Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Kwanza unatakiwa umu inspect huyo mtoto anawaza nini kichwani ujue familia yake na nani yupo nyuma yake wewe unaweza ukamsaidia kwa hayo halafu akaja kufelishwa na watu/mtu wa karibu yake either baba, mjomba, kaka au somebody else anaemuheshimu changa karata zako vzr jua anapendelea kufanya nini cha kumuingizia kipato.

Kuhusu biashara mpe kozi kwanza ndogo ya kujua ufundi pikipiki/bajaji kwenye kijiwe chochote cha mafundi then mfungulie Duka la spare parts na kwa kuwa yeye mwenyewe atakua na ufahamu atamudu na kwa kuwa ana wadogo zake nao watamsaidia na watapata elimu ya ufundi
 
Wakuu nahitaji ushauri wenu ili niweze kufaulu katika huu mtihani, nimepewa kazi kubwa ambayo nikifaulu basi milango mingi itafunguka huko mbeleni.

Kuna Mzee flani huwa tunashirikiana kikazi na mara nyingi mizigo yake huwa anaiagiza kupitia Kampuni yetu, ni Mfanyabiashara na ameanza Biashara miaka ya 90s alivyomaliza tu O level, Sasa huyu Mzee kijana (1971) huwa tunaongeaga mambo mengi kuhusu Biashara huku nikitaka anipe miongozo ili na mimi nielekeze nguvu na akili huko

Huyu Mzee akijaga Ofisini ni lazima nionane nae japokuwa muda mwingi Mimi huwa nakuwa nje ya ofisi kutokana na majukumu yangu mengi si ya kufanyia Ofisini nimesema ni lazima nionane nae ni kwasababu zangu Binafsi na si za kiofisi, Huyu Mzee ndio ameni inspire mm kutaka kufanya Biashara si kimafanikio tu bali hata lifestyle yake, Yani kifupi ana enjoy mafanikio yake anafanya kazi huku amerelax nyakati za kujituma usiku na mchana kwake zilishapita, sio kama wazee wengine wenye Utajiri lakini Bado anajitesa siku nzima kama yeye ndio kaajiriwa jambo ambalo ni tofauti kwa huyu mzee, huwezi kujua ratiba yake muda wowote yupo Ofisini na muda wowote pia anaweza akawa nyumbani, Ni siku ya Ijumaa tu ndio Najua kwamba haendagi ofisini kwake labda kuwe na jambo muhimu sana ambalo linahitaji uwepo wake.

Sio mtu wa mitandao sana hasa kama hii Jf pengine hata haijui, Kuna siku nilimuuliza kuhusu mitandao akanambia anatumia Twitter na Whatsapp tu, so hii story Najua itakua ngumu kwake kuiona, maana hata kwa codes nitakazoweka kama akiiona atajua tu ni Mimi na ndio mchongo mzima utaishia hapo

Sasa nikibahatikaga kukaa na huyu Mzee mtu mbili huwa namuonesha shauku ya mimi kutaka kufanya biashara lakini kila nikimgusia swala hilo ni kama anaona sipo serious, anahisi nataka kufanya biashara kwa kufuata mkumbo tu, Kwasababu nakumbuka aliniuliza nataka kufanya Biashara gani mimi nikamwambia nataka kufanya Biashara kama ya kwake, aliishia kucheka tu

Nakumbuka siku moja nimetoka Zanzibar kupokea mizigo ya ofisi ya wateja, nimefika Dar Huyu Mzee akanipigia simu kuniomba kwamba mzigo wake nisiupeleke store Bali niende nao Ofisini kwetu ili nikitoka kazi nimpitishie kwake, na ndio ilikuwa mara ya kwanza kufika kwa huyu Mzee, Asee vile nilivyokuwa namdhania ni robo yake, Kuna watu wanaishi acheni nyie

Basi Mzee alinikaribisha vizuri sana mjengoni mjengo mjengo kweli! Wakati naingia kwenye Parking sijaona Gari yake niliozoea kumuona nayo siku zote (Land Cruiser ZX V8) nilimkabidhi vitu vyake Mzee akapanda juu Nadhani ni Bedroom kwake alivyorudi akanipeleka Backyard tukakaa, Sasa tulivyokuwa mule ndani sikuona mtu mwingine yeyote ikabidi nimuulize Mzee nyumba yote hii unaishi peke yako? akanambia "hapana mabinti zangu na Mama yao wameenda Kibaha watarudi Jumapili" (Siku hiyo ilikuwa Ijumaa)

Story zikaendelea pale Mzee akanambia "Kijana wangu nilikuambia uniletee mzigo kwa makusudi, mm kila Ijumaa huwa na utaratibu wa kupata chakula Cha jioni na familia yangu ya ndani na ya nje hivyo nilitaka na wewe uwepo" alivyosema familia ya nje niliwaza mbali, nikamuuliza kwani Mzee wewe una wake wa ngapi? kabla hajajibu alitabasamu "mmoja tu na Najua umeuliza hivyo kwasababu gani, nilivyosema familia ya nje nilimaanisha watoto wa mitaani ambao hawana makazi maalum, kwahiyo badae tutatoka kwenda kuwachukua" nikasema sawa ni jambo zuri Mzee

Wakati tumekaa na kuendelea na story Mzee akanambia kama nitataka kunywa chochote niende kwenye fridge nijihudumie, Nikamwambia haina shida, Mara ghafla Mzee akapokea simu Wakati anazidi kuongea akachange ni kama kapokea Taarifa mbaya, yule Mzee aliinuka pale alipokuwa amekaa akiwa bado anaongea na simu huku akiingia ndani, alivyotoka alikuwa kashika funguo mkononi akanambia "Kijana wangu nimepata dharula itabidi nikuache kidogo ila nitajitahidi niwahi kurudi ili tufanye lile jambo nililokuambia, in case of anything utanipigia simu" Nikamwambia sawa Mzee

Tukatoka kule backyard hadi Parking pale kulikuwa na Magari mawili ambayo sikuwahi kumuona nayo akaingia kwenye Jeep, Yale majeep yenye muundo kama wa Benz G Wagon, Mzee alifungua geti na Remote control akasepa, Mtu mzima nikachoma ndani, nikajiachia kwenye Sofa huku nikiperuzi, Giza likaanza kuingia na saa Ile Mzee anaondoka ilikuwa ni around saa kumi jioni.

Simu ikaita, kucheki ni Mzee, akanambia "Kijana wangu ni kama nitachelewa kurudi Sasa wewe Fanya hivi, umeiona hiyo gari hapo parking?" nikamjibu ndio "Sasa panda juu mkono wa kulia chumba Cha mwisho fungua mlango ingia ndani nenda hadi kwenye dressing table utakuta funguo ya Gari ichukue, si unajua kuendesha gari?" nikamwambia ndio lakini Sina leseni Mzee "Wachana na mambo ya leseni, kwani Driving licence ndio inaendesha gari? Sasa si umesema unajua ku drive, nenda jikoni kachukue hicho chakula pakia kwenye gari wapelekee wenye uhitaji sababu ninaweza nisirudi halafu hicho chakula kikaharibika" nikamjibu sawa Mzee akakata simu

Nikawa najiuliza pa kwenda kuwapata hao watoto, Basi bhana Mimi nikapanda juu kuchukua funguo ya Gari, nikazama hadi chumbani asee ni noma, Chumba kama sebule nikawa sielewi dressing table Iko wapi, kilichonisaidia ni kioo, nilivyoona kioo nikajua tu hii ndio yenyewe hadi kesho sijaelewa Ile dressing table imetengenezwaje, kweli nikakuta funguo pale juu Ile kupiga jicho pembeni nikakuta maburungutu ya pesa elfu tano tano, hata sijayagusa maana nilijua nyumba kama Ile haiwezi kukosa CCTV camera, me nikabeba funguo kikashuka chini hadi jikoni nikakuta mahotpot yana msosi wa kutosha (Wali njegere maini) nikayabeba hadi kwenye Gari (Alphard) nikarudi jikoni kucheck sahani zote za dongo nikaachana nazo nikarudi kwenye Gari nikafungua Geti nikasepa ila sasa nimetoka na sijui naelekea wapi nikicheki saa ni saa moja kasoro, nikaenda hadi Mwenge, nikapark kando ya Barabara nikawa nawaza hao watoto nitawapata wapi, mawazo yakaja niende kwa sister angu flani anakaa uswahilini huko ndiko nikagawe hiki chakula, nikapiga mahesabu ya masaa nitakayo tumia hadi kufika huko muda utakuwa umeenda hata hivyo nitakuta watoto wengi wapo majumbani mwao na watakuwa washakula nikaona nikifosi kufanya hivyo nitaendelea kuipa nguvu ile kauli ya "mwenye nacho huongezewa"

Nikatoka pale Mwenge nikaenda Buguruni, nimepitia Ile footbridge na Mataa nikaingia Barabara ya kama naelekea Ilala, sijafika hata mbali nikapark pembeni kusikilizia, sijakaa sana nikaona madogo wawili nikawasimamisha Nikawauliza wanapoishi hawakunijibu, nilivyoona hivyo sikutaka story nyingi tena niwaambia ninachakula nataka niwapatie lakini nyie wawili hamtakimaliza mnaweza kuwaita na wenzenu? mmoja akaniuliza "kiko wapi hiko chakula chenyewe?" nyie kawaiteni wenzenu mkija mtakiona chakula, nitawaambia hivyo wakaondoka nikakaa kama Dakika 8 nikaona wale madogo wanakuja na rundo la madogo wenzao nikajisemea Leo kazi ipo maana kwa Ile idadi niliyoiona ya wale watoto na nikipiga mahesabu ya kile chakula nilichobeba ni kama hakitatosha kabisa halafu saa hiyo hiyo nikakumbuka nilibeba tu chakula na sikubeba sahani nilipanga nipitie supermarket ninunue zile sahani za karatasi nikasahau

Madogo wakafika hadi kwenye gari, nikawauliza mgahawa wa karibu uko wapi?wakanionesha lengo nikwenda kununua chakula ili niongezee na hapo hapo nitapata sahani za kutumia kwasababu kwa kile chakula kilichopo kinatoshea kwa watu kama 9 ivi na kile kikosi Cha madogo 15 wamefika, nikalock gari nikawaacha madogo pale kwenye gari nikavuka Barabara hadi upande wa pili nikaulizia chakula nikaambiwa kipo, saa hyo ni saa 2 usiku na madakika yake, Nikwambia Mama ntilie nataka chakula Cha watu kama kumi, Yani sahani kumi za wali, akanipakulia akaniwekea kwenye ndoo, nikatumia ujanja wa kumwambia kila sahani ifunike ili chakula kisipoe ili nipate sahani excess, alivyomaliza nikampatia 20k Nikamwambia siendi mbali sana sahani nitakuletea mwenyewe, akakubali bila wasi na sijui kwanini aliniamini kiwepesi vile

Nikafika kwa madogo nikafungua gari nikatoa Yale mahotpot ujinga mwingine ambao niliufanya sikubeba vijiko vya kupakulia na kule kwa Mama ntilie sikuchukua Maji ya kunawa, Sasa ule msosi wa Kwenye hotspots nikaupakua kwa kutumia sahani nikakigawa kile chakula wengine ilibidi wale wali wa mama ntilie na baadhi yao wakala ule niliokuja nao ila ngegere na maini nilizigawanya katika Kila sahani, sasa nikawa nawauliza madogo mtanawa wapi mikono?, dogo mmoja akasema blaza haina haja mikono yetu misafi[emoji3] basi nikawaruhusu wafinye msosi na mm nikichukia sahani moja, walivyomaliza Nikaingiza mahotpot kwenye gari nikalock nikamchukua dogo mmoja Nikamwambia abebe ndoo yenye sahani anifuate wale wengine niliwaambia watusubiri, tukaenda hadi kwa mama ntilie nikampatia sahani zake akanirudishia balance yangu elfu 5, nikamuomba chenchi ya elfu 10 buku buku, akanipatia, tukarudi hadi kwenye gari na yule dogo, Nikawaambia Sasa Mimi na nyie tushamaliza nikampatia Kila mmoja buku buku angalau kesho Asubuhi wawe na uhakika nikaagana nao pale nikasepa, Wakati nipo Njiani nikampigia Mzee kumjulisha kwamba nishafanya kile alichoniagiza akanambia "sawa Sasa wewe unaweza kwenda na hilo gari kesho utalileta nyumbani, si ulifunga vizuri nyumba?" aliniuliza Nikamwambia ndio na funguo Niko nazo, "Haina shida ww unaweza kwenda kupumzika Sasa" okay Mzee, Sasa wakati huo naongea nae kwenye simu Mimi nilikuwa nishapita Ubungo Interchange naitafuta Mwenge, nikielenda nyumbani kwake, ilibidi nigeuze gari nilirudi nilikotoka sababu mm naishi Tabata, Yani kama ningewahi kumpigia simu basi nisingejisumbua kufika mbali kote huko

Kwa mara ya kwanza nafika mtaani kwangu na Gari, siku zote Mimi niwakufungua kale kageti kadogo Leo nafungua Geti lote kubwa ili kuingiza ndinga, maana nilipopanga tunakaa watu 3 nyumba zinajitegemea ila tunashea Compaund, nikapark gari nikaingia ndani kulala, kukakucha, Jumamosi mara nyingi huwa siendagi ofisini labda itokee naenda Zanzibar, so nikawa Sina ratiba ndefu nikafua nguo kadhaa nikaingia mtaani kupiga chai, nilivyomaliza nikarudi home direct nikakuta missed call ya Mzee maana nilivyotoka simu niliiacha, nikampigia akanipa maelekezo fulani pale ya kwamba atarudi Jumapili Pamoja na familia yake hivyo kama Nina muda nilipeleke Gari kule nyumbani au nibaki nalo hadi Jumatatu aje alichukulie Ofisini, nikamjibu sawa yote yanawezekana ila acha niangalie lipi litakuwa rahisi zaidi

Baada ya kukata simu nikapiga hesabu kurudisha hili Gari hadi kule mwisho wa mji, nikaona uvivu isitoshe gari lenyewe lilikuwa rafu mavombo machafu humo ndani, Yani ukifungua mlango wa gari Gari lote linanuka wali, nikatoa vyombo vyote, nikajikaza kuviosha hakuna Kitu kinanikera kama kuosha vyombo ndio maana huwa sipikagi mara kwa mara. nilivyomalizana na hiyo Kero nikalipeleka Gari Car Wash nikalirudisha kulipark home, hamuwezi amini nilishinda ndani hiyo weekend yote hadi inaisha na Gari limepark tu uwani

Jumatatu hii hapa, Asubuhi na mapema nikawa najianda kwenda kazini, Nikaingiza vile vyombo kwenye gari ila Sasa nikawa nawaza hao police huko Barabara kwasababu Sina Driving licence, nikasema potelea mbali nikatekenya mchuma hadi kazini nikalipark kimya kimya kama sio Mimi nikaingia Ofisini kwaajili ya kuchapa kazi

Imefika Lunch time najiandaa kwenda kupiga Menu yule Mzee nikamuona anaingia Ofisini halafu ana hasira amekunja sura, nikajisemea hapa kimeshanuka nikaanza ku recall matukio ili nijue ni wapi nimekosea hasa kule nyumbani kwake, kote nilicheza safe na mara ya mwisho kuongea na huyu Mzee ilikuwa ni Ile Jumamosi akinipa mabadiliko ya ratiba yake huku akinipatia option mbili za yeye kupata gari yake, na Mimi nilivyochagua kubaki na Gari hadi Jumatatu sikumpigia tena simu kumjulisha uamuzi niliouchukua....nikapata majibu kwamba inawezekana hapo ndipo nilipo haribu, alikuja kwenye desk langu na kuniambia "nipatie funguo ya Gari na ukimaliza kazi nitafute" hata hakunisalimia akatoka nje ya ofisi akaondoka....

Inaendelea badae acha nipate msosi.....story yangu ina episode 6 tu, episode ya kwanza na ya mwisho (1 & 6) ndio muhimu zaidi Sababu ushauri wako ndio unahitajika hapo

1. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

2. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

3. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

4. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

5. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
Kichwa cha habari kilitakiwa kuwa "hatma ya maisha yangu yapo mikononi mwa Accountant na mafanikio ya kijana wa Buguruni".
 
Hata hivyo Caryn mm namuogopa, nishamzoea mnyonge wangu Annie, nikimuambia nyamaza ananyamaza, huyu Caryn tutawezana kweli?
Na kwann umfanye Annie mnyonge?? Kisa leo unacho..kisa hupendi kusikia ukweli..au kisa ni mnyenyekevu na mpole and she loves you dearly... Au ni kwamba kujikuta mi ndo mwanaume huku ukiwa kwa accountant na mama ake unachutama na kwa Caryn mwenyewe unasalute ngoma isambee....

My take fanya maisha yako. Hapo ofisi ulioko ni shetan alipomuonesha Yesu vingi akamwambia ukinisujudia....if you can be ready kutoka hapo. Kwa mzee kuna mtu katoa ushauri mzuri sana i think Dona..kuwa anaweza aje kukufanya his puppet...not actively rather passively so every time you be submissive..usije jikuta waabudu mwanadamu..just be careful wit this option too...

Ushajifunza meng up to now mkuu its high time you get a life. And dont treat Annie like a clown simply coz she is too weak to get back to you. If you lose her one day you will wish you treasured her more...thamini mwanamke mzuri na good thing kila mtu anaesoma uzi huu kamcommend so akili kumkichwa. She is a woman and a half..usijitie alpha male kwake...ukastep on her beautiful and submissive heart...

Actually fanya uonavyo maisha ndo haya haya...
 
1. Umeshamchapa accountant, Unaendelea kula Annie hakikisha unamalamba kisimi Cyree.

Kwanini?? Cyree Hana adabu.

2. NGO ya Watoto wa mtaani( tuite UFUMBUZI WA WATOTO WA MTAANI)solution for street children

Wazo hili Lina logic kubwa Sana kwanza. Watapata Elimu ya maisha Yao. Na kiimani pia., Pili. Itasaidia si wao tu lkn pia wengine Kwa sababu wapo na mwisho wazo hili creen asiye na adabu atalikubali Sana. Watasoma watakwenda shule, nk

3. Unahabari kwamba Kwa kitendo anachokulazimisha Akauntant, uhakikishe unamwambia mama nje ndani. Na kwamba hujawahi lala naye. Mpe sababu.

Kwa tabia hizi,au Watu wenye hurka hizi like mama like binti. Akauntant atashangaa siku unakula mamaake. Kaa mbali na familoyzenye watoto wa aina hii.

Niongezee kidg kuhusu Karen kameniudhi Kwa sababu sipendi mwanamke hata siku Moja anifanyoe upuuzi huo. Hakuna mwanamke mwenye confor mbele yangu. Unisamehe ni maumbile tu tunatofautiana.
 
Caryn ana dharau sana sijaona sababu ya yeye kumdhihaki dada yake vile tena mbele za watu wasiowafahamu anamshusha na mzee pia hajamtendea haki michelle eti kisa kapenda kijana wanayemuona sio hadhi yao.

Mwisho wa siku wanakuandaa kuifahamu biashara uje umuoe caryn ambayae hatakuheshimu kamwe. Sijaona akili zake zaidi ya kebehi tupu.

Mwisho ukimuweka annie mbele utapoteza kazi maana mshadanganya kwa mama accountant pia utampoteza mzee maana anakuandaa kuwa kijakazi wake kupitia caryn
Naunga mkono hoja.. [emoji4]
 
BM X6 wewe ni kijana mdogo sana bila shaka na pia ni rika la vijana wa kileo , najua una ndoto ndugu na unahitaji kuzifikia kabla haujaswaliwa au haujazikwa, sasa ndugu BM X6 ipo hivi÷

Kama ujuavyo kwa kimalikia wahenga wanasema GOLDEN CHANCE NEVER COME TWICE , ila pia binadamu hubadilika si Annie wala accountant sasa jitizame wewe ni wapi umetoka kimaisha na kimaadili alafu waza ni kipi unahitaji mbele

Annie ni mwanamke wa moyo wako na maisha yako ila accountant n passer girl kama wale wengine uliolala nao hivyo

Annie hata umsaliti leo ila ataendelea kuwepo kama ni mipango ya yule Mungu unayemuabudu ila kama si mipango yake hatakuelewa na mtaishia hapo

Sasa ni hivi nenda kamvishe pete Accountant ili ule shavu ila kumbuka kujiwekeza mpaka pale utapoona sasa unaweza kujisimamia bila kampuni huku binti kimwali Annie mueleze uhalisia akupe muda kama ni miaka miwili hata saba sawa ili ukamilishe mission yako

Akikubali akikataa ni non of your bussiness ili ufikie kwenye ndoto zako kwanza , usiseme ni dhambi kwani umefanya mangapi mpaka sasa ambayo mengine hata kuyasema huwezi na usisaha hautakuwa wa kwanza kupambania ndoto zako kwa ubaya ilimradi ufike pale unapoota .

Sasa huyo kijana wa buguruni , ndipo penye sehemu ya kukusaidia wewe na Annie mdumu au muachane kwanini ?
Sababu ikiwa huko utafanikisha basi hata kazi waweza kuacha ili ufanye mambo yako na binti kimwali Annie .

Nenda sehemu za stand either makumbusho au mbagala zakiem au keko karibu na kituo cha polisi omba nafasi fungua duka lenye atleast wa mtaji wa milioni tano na huduma za m_pesa na huduma za kibenki hasa za miamala na pia uza vinywaji hapo vya kila namna , hii itakufanya hata kwa siku asikose hata elfu sabini kwa siku .

