Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Ukimaliza kukusanya kura ndio utaleta next episode au ndo umemaliza tufanye ku unsubscribe uzi?
Sijajua kwakweli, sema unaweza uka Unsubscribe tu nisije kukupa Ahadi feki bure
 
TAHADHARl, vipepeo weusi haiishi itakupa alosto tu[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami ngoja nitoe ushauri wangu kutokana na experience iliyowahi kutokea huko nyuma ,wanawake hawaaminiki, sisi wanaume tunaweza kucheat lakini huwez kumsahau mke wako ,wanawake hawapo hivyo .
Nakushauri nenda kwa caryn ,naamini kama umeshatembea nae ulimkuta sealed pia ,but hutakiwi kukurupuka kumuacha Annie mtafutie sababu ,.
Mwanamke mnaweza kupitia ups and downs kibao lakini akaja kukuacha kwa sababu isiyo na mashiko kabisa
Utapofanya maamuzi fanya maamuzi ya maisha ,mapenzi tu hayatoshi .
Fanya maamuzi sehemu ambayo uta grow ,fanya maamuzi sehemu ambayo Kuna future
Kwa carryn utajifunza mengi kuhusu biashara na hutojutia .
Good luck

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Asante sana kwa ushauri mzuri, hizi ndio aina ya kura ambazo nazi double Count


This vote counted to Caryn [emoji294][emoji294]
 
Hii story nimeianza juzi nasonga nayo,sema nasikitika nimemaliza (episode 12 season 2 ikaja episode 15 season 2)[emoji22]sijajua izo mbili zimefutwa au zimerukwa?ngoja niendelee nayo tu sina namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii stori nilikua nayo bega kwa bega toka ilivyoonza......!

Nikupongeze bmx6 kwa kuamua kushare nasi hii banger, kiukweli tumeburudika na kujifunza vingi mno.

Sijawahi comment ila nilikua msomaji na mfuatiliaji mzuri tu,

sikua na huo mpango, ila kuna kitu kimenisukuma na kuhisi kama nami nahitaji kutoa mtazamo na fikra zangu...!

Tuanze kuwachambua nyie watu watatu tuone yupi anamfaa yupi.

kulingana na ulivyojieleza na kuwaelezea kwenye hii stori...! Yaani bmx6,carren na annie

1. BMX6
anaonekana ni kijana mstaarabu sana, mwenye heshima, mwenye utu na asiye na makuu..!mchapa kazi(akipewa kazi anahakikisha anaifanya vyema na kwa uadilifu) .Ni aina ya mtu ambae hapendi mambo meengi sana(nice guy). Ni kijana ambaye akiwa kwenye mahusiano ni loyal na mtulivu.

Madhaifu yake> hana misimamo thabiti(anayumbishwa yumbishwa), akipenda hutumia hisia zaidi kufanya maamuzi kuliko akili

2. CARREN
Ni mwanamke mwenye misimamo thabiti isiyoyumbishwa kirahisi, anajua nini anataka katika maisha, mwenye huruma kiasi, mchapa kazi na anajiamini sana.

Madhaifu yake> ni mwanamke mbinafsi anayejiangalia yeye bila kujali wengine, ni manipulater Mzuri sana, sio muaminifu wala muadilifu katika kazi(kufungua miradi bila kumshirikisha mzee, ikiwa mzee anamuamini sana)

3.ANNIE
Ni mwanamke mpole asiye na makuu, anayejali na kuguswa na matatizo ya watu wake wa karibu, ana tabia za kikike(feminine), she is a family oriented woman

Madhaifu yake> anaonekana ni mwanamke wa yes kwa vitu vingi( sio mdadisi), amepoa yaani hana vibe anatakiwa achangamke kidogo, sio mwepesi wa kuelezea hisia zake kwa urahisi ( jinsi anavyojisikia)

Kwa kuangalia uchambuz wa kila mmoja hapo juu tuone nani anamfaa bmx6 kulingana na tabia zao...!

1.BMX6 na CARREN
Hawa watu wawili tukijaribu kupima uzani wa upendo miongoni mwao...

utagundua ya kuwa bmx6 anampenda sana carren.. kwanini, kwanza mwenyewe kakiri hapa ya kuwa tokea alivyomuona alimpenda(love at first sight).

