Hatimisho: Nimefika salama Marekani

Invigilator

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Posts
3,203
Reaction score
5,997
Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kukamilisha ndoto zangu.

Pili napenda kuwashukuru wadau wakubwa humu jukwaani kwa support kubwa ya mawazo tangu nilipoweka nia ya kuondoka nchini kwetu, Mungu awabariki sana (wote mnaotambua uwepo wake na utendaji kazi wake).

Kwa kutaja baadhi, Bufa Kiranga Matola Smart911 na wengine wengi.

Hakika USA ni nchi ya ajabu sana, ni nzuri kwa namna ambayo siyo rahisi kusimulia kwa maneno, miundombinu mizuri sana kila kitu ni kizuri sana tofauti na kwetu, wameendelea sana (sidharau kwetu nasema uhalisia).

Nilianza safari yangu, kutoka Dar hadi Schiphol airport - Netherlands kwa KLM, kisha Amsterdam - JFK Airport New York kwa Delta.

Kutoka hapo, nikachua bus (42nd Port Authority, gate 66, Greyhound, kuelekea Pittsburgh - Pennsylvania. Kutoka hapo nikabadilisha gari hadi Columbus Ohio.

Namshukuru Mungu nimefika salama, nimepokewa vizuri, nina furaha, kwa wajuzi na wenyeji huku naombeni mnipe mawazo ili iwe rahisi kwangu kupata michongo na kutimiza adhma ya moyo wangu.

Natamani kubaki huku baada ya kumaliza course yangu ya miaka 3, nitafurahi ikiwa mtanisaidia njia zaidi ndugu zangu.

Niwasisitize vijana wenzangu tupambane tu haijalishi kipindi gani tunapitia, ikiwa umeweka nia thabiti Mungu hawezi kukuacha, juhudi na maombi huleta fanaka.

Ahsante sana.View attachment 2358267
 
Umekomaa asee

Mimi imenichukua miaka 5 toka nia hadi kutua Canada

Cha msingi Mungu atukumbuke

Kazi zipo za kutosha, nina wiki 3 sasa, nimepata kazi 4 zote full time job. Mpaka nashangaa

Cha msingi Usije jaribu kukiuka vigezo na masharti mzee hasa ya 20hrs per week kwa mwanafunzi kufanya kazi
 
Mkuu Invigilator I couldn't be happier for you. Hongera sana na karibu kwenye nchi ya maziwa na asali. Land of the free and home of the brave. Sasa umevua gamba na umekua brave 🤣

Michongo ipo mingi na kubaki inawezekana kabisa hata sisi tulikuja kama wewe ila hadi leo tunadunda hapa bongo tunaenda tukimiss kupigwa vumbi tu.

Aluta Continua.
 

Hivi kwa Marekani ukitaka kubaki baada ya shule kuna process gani za Immigrarion
 
Sawa mkuu.
 
Ahsante sana Mzee umenisaidia pakubwa mno,una moyo wa dhahabu sana.
 
Hongera Kwa kuingia land of opportunity USA.

Utakuwa ni kichaa tu ukiishi sehemu miaka 3 ukose maarifa ya kuextend ukaazi wako, utakuwa na tatizo kichwani.

Usiache kufuatilia video za EBM jamaa amedevort muda wake kutowa mwongozo halisi hata ukiwa ndani ya Marekani, mmfolow Facebook na YouTube utapata mwongozo mzuri.

Muhimu kuliko vyote Sasa tafuta new connection, unasoma na watu tofauti utakuwa binadamu wa ajabu kukosa marafiki wapya miongoni mwa wanachuo wenzanko.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…