Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Hujui unachoongea,
Hao wanachama kwa miaka zaidi ya 50wameshindwa kufanya ayo unayoyasema.
Wameshindwa kudhibiti nembo inatumika ovyo, jezi,.

Sasa acha apewe mtu ambae atadhibit kibiashara,
CHA msingi ni mikataba ikae sawa tu
Hiyo miaka 50 unaanza kuhesabia wanachama gani, nadhani tuseme zaidi ya miaka 30 maana ndo usanii kwenye soka ukaingia tena hii miaka 20 ya hivi karibuni but before that wanachama walikuwa wanazitumikia timu zao na hapo elimu za uendeshashaji na uwekezaji walikuwa hawajui na bado hata hayo majengo walisimamisha. Issue hapa ukikodisha kitu si lazima ulipe fedha kidogo alafu unakabidhiwa timu uanze kuendesha ili ukila loss wamilki wa timu wanakuwa na mtaji wa kuanzia. Ngoja tuone kwanza maana watz huwa tunahofu na mabadiliko hivyo let's wait and see hiyo modality wanayotumia kama ni nzuri
 
Katika hiyo miaka 80 wanachama waliokuwa na maamuzi hizi timu wamezifikisha wapi kama sio kutia aibu tuu
 
Nikuulize sisi wana chama tuna faidika nini sasa hivi zaidi ya ubishi bora manji awekeze tu maana wataweza pata ajira kuliko sasa hivi
Si unajua upande wa pili imewakera na inawauma. Wanaanza kubashiri mabaya huku wakiyapiga teke mazuri ya Kuwepo kwa Manji, wataisoma.
 
Yenu ya Simba yanawashinda yakwetu wa Kimataifa mtatuweza? Sisi tupo kimataifa nyie pambaneni na Rais wenu mna rushwa kwanza ndo mje yanga
 
@Puto.Nimekunari mchango wako nikweli Kukodisha bado Mali yako Kwa asilimia mia moja Na mkataba were ndio unauandaa.Sasa Viongozi kuona wanakaa Na kuaandaa mkataba utakao mbana mkodishaji ili heshima ya Yanga iendelee Na

Kwenye terms za mkataba huo nashauri kuwe Na kipengele chakuupitia kila baada ya miaka Mitano Nakama mkataba utakuwa umekiukwa basi usitishwe Vipengele hivyo huweza kumfanya MPANGAJI awemakini Na anachotaka kukifanya ili kiwe Na mafanikio.[emoji574] Tuendelee kuwa wakimataifa wao(SIMBA) wanakebehi eti wanacha wayanga tutafaidika VIP huo ni Umaskini wa Mawazo kwani wao kama wanachama wafaidika Na nn had I hapo timu yao ilipo fikia wamechangia ? Mbona wameshindwa kuipeleka wanapotaka mwishowe wamegeuka kuwa kikundi cha ushangiliaji.

Wanachama Na wapenda Soka tunachotaka Duniani kote ni timu ishinde , icheze Soka safi Na tuchukue VIKOMBE. Hakuna Shabiki anayetaka kujaza tumbulake Kwa sasababu za Club hao Sio wanamichezo ni wachumia Tumbo.

Ilikufikia mafanikio hayo lazima watukamahao (manji) wawepo Na tuwaunge mkono.mpila wabongo utakuwa Na tuchacheza mashindano makubwa.

Jaribu kufikilia fedha alizo wekeza azam kwenye mpira wewe unafiri kunatimu za wanachama ambazo zingiweza kumpa presha azam ? Angejimilikisha Ubingwa wa ligi kuu .Ona manji alivyo amua kuwepesa yanga Azam ikapata kigingi Na Tanzania mbakasasa upinzani wa Soka ni Yanga Na Azam.

SIMBA nao wakipata MTU akaweka pesa kutakuwa Na gamekali sana dangote naye ashiwishiwe achukue ndada
 
Mi nasubiri Yanga asili wauwashe moto baada ya mwaka 1 mana hela waliopoozwa ni ndogo huku wajanja wameramba parefu...
 
Na wale wa msimbazi sijui tuaiteje na ile 20b..
Heri kukodisha kuliko kuuza.
Pale anamiliki sehemu ya hisa mzee. Hisa nyingine zinabaki msimbazi.

Hebu nambie jamaa amekodi... atalipia shingapi kwa mwezi??
 
Kukodisha na kupata chochote na kumpa bure kipi bora?
Hizo hisa alizonunua Mo, hela kapewa nani? Bado zipo kwake! Kachukua timu bure kuwa mali yake bado watu wanakenua meno.
Bei kajipangia na bado hela atakuwa nayo yeye mwenyewe.
Jengo na uwanja Bunju vitakuwa mali yake.
Ili Yanga au Simba ziwe kampuni Ilikuwa lazima kubadili katiba kwanza ili akina Mo wanunue hisa toka kwa wenye kampuni yaani wanachama!
Katika kikao walichokaa cha Kuikodisha Timu ya Yanga kwa Mkodishaji kati ya wateja wanaotaka kukodishwa Yanga na Wenye timu ya Yanga , Mtu mmoja aitwae Manji alihudhuria kikao hicho kama Mkodishwaji Mkuu (Tenant) na pia mtu huyohuyo alihudhuria hicho kikao kama Mkodishaji Mkuu(Landlords).

