Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Huwa nasema kila siku ya kwamba,baadhi ya watanzania wana matatizo ya utindio wa ubongo lakini sieleweki,yaani mtu kavurugwa na maisha huko anataka hasira zake aje azimalizie kwenye nyuzi za watu hapa Jamii forum,Kwanini hambadiliki?

Kila stori zinapoletwa hapa Jamii forum ziwe za maisha ya kweli au zile za kutunga basi lazima hao watanzania baadhi niliowataja hapo juu wataanza vituko,iwe kupinga,iwe kukatisha tamaa,iwe kukejeli,iwe matusi n.k,huu ni utindio wa ubongo kwasababu hakuna mtu aliye na akili timamu akawa kila uzi ni kupingapinga tu na kukejeli bila sababu za msingi.
Hebu badilikeni,acheni haya mambo ya kipumbavu.

Kama unaona ni chai na wewe nenda kachemshe yako ukanywe na familia yako!.

Kama unaona stori inawekwa mambo mengine yasiyokuwa na ulazima nenda kaanzishe ya kwako na ukaweke mambo ya msingi ili wanaopenda mambo ya msingi waje wasome.

Mleta mada kaamua kuweka kila kitu ili kupunguza maswali ya baadhi ya watu ambao huwa wanapenda maswali yasiyokuwa ya msingi,lakini bado pamoja na hilo kuna wajinga hawataki!.

Bado mtu anatumia muda wake mwingi kuandika stori yake akiwa na maana watu wajifunze lakini baadhi ya wapumbavu wanakejeli na kukatisha tamaa!

HIVI NYIE WAPUMBAVU MTABADILIKA LINI?,MBONA MENGI YENU NI MAJITU MAZIMA LAKINI AKILI MNAZIDIWA NA KUKU?

HAMTAKI KUSOMA PITENI KUSHOTO LAKINI SIYO KUMPANGIA MWANDISHI NINI AANDIKE NA NINI AKIACHE!.

BADILIKENI WAPUMBAVU NYIE!

#USIPOBADILIKATUTAKUBADILISHA
Umekech bro, though siko miongoni mwa hao unaowaita wapumbavu ila sidhan km its even that serious bro
 
Watu mnaofarakana humu kwny huu uzi mnazngua,your life your choice,msilazimishane watu waishi kwny njia zenu,story ndefu achana nayo pita kushoto,Stori ya uongo achana nayo pita kushoto!!

JF ina mitaa mingi,tafuta chimbo lako uko kaengage uache matusi ya kisenge

Wabantu tujifunze kuwa positive kwny mambo kama haya ambayo hayavunji sheria za nchi wala kuingilia uhuru wa mtu!![emoji419][emoji419]
 
Huwa nasema kila siku ya kwamba,baadhi ya watanzania wana matatizo ya utindio wa ubongo lakini sieleweki,yaani mtu kavurugwa na maisha huko anataka hasira zake aje azimalizie kwenye nyuzi za watu hapa Jamii forum,Kwanini hambadiliki?

Kila stori zinapoletwa hapa Jamii forum ziwe za maisha ya kweli au zile za kutunga basi lazima hao watanzania baadhi niliowataja hapo juu wataanza vituko,iwe kupinga,iwe kukatisha tamaa,iwe kukejeli,iwe matusi n.k,huu ni utindio wa ubongo kwasababu hakuna mtu aliye na akili timamu akawa kila uzi ni kupingapinga tu na kukejeli bila sababu za msingi.
Hebu badilikeni,acheni haya mambo ya kipumbavu.

Kama unaona ni chai na wewe nenda kachemshe yako ukanywe na familia yako!.

Kama unaona stori inawekwa mambo mengine yasiyokuwa na ulazima nenda kaanzishe ya kwako na ukaweke mambo ya msingi ili wanaopenda mambo ya msingi waje wasome.

Mleta mada kaamua kuweka kila kitu ili kupunguza maswali ya baadhi ya watu ambao huwa wanapenda maswali yasiyokuwa ya msingi,lakini bado pamoja na hilo kuna wajinga hawataki!.

Bado mtu anatumia muda wake mwingi kuandika stori yake akiwa na maana watu wajifunze lakini baadhi ya wapumbavu wanakejeli na kukatisha tamaa!

HIVI NYIE WAPUMBAVU MTABADILIKA LINI?,MBONA MENGI YENU NI MAJITU MAZIMA LAKINI AKILI MNAZIDIWA NA KUKU?

HAMTAKI KUSOMA PITENI KUSHOTO LAKINI SIYO KUMPANGIA MWANDISHI NINI AANDIKE NA NINI AKIACHE!.

BADILIKENI WAPUMBAVU NYIE!

#USIPOBADILIKATUTAKUBADILISHA
Afu kweli.Kun watu wapo hvy humu.Anasoma uzi au wakat mwngn hasomi.Neno analowaza kichwani tu nikusema CHAI
 
huyo kijana wa buguruni ambae kashikilia hatma ya maisha yako mbona kama anakuwa minor character, hujamgusia hata chembe kama uzi unavosomeka.
 
Ilipoishiaa[emoji1484]

Tukaagana mzee alinichukulia moja ya tax zilizokuwa zimepark nje ya Ile hoteli, yeye akaingia ndani ya Alphard akaondoka na Mimi nikashika njia ya kuelekea Tabata

Inaendelea [emoji1484]

Tax ilinifikisha hadi mjengoni kwangu Tabata I mean nilikopanga, (hamkawii kusema "mbona mwanzo wa story hukusema kama umejenga[emoji849]) nikaingia mjengoni, nikakuta nyumba ipo kimya, Leo nilikuwa nina jambo na Wifi/Shemeji yenu, so nilijua nitamkuta kashafika nikampigia simu ikawa inatumika, nikaachana nayo nikaenda zangu kuoga, natoka kuoga nikasikia simu inaita nikaipuuzia nikawa nachagua nguo za kuvaa, Sasa nimemaliza kuvaa nashika simu ili nimpigie wifi yenu kumbe Ile missed call haikuwa ya kwake kama nilivyodhania, