Hatimaye Warioba Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Jumanne Tarehe 18 Machi 2014

Hatimaye Warioba Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Jumanne Tarehe 18 Machi 2014

Status
Not open for further replies.
Baada ya jana jioni bunge la katiba kuingia katika hali ya sintofahamu iliyochangiwa pia na wabunge wa chadema,cuf na nccr- mageuzi leo asubuhi bunge litaendelea na shughuri zake kama inavyoonesha hapa chini.

1. Kuanzia saa tatu asubuhi mwenyekiti wa bunge maalumu mh samweli sitta ataweza kuwaapisha wabunge waliosalia kuapa ambao idadi yao yapata kama thelathini hivi.

2. Baada ya wabunge hao kumaliza kuapa jaji warioba ataweza kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba ambapo imepangwa kuanza saa tatu na nusu au na dakika arobaini na tano mpaka saa saba kamili mchana.

3. Baada ya warioba kumaliza kuwasilisha rasimu mwenyekiti atalieleza bunge nini kitafuata baada ya zoezi hilo kukamilika.

Hivyo ndivyo utaratibu utakavyokuwa kwa leo karibu sana tuendelee kufuatilia katiba yetu inavyotungwa.
Mkuu, pamoja sana kwa ufafanuzi huu
 
Mzee wa speed*standard naona kaanza vibaya jana kambi ya mama makinda inayoongozwa na ndugaii naona walishangilia sana hivi kuna uhasama wa hizi pande mbili? All in all Jembe WARiOba hata akipewA saa moja anawanyamazisha akina kigunge
 
Mkuu, kwa mtazamo wangu ni kwamba hakuanza vibaya. Ila kuna hali ya kutoaminiana baina ya CCM na vyama vya upinzani. Pia kuna fear of unknown.
 
Ngumi zitapigwa tu.
Mkuu, dalili hizo zipo wazi. Ila tukifikia hapo kuna mawili, aidha tutavuruga kabisa mchakato au watu wataheshimiana. Tuombee hilo namba mbili litokee
 
Haya majitu yana hasira ya kipigo cha kalenga, sasa yanazihamishia bungeni
 
Mzee wa speed*standard naona kaanza vibaya jana kambi ya mama makinda inayoongozwa na ndugaii naona walishangilia sana hivi kuna uhasama wa hizi pande mbili? All in all Jembe WARiOba hata akipewA saa moja anawanyamazisha akina kigunge
Vipi kalenga
 
.. .. eti kama wasaa utamruhusu! Au ndiyo kusema amebanwa na uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze?
Walioleta ushindi wa kimbunga kalenga wataleta ushindi wa kishindo chalinze. Mtaendelea kuchapwa fimbo za mgongo milele.
 
Mkuu, wakati mwingine Mkuu wa nchi anakuwa na majukumu mengi ya lazima nje na ndani ya nchi. Inategemea jukumu hilo lipo wapi.

Majukumu muhimu kuliko katiba? mbona kwenye misiba ya kina Bi kidude alienda ghafla tu akala had I wali!!
 
umeshaambiwa kanuni ilitenguliwa asubuhi na wakakubaliana,au unasemea kanuni ipi tena?

Ilitenguliwa kwa maslahi ya nani? kama ilitenguliwa (kukiukwa) ndo bunge liendelee kuvunja kanuni hadi mwisho ilihali zimetimika wiki tatu kuzitunga hizo kanuni? Rationality ya kutungwa ni nini sasa?
Jaribu kuwa rational kidogo basi.
 
Mkuu, wakati mwingine Mkuu wa nchi anakuwa na majukumu mengi ya lazima nje na ndani ya nchi. Inategemea jukumu hilo lipo wapi.

Majukumu ya LAZIMA kama yapi kwa mfano yanayozidi umhimu kuliko KATIBA YA NCHI??

Hayo majukum yanatoka wapi km sio kwenye katiba?

Think Big!
 
Duniani kunavituko sana hasa tanzania wapo watu wanafanya mambo ili tu waonekane walichokataa wapinzani jana na kile walichokubari tofauti yake ni nini au kwa sababu ya live tv.
 
Wenye akili timamu wanapigana kwa hoja, nyie misukule mnafanya vurugu za chekechea
Jana mlisema Jaji kazomewa na wabunge, mwenzio ze mutuz akaweka pumba hapa, leo mmegeuka, sio warioba tena kazomewa. Hivi nyie maccm mna kiherehere cha aina gani??
 
Majukumu ya LAZIMA kama yapi kwa mfano yanayozidi umhimu kuliko KATIBA YA NCHI??

Hayo majukum yanatoka wapi km sio kwenye katiba?

Think Big!
Pamoja na yote unayosema rais hakuna sheria inayomlazimu kuja kufungua bunge ila ni kanuni ndiyo inataka hivyo kwa mantiki tu rais anapoitwa huwezi kumpangia aje lini ila wewe utapeleka mwaliko halafu yeye ndiye atakwambia kuwa anakuja lini zingine porojo za kitoto tu.
 
Mkuu, wakati mwingine Mkuu wa nchi anakuwa na majukumu mengi ya lazima nje na ndani ya nchi. Inategemea jukumu hilo lipo wapi.

Nafikiri JK safari hii anaenda kushiriki kutafuta Ndege ya Malaysia iliyopotea
 
Tatizo la Rais wetu hana vipaumbele. Hivi kipaumbele cha Rais wetu kwa sasa ni nini? Ana nini cha maana kwa sasa kilicho muhimu kuliko kutengeneza mkatabakali wa Taifa letu? Rais wetu huwa anapata muda mpaka wa kuhudhuria graduation ceremony za watoto wa sekondari lakini anakosa muda wa kwenda kufungua kikao cha Bunge maalumu. Tuna balaa nchi hii.

Mkuu, wakati mwingine Mkuu wa nchi anakuwa na majukumu mengi ya lazima nje na ndani ya nchi. Inategemea jukumu hilo lipo wapi.
 
Kama hakuna umuhimu, basi asiende kabisa. Maana haileti maana Rais aende kufungua wakati mjadala ulikwishaanza.

Pamoja na yote unayosema rais hakuna sheria inayomlazimu kuja kufungua bunge ila ni kanuni ndiyo inataka hivyo kwa mantiki tu rais anapoitwa huwezi kumpangia aje lini ila wewe utapeleka mwaliko halafu yeye ndiye atakwambia kuwa anakuja lini zingine porojo za kitoto tu.
 
Stress ni ugonjwa mbaya sana,wachangiaji wengine hapa duh.

Toka umepewa ukuu wa Wilaya kwa fadhila,ukapata na hela ya mahali ya kuolea,unajiona umemaliza sana maisha....acha dharau,stress za maisha unazijua wewe???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom