Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

BM story haijaisha Mana hujatuambia jibu ulilompa carren baada ya kusema kuwa atabadili tabia ambazo huzipenda na kuwa Yuko tayar kukuvumilia
Hadi nawapigisha kura hapa hujajua tu nimemjibu nini?
 
Hahahaha hii comment imenichekesha sana
 
Caryn ni aina ya wale wanawake Wanajuaga ku adapt na mazingira, so hata misimamo yake ya ajabuajab nikwa Sabab ya aina ya uhusiano mlionao (marafiki), mkiingia kwenye huba atabadili frequency kuwa kama mke, Tena uzuri yeye ndie amekupenda kwanza, Cha zaidi caryn ana kila kitu knachompasa mwanamke kua nacho bro, kama ni kuhusu tabia na misimamo yake ameshaahidi kubadilika, na hata kama wanaomzunguka wanaona hawez kubadilika basi jua hilo litawezekana kupitia penzi, nadhani unajua penzi lilivo na nguvu, kwa Sasa Naweza kusema kwa Sabab Annie Yuko mbali basi Caryn ni sawa na fisi unaemjua lakin Annie ni sawa na kondoo usiemjua coz huko aliko hujuw Nini kinaendelea, bnafsi huwa naamini nnachokiona[emoji120]
 
Unapigisha watu kura ambazo kwa huyo Annie umemuelezea kiasi kidooogo sana, hatujui mlikotoka ups n down zenu tujue zikoje toka mwanzo, huyo Carryn vijana wenye hawajakaa kwa ndoa watampenda sababu ya mseleleko.......na mkiingia kwenye mahusiano ya kimapenzi haimaanishi lazima mfikie marriage, mnaweza kuwa vizuri kwenye urafiki ila mapenzini mkazinguana hata msifike tank bovu🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nasema hivi " ukianza mahusiano ya kimapenzi na carryn mgombane muachane kwa aibu kubwa na kila kitu upoteze" nimekufokea na laana juu
 
Oyah Kiduku 42774277 shusha ego chini then vote
Dah sikutaka kucomment ila ngoja tu nicomment.

Sijajua kama kumbukumbu zangu zipo sawa ila namuona Annie kama mtu wa ndio mzee. This is my only problem kwa Annie[emoji777].

Pia kitu Kingine ambacho sijajua kuhusu Annie, Sijui anabehave vipi akiwa na pesa, Na kama hajawahi kuwa na pesa(Pesa nyingi) Siku akizishika sijui atabehave vp?

March 2020 nikiwa Kenya, niliingia kwenye uhusiano na Dada mmoja hivi, Japo nilianza kufahamiana naye toka 2019 yeye alikuwa anasoma mwanza, Ni mtu wa Moshi. Huyu tumwite X.

X ni type ya wanawake ambao wanaume wengi wanatamani kuoa, hata mimi nilikuwa nawaza hivo, kwanza mpole, hana maneno mengi, beside kuwa mchaga lakini hakuwahi kuwa ombaomba, Ni mtu ambaye hakuwa na tamaa, Pia alikuwa na huruma sana.

Nakumbuka kuna siku nilikosea kumtumia hela badala ya kutuma Mpesa 22k nikatuma kama Vocha, Aiseeee aliumia sana mpaka tena me mwenyewe nikaanza kumuonea huruma, ingawa nilikuwa nineshatuma 22k nyingine.

Maisha yakasonga, August 2020 nikaanza kujisogeza kwa dada mmoja hivi,

Huyu alikua UDOM na nilianza kufahamiana naye toka 2018, Kiukweli lengo la kumtongoza huyu Dada ilikuwa ni kumla tu, Maana umbo lake kila nikimuona status whatsapp nilikuwa nadata sana. Huyu tumwite Y.

Y alikuwa anapenda sana utani, na hii ndio ilikuwa gear yangu ya kumuingia, Nilianza kumuita Romantic names kama utani, na yeye akawa ananiita hivohivo, mwezi wa 9 tukaja tukaonana, maisha yakaendelea na mpaka kufika december 2020 lengo langu likawa limeshatimia,

Huyu Y toka tukiwa marafiki alikuwa anaomba sana Pesa, Lakini ilikuwa ni katika utani so sikuwahi kumtumia, nilipoanza kujisogeza kwake kuna vitu kweli nikawa nampa hela na vingine napotezea. Mfano 2020 october alipoteza simu, me nikamnunulia simu nyingine, Pia kuna blanda alifanyaga huko Chuo me nikamfinance tu bila shida.

Mpaka 2021 inaanza huyu Y alikuwa ni very different person, Kwanza nilimkuta yuko sealed(Aiseee hawa wadada wanaopost memes waoneni tu hivihivi, wanaficha mengi). Kiufupi tu nilianza kufall mazima pia kwake. Japo huyu ni muongeaji kiukweli.

Sasa nikawa na watu wawili wote niko nao sambamba. Kibarua kama Chako cha sasa. [emoji23][emoji23][emoji23].

Late April 2021 nikaenda mwanza kwa X, nikaspend naye almost week nzima. It was my first time kuwa naye pamoja tangu nimtongoze. Things went very well. I saw X as more wife material kuliko Y.

At the same time, Niliona Loop ambayo naweza kumwacha Y japo kwa kosa la kutunga ila nilisuka mpango in such a way yeye ndio angejiona mkosaji.

Ipo hivi the moment nmemnunulia simu Y, hiyo simu nilikuwa naitrack na kuona Message zake, Calls, whatsapp text, pictures n.k. Nilifanya hili ili siku nikitaka kumuacha niwe na escape route. Ambayo hatokaa anilaumu kwamba nimemchezea na kumuacha.

Honestly demu alikuwa Loyal sana kwangu, masela kibao walikuwa wanaslide DM kwake ila alikuwa anawachomolea au kutowajibu kabisa.

Kuna picha nilizipata alipiga na mshikaji mmoja hivi, sasa hizo picha nilizitunza hiyo April, nikatengeneza fake whatsapp conversation kwamba kuna mtu anasema wewe ni mtu wake na amenitumia hizi picha na nikamind sana. Kiukweli hakuwa mtu wake,

Weeee demu akakaza, akasema yule siyo mtu wake, nikamuambia we umeamua kunidanganya, sikua ukiwa ready kuopen up tutazingumza, Bhana eeeeh tukapotezeana mwezi mzima,

Kiukweli nilijua ndio tumeachana, nikaendelea zangu na X, Mwezi mmoja baadae Y akaanza kunicheck Me nikawa namuignore, Alikuwa anataka sana tukutane tuyajenge na yale yaliyotokea aliamini tu kuna mtu alimzunguka na kutuma hizo picha kwangu,

Nilimkazia mpaka 09/2021 ndio tukaja tukarudiana, Honestly huyu mtu niliona ananipenda kuliko nilivyokuwa namuwazia. Basi nikaendelea nao wote wawili.

Sasa kuna kuna kitu kilikuwa kinanipa shida kwa X, Ni mtu asiyejali, Urudi saa 8 usiku nyumbani sawa, usafiri uende mkoa hatokuuliza chochote, kwamba ulifika salama, conversation zetu ziko very short, No stories between us labda mara mojamoja sana akiwa na mood. Hata calls zetu ni dakika moja au mbili. This was a redflag to me. Na yuko hivi toka nimeanza kumjua.

Mwaka jana mwezi wa 9 kuna siku niliongea naye muda mrefu sana kama Dakika 40 hivi, sijawahi kuongea naye muda mrefu hivi. Aiseee hii simu ilibadili mtazamo complete kuhusu X, Kuna vitu alijikoroga akaongea akaexpose attitude yake. Nikamuona kabisa huyu ni wale wanawake wa 50% 50%.

Kuanzia hapo nikaanza kukaa chonjo, Mwezi wa 12 nikaacha kabisa kumtafuta, na hajawahi kuniuliza chochote, tumeshaongea kwenye simu mara kadhaa na kuchat whatsapp mara kadhaa. So kwa sasa simuhesabii.

Nimebakia na Y, Last year alikula kitengo mahali, Yupo financially good na ameshaniback up sana baadhi ya vitu, Mungu akipenda mwezi 8 ntaenda kumtambulisha Home.

So narudi kwako @BMX6 angalia strength na weakness za kila mmoja, mwisho siku fanya maamuzi kwa usahihi.

Kuhusu Careen, Watu wanaosema kwamba hamtawezana sababu ya Attitude yake napingana nao, Hiyo attitude aliionesha wakati ambao hamkuwa kwenye mahusiano.

Hiyo kauli aliyosema kwamba "kama kuna vitu huvipendi kwake umwambie na yupo tayari kujirekebisha" Ina maana kubwa mno, Usiichukulie kurahisi.

All in all kila la heri mkuu, Usikurupuke kwenye maamuzi yako.

Sorry kwa post yangu ndefu.
 
Nakumbuka kisa kimoja cha jamaa kuwapa pesa wa chumba wake watatu ili apime uwezo na busara zao kisha amuoe mmoja, jamaa akawapa pesa wa chumba wake ambao hawajuan kisha aka akawambia Ana safiri kwa mwaka mzima 34

Mke mmoja huyu Ali wekeza ile pesa badae a kanuna kiwanja akajenga nyumba ya kisasi Lakin Hati na kila kitu jina la mme wake,


Wapili yeye akafungua biashara ikakua aka sev pesa bank ikawa Mala tatu ya ile

Watatu yeye alikula Bata ikaisha

Jamaa alipo rud kila mwanamke aka mweleza jamaa kilicho tokea.

