Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Kwa mtu mwenye akili akili timamu hawezi asilali kukubali mkataba huo...
" eti ikipatikana hasara inabaki juu yangu ila faida club inapata 25% yeye 75% " seriously,? Wanachama wa Yanga wana akili timamu kweli ama walikua "intoxicated"??
We ni mwanachama simba?
 
tena jamaa anawaingiza chaka kwa akili kweli,faida ya wote hasara yake,waswahili tusivyopenda hasara na kupenda njia ya mkato hapo lazima tuingie tu kingi kiulainii
Wacha upotoshaji wewe,
Mchakato wenyewe huujui,umesoma mitandaoni unawahi huku jf kujidai eti nawewe upo.Tukikuuliza swali moja hutatujibu,haya tuambie katika uongozi wa yanga,we una nafasi gani?
 
mkuu asnte kwa kuntukana, japo nlitoa maoni kama mtu huru, nisamehe kama umekwazika na mchango wangu mkuu
Acha kununa bhana, sposi na kununa wapi na wapi? 'Taahira' ni kasoro tu. Kwa mfano, taahira ya macho (makengeza), taahira ya mguu (kilema) taahira ya mawazo (kudhani Yanga inaweza kushuka daraja), taahira ya siasa (kunyima wapinzani kufanya mikutano) na kadhalika.

Lakini tukitoka kwenye utani, kinachokuuma ni kuambiwa ukweli au kufungwa 2 x 2 = 6?
 
Acha upuuzi wewe ni nani alitaka kutoa bilioni 65? Mtaje hapa...Wewe umeshaichangia Yanga sh.ngapi?
Habari za mwanzo ni ilikua nae atoe bilioni 25 kisha achukue 50% lakini mpango huo ukavurugwa na kigogo mmoja alietaka kutoa bilioni 65 kwa asilimia hzo hzo ndo ili kumvua huyo mshindani akaamua kujikodisha, swali linakuja hivi ndani ya miaka kumi akiishusha daraja je, akiamua kuitumia yanga kukopea hela benki je, tujiulize maswali kabla ya kumkubalia
 
Ubingwa wenyewe tunanunua wachezaji wanasajiliwa kwa pesa chafu wanalipwa pesa ndefu halafu tunawahonga wachezaji wa timu pinzani ili tushinde kirahisi halafu tunajisifu ujinga kuwa sisi wakimataifa
Timu tunakodisha kwa uoga wakupambana kama wanaume bora niendelee kushabikia ARSENAL
Povu hilo, Mama Chiku na Family Detergent.

Wachezaji wako walihongwa na Yanga, je Toto Africa nao waliwahonga ndio wakawapiga kidude? Hebu funguka mwagito
 
Acha upuuzi wewe ni nani alitaka kutoa bilioni 65? Mtaje hapa...Wewe umeshaichangia Yanga sh.ngapi?
Acha ubwege wewe nikutajie nimetoa ngapi ili ufanyaje, au nyie ndo mashabiki maandazi akat hata sumni hutoi yanga sio ya kuikodi ila kama hujui history yake waeza sema hivyo sio kosa lako.
 
Nimemuelewa MANJI ana nia nzuri kitu cha muhimu ni uwazi naota kuanza kuona vitu vifuatavyo
1:YANGA FC TV
2:JEZI ZIKIUZWA KWA MPANGILIO MZURI NA WA FAIDA
3:bidhaa mbali mbali zenye logo ya YANGA FC
TIMU YETU ITATUMIKa kibiashara zaidi tuache wanao sema tuna kodisha timu ila baadaye wata tuonea wivu 25% ya faida sio mbaya kwani sasa ivi atuitumie club yetu ki biashara ila ni vema tukawekeana mkataba pia napenda tuiboreshe katika
1:mitandao website na social network page ziendeshwe na wataalamu
2:Magazeti yaongezeke
3:tuwe na kituo cha radio Jangwani fm
4:tuwekeze kwenye usafiri
5:kituo cha kulelea vipaji mbali mbali
Hahahahaha jangwani fm na pale dimbwini jangwani sea breeze
 
Hivi ili simba ifanye vizuri ni lazima waiombee mabaya yanga hata kwenye maswala ya maendeleo ya club?
 
Swali la nyongeza: Huu utaratibu unaotaka kutumika Yanga, ulishawahi kutumika katika uendeshaji wa timu gani duniani? Je ulifanikiwa kwa kiasi gani?
 
Tukiweka ushabiki pembeni tunakuta kuwa kitendo cha wana yanga kumpa Manji hizo asilimia 75 kwa kipindi cha miaka kumi kinawafanya waonekane ni watu wanaoongozwa na hisia za kishabiki katika kufanya maamuzi ni sio uhalisia.........
Sasa utapimaje ufanisi kwa kipindi cha miaka kumi...!!??
 
Nimefurahishwa na wanachama wa Yanga kumkubalia Manji kujikopesha Klabu ya Yanga kwa asilimia 75% huku wanachama wakibaki kuhudhuria mechi tu ambazo klabu yao itakuwa inacheza na kushangilia ikishinda au kuzomea ila hawatakuwa na sauti hata kidogo ya mwenendo wa klabu yao. Manji akiamua Yanga ipate matokeo mabaya hakuna wa kumpinga, kwani wanachama hawatakuwa na sauti.

Nilitegemea wanachama wa Yanga wangekubaliana kuwa Manji auziwe hisa tena asilimia 50% na zilizobaki ziwe za wanachama ili pande zote mbili zishiriki kwenye maamuzi ya Klabu, lakini kwa utaratibu wa kumkopesha Manji kwa asilimia 75% wanayanga make mkao wa kulia tu hamtakuwa na maamuzi kwa miaka 10 bora mngempa hata miaka 5 kwanza ya majaribio.

Amejikopesha bure au??
 
Back
Top Bottom