Katika kikao walichokaa cha Kuikodisha Timu ya Yanga kwa Mkodishaji kati ya wateja wanaotaka kukodishwa Yanga na Wenye timu ya Yanga , Mtu mmoja aitwae Manji alihudhuria kikao hicho kama Mkodishwaji Mkuu (Tenant) na pia mtu huyohuyo alihudhuria hicho kikao kama Mkodishaji Mkuu(Landlords).
Akiwa kama Mkodshwaji Mkuu (Tenant), Mtu huyo aliweka terms za mkataba anaoutaka (proporsals) yeye mteja ambao alidhani kama Mkodishwaji Mfanyabiashara angefaidika nao, lakini Mtu huyohuyo mmoja akiwa kama Mkodishaji Mkuu (mwenyemali) ambae alitakiwa kufikiri kwa faida ya wenye mali wenzie alikubaliana na terms/proporsal zilizowekwa na mteja ambae nae ndio yeye yeye mwenyewe!!
Yaani katika Meza ya majadiliano iliyohusisha pande mbili za Landlord v/s Tenant, mtu huyo ikifika zamu ya Landrod kuongea basi anahamia upande wa Yanga na anaanza kuongea kama mwenyekiti na anatoa hoja, na ikifika zamu ya tenants kuongea basi nae ananyanyuka kwenye kiti na kuhamia upande waliko wafanyabiashara wenzake anaongea kama tenants Mkuu akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa mwenyekiti ambae ni yeye mwenyewe.
Na wakifikia makubaliano basi katika Mkataba mtu huyohuyo anasaini sehemu ya Landlord na anasini sehemu ya Tenants. Yaani Mwenyemali Mkuu ni yeye, na mteja Mkuu ni yeye pia,
Only in Tanzania, specifically at Kandambili F.C. a.k.a Timu ya Chama!!