Ila kaa kitako na huyo kijana muombe awe msiri kwa mzee hiyo biashara ifanye yako ila yeye ndiye msimamizi ila baada ya miezi sita utamkabidhi , ndugu BM X6 hakikisha hiyo biashara unaisimamia vizuri mauzo na kila kiingiacho na kitokacho ila usisahau kijana ana wadogo zake hivyo wanahitaji huduma pia

Ndugu yangu poteza kidogo upate kikubwa hivyo jitahidi sana uwe unatoa kidogo katika kale kamshahara kako ili uwatunze wale watoto pasipo kujali kwenye biashara uliyofungua ukizingatia nahisi kapochi kako katanona baada ya kupanda cheo hapo kwa mama mkwe [emoji1787][emoji1787].

Mwisho ni kuwa hakikisha faida ya kipindi chote cha miezi sita aliyotoa mzee , hakikisha unaitunza kwa account ili baada ya miezi sita iwe ni starting point ya KIJANA WA BUGURUNI ili aishi vyema

Kaka kama ukifeli katika biashara hiyo basi nenda chuo chochote ila nakushauri vyuo vifuatavyo DUCE , NIT NA UHASIBU mara nyingi tenda za wauza vyakula(wazabuni) maeneo hayo uwa hazidumu sababu ya usimamizi mbovu hivyo kushindwa kulipa kodi kwa vyuo husika .

Sasa nenda mtafute muhusika mpoze kidogo akupe tender kwenye hiko chuo utachopata na hapo tayari utatakiwa kuwatafuta wapishi ambao ni akina mama ila hakikisha kijana wa buguruni awe ni msimamizi wa mwisho katika hiyo biashara na kipindi ambacho wewe haupo ila faida na expenses za hiyo biashara zote zipite kwako .

Nakuona unaniuliza mbona vyuo vinaenda kufunga sasa , hapana BM X6 nimekutajia vyuo ambavyo the whol3 year wanafunzi wapo sababu hawatoi degree tu ila hata certificate na diploma hivyo kujikuta mwaka mzima wapo wanafunzi around hayo maeneo

Ndugu kwa haya nakuona ukipewa hiyo hela ya biashara na kuanza mambo yako na kumrudia binti kimwali Annie kwa kumpa talaka takatifu ndugu ACCOUNTANT .

Japo katika biashara hiyo ya vyakula hakikisha mzee akupe angalau milioni kumi ya kufanya biashara ila usisahau kuwa systematic katika kila jambo ili hata mzee asikuwaze vibaya kuwa muwazi na ukiamua kumpiga mpige kisomi au sio ndugu yangu Mtanzania ? (In magufuli's voice)
USIOGOPE KUFANYA LOLOTE SABABU MPAKA SASA NI MENGI YA DHAMBI UMEFANYA HIVYO TENDA KADRI YA MOYO NA HULKA ILI UIONE KESHO ANGAVU

Ushauri tu ndugu yangu BM X6

TEKERI.
Kama ni muislam aoe wote tu maana kila mmoja anamchango mkubwa kwa maisha yake.
 
ILIPOISHIA [emoji1484]

Caryn: "Sorry Dad, first of all I want to know where these kids came from?

Tukaanza kuangaliana na yule jamaa aliyekuwa anaendesha Gari, Wakati najipanga kujibu.....

Caryn: BM, You should answer this question

Nikamuambia wametoka Buguruni Rozana

Caryn: "Dad, I think you should change your strategy on how to help these kids

The food we're gonna give them was it gonna change their life?
So as a rich man if you think you want to help someone give them the kind of help that would transform their life not leaving them with food in my opinion"


MUENDELEZO [emoji1484]

Mzee akamuangalia Caryn halafu akaniangalia na Mimi, Akasema "Kwahiyo unashauri tufanye nini Binti yangu"

Caryn: Let me speak swahili so that they can understand me, Hawa watoto kwa umri waliokuwa nao wanatakiwa wawepo shuleni, labda mtasema mnawapatia chakula kwasababu hawajafika umri wa kujishughulisha na shughuli zozote za kujiingizia kipato, huyo Kaka yao je maana anaoneka ni mtu mzima

Caryn: "How old...ooh sorry, Una miaka mingapi kaka?"

Kijana: "Kumi na Saba"

Mzee: Kumi na Saba Bado mdogo sheria haruhusu

Caryn: Come on Dady, Kwahiyo kama sheria hairuhusu ndio abaki kuomba omba, Kuna situation ikikufika hutakiwi kuangalia Sheria inasemaje inakubidi kufanya kile unachotakiwa kufanya ili u survive, Kijana you have to do whatever it takes to survive out here in this jungle called life

Michelle: Sometimes you sound more like an adult than a teenager

Caryn: And you sound like you're better than me, and you're not

Mama: Na nyie mshaanza sasa na malumbano yenu, ebu Kuweni na adabu hata kidogo mbele za watu msiowajua

Caryn: Ambae hana adabu ni huyo mwanao mama, Watu tunaongea vitu serious yeye analeta utani, mm teenager sawa, yeye huo utu uzima umemsaidia Nini hadi sasa, Anawaza Mapenzi tu......

Mzee: "Caryn basi Inatosha, unajua huyo atabaki kuwa Dada yako inabidi umuheshimu, halafu kwanini siku hizi nyie watu hampendani?"

Caryn: "Kwasababu nimekuambia Habari za huyo bwana ake wa huko Kibaha, I told you Dady na nakuambia tena the guy is more interested in money hakuna Mapenzi hapo"

Mzee: Caryn hiyo ni topic ya siku nyingine all in all nimeipenda maoni yako kuhusu Hawa vijana wadogo

Ila Caryn hapana asee [emoji1544] yule Demu kachukua akili za Baba yake, ni PISI KALI halafu sauti yake ni kama ya Bahati Bukuku na mara nyingi anakuaga serious, nyumba nzima hapa kwa Mzee ni yeye tu ndio sijawahi kumuona akicheka

Tukamaliza kula, Mzee akawahoji wale watoto mambo kadhaa, akawapatia na Pesa halafu akanambia "BM Nadhani Ushauri wa Caryn ni mzuri, Sasa ule mtihani nililokuambia nitakupa umekaribia get yourself ready. chukueni Gari warudisheni Hawa watoto halafu na Kijana atakudrop kwako,

Basi tukaondoka, tukawadrop madogo na mm nikadropiwa, kufika kwa nyumba nikamkuta Annie nikakuta ameandaa my favorite food Wali Nazi Njegere Nazi, Asee halafu nimetoka kubonya Pilau la Kuku kwa Mzee, nikaona hapa busara ni kula hata kama ni nusu sahani, Unajua Annie anajua natoka Kazi hakujua ratiba yangu imeendaje na Wala hajui Mahali nimetoka

Akaniwekea food kwa meza nimeipiga kama vijiko vitatu ivi nikamuuliza "Are you sure it's not Christmas yet?"

Annie: "of course it's not"

Maana sio utamu huu wa msosi, saa hiyo mm nikiendelea kula Annie alionyesha kuwa na mawazo, nikamuuliza nini mbaya?

Annie: "You know what BM, now i believe that circumstances change people"

Me: "Unamaanisha nini?"