Pili bmx6 alivyoanza kuzoeana na carren mara nyingi alikua nervous wakiwa kwenye mazungumzo, kiasi kwamba mpaka carren akagundua bmx6 hana confidence kama alivyokua akiamini..! Ki kawaida ukimpenda sana mtu na ukiwa hujamzoea, alafu mkawa kwenye maongezi unajikuta tu automatic unakua nervous

Tatu bmx6 amekua akisikiliza na kufuata sana ushauri wa carren kuliko wa mtu yeyote ndani ya muda mfupi waliofahamiana....!

Carren anamuamini sana bmx6 ila hana upendo nae kama wengi na bmx6 mwenyewe wanavyodhania... kwanini

Kwanza mwanamke aliyependa yuko radhi kufanya chochote kwa ajili ya ampendae..!

Lakini carren amekua anafanya kinyume, wakati bmx6 anataka kuacha kazi kwa mara ya kwanza alimuomba ushauri Carren ambaye alikua mtu sahihi sana wa kuweza kumpa ushauri utakaomsaidia na kumvusha bm kimaisha...! Carren alijua kampuni ni ya baba yake ila hakutaka kumsanua bm, angekuwa kweli amempenda angemuibia siri na kumweleza ukweli wote...! Badala yake alimpa ushauri uliopelekea bm kuacha kazi na ajabu ile nafasi akapewa Carren. Na mzee tokea hapo akaanza kumchukulia bm poa na kupelekea mzee kumwondoa kwenye kundi la watu wake muhimu( hapa mkuu bm jaribu kukumbuka hili tukio then jiulize Carren anakupenda kweli??? Maana ushauri wake hapa kiukweli ulikuathiri pakubwa)

Pili mwanamke aliyependa hayuko tayari kumpoteza ampendae kwa gharama yeyote ile......!

Carren kwake ni tofauti kabisa yuko tayari kumpoteza bm, maana alikustopisha kazi kwa week kukuonyesha tu ya kwamba yuko tayari kukupoteza na hilo kwake sio ishu. Utasema mbona hatukua kwenye mahusiano, ukweli ni kwamba mwanamke akishapenda hata kama bado hamjaingia kwenye mahusiano atakua anafanya vitu kama vile mko kwenye mahusiano, maana yangu ni kwamba atakua anatumia hisia zaidi kwa ampendae kuliko akili, ila tumeona kwako Carren akitumia akili zaidi kuliko hisia

Tatu mwanamke aliyependa yuko tayari kumsaidia ampendae kwa yaliyo ndani ya uwezo wake...! Alikupa gari yake kwa bahati mbaya ukaenda ukagonga( hukupenda ila ilitokea bahati mbaya) lakini alikubadilikia mbaya,ukaingia gharama kubwa wala hakujali mwana ndo kwanza unajitafuta akuchangia hata nusu gharama.( jiulize anakupenda kweli au anataka akutumie kufanikisha malengo yake)

Nne mwanamke akipenda anakua na kahofu fulani hivi anapokua mbele ya ampendae.... Carren kwako anakua very comfortable, mpaka anapata guts za kukusema unakojoa bila kuflash, na ukizingatia uko kwako, damn bro, what the fu*k*.....! Mlilala kitanda kimoja mpaka asubuhi bila kufanya chochote, ni ngumu sana kwa mwanamke kulala kitanda kimoja na mwaume anayempenda kwa mara ya kwanza mpaka asubuhi bila kufanya chochote

Kwanini umchague carren
1. Ni mwanamke mpambanaji na mwenye maono ya mbali, mtafika mbali kichumi kama familia.

2. Ataweza kuitunza familia hata kama haupo in any case...! (Watoto watakua safe financially)

3.sio rahisi kuliwa nje, unless apende mwenyewe ( wanawake aina ya Carren hawatoi nyuchi hovyo)...! Sio maharage ya mbeya

4.Anakuamini sana miongoni mwa watu wake wa karibu

5.utapata watoto smart and sharp

6.unampenda kwa dhati, hence nafsi yako itakua na faraja ukiwa nae. Na hauko tayari kumpoteza kwa sasa

Kwanini usimchague Carren
1.hana upendo wa dhati na wewe, ila tu anakuamini sana baada ya kukufanyia majaribio mbali mbali na kujiridhisha ya kuwa wewe ni mtu anayekuhitaji kufanikisha mambo yake...! Kumbuka mahusiano msingi wake unatakiwa kuwa upendo wa dhati baina ya pande mbili

2.ni mbinafsi, rejea jinsi anavyomfanyia dada ake kwa kumchongea kwa mzee ili yeye aonekane bora zaidi, ilihali yeye mwenyewe ana mapungufu yake mengi tu

