Caryn anajua wewe uko na mtu. Na Carln anakupenda sana,toka kitambo. Mengi ameyaonyesha toka kitambo mapenzi yake kwako. Na ndio maana akakuchezeshea ili usiwe upande wa Acauntant.
Sasa kwa mawazo yangu acha akupambanie kivyake nae. Endelea kukaza kama mwanzo. Tena zidisha ugumu. Najua pamoja na mzee kumzuia kuanzisha uhusiano na wewe lakini yule binti kajifia kwako na mapenzi daima yana nguvu kuliko chochote. Hivyo atajitahidi sana kujizuia ikiwa ni pamoja na kukumbuka ushauri wa mzee. Lakini mwisho wa siku atashindwa ataamua tu yeye mwenyewe kuwa wazi mpaka kwa mzee kumwambia jinsi gani anakufeel.
Potelea kokote ngoja tubet kwa Caryn mdogoangu. Huyu ana mambo mengi ya kutusogeza mbele.
Nimesoma pia comments za wengi,wamenukuu usemi wa mzee kwa Caryn,kwamba mapenzi yakiyumba hata mambo mengine kikazi yanavurugika,anakuwa amekupoteza mtu muhimu. Kwa akili za Caryn ana hofu na hilo pia,lakini kwa ile lugha tu kama kuna lolote nakosea niambie. Hapo tayari ameanza kuunda namna ya kujibadirisha kitabia. Naamini hata mapenzi yakiharibika haiwezi kwenda mbali mpaka kukuvurugia kikazi,wakati huo tayari unakuwa na mizizi kwenye kampuni Ikiwezekana akifungua.
Mbali na hivyo tayari na sisi tutakuwa tuna back up,either tutakuwa tumefungua ofisi yetu kificho,au tuna mtaji mwingine. Isitoshe tayari tuna mtaji mkubwa jamaa yetu yuko China. Tukifungua ofisi yetu jamaa China atakuwa anafanya na kazi yetu pia. Twende na Caryn.