Annie: "Hadi hapa tulipofikia life has taught me not to plant my seed in other people's garden"

Nikawa nishajua alichokuwa anamaanisha, TURUDI NYUMA Kidogo ili na wewe umuelewe Annie

Ukisema "Table turns" Mtu wa kwanza kuelewa ni Annie, niulize kwanini? Okay ilikuwa hivi, Miaka mitano nyuma Annie alikuwa mtoto wa kishua nikisema wakishua wakishua haswa haya maisha acheni nyie,

Natamani niandike mengi kuhusu Annie lakini haitawezekana kwasababu code yake nimeifungua, ndio muhusika pekee Jina lake ni halisi kwenye hii story wengine wote nimetunga majina na baadhi yao niliishia kuwaita Mzee, Mama, Jamaa nk

Ila kwa kifupi ni kwamba Annie alipiga taff sana enzi hizo wakiwa bado wako vizuri, Alinilipia hadi ada ya mwaka wa mwisho chuoni. Baba yake alikuja kupata matatizo flani kipindi Cha awamu ya 5, na Annie Mama yake Alishaaga kitambo so alibaki na Baba, Baba nae ndio hivyo akapotezwa, acheni asee kila nikikumbuka roho inaniuma ndio maana nakuwa mzito kumuachia huyu mwanamke

LEO

Nikamwambia Najua unachoniwazia ila nikwambie tu unaniwazia vibaya, acha nikuambie ukweli pengine utakuumiza ila ni Bora kuliko kudanganyana, inawezekana nimekucheat lakini sio kwa mazingira niliyoyaandaa, Najua nilishakuambia mengi kuhusu yule mwanamke (Accountant) lakini hili la kucheat nilikuficha kwasababu sikudhamilia mimi na kuhusu swala la kuacha kazi ili kumkwepa yule mwanamke sidhani kama ni sahihi kwasababu unajua hali halisi ya maisha ilivyo Mimi nakuomba tu uridhie Mimi kundelea kufanya kazi Mimi nitajua tu jinsi ya kudeal na yule mwanamke na nakuahidi sitarudia kosa, Nakuomba usikatae, ni swala la muda tu nikakamilisha malengo yangu flani naachana rasmi na Ile Kampuni

Annie: "Okay! i trust you BM, you can go ahead, but remember not everyone in this life gets a second chance to write their wrongs"

BM: "Nakuahidi haitojirudia, na nakupenda sana japokuwa ww mara nyingi husemi kwa Mdomo kama unanipenda"

Annie: "Ushaanza, listen BM 'I trust you' is better compliment than 'I love you' because you may not always trust the person you love but you can always love the person you trust"

BM: "Wow! thanks, i didn't even know that"

Basi Mama lao akatoa vyombo pale, Leo hajaachwa mtu Sebuleni, Najua mshaelewa. siku zilikatika mambo yalikuwa mswano na Annie

Asubuhi ya Jumamosi moja nimeamka nimechelewa sana kwenda job, nikajiandaa fasta nikasepa nikafika eneo langu la kazi Sasa wakati naingia Ofisini nikamkuta Accountant kakaa kwenye kiti changu ni kama alikuwa ananisubiri kwa hamu, nikamsalimia akaitikia halafu akanambia

Accountant: "Naona maisha yako yanaenda kuwa mazuri ila endapo tu utafanya Maamuzi sahihi"

BM: "Nikamuuliza Maamuzi gani?"

Accountant: "Usiwe na haraka BM, Mama alikuwa anakuulizia amesema ukifika tu nikwambie uende Ofisini kwake so we nenda kaonane na Mama"

Nikawa najiuliza Kuna jipya gani maana Accountant anafuraha kupita maelezo na si kawaida yake, basi Mimi nikaelekea ofisini kwa Mama, nikasalimia nae halafu nikakaa kwenye kiti

Mama: "Mwanangu si kawaida yako kuchelewa kazini, Leo imekuaje?"

BM: "Jana nilichoki sana Mama, hali iliyosababisha kupitiwa na usingizi Leo na kuchelewa kuamka"

Mama: "Ooh, halafu hata hivyo hukuwahi kuchukua likizo ya kueleweka tangu uanze kufanya kazi kwenye hii Kampuni"

BM: "Yeah ni kweli Mama lakini sikuona ilazima huo"

Mama: "Sasa Mimi nakupa likizo ya mwezi mmoja ya lazima hata kama hutaki, japokuwa hapa nilikuitia jambo lingine lakini Nadhani tutapata nafasi Nzuri zaidi ya kulijadili hilo jambo akili yako Ikiwa refreshed"

BM: "Ni jambo gani hilo Mama?"

Mama: "Nilijadili na mwenzako lile swala la wewe kurithi hii nafasi yangu, amefurahi sana lakini ametaka mvishane kwanza Pete ya kabla ya kukalia hiki kiti, na Mimi Nadhani ni jambo zuri so nilikuitia hapa ili tupange siku ya kufanya zoezi hili, lakini wewe nenda kwanza likizo ukirudi tutapanga vizuri"

Nikamuitikia tu "Sawa Mama" huku nikimuwaza Accountant, ndio kashaanza kuchezesha Karata zake kama alivyoniahidi, Basi mm Nikatoka Ofisini kwa Mama, nilimkuta Accountant Bado yupo pale kwenye kiti changu, Nilifika tu nakumwambia kwa userious wa hali ya juu "nipishe Mimi niendelee na Kazi"

Accountant: "I hope umefanya Maamuzi ya kiume, halafu kumbe huwa mnaongeaga mambo mengi na Mama bila kunishirikisha, ivi unajua maamuzi mengi anayoyafanya mama juu yako ni kwasababu anajua Mimi na wewe ni wapenzi, Sasa isije ikawa umeshaharibu mambo huko"

BM: "Sikiliza **** (Accountant) naomba kwasasa uende kwenye ofisi yako, Nina mambo mengi ya kufanya, sitakiwi kuacha kiporo Cha aina yoyote kwasababu kuanzia Jumatatu siji kazini"

Accountant: "Unasemaje wewe?"

Alivyosikia "Kuanzia Jumatatu siji kazini" alipagawa sijui alidhani nimeshaacha kazi, Alitoka mbio sijui kaelekea wapi ila itakua tu kwa Mama yake bila shaka

Nimekaa kidogo akarudi akanambia "Inawezekana wewe ndio umeomba hii likizo ili ukajipange maana inaonesha Kazi unaitaka lakini mwenye kazi humtaki, Sasa Mimi nakuambia hivi, we nenda hiyo likizo lakini siku utakayorudi hapa uwe umeshaamua jambo moja kati ya haya mawili, UNIOE au uandike barua ya kuacha kazi, Sitakubari uwe Director wa hii Kampuni a halafu raha unakula watu wengine" alivyomaliza hakutaka nimjibu akaondoka

Aliniacha na mawazo, kusema ukweli hii nafasi naitaka ili niweze kufikia malengo yangu lakini ndio hivyo tena ili ni qualify kwenye hiyo nafasi basi nilazima nimuoe Accountant, nikifanya hivyo Annie wangu nitamuweka katika nafasi gani na Jana tu tumetoka kula kiapo, na huyu Accountant mwenyewe hana sifa hata moja ya wife ila kitandani kwakweli yupo vizuri japokuwa ilikuwa ni mara moja na kwa bahati mbaya na hiyo dhambi nishaimbea msamaha kwa Annie na kanisamehe kwa kumuahidi kutorudia tena

Siku ikaisha na ndio ikawa nimeianza likizo yangu ya mwezi mmoja rasmi, lakini ya mawazo kwasababu natakiwa kufanya uamuzi sahihi, hapa kichwa kiliniuma zaidi kwasababu ya mtihani wa Mzee niliopewa,

Wakati naandika huu Uzi nilikuwa Bado sijapewa likizo, Uzi nimeuanza kuaandika jumatano ya tarehe 6/7/2022 na likizo nimepewa juzi Jumamosi tarehe 9/7/2022 hii siku kama mnakumbuka nilicomment hapa hiyo comment ipo namba 272 kama sikosei nilitoa maelezo kwanini hii story imekua ndefu Sasa siku hii ndio nilipewa likizo ya lazima so hili tukio ndio nimeliunganisha kwenye Uzi.