3.hatoweza kuyavumilia mapungufu na makosa yako ya kibinadamu, rejea kisa chake na Michelle walikua marafiki sana ila alivyomkopesha pesa na Michelle kufanya aliyoyafanya, mwenyewe unajua kilichotokea...! Kama dada yake aliweza kumchukulia vile alivyomchukulia kisa pesa unadhani kwako itakuaje? Au labda unaweza kuwa special sana ikawa tofauti. Japokua amesema atakuvumilia ila siku zote (actions speak loud than words)

4.ni mtu ambaye yuko attached mno na pesa pamoja na vitu( yeye ndo anapenda aendeshe jeep la mzee ikiwa mzee hayupo na si Michelle wala mama ake), alikuita mahali akaagiza juice, na we ulikua na njaa ukaagiza msosi, kilichotokea ilikubidi ulipie msosi wako bila kupenda, sababu ulikutana na Carren anayeijali pesa mno kuliko undugu,urafiki na mahusiano,

5.hana sifa za kuwa mama bora wa watoto wako...! Wanawake aina ya Carren huwa si wazuri katika malezi ya watoto. Wao huwa wako obsessed na kazi zaidi

1.BMX6 NA ANNIE

Annie anampenda sana bmx6, sababu aliweza kumsaidia kipindi kwao maisha safi kwa hali na mali, hakujali bmx6 alikua na hali gani.

Annie anamheshimu bm, maana amekua akimsikiliza kwa kila anachomwambia. Alipata kazi mwanza akataka aende bm akamzuia akatii, baadae bm akabadili mawazo akamwambie aende tu akatii

Annie hakua tayari kumpoteza bm, alipambana kuhakikisha bm wake hachukuliwi na accountant...!

Bmx6 hampendi kiivyo annie ukilinganisha anavyompenda Carren..! Maana hata kabla ya kukutana na carren bm alikua akimfanyia annie vituko vya hapa na pale, ila Annie alivumilia

Bmx6 anamuonea huruma annie na kuhisi guilty juu yake, sababu ya wema aliomtendea hivyo anataka amtafutie sababu ndo amuache...!

Kwanini umchague Annie
1.ni mwenye huruma hivyo atakua mtulivu kwako

2.Anakupenda kwa dhati( japo sidhani kama bado anakupenda kama mwanzo)

3.atakua mama bora kwa watoto wako

4 .atakujali na kukuheshimu kama mume wake

5.atakusikiliza, hivyo mtakua na maelewano ndani ya nyumba

Kwanini usimchugue Annie
1.humpendi kwa dhati, hivyo nafsi yako haitokua yenye furaha ukiwa nae

2.ni rahisi kuliwa nje, wanawake wapole wapole wakipataga mwanaume atayewachangamsha na kuwafurahisha hujikuta wanaliwa bila kutarajia ( inawezekana hata huko mwanza kuna ngosha ashafanya kweli, tehetehe natania tu)

3.hana mawazo mbadala, sio mwanamke wa kuuimiza kichwa anayeweza kukupa ushauri ukakuingia kichwani. Kiufupi hana ushawishi

Mwisho: combination yako na Carren kwenye kazi is awesome bro...! Ndo maana hata mzee alipenda sana iendelee kubaki hivyo. Maana anamjua vyema mwanae na wewe ameshakujua vya kutosha, na "you must be very carefully" mkali, maana una deal na watu wanaokujua kuliko ww unavyowajua. Na bahati mbaya kuna matukio yanatokea kama "wake up call to you" ili uweze kuchukua hatua ila huoni sababu umekingwa na ukuta mnene wa mapenzi kwa carren, na yeye amegundua hilo anatumia kama udhaifu wa kukufanya atakavy.

Kama ungekua katika misingi ya mzee aliyotaka uende nayo toka mwanzo ungekua mbali sana...! Ila bado hujachelewa,

"This is Africa broe", na Africa wanaume ndo huwa tunaoa.

na kuoa ni pamoja ya kuwa kiongozi wa familia katika nyanja zote, mwanamke ni msaidizi tu.

Na ukweli ni kwamba kuwa mwanaume sio rahisi, "ila kuwa mume wa mtu, kuwa baba wa watoto ni mtihani unayopaswa kuufaulu siku zote za maisha yako" na huo mtihani watu wengi huwa wanafeli vibaya, hasa katika msingi wa kuchagua mwanamke sahihi

kuwa makini usije kudhani umeoa kumbe umeolewa, na ukajashtuka muda nao ukawa hauko upande wako....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…