Lakin unajua kilicho tokea? Jamaa aliamua kumuoa mwanamke mwenye matako makubwa as we know Kati Yao mwenye matako makubwa msha mjua

Annie ndio wife material kula yangu kwake.
 
Caryn huyu anawezakukufanya uishi kwa majuto sana Annie ndo aina ya mwanamke anakufaa seems Yuko humble sana
 
Another Day! Another Sunday! I hope wote wazima, kwa wagonjwa Mungu awafanyie wepesi

Jana kuna mida niliopotea humu sikupata nafasi ya kupiga kampeni kuna vitu nilikuwa naweka sawa, inshort nilikuwa nafanya mfanya mchakato wa kuhama lakini bado sijafanikiwa, hii Idea nimeipata humu baada ya kuanzisha zoezi la kupiga kura, Wengine waona kama kupiga kura ni changamsha Genge tu, Hapana! hizi kura zinasaidia, na zimeanza kunisaidia sasa hivi

Katika kura hizi Kuna watu wanatoa maoni na shauri, Nadhani ilikuwa Day 1 kama sio Day 2 ya election kuna members walipiga kura, kura zao hazikuwa dry, walitoa na ushauri vile vile, na ushauri wao ndio umenifanya nichukue maamuzi ya kuhama,

So kwakifupi Kesho au kesho kutwa naweza nikahama. Uzuri rent yangu ndio ilikuwa inaisha mwezi huu hivyo Ushauri umekuja Wakati sahihi

So endeleeni kupiga kura, mpiga kura unaweza kuona kura hazisaidii lakini kwangu kwa kiasi Fulani zinasaidia tena zile kura zenye ushauri

Kuanzia Sasa hivi hizi kura nazi count kwa utofauti, hizi kura Dry mf mtu ana mention tu jina la Candidate nitazi count once na zinabeba asilimia 30 tu ya maamuzi nitakayoyafanya, ila hizi kura zenye ushauri, tena nyingine zimebeba maoni yenye hisia aina ya kura hizo nitazi double Count, na zitabeba asilimia 70 ya maamuzi nitakayoyafanya

Kwa maana hiyo nitapitia upya kura zilizopigwa kwa Candidates wote wawili na kuanza kuzihesabu upya, so msije mkashangaa kwa matokeo mtakayoyaona

Mfano Comment namba 3412 haikuwa tu kura kwa Candidate aliyepigiwa kura bali pia kuna Maokoto, Kura ya aina hiyo naipa uzito kwa 70% haiwezi kuwa kura ya kawaida sawa na mtu aliye mention tu jina la Candidate

Mfano mwingine ni Comment namba 3450, japokuwa muhusika alisema niihesabu kama kura iliyoharibika lakini Mimi nikaihesabu kama kura kwa Candidates wote maana kama ningeihesabu kama kura iliyoharibika nisingeitendea haki kwakweli

Eniwei! Kwa ambao hamja-vote endeleeni kupiga kura, Matokeo ya jana nitayachanganya na ya leo
 
Asante sana, Aina hizi za kura ndio nitazi double Count

Vote counted to Caryn
 
Mzee wangu tangu ile story ya Hamida sijawahi kukusahau..
Nakusalimu
 
Ni sawa tu, lakini mm mwenyewe sijajua nitaingia kwenye mahusiano na nani, kwasababu Annie mwenyewe kabla ya kuendelea nae kuna vipengele itabidi niviangalie kabla sija renew mkataba wa kuwa nae tena siunajua tulikuwa hatupo karibu muda mrefu

So nitaangalia vipengele vyangu halafu nitaangalia na kura/maoni ya humu ili kukwepa kufanya maamuzi ya kibinafsi

Pengine labda mwenzangu alivyokuwa Mwanza hakufanya maamuzi ya kibinafsi so mimi nikija kufanya maamuzi ya kibinafsi pengine hiyo laana yako na yake ndio inaweza kunipata,

Kwa Caryn pia ni hivyo hivyo Kuna mambo nitaangalia na nitachungulia kura za humu zinasemaje kumuhusu ndio nifanye maamuzi

Eniwei! Nadhani hii kura umempa Annie bila shaka
 
Ukimaliza kukusanya kura ndio utaleta next episode au ndo umemaliza tufanye ku unsubscribe uzi?
 
Nice Kiduku, umetiririka vizuri umenyoosha kama unavyonyooshaga kwenye ICBM

Nimependa kura yako umei direct kwa Caryn Lakini umeniachia ulingo nipambane mwenyewe

Vote counted to Caryn [emoji294][emoji294]
 
Aysee, Haya bhana

Vote counted to Annie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…