Na Uzi ulikuwa una muhusi Mzee ila niliongea story zingine kwasababu ili kufaulu mtihani wa Mzee inategemea pia mm kuendelea kubaki kazini

Inatakiwa Utulivu wa hali ya juu kuelewa, TURUDI NYUMA KWENYE MTIHANI NILIOPEWA NA MZEE

Ilikuwa Alhamisi, saa nne na dakika thelathini na saba sekunde ya sita simu ya Mzee iliingia nikiwa Ofisini najiandaa kwenda Zanzibar na Boti ya mchana

Mzee: [emoji338]"Kijana wangu hujambo?"

BM: "Sijambo Mzee, Shikamoo"

Mzee: "Marhaba, Sasa nataka kukujuza kwamba siku ya Jumapili jioni nasafiri hivyo nakuomba tuonane siku hiyo kabla sijaondoka

BM: "Sawa Mzee Haina shida"[emoji3513]

Basi nilienda Zanzibar nakurudi kesho yake, Jumapili Ikafika nikajua kabisa LEO NDIO ILE SIKU, Ile siku ya kupatiwa mtihani, Nakumbuka nilienda kwa Mzee mida ya saa sita mchana, nimeingia kwenye Ile nyumba harafu za misosi tu ndio zimetamalaki,

Kama kawaida chimbo langu na Mzee ni Backyard tukaongea sana mambo mengi, Sasa bhana safari yenyewe kumbe ni ya nje ya nchi, Mimi nilijua ni zile safari zake za mkoani kumbe Mzee anaenda United Kingdom (Uingereza) na atakaa huko kwa muda wa miezi miwili na nusu

Acha nifungue code kwenye Biashara moja ya Mzee, Ni hivi, Mzee ana mabiashara mengi ila moja ya hizo Biashara ni maduka ya Ex UK, Sasa huko UK alikua anaenda kibiashara zaidi, Sasa Mzee alinambia kwa muda wote. huo ambao atakuwa nje ya nchi niwe natembelea familia yake mara kwa mara, muda wa msosi ukafika tukakutana wote mezani yani Mimi, Michelle, Caryn, Mama na Mzee, Wakati tunaendelea kula mazungumzo nayo yaliendelea

Mama: "BM usipotee sana kwasababu Baba hayupo, uwe inakuja nyumbani tena mara kwa mara zaidi

Mzee: "Nimeshamsisitizia hilo, halafu BM kuhusu ule mtihani niliosema nitakupatia maelezo yote anayo Caryn, So ni wewe Tu kutafuta muda ukae chini na Caryn akuelezee

Nikajibu "Sawa Mzee" (huku nikimuangalia Caryn na yeye akinipiga jicho la kimtindo)

Michelle: "Baba kwani ni mtihani gani huo?"

Mzee: "Hili halikuhusu Michelle, wewe si ulishafeli wa kwako, Majukumu anayofanya Caryn ulipaswa kufanya wewe. Na Caryn zidisha umakini katika kumsaidia Mama yako majukumu ya Ofisini, Kuna baadhi ya mambo Mama yako anasahau"

Caryn: "Okay Dady, we will miss you"

Eeh!!! nilishangaa, kumbe Caryn ndio anapewa majukumu makubwa kiasi hiki, basi tulimaliza kula tukakaa kama 1 hour tukaanza safari ya kuelekea Airport, hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda 'Jeep Wrangler' halafu Mzee akaniambia nikae mbele, Guess Sasa nani anaendesha? ni Caryn jamani dah!

Tukafika Airport Wakati tunamuaga Mzee akanambia "BM nikirudi nikukute ushapata Driving Licence" Nikamwambia "nitajitahidi Mzee" Basi ndio hvyo tena Mzee akaingia kwenye kale ka mlango kalikoandikwa DEPARTURE sisi tukaenda kwenye Gari na kurudi nyumbani,

Wakati tumefika Tazara tunacross kuelekea Buguruni Nikamwambia Caryn "Mimi mtanidrop hapo Tabata"

Caryn: "Okay, I will text you, Dady gave me your number"

Tukafika Tabata wakanishusha nikatafuta Daladala la kuelekea Tabata Kimanga

Blue Monday mapema kabisa nimeamka kwaajili ya kwenda kazi, nashika simu kuangalia muda naona meseji ya namba ngeni kuifungua "Hey! Mornie, It's me Caryn" Nika reply "I got you" then nikasave namba yake

Wakati nipo Ofisini Caryn akanipigia akanambia kuwa yupo ofisini kwa Baba yake atatoka jioni na kuelekea **** ni Ile Hotel ambayo nilikutana na Baba yake, hivyo akaniambia nimkute hapo

Sasa yeye aliwahi sana kutoka siunajua wao ndio mabosi so wanajiamulia muda wa kutoka, mm ilibidi nisubiri Hadi ifike angalau saa kumi na nusu, Mida ikafika ya kutoka kazi moja kwa moja nikaelekea Hotelini lakini hiyo foleni niliyokutana nayo Njiani siyo ya kitoto, nikajua yule mtoto (Caryn) alivyo serious katika Kila Kitu sidhani kama nitamkuta, Mungu alisaidia nikamkuta Ile nimefika tu nikakaribishwa na

Caryn: "why are you late, you kept me waiting almost 2 hours?"

BM: "It wasn't deliberate the traffic was crazy it was terrible"

Caryn: "That is the senseless excuse"

BM: "Ok, let's discuss what brought us here"

Caryn: "let me start by asking you a question, Have you ever...."

BM: "Wait pls, Sijawahi kusikia ukitumia kiswahili japo kwa sentensi 3 mfululizo, naomba Leo tutumie kiswahili kwenye haya mazungumzo"

Caryn: "Ni sawa tu, as you wish"

Nikasema 'Yes' maana Nisingemuwahi huyu angenitemea Yai[emoji1639] hapa mwanzo mwisho na hata misamiati mingine nisingeielewa"

Caryn: "Umeshawahi kufanya Biashara?"

BM: "Kama Biashara gani labda?"

