa UKAWA watakataa muafaka uliofikiwa kupitia Kamati ya Mashauriano. Upo uwezekano kwamba baadhi ya wabunge wa UKAWA wakaendelea na msimamo wa kutaka Rais aanze kuzindua Bunge ndipo Warioba aje kuwasilisha Rasimu ya Katiba.
Hata hivyo, tuwashukuru viongozi wa kiroho ambao wameamua kuwaeleza ukweli wanasiasa. Katika kikao hicho cha Kamati ya Mashauriano, viongozi hao wa Kiroho wamewaambia bayana wanasiasa kwamba wanaonesha jeuri isiyokubalika mbele ya Mungu kwa kuweka misimamo isiyo na tija. Kwamba, wanasiasa wengi wamekuwa viburi na wamejawa na dharau kitu ambacho hakimpendezi Mungu.
Ni hayo tu wakuu.