Hatimaye Warioba Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Jumanne Tarehe 18 Machi 2014

Hatimaye Warioba Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Jumanne Tarehe 18 Machi 2014

Status
Not open for further replies.
Ilitenguliwa kwa maslahi ya nani? kama ilitenguliwa (kukiukwa) ndo bunge liendelee kuvunja kanuni hadi mwisho ilihali zimetimika wiki tatu kuzitunga hizo kanuni? Rationality ya kutungwa ni nini sasa?
Jaribu kuwa rational kidogo basi.
Tatizo lako unaeleweshwa halafu unajifanya hutaki kuelewa kwani kanuni ikitenguliwa huwa kwa manufaa au maslahi ya mtu binafsi? Kwa nini unauliza maswali yenye majibu.
 
halo viongozi wakiroho si ndio walewale wa bakwata wanaoteuliwa na rais badala ya kuchaguliwa na waumini wao unadhani watamtetea nani wasipojipendekaza kwa serikali inayoongozwa na bos wao
 
Kwani bunge lisipozinduliwa ina maana vikao havitaendelea?

Kimsingi bunge limeshazinduliwa. Kisheria bunge la katiba linaitishwa kwa tangazo la rais kwenye gazeti la serikali, jambo ambalo tayari lilishafanyika, hivyo bunge hili limeshazinduliwa.
Anachokuka kufanya Kikwete ni kuzungumza nao tu wabunge na si kulizindua bunge. Hiyo hotuba yake haielezwi kwenye sheria na hata kwenye kanuni imepachikwa tu
 
Hao "Viongozi wa kiroho" wana roho nyingine, wana mapepo, yakemewe. Wakati kanuni hizo zinatungwa, "Viongozi wa kiroho", hao, hawakuwepo????? Hao "Viongozi wa kiroho", ni mapandikizi ya CCM!!! Hakuna cha "Viongozi wa kiroho" hapa, wala cha nini, KANUNI LAZIMA ZIZINGATIWE!!!! Katiba inaanza kwa kusema,"Sisi wananchi tumeamua rasmi". Katiba ya sisi wananchi, haiwezi kupatikana kwa ubabe wa Sita, asiyekubali kushindwa !!!!!! UKAWA, hakuna kuweka silaha chini, wananchi tuko nyuma yenu!

tupitie njia yoyote cha msingi katiba ya wananchi iuundwe.
 
Toka umepewa ukuu wa Wilaya kwa fadhila,ukapata na hela ya mahali ya kuolea,unajiona umemaliza sana maisha....acha dharau,stress za maisha unazijua wewe???
Tatizo ukweli hutaki kuusikia inabidi wakuache ubaki kama ulivyo lakini leo warioba anawasilisha rasimu ya pili na rais atafuata.
 
wainame wainuke cha msingi katiba yetu wazawa wa tanzania tunaiitaji, tulishamaliza kuiunda na tume ya warioba.
 
Tunawapongeza UKAWA maana haya maccm yalishamkejeli Warioba tangu muda mrefu na sasa yanataka kuifanya kazi yote ya tume haina maana.
UKAWA tunawaunga mkono kama tunavyo muunga mkono jaji Warioba.
 
Mkuu, kwa mtazamo wangu ni kwamba hakuanza vibaya. Ila kuna hali ya kutoaminiana baina ya CCM na vyama vya upinzani. Pia kuna fear of unknown.

Kama walidhani chenge camp watakubali kuukosa uenyekiti kirahisi rahisi basi walifanya makosa makubwa
 
Viongozi wa Kiroho (Penguin) ukiwapa tu samaki (Vipande 30) wanalainika sana. Yaani maharage ya Mbeya..

Penguins-006.jpg
 
umeshaambiwa kanuni ilitenguliwa asubuhi na wakakubaliana,au unasemea kanuni ipi tena?
Nani alitengua?Usiniambie ujinga wa kuwauliza nani anakubali na nani anakataa.Halafu spika ana ibuka waliosema itenguliwe wameshinda!
 
Ilitenguliwa kwa maslahi ya nani? kama ilitenguliwa (kukiukwa) ndo bunge liendelee kuvunja kanuni hadi mwisho ilihali zimetimika wiki tatu kuzitunga hizo kanuni? Rationality ya kutungwa ni nini sasa?
Jaribu kuwa rational kidogo basi.

Na ikumbukwe kuwa wakati wanajadili kanuni hizi majuzi ubishi huu huu wa nani atangulie kuja kati ya rais na warioba ulitokea na mwisho wakakubaliana kuwa aanze rais na baadae aje warioba. Sasa kwa nini watengue makubaliano saa chache tu baada ya kukubaliana?
 
Kwani Raisi kuanza kulifungua bunge kunatatizo gani kama zise mavyo kanuni?Kwanini ccm na Sita wamepania kulipindua hilo?
 
kuwepo serikali moja,mbili ama tatu hakutoi uhakika wa chama fulani kutawala,think.
ila KUNATOA NAFASI YA KUVUNJIKA MUUNGANO JAMBO AMBALO WAZANZIBAR WENGI NDIYO WANALITAKA, NADHANI HAPO SASA UMEELEWA LENGO LA WANANCHI - YAANI KUUVUNJILIA MBALI MUUNGANO WA KISANII.
 
Baada ya jana jioni bunge la katiba kuingia katika hali ya sintofahamu iliyochangiwa pia na wabunge wa chadema,cuf na nccr- mageuzi leo asubuhi bunge litaendelea na shughuri zake kama inavyoonesha hapa chini.


1. Kuanzia saa tatu asubuhi mwenyekiti wa bunge maalumu mh samweli sitta ataweza kuwaapisha wabunge waliosalia kuapa ambao idadi yao yapata kama thelathini hivi.


2. Baada ya wabunge hao kumaliza kuapa jaji warioba ataweza kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba ambapo imepangwa kuanza saa tatu na nusu au na dakika arobaini na tano mpaka saa saba kamili mchana.


3. Baada ya warioba kumaliza kuwasilisha rasimu mwenyekiti atalieleza bunge nini kitafuata baada ya zoezi hilo kukamilika.


Hivyo ndivyo utaratibu utakavyokuwa kwa leo karibu sana tuendelee kufuatilia katiba yetu inavyotungwa.
Mtu unatunga kanuni halafu ndiyo unakuwa wa kwanza kuzivunja ndiyo maana miji yetu ni michafu kila mahali,watawala ccm ndiyo wanaongoza kuvunja sheria.UKAWA leo pia fanyeni kama jana vinginevyo waseme Warioba ndiye analiZindua Bunge halafu Kikwete ni mtoa mada ya blah blah
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom