Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

What a story! Bravo and all the best in your mtihani!
 
I hope hutofeli mtihani mdogo namna hiyo, na kabla ya kumfungulia biashara huyo dogo ni lazima umjenge kisaikolojia ili ajue ndio anaenda kuanza maisha yake na kusaidia ndugu zake.
Noted
 
Asante mkuu, Ushauri mzuri sana, hiyo Delay Method sikuifikiria kwakweli na kuhusu hiyo Biashara ni mtaji kiasi gani unahitajika?
 
Kuwa tuu makini na trusted,hasahasa kuwa truthful kwa Anne
 
Huu mtihani mgumu...

Kumbuka kuwa...
Watoto wa mitaani washazoea kuomba..

Ni ngumu kusimamia biashara...

Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote...

Hakuna njia ya mkato ktk maisha
 
Ndo hivyo hakuna vya bure duniani

Ila bado najiuliza sijaelewa ama. Hapo ulipoulizwa huna hela yaani mtaji na kodi ya kijana unatoa wewe kwanza ama?
Mbona kama wewe ndio umeniweka katika Wakati mgumu zaidi kama haya unayoyaeleza yataenda kuwa kweli, ila Caryn kweli ana kadharau flani nadhani inasababishwa na overconfidence
 
Asante mkuu, Ushauri mzuri sana, hiyo Delay Method sikuifikiria kwakweli na kuhusu hiyo Biashara ni mtaji kiasi gani unahitajika?

Mtaji hapa ni kuangalia mfukoni mwako maana unaweza kuweka hat 5 M ,ila anaweza kuanza hata na 2 M, ongea na fundi akupe orodha ya vifaa vinavyobadilishwa sana kwenye pikipiki na bajaji ndio unaanza navyo kisha utaendelea kujaza na vifaa vingine kadri mtaji unavyokua, ila hakikisha huyo dogo nae anajifunza huu ufundi awapo na hawa mafundi wengine ili baadae akishaiva na yeye anakuwa anatengeneza hivyo anaongeza mapato.

Hii project akiipenda huyo kijana ipereke nnje ya mji kidogo, nishawahi kukaa Majohe huko nilipanga nyumba nzima na fance yake ipo road kabisa kwa 150k kwa mwezi, nilikuwa kama kwangu maana nilikuwa mwenyewe tu, sasa mazingira kama haya unaweza ukafanya sehemu ya kulazia vyombo vya moto pia.
 
Nauzingatia ushauri wako mkuu, utajua pia nikiacha Kazi huu mtihani wa Mzee nitashindwa kuufanya maana unahitaji pesa na Mzee kasema nitumie Pesa yangu, hapo nambie inakuaje?
 
Unaweza kuwa mwandishi mzuri w scripts na muongoxaji mzuri.

Fanyia kazi hili mkuu
Kweli? Sijawahi kuambiwa hili labda kwasababu ndio mara ya kwanza kuandika story, ila kipindi Cha nyuma niliwahi kuwa muandishi wa habari za kuandika kwenye website (Entertainment news)
 
Mkuu tuendelee na story ninaifurahia na ina kitu cha kujifunza.
Lkn sio halisi...hili niachie mimi naomba nisikutoe kwenye reli.
[emoji849] Haya bhana
 
Inaonekana Mr BM X6 ana moyo wa huruma sana, ana "empathy" ya hali ya juu sana.

Kijana wa Buguruni ana wadogo zake wawili, kama sijakosea, na mmoja ni mgonjwa mgonjwa na hajawahi pata matibabu asilani! Kijana wa Buguruni ana umri wa miaka 17, ndio anaweza fanya biashara lakini sioni ni kwajinsi gani ataweza kujiendeleza baada ya miezi sita...sustainability! Tunaijua hali halisi ya nchi yetu.

Ninashauri kabla ya yote Mr. BM X6 apate historia yote ya hii familia ya watoto hawa.....ndugu wa pande zote wako wapi nini kiliwakumba hadi kuwa hapo walipo. Ninashauri, kama itampendeza BM X6 awaasili (adopt) hao watoto kwa kufuata taratibu zote za serikali.

