Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Me Najua basi, hilo neno mm si nimelirukia kwa Michelle ambaye ni Dada yake na Caryn
Hahaha uko smart sana mkuu, ila story bado sio ya kweli. Uko tayari nikupe mtego mwingine au niache?
 
Hahaha uko smart sana mkuu, ila story bado sio ya kweli. Uko tayari nikupe mtego mwingine au niache?
Leta huo mtego, nataka uridhike kwamba hii story ni ya kweli
 
Carleen unamuona mnyamwezi mwenzio 😅😅😅🔥🔥🔥
 
Kuna episode ulisema ulipokea SMS ya Mzee na Annie asubuhi. Je, unaweza kuscreenshot hizo sms tuzione.

Ukiscreenshot nakuruhusu kucrop ili tusione namba zao ila ukicrop pale kwenye tarehe paache ili tuhakikishe tu kwamba sio za leo..
Mkuu Ile simu ilipotea bhana, tena nilipoteza kizembe sana, nakumbuka hiyo siku nimetoka Zanzibar nikapeleka mizigo store Sasa nahakiki mizigo niyoifikisha niliwasha tochi ya simu nikampa mmoja wa wale waliokuwa wanashusha mizigo animulikie maana umeme ulikatika, Sasa nilivyomaliza nikaondoka zangu nikasahau kuchukua simu, kesho yake namuuliza yule jamaa akakataa kabisa kuwa sijampa simu, akadai eti nitakuwa nimechanga labda niliyempatia nimemsahau

Ila wale vijana paka Leo wapo wote wanapiga kazi hakuna aliyeondoka, ange'miss' mmoja ningemshuku huyo huyo
 
Hahahahahaha sawa mkuu..

Tuendelee na episodes..
 
Hahahahahaha sawa mkuu..

Tuendelee na episodes..
Likizo yangu inaisha August 9, na Mzee sijajua tarehe rasmi ila kuanzia September 20 maana ndio itakua imepita miezi miwili na nusu, Kuanzia hapo kama kutakuwa na jipya tutajuzana mkuu

Ila kwasasa matukio ni ya kawaida hayana changamoto, labda Kijana wa Buguruni alete miyeyusho
 
Kwahiyo Kazini kule nisiwaze sio....haya je ikitokea kama ulivyosema kati ya Annie na Caryn unadhani wapi ni chaguo sahihi?
Hapo ni annie tu, kama huyo caryn ana akili timamu ukimueleza kilichojiri ataelewa.
 
Ushaur gan ni ushauri gan.wewe tulia mpe huyo kijana mtaji wa kufanya biashara ya vitumbua na juis wewe mtafutie baiskel design jiko lake awe anachoma vitumbua pia hapo jipange
 
Duh! Huu ushauri wako kiboko, ila wala sio kupenda vya bure Dada angu, sema unajua nini? Opportunities kama hizo are very rare to find, so if you find them, grab them keep them and handle with care
 
Annie: Okay! i trust you BM, you can go ahead, but remember not everyone in this life gets a second chance to RIGHT their wrongs
[emoji848]Mimi sijaandika hivi mkuu
 
Hapo ni annie tu, kama huyo caryn ana akili timamu ukimueleza kilichojiri ataelewa.
Hata hivyo Caryn mm namuogopa, nishamzoea mnyonge wangu Annie, nikimuambia nyamaza ananyamaza, huyu Caryn tutawezana kweli?
 
Mhh bro hapo kipengele,mzee anakupima hapo sidhan kama kweli mtu unaanza life kwakupanga room ya gharama namna hyo na biashara ya mtaji kama huo....hapo kaka inabidi ufanye mambo katika uhalisia isionekane unaamrishwa cha kufanya fanya kama ambavyo anataka but be realistic.

Kuhusu likizo nadhan hapo inabidi ujiandae kisaikolojia kwamba kazi hamna na mzee itakuwa vyema asipojua...focus na shamba darasa la dogo ila be really[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ni wapi ulisema ana hiyo miaka? Umemwita teenager au maana ya teenager hujui?
Hakumuita teenager, ila alisema dada yake yaan Michelle ndo alimuita hivyo wakat Caren anatoa ushauri wa kuwasaidia hao watoto
 
Dah mkuu sawa kama huamini lakini mazali yanatokeaga tu mkuu japokuwa Mimi siyachukulii kama ma'zali'

Kuhusu Dada wa kazi yupo yule wa kuja na kuondoka na haendi Kila siku

Mlinzi pia Sasa hivi ameshawekwa ila mwanzo alikuwa hayupo, unajua na nyumba yenyewe ni mpya mpya sio ya kitambo, kama unakumbuka katika story nilielezea kwamba Mzee anajenga nyumba ya mlinzi pembeni ya Geti, so alifanikisha Hilo kabla ya kusafiri
 
BM X6 wewe ni kijana mdogo sana bila shaka na pia ni rika la vijana wa kileo , najua una ndoto ndugu na unahitaji kuzifikia kabla haujaswaliwa au haujazikwa, sasa ndugu BM X6 ipo hivi÷