Akiwa kama Mkodshwaji Mkuu (Tenant), Mtu huyo aliweka terms za mkataba anaoutaka (proporsals) yeye mteja ambao alidhani kama Mkodishwaji Mfanyabiashara angefaidika nao, lakini Mtu huyohuyo mmoja akiwa kama Mkodishaji Mkuu (mwenyemali) ambae alitakiwa kufikiri kwa faida ya wenye mali wenzie alikubaliana na terms/proporsal zilizowekwa na mteja ambae nae ndio yeye yeye mwenyewe!!

Yaani katika Meza ya majadiliano iliyohusisha pande mbili za Landlord v/s Tenant, mtu huyo ikifika zamu ya Landrod kuongea basi anahamia upande wa Yanga na anaanza kuongea kama mwenyekiti na anatoa hoja, na ikifika zamu ya tenants kuongea basi nae ananyanyuka kwenye kiti na kuhamia upande waliko wafanyabiashara wenzake anaongea kama tenants Mkuu akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa mwenyekiti ambae ni yeye mwenyewe.

Na wakifikia makubaliano basi katika Mkataba mtu huyohuyo anasaini sehemu ya Landlord na anasini sehemu ya Tenants. Yaani Mwenyemali Mkuu ni yeye, na mteja Mkuu ni yeye pia,

Only in Tanzania, specifically at Kandambili F.C. a.k.a Timu ya Chama!!
 
Nothing is settled yet. Mkataba ataingia na Board of Trustees ya Yanga. Huko ndiyo details zitakuwa ironed out. Mbivu na mbichi ni huko. Wanachama wametoa blessings hayo yafanyike.
 
Nimemuelewa MANJI ana nia nzuri kitu cha muhimu ni uwazi naota kuanza kuona vitu vifuatavyo
1:YANGA FC TV
2:JEZI ZIKIUZWA KWA MPANGILIO MZURI NA WA FAIDA
3:bidhaa mbali mbali zenye logo ya YANGA FC
TIMU YETU ITATUMIKa kibiashara zaidi tuache wanao sema tuna kodisha timu ila baadaye wata tuonea wivu 25% ya faida sio mbaya kwani sasa ivi atuitumie club yetu ki biashara ila ni vema tukawekeana mkataba pia napenda tuiboreshe katika
1:mitandao website na social network page ziendeshwe na wataalamu
2:Magazeti yaongezeke
3:tuwe na kituo cha radio Jangwani fm
4:tuwekeze kwenye usafiri
5:kituo cha kulelea vipaji mbali mbali

ndoto hizo,yupo yanga leo mwaka wa 4 mbona hakuna hata moja? sasa mnamkabidhi yeye na faida ya wote hasara yake,lwa akili ya kawaida nani anataka hasara?
kuanzia zile free game za Mazembe na nyngine ndio wakati wakujilipa mlidhani anatoa bure,
 
Manji ana tabia za uchwara kabisa,maana hataki kuona mtu anampinga lazima avuliwe uanachama amzibe mdomo kabisa,
hapa yanga wamebugi,nadhanii wanahitaji muda zaidi kujadili jambo hili kwa upana wajue faida na hasara,lakini manji katumia mbinu za kimafia kwa kujua kuwa wanachama wengi vihiyo tu na watashangilia jambo lile,ili kuwajengea khofu wapinzani wake,Manji ni Dikteta kabisa sio uchwara
 
Habari za mwanzo ni ilikua nae atoe bilioni 25 kisha achukue 50% lakini mpango huo ukavurugwa na kigogo mmoja alietaka kutoa bilioni 65 kwa asilimia hzo hzo ndo ili kumvua huyo mshindani akaamua kujikodisha, swali linakuja hivi ndani ya miaka kumi akiishusha daraja je, akiamua kuitumia yanga kukopea hela benki je, tujiulize maswali kabla ya kumkubalia
sasa bil 25 ni sawa na bil 5 kwa mwaka mechi za simba fc vs yanga kwa mwaka zinaingiza bil 1
 
Unafki utawaua nyie mikia fc wa matopeni. Timu lenu linakufa kwa ukame wa vikombe mmekalia kushupalia ya Yanga. Hata huo mkataba wa kukodishwa hamjauona tayari mavi yanawagonga vyupi vyenu. Tuacheni wa kimataifa kama tulivyo hatuwahusu nyie. Nyambaaaaffff
Ubingwa wenyewe tunanunua wachezaji wanasajiliwa kwa pesa chafu wanalipwa pesa ndefu halafu tunawahonga wachezaji wa timu pinzani ili tushinde kirahisi halafu tunajisifu ujinga kuwa sisi wakimataifa
Timu tunakodisha kwa uoga wakupambana kama wanaume bora niendelee kushabikia ARSENAL
 
Mnafiki ww ulianza kuishabikia yanga lini hebu baki na hiyo mikia yako hapo msimbazi waache wenye jangwa lao wayajadili .amini Manji atapiga noti ndefu sana yanga kuliko hata anazopiga kupitia Quality Group ltd
 
Back
Top Bottom