Invigilator
JF-Expert Member
- Aug 16, 2016
- 3,203
- 5,997
Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kukamilisha ndoto zangu.
Pili napenda kuwashukuru wadau wakubwa humu jukwaani kwa support kubwa ya mawazo tangu nilipoweka nia ya kuondoka nchini kwetu, Mungu awabariki sana (wote mnaotambua uwepo wake na utendaji kazi wake).
Kwa kutaja baadhi, Bufa Kiranga Matola Smart911 na wengine wengi.
Hakika USA ni nchi ya ajabu sana, ni nzuri kwa namna ambayo siyo rahisi kusimulia kwa maneno, miundombinu mizuri sana kila kitu ni kizuri sana tofauti na kwetu, wameendelea sana (sidharau kwetu nasema uhalisia).
Nilianza safari yangu, kutoka Dar hadi Schiphol airport - Netherlands kwa KLM, kisha Amsterdam - JFK Airport New York kwa Delta.
Kutoka hapo, nikachua bus (42nd Port Authority, gate 66, Greyhound, kuelekea Pittsburgh - Pennsylvania. Kutoka hapo nikabadilisha gari hadi Columbus Ohio.
Namshukuru Mungu nimefika salama, nimepokewa vizuri, nina furaha, kwa wajuzi na wenyeji huku naombeni mnipe mawazo ili iwe rahisi kwangu kupata michongo na kutimiza adhma ya moyo wangu.
Natamani kubaki huku baada ya kumaliza course yangu ya miaka 3, nitafurahi ikiwa mtanisaidia njia zaidi ndugu zangu.
Niwasisitize vijana wenzangu tupambane tu haijalishi kipindi gani tunapitia, ikiwa umeweka nia thabiti Mungu hawezi kukuacha, juhudi na maombi huleta fanaka.
Ahsante sana.
View attachment 2358267