Hatimaye Warioba Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Jumanne Tarehe 18 Machi 2014

Hatimaye Warioba Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Jumanne Tarehe 18 Machi 2014

Status
Not open for further replies.
Katika kanuni wamesahau kuweka hi I "Bunge likihairishwa na posho zihairishwe" hapa kidogo heshima ingekuwepo.
 
umeshaambiwa kanuni ilitenguliwa asubuhi na wakakubaliana,au unasemea kanuni ipi tena?

walikubaliana wapi kama sio unafiki wako walipoulizwa pande zote walishikilia misimamo yao sita akasema waliokubali kanuni kutenguliwa wameshinda kwa maana hyo alilazimisha zee penda sifa za kijinga sana.
 
Alivyoandika Julius Mtatiro kwenye wall yake ya fb

Jaji Warioba atawasilisha rasimu ya katiba leo JUMANNE kwa saa takribani nne. Ataanza saa 3.30 asubuhi hadi saa 7.30 mchana. Baada ya VUTA NIKUVUTE ya jana bungeni, Mwenyekiti wa Bunge Maalum aliwaita wawakilishi wa makundi mbalimbali na hasa UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA) ambapo imekubalika kuwa masuala ya uendeshaji wa bunge yatafuata kanuni na taratibu.
Suala la Rais kuja kuzindua bunge la katiba siku ya ijumaa na baada ya uwasilishaji wa rasimu limeridhiwa na pande zote kwa kuzingatia kuwa hivi sasa tume ya Jaji Warioba yote ipo Dodoma na itakuwa usumbufu mkubwa iwapo watapangiwa siku ya ijumaa jioni au jumamosi baada ya ratiba ya Rais kama kanuni zinavyoelekeza.
Wale watoa mada wa CCM kina waziri MAPURI na wenzie wameondolewa. CCM walijipanga ati watoa mada wawe watu wao ili waje kufanya watakayowaelekeza, tumewakataa. Watoa mada kutoka Kenya akiwemo AMOS WAKO watakuja na kuseminisha.
Tumemweleza mwenyekiti Samwel Sitta kwa uwazi kabisa, kwamba hatutakubali kuburuzwa, huu ni mchakato wa katiba, siyo bunge la bajeti la ndiyo mzee.
Katiba hii itatumiwa na vizazi na vizazi, kwa vyovyote vile lazima itengenezwe kwa misingi ya kujali utu wa kila mtu, kuheshimiana, kuridhiana na kukubaliana. Ubabe na kukiuka kanuni kwa mwanya wa Busara za mwenyekiti havikubaliki. Mwenyekiti atumie busara pale tu ambapo kanuni hazielekezi chochote.
Nichukue fursa hii kumpongeza Mhe. Samweli Sitta kwa kujua alipoteleza na kuanguka, niendelee kumpa moyo kuwa yeye ndiye mwenyekiti wetu katika mchakato na kwamba tunamheshimu sana, lakini atambue atakapovunja taratibu au kutaka kutuburuza hatutakubali.
Tutaendelea kuunga mkono masuala yote yenye nia njema katika mchakato huu wa katiba, lakini tutapinga kila lililo na nia ovu dhidi ya matarajio ya watanzania katika katiba.
Kikao cha maridhiano kimemalizika saa 4 usiku wa jana baada ya bunge kuahirishwa.
===>Naamini Mr Six somo limemuingia vizuri tu.
 
Last edited by a moderator:
Tanzania hakuna upinzani wa kweli,wengi wao ni wanafiki,msimamo si jambo lelema,ukiamua jambo huwa hivyo bila hata kutetereka,Mungu alisema waoga hawataingia mbinguni hata kidogo.
 
Maoni mengi ya wananchi ni kuhusu ardhi, yaani wawekezaji wanapendelewa hali ya kua wananchi wanakosa ardhi-Warioba
 
Kweli mzee Warioba kiboko, pana jamaa hapa kakunwa na hotuba yake na kuamua kutununulia soda sote tuliopo, tupo sita hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom