Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

ni hatua nzuri lakini mkataba unatakiwa uwe clear. Ijulikane vitu gani anatakiwa afanye. na je maendeleo ya timu yakiwa hayaridhishi nini kinatakiwa kifanyie lazima ielezwe kwenye mkataba. Pia iwepo utaratibu wa kuuvunja huo mkataba kama wanachama hawaridhishwi na uendeshaji wa club.
 
Kandambili ovyo sana.. yaani klabu inakodishwa.!?

kiukweli hizi club mbili za simba na yanga zimekuwa zikiendeshwa kwa kukodishwa sema haikuwa rasmi. Club hazikuwa na mfumo mzuri wa uendeshaji na upatikanaji wa pesa, zinategemea watu binafsi watoe pesa za kusajili wachezaji, watoe pesa za kupeleka timu kambini n.k. Ni wazi hao watu waliokuwa wakisaidia timu walikuwa wanajuwa ni namna gani pesa yao itarudi. Je hiyo 25% wanachama wananufaika nayo vipi? Ni wazi club sasa ni lazima zitoke katika club kuwa chini ya wanachama bali wanachama wabadilishwe na kuwa wanahisa. Hii itasaidia wanachama kuichangia timu na kuchangia uendeshaji na maendeleo ya timu na faida ikipatikana kla mwanachama apate kutokana na alivochangia, kwa mtindo huo upo wa uwezekano wa timu kuendeshwa kisasa na kibiashara. Tatizo ambalo naliona hapa ni Manji anapewa 75% ya hisa za club kwa miaka 10, je kwanini apendelewe peke yake tu? kwanini haikutangazwa ili kama kuna mwanachama mwingine pia mwenye uwezo kama wa Manji naye awekeze kwenye uendeshaji wa timu?
 
Naona Mwalimu Nyerere asingeliongelea maradhi na umasikini bali angeweka wazi UJINGA kama adui pekee.
Naendelea kuamini kuwa ujinga huu ndio unapelekea umasikini na maradhi na sio kinyume chake! Wapi Mzimba!
 
Sheria zote za kimataifa zinasema mita 40 kutoka bahari inakoishia ni mali ya umma lakini huyu mtu from kusikojulikana alimilikishwa coco beach sembuse kumilikishwa Yanga isiyo na sheria wala mwenyewe!
 
Wakuu,hebu nisaidieni mfano wa timu moja ya mpira iliyowahi kukodishwa ili tuseme yanga wameitumia kama kiolezo katika kufanya maamuzi yao..
Kwahiyo wewe huwezi kuanzisha kitu wenzako watumie kama kielelezo. Unataka kila jambo tuangalie kwanza kwa wengine.

Poor Africans
 
..orodha ya nini sasa.,stick kwenye mada!
..yani pamoja na uzee unaojinasibu nao umeshindwa kujenga hoja kuonesha hiyo TIJA uliyoitaja!...
...aisee bora ujifie tu!
.nenda mwalimu!
Nashukuru kijana wangu. Ila wote ni njia moja. Siku mifupa yako ikichoka ndipo utatamani kuungama kwa kauli zako.
 
Huenda wajumbe wa mkutano mkui wa yanga walikuwa wamelala siku hiyo.
Hata MZEE akilimali hakuona kuwa yanga wamempa jamaa apigie pesa Tu? Au mpaka yanga apigwe tano na simba ndiyo akilimali agutuke?
 
Nashukuru kijana wangu. Ila wote ni njia moja. Siku mifupa yako ikichoka ndipo utatamani kuungama kwa kauli zako.
....dah.,umenijibu kwa hek'ma hadi nimeona aibu!
..nafuta kauli mzee wangu!
....niwie radhi.
 
Mimi ni yanga damu ila nasema kuwa Ni hasara tupu miaka yote 10 na gawiwo la 25% TUSAHAU Wana yanga.

Ila ushindi Unaweza kuwepo ndo nafuu yetu wapenzi. Miundombinu na maboresho ya klabu TUSAHAU.

Asante MANJI.
 
Ulivyoandika kwa herufi kubwa mi nikajua nakutana na mkataba mubashara....... kumbeeee.......
 
Actually jamaa akija kusema amepata hasara kwa miaka yote 10 hakuna mtu atakayekuwa na ushahidi wa kupinga, maana management ameichukua yeye hivyo wahasibu na mameneja ni watu wake yeye na wana uwezo wa kuficha mahesabu ya faida iwapo itatokea, halafu akawaonyesha mahesabu ya hasara.
 
Sheria zote za kimataifa zinasema mita 40 kutoka bahari inakoishia ni mali ya umma lakini huyu mtu from kusikojulikana alimilikishwa coco beach sembuse kumilikishwa Yanga isiyo na sheria wala mwenyewe!

duh, na kweli haina mwenyewe, maana ukiuliza utaambiwa timu ya wanachama, wanachama wenyewe wako active wakati wa uchaguzi tu. Timu inaendeshwa kijanjakijanja tu. Wanachama utawaona kulalamika timu ikifungwa na Simba tu. Kwa mpira wa kisasa timu haziendeshwi hivi. Manji anaonekana anataka kununua hisa ila dhana ya hisa inapigwa na wachumia tumbo. Manji ashawishi wanachana wakubali mfumo wa kumiliki timu kwa hisa alafu sasa baadae mwanachama asiyeweza kumudu kuchangia hisa zake aziuze kwa manji au mtu mwingine yeyote yule anayeweza kuzimiliki.
 
Mimi ni yanga damu ila nasema kuwa Ni hasara tupu miaka yote 10 na gawiwo la 25% TUSAHAU Wana yanga.

Ila ushindi Unaweza kuwepo ndo nafuu yetu wapenzi. Miundombinu na maboresho ya klabu TUSAHAU.

Asante MANJI.
Hebu tuwekee huo mkataba hapa, na uache blah blah.
 
Kwani kwa MO hakutakuwa na mgt mkuu? Kumbuka 49% zilizobaki inawezekana wanachama wachovu wasipate zitakuwa za kina dewji na Poppe etc wewe mwanachama wa kawaida subiria timu ishinde ufurahi.
 
Kabla ya Manji kuchukua team, miaka yote hiyo Yanga walipata faida gani? Mimi ni yanga 100%,ila kiukweli cc huwa tunachoangalia ni ushindi wa vikombe na mechi za watani... Laiti tungekuwa na faida inayopatikana, tungelishaujenga uwanja.... Acha aichukue tu... Ukodishaji ni lugha tu, lakini ni yale yale ya kampun kuingia ubia.
 
Kwani kwa MO hakutakuwa na mgt mkuu? Kumbuka 49% zilizobaki inawezekana wanachama wachovu wasipate zitakuwa za kina dewji na Poppe etc wewe mwanachama wa kawaida subiria timu ishinde ufurahi.
Hao akina Pope ndio wanachama wenyewe, uwepo wao unahakikisha kinachovunwa na klabu kinabaki klabuni, tofauti na YM ambapo mkataba unasema atachukua management klabu ibaki na majengo na viwanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…