Caryn: "Typical Tanzanian man you're answering questions for questions"

BM: "Madam anayejibu swali kwa swali mwisho wa siku jibu lake linakuwa la uhakika, yani hiyo ni njia ya kulielewa swali vizuri zaidi, ila na wewe Kingereza unakipenda sana bhana"

Caryn: "Okay, Just any Business hata kama ya kuuza chupi"

BM: "Hapana, sijawahi Fanya Biashara"

Caryn: "Interesting, kama ni hivyo hukuwa katika nafasi ya kujibu Swali kwa swali kama ulivyofanya"

BM: "Nimekosa mimi, twende kwenye Point"(Nikajisemea moyoni Leo kazi ninayo)

Caryn: "Ebu kwanza nieleze kuhusu yule kijana aliyekuja na wadogo zake pamoja na watoto wengine"

BM: "Nikueleze nini?"

Caryn: "Ooh shit! same mistake, Are sure you will handle this?"

BM: "You wasn't specific enough, ukiuliza swali jaribu kuwa specific zaidi"

Caryn: "You're not smart enough as I expected, I see that you're even worse than i imagined"

BM: "Madam mimi naomba niende tu, maana naona Sasa umekuja kunichora tu"

Nikanyanyuka kwenye kiti, kabla sijapiga hatua akanambia "Ebu acha utoto Kaa chini na unisikilize kwa Makini, naku challenge kidogo na wewe umejaa kweli"

Nikakaa chini moyoni namsema huyu mtu inabidi nimsome akili yake ndio nitaenda nae sawa lasivyo atanitoa knock out

BM: "Caryn jaribu kuwa serious kidogo, unajua kama ningekuwa na Mzee hapa tungekuwa tushamaliza maongezi"

Caryn: "Thus why I am not Mzee, you know what BM, kwa muda huu mchache tuliokaa hapa Kuna Kitu nishakisoma kutoka kwako

BM; "Kitu gani?"

Caryn: "Unakosa some confidence pengine hasa ukiwa na mtu ambae hujamzoea, kwa Mfano kwenye swala la Kingereza sidhani kama ww hujui Kingereza, unakijua vizuri tu lakini ukataka niongee kiswahili, chaajabu nikawa naongea Kingereza makusudi na wewe unanijibu Kingereza, hiyo maana yake Nini?"

BM: "Sawa nimekusikia, nitayafanyia kazi si ni hayo tu?" (Katika siku ambayo nimejihisi mdhaifu ni leo)

Caryn: "Hapana! sio hayo tu, Pia una shida katika kuongea japokuwa tuko pale pale kwenye confidence, nimekusoma wewe ni mjanja ambae huna confidence, Sasa ukiongea mbele ya mtu ambae hayupo Makini atajua una confidence kumbe ni ujanja tu, So you should talk like gentleman with confidence"

BM: "Dah! Leo kazi ninayo, kama mambo yenyewe ndio haya nyumbani kule si wanapata shida sana?"

Caryn: "Nadhani utakuwa umenielewa, acha niende straight tu the point, Japokuwa nilikuuliza swali mara ya kwanza ila ukaleta ujuaji, Yule kijana uliyemleta siku ile nyumbani na wadogo zake, Mzee kasema kamtafutie nyumba umpangie halafu utaniambiaa Kodi ni kiasi gani nikupatie pesa ya Kodi ya miezi sita, hiyo ni moja mbili Sasa, Amesema umpatie pesa ya mtaji afanye Biashara na uhakikishe katika hiyo Biashara atakayofanya huyo kijana ndani ya miezi sita iwe imeshasimama na waweze kujilipia Kodi,"

BM: "Biashara gani sasa na mtaji kiasi gani?

Caryn: "Hapo kwenye Biashara amesema wewe ndio utakayemchagulia na mtaji pia hajakuwekea limitation kwasababu wewe ndio utakayetoa hiyo pesa ila ameweka vigezo katika nyumba utakayo watafutia, Amesema Nyumba isiwe chini ya shilingi laki 1"

BM: "Dah! Baba yako sijamuelewa hapo kwenye swala la nyumba tu, kwasababu kama mm mtu ambae najiweza nakaa nyumba ya laki na nusu iweje yule kijana tumtafutie nyumba ya pesa yote hio Ikiwa ndio anaanza maisha?"

(Kabla ya kujibu Caryn akacheka kwanza)

Caryn: "I'm so proud to have him as my Dady, Sasa acha nikuambie ni Kwanini amekuwekea vigezo hapo kwenye nyumba, Cha kwanza hapo Dady ameshaku limit katika upande wa kuchagua Biashara, kwasababu asingefanya hivyo ungemtafutia tu yule kijana chumba Cha elfu 10 halafu ungempa na mtaji wa Biashara ya karanga"

BM: "Mbona kama mtihani wenyewe nishafeli, kwasababu ili mtu aweze kula na kufanya mambo mengine na aweze kulipa Kodi ya laki moja kwa mwezi basi hiyo Biashara mtaji wake usiwe chini ya milioni 1"

Caryn: "What do you mean? huna hiyo pesa?

BM; "Tatizo sio Pesa, nawaza ni Biashara gani hiyo yule kijana ataimudu kuendesha ya kiwango hicho Cha pesa"

Caryn: "Ndio maana mwanzo nilikuambia nieleze kuhusu kijana ili nikishakupa haya maelezo niweze kukushauri lakini ukajifanya mjuaji"

BM: "Yule kijana kwanza kaishia form 3, katika kumuhoji kanambia hajawahi kufanya hata Biashara ya mtualikua anaishiaga kupata vibarua vya kawaida tu"

Caryn: "Too late, hili swali ulitakiwa ulijibu pale pale nilivyokuuliza, kwasababu unaweza kuulizwa swali Dar ukiwa unaelekea Mwanza na usione mantiki kwenye swali uliloulizwa ila ukifika Mwanza sasa ndio akili inakukaa sawa na hapo inakuwa too late, So next time uwe Makini ukiwa unazungumza na Mimi"

BM: "Kwahiyo unanisaidiaje katika hili?"

Caryn: "Cha kukusaidia labda nikupe maelezo ya mwisho ambayo ndio ya umuhimu zaidi, Baba Amesema ukifaulu kwenye huu mtihani basi na wewe utakuwa katika nafasi ya kutaja kiasi chochote cha pesa as mtaji wa kufanyia Biashara

BM: "Caryn! some jokes are too experience, you don't meat it.... right?"

Caryn: "I am serious but don't cheat on this, I know my Dady....have a wonderful night"

Caryn ndio ameenda hivyo, na mazungumzo yakaishia hapo


Nakumbusha huu mtihani nilipewa kabla sijapewa likizo ya lazima, so Wakati nikitafakari vile nitafanya ili kufaulu mtihani wa Mzee ndio stress nyingine ya Ofisini ikaja

Wadau natoboa kweli hapa kwenye Situation zote mbili? TRUE STORY



MWISHO
Hongera. Story inaweza kuwa ya kweli lakini maneno mengine ni ubunifu wako.

Skia kijana, wewe na Careen wote mko ktk kipimo ila mzee anajifanya kama amemkamisheni Careen kwako. Ila ambaye yupo zaidi katika mtihani ni Careen na siyo wewe. Mzee anataka kumpima bintiye kama anaweza kuhimili biashara na mahusiano. Hiyo biashara unayotaka kuanzisha ni kipimo cha Careen kuisimamia. Wewe utaripoti kwake na yeye ataripoti kwa mzee. Na wote kwa wakati wenu mtakuwa mnaripoti madhaifu yenu kwa mzee.
Mzee anaona bintiye hana uelekeo ktk jambo fulani la biashara au mahusiano. Na dada mkubwa alikuwepo kukusoma. Yule kijana anayekudrop anafahamu kuhusu Anne na mengi ya kwako na anaripoti kwa mzee kwa mamamuzi why? Hawezi kukuamini hivyo bila kujua vitu kadhaa kuhusu wewe.