Kama ujuavyo kwa kimalikia wahenga wanasema GOLDEN CHANCE NEVER COME TWICE , ila pia binadamu hubadilika si Annie wala accountant sasa jitizame wewe ni wapi umetoka kimaisha na kimaadili alafu waza ni kipi unahitaji mbele

Annie ni mwanamke wa moyo wako na maisha yako ila accountant n passer girl kama wale wengine uliolala nao hivyo

Annie hata umsaliti leo ila ataendelea kuwepo kama ni mipango ya yule Mungu unayemuabudu ila kama si mipango yake hatakuelewa na mtaishia hapo

Sasa ni hivi nenda kamvishe pete Accountant ili ule shavu ila kumbuka kujiwekeza mpaka pale utapoona sasa unaweza kujisimamia bila kampuni huku binti kimwali Annie mueleze uhalisia akupe muda kama ni miaka miwili hata saba sawa ili ukamilishe mission yako

Akikubali akikataa ni non of your bussiness ili ufikie kwenye ndoto zako kwanza , usiseme ni dhambi kwani umefanya mangapi mpaka sasa ambayo mengine hata kuyasema huwezi na usisaha hautakuwa wa kwanza kupambania ndoto zako kwa ubaya ilimradi ufike pale unapoota .

Sasa huyo kijana wa buguruni , ndipo penye sehemu ya kukusaidia wewe na Annie mdumu au muachane kwanini ?
Sababu ikiwa huko utafanikisha basi hata kazi waweza kuacha ili ufanye mambo yako na binti kimwali Annie .

Nenda sehemu za stand either makumbusho au mbagala zakiem au keko karibu na kituo cha polisi omba nafasi fungua duka lenye atleast wa mtaji wa milioni tano na huduma za m_pesa na huduma za kibenki hasa za miamala na pia uza vinywaji hapo vya kila namna , hii itakufanya hata kwa siku asikose hata elfu sabini kwa siku .

Ila kaa kitako na huyo kijana muombe awe msiri kwa mzee hiyo biashara ifanye yako ila yeye ndiye msimamizi ila baada ya miezi sita utamkabidhi , ndugu BM X6 hakikisha hiyo biashara unaisimamia vizuri mauzo na kila kiingiacho na kitokacho ila usisahau kijana ana wadogo zake hivyo wanahitaji huduma pia

Ndugu yangu poteza kidogo upate kikubwa hivyo jitahidi sana uwe unatoa kidogo katika kale kamshahara kako ili uwatunze wale watoto pasipo kujali kwenye biashara uliyofungua ukizingatia nahisi kapochi kako katanona baada ya kupanda cheo hapo kwa mama mkwe [emoji1787][emoji1787].

Mwisho ni kuwa hakikisha faida ya kipindi chote cha miezi sita aliyotoa mzee , hakikisha unaitunza kwa account ili baada ya miezi sita iwe ni starting point ya KIJANA WA BUGURUNI ili aishi vyema

Kaka kama ukifeli katika biashara hiyo basi nenda chuo chochote ila nakushauri vyuo vifuatavyo DUCE , NIT NA UHASIBU mara nyingi tenda za wauza vyakula(wazabuni) maeneo hayo uwa hazidumu sababu ya usimamizi mbovu hivyo kushindwa kulipa kodi kwa vyuo husika .

Sasa nenda mtafute muhusika mpoze kidogo akupe tender kwenye hiko chuo utachopata na hapo tayari utatakiwa kuwatafuta wapishi ambao ni akina mama ila hakikisha kijana wa buguruni awe ni msimamizi wa mwisho katika hiyo biashara na kipindi ambacho wewe haupo ila faida na expenses za hiyo biashara zote zipite kwako .

Nakuona unaniuliza mbona vyuo vinaenda kufunga sasa , hapana BM X6 nimekutajia vyuo ambavyo the whol3 year wanafunzi wapo sababu hawatoi degree tu ila hata certificate na diploma hivyo kujikuta mwaka mzima wapo wanafunzi around hayo maeneo

Ndugu kwa haya nakuona ukipewa hiyo hela ya biashara na kuanza mambo yako na kumrudia binti kimwali Annie kwa kumpa talaka takatifu ndugu ACCOUNTANT .

Japo katika biashara hiyo ya vyakula hakikisha mzee akupe angalau milioni kumi ya kufanya biashara ila usisahau kuwa systematic katika kila jambo ili hata mzee asikuwaze vibaya kuwa muwazi na ukiamua kumpiga mpige kisomi au sio ndugu yangu Mtanzania ? (In magufuli's voice)
USIOGOPE KUFANYA LOLOTE SABABU MPAKA SASA NI MENGI YA DHAMBI UMEFANYA HIVYO TENDA KADRI YA MOYO NA HULKA ILI UIONE KESHO ANGAVU

Ushauri tu ndugu yangu BM X6

TEKERI.
 
Blaza huu ushauri wako ni konki sana[emoji1544], nimeusoma wote ila kwa heshima zaidi naomba niusome tena badae kwa utulivu kabisa ili kama Kuna Cha kukuuliza nikuulize mapema[emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…