Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Bmx ulianza kuleta habari hii kwa kutuom a tukupe ushauri hivyo basi maliza story yote haraka kusudi tuone na tutafakari namna ya kukuoa ushauri
 
BM X6 kongole kwa kutupunguzia arosto, ila katika episode hii baada ya kuona caryn amehamia mjengoni akili yangu ikahamia kwenye "KULA TUNDA KIMASIHARA", Hivyo nimesoma haraka haraka mkuku mkuku kidogo nijikwae, nikitaraji kukutana na hiyo scene lakini nimetoka kappa!

Nasemajeee, kukosekana kwa hiyo scene arosto ndio imezidi. [emoji2817]
Labda itakuwepo mbele ya safari, huwezi jua
 
Lazima aambiwe ukweli bhana ili ajue, mbona wasanii huwa tunawadai nyimbo Sisi mashabiki? Unadhani huwa tunawalipa kutupa huduma ya muziki?

La huwa hatuwalipi lakini mwisho wa siku huwa tunawadai na wanajitetea kwetu kwa kutupa kile tukitakacho.

Mfano mzuri ni Alikiba. Alikiba aliwahi kuwa kimya Kwa kipindi kirefu kiasi hadi mashabiki wakawaka na hatimae akaja na mangoma ya kila aina na moja ya ngoma ya kwanza kuachia ilikuwa inaitwa 'Mwana Dare es Salaam' kisha zingine zilifuata. Unadhani mashabi tungekaa kimya angesanuka? La hasha asingesanuka mwishowe pengine angepotea.

Ukiwa msanii wa Sanaa yoyote na ukiwa chumbani kwako hujafahamika mathalani, wewe hudaiwi na mtu. Lakini ukatoka nje kwenye hadhira nayo hadhira ikakukubali, basi lazima udaiwe tu. Hii ndio maana halisi ya huyu msanii wetu bwana BM.

Bwana BM tayari yupo nje na hadhira inamtazama, ameifanyia uraibu mkubwa hadhira hiyo na hainabudi kumdai kazi yake aliyoianzisha.

Vuta taswira Hayati Mh.Mkapa angefariki bila kumalizia hadithi ya Maisha yake aliyoisimulia kitabuni unadhani tungemuelewa? La hasha asiingeeleweka ila kwavile aliimaliza basi hamna deni.

Hivyo basi huyu bwana BM inampasa kuituliza hadhira hii kwa uraibu mkubwa iliyonao.
Atusimulie amalize. Aweke vipande hata vinne ili akiondoka hata wiki mbili kusiwe na shida, lakini eti tu kipande kimoja halafu anatokomea karibu majuma mawili aaa siyo sawa kabisa.
Masimulizi ni true story hivyo inamlazimu BM X6 muda wa kukusanya matokeo, kuandaa hadithi, kuihariri na kuturushia
 
Back
Top Bottom