Siku utakayoamua kulala na Careen umefeli. Ukioa Accountant umefeli. Acc, Carleen na Anne Wakigombana umefeli.
Biashara ikifa unaweza usifeli.

Baishara ni hiyo ya vifaa vya pikipiki, nguo hapa tafuta meza Manzese au karume au sehemu yoyote au chakula good luck.


Na wamekupa Careen as a lamb to hyena wakupime na wampime pia.
 
Kwanza unatakiwa umu inspect huyo mtoto anawaza nini kichwani ujue familia yake na nani yupo nyuma yake wewe unaweza ukamsaidia kwa hayo halafu akaja kufelishwa na watu/mtu wa karibu yake either baba,mjomba,kaka au somebody else anaemuheshimu changa karata zako vzr jua anapendelea kufanya nini cha kumuingizia kipato....
Kuhusu biashara mpe kozi kwanza ndogo ya kujua ufundi pikipiki/bajaji kwenye kijiwe chochote cha mafundi then mfungulie Duka la spare parts na kwa kuwa yeye mwenyewe atakua na ufahamu atamudu na kwa kuwa ana wadogo zake nao watamsaidia na watapata elimu ya ufundi
Yeah dats true, ndugu zao wengi amedai wapo Mkoani aliambiwa mama yake kipindi yupo hai ila hajawahi kuwaona, na Mama yao alivyofariki Mzee alioa tena mwanamke mwingine na matatizo ndio yalianzia hapo

Mzee wao ni Mr Don't care madogo walivyoona matatizo yanazidi wakajikaa...ila pia haya yote Bado yanahitaji uchuzi
 
Kichwa cha habari kilitakiwa kuwa "hatma ya maisha yangu yapo mikononi mwa Accountant na mafanikio ya kijana wa Buguruni".
Hiko pia kipo sawa lakini kirefu sana bhana, nilikuwa nataka kifupi, Yani mtu bila kufungua Uzi awe ameshasoma heading yote
 
Acha tuone likizo yangu ya job ikiisha mambo yatakuaje huko Ofisini maana hadi Sasa hivi nipo njia panda sijajua niamue lipi

Halafu na Mzee nae Hata hajamaliza mwezi tangu ameondoka, so wacha tuone itakuaje akirudi Bongo kwasababu hapa ndio nipo mikakati ya kufanya zoezi lake, So let us wait and [emoji102]

Kuhusu mapenzi sina msaada nawe kama n muislamu chukua wote( ulinde future)

Tuje kwa huyo kijana wa buguruni, kwanza biashara sio kila mtu anaweza ukizingatia umri wake.

Mtafute jenga urafiki nae umuulize ndoto zake ni nini?

Msome ni mtu wa dizaini ganii? Kwamba akipata kitu anajisahau au atapambana ili wadogo zake nao waishi maisha bora.

Kwa umri huo anaweza kujifunza vitu vilivyo ndani ya ndoto zake lakini sio katika mfumo rasmi( kuingia secondary) kama vile ucapenta,gereji,udereva,lugha ukishamjengea uwezo atasimama kujipambania yeye na ndg zake,hawa watu wakipataga upenyo wanatoboa.

Kuhusu kufaulu ili upewe mtaji kwa bei uitakayo wewe usiingie tamaa mzee anakutengenezea konection kubwa sanaa ambayo hiyo unayowaza wewe kwa sasa haitafikia iyo thamani.

Nikimaanisha kijana kwa mazingira aliyopitia Mungu akamsimamia akawa ana nidhamu ana nafasi kubwa ya kutoboa kimaisha na wewe utakua ndie God Father wake.
 
Na kwann umfanye Annie mnyonge?? Kisa leo unacho..kisa hupendi kusikia ukweli..au kisa ni mnyenyekevu na mpole and she loves you dearly... Au ni kwamba kujikuta mi ndo mwanaume huku ukiwa kwa accountant na mama ake unachutama na kwa Caryn mwenyewe unasalute ngoma isambee....

My take fanya maisha yako. Hapo ofisi ulioko ni shetan alipomuonesha Yesu vingi akamwambia ukinisujudia....if you can be ready kutoka hapo. Kwa mzee kuna mtu katoa ushauri mzuri sana i think Dona..kuwa anaweza aje kukufanya his puppet...not actively rather passively so every time you be submissive..usije jikuta waabudu mwanadamu..just be careful wit this option too...

Ushajifunza meng up to now mkuu its high time you get a life. And dont treat Annie like a clown simply coz she is too weak to get back to you. If you lose her one day you will wish you treasured her more...thamini mwanamke mzuri na good thing kila mtu anaesoma uzi huu kamcommend so akili kumkichwa. She is a woman and a half..usijitie alpha male kwake...ukastep on her beautiful and submissive heart...

Actually fanya uonavyo maisha ndo haya haya...
Sijamaamisha kumfanya mnyonge Ile Pasee ila nilimaanisha heshima na utii anayotakiwa kuwa nayo Mwanamke kwa Mume wake

All in All nimependa mstari wako wa mwisho
 
Endapo hii story ni ya kweli....Basi ushauri wangu ni huu ufuatao..

1) Usithubutu kumuacha Annei

2) Mwambie mama hali halisi kuwa kwa bahati mbaya huwezi kumuoa binti yake kutokana na sababu za msingi ambazo unaweza kuziweka wazi

3) Mwambie mama upo tayari kuendelea na kazi hapo ofsin kwao hata kwa cheo hicho hicho ulichonacho na asikupe huo U-director kama incentive ya kumuoa bintiye. Kama wewe ni mtu wa masuala ya imani, kuna kitu inaitwa KARMA ambayo huwa ni real kwenye maisha japo watu huwa tunapuuzia.

4) Ukifukuzwa kazi kwa sababu umekataa offer ya kumuoa binti yake usiogope, unaweza kupata misukosuko kidogo ila baada ya muda utakuwa sawa na utakuwa na nafasi ya juu zaidi baada ya misukosuko. As long as unafanya mambo yako kwa uaminifu, narudia tena KARMA is REAL.

5) Usithubutu kabisa kufanya mahusiano ya kimapenzi na hao binti wa huyo mzee. Acha kabisa, USITHUBUTU (Huu ushauri hujaomba ili nimeweka kama bonus tu).

6) Kuhusu biashara ya huyo kijana, pitia mawazo ya watu hapa kisha utafanya uchambuzi uchukuwe wazo mojawapo. Ila kwa upande wangu, kutokana na ulivyomwelezea huyo kijana wa Buguruni, unaweza kumsaidia awe na CAR WASH pamoja na Saloon (A decent barbershop) ya Kiume. Hivyo vinaweza kumfaa endapo utafanikiwa kupata location nzuri na SALOON ikawa ya kisasa, provided Mzee yupo tayari kulipia gharama yoyote.

Ni hayo tu. Za kuambiwa changanya na zako. Kila la kheri Mkuu.
 
Back
Top Bottom