Kama wazo la adoption sio muafaka kwako, basi fungua NGO itakayojishughulisha na watoto walio katika mazingira magumu na tafuta nyumba anza na hao watoto watatu kwanza. Nina imani, mfadhili wako wa kwanza atakuwa huyo Mzee. Katika nyumba hiyo, watoto watapata nafasi ya malazi, chakula, elimu na matibabu. Sioni mantiki ya biashara Kijana wa Guguruni ilahali wadogo zake wanahitaji sana elimu.
Inaonekana Mr BM X6 ana moyo wa huruma sana, ana "empathy" ya hali ya juu sana.

Kijana wa Buguruni ana wadogo zake wawili, kama sijakosea, na mmoja ni mgonjwa mgonjwa na hajawahi pata matibabu asilani! Kijana wa Buguruni ana umri wa miaka 17, ndio anaweza fanya biashara lakini sioni ni kwajinsi gani ataweza kujiendeleza baada ya miezi sita...sustainability! Tunaijua hali halisi ya nchi yetu.

Ninashauri kabla ya yote Mr. BM X6 apate historia yote ya hii familia ya watoto hawa.....ndugu wa pande zote wako wapi nini kiliwakumba hadi kuwa hapo walipo. Ninashauri, kama itampendeza BM X6 awaasili (adopt) hao watoto kwa kufuata taratibu zote za serikali.

Kama wazo la adoption sio muafaka kwako, basi fungua NGO itakayojishughulisha na watoto walio katika mazingira magumu na tafuta nyumba anza na hao watoto watatu kwanza. Nina imani, mfadhili wako wa kwanza atakuwa huyo Mzee. Katika nyumba hiyo, watoto watapata nafasi ya malazi, chakula, elimu na matibabu. Sioni mantiki ya biashara Kijana wa Guguruni ilahali wadogo zake wanahitaji sana elimu.
 
Ndo hivyo hakuna vya bure duniani

Ila bado najiuliza sijaelewa ama. Hapo ulipoulizwa huna hela yaani mtaji na kodi ya kijana unatoa wewe kwanza ama?
Hapana, According to Caryn, Mzee kasema atatoa Kodi ya miezi sita ila Mtaji ndio natoa mm ila tu nihakikishe baada ya miezi sita kijana aweze kujilipia Kodi kupitia Biashara nitakayomfungulia
 
Huu mtihani mgumu...

Kumbuka kuwa...
Watoto wa mitaani washazoea kuomba..

Ni ngumu kusimamia biashara...

Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote...

Hakuna njia ya mkato ktk maisha
Kwahiyo ili nisitake yote, wewe unahisi nibaki upande upi hapo ambao utakuwa sahihi?
 
Sasa huo mtihani niliopewa ndio natakiwa nifaulu ili hayo yote yatendeke ikiwemo na madogo kwenda shule, yako kwa kifupi natakiwa nimuwezeshe kijana aweze kuhudumia wadogo zake
 
Kwahiyo ili nisitake yote, wewe unahisi nibaki upande upi hapo ambao utakuwa sahihi?
Hakuna upande wa kubaki...

Kwanza umekosea sana kuingiza mapenzi sehemu za kazini, Acha kabisa...
Accountant atakuharibia kazi...

Hivyo huna kazi...

Pili umekuwa umekuwa unapenda vya bure, wewe mtoto wa kiume pambana kwa jasho...

Mzee anakupelekesha tu ka mtumwa...kama anataka kukusaidia mbona masharti...

Pia msaada angetoa yeye mwenyewe kwa hao watoto wa mtaaani...

Anataka kitu kutoka kwako mwishoe utaambiwa uoe mtoto wake...

Mi nafikiri Acha vyote ufanye biashara yako mwenyewe achana na Mzee na Achana na kazi ya mama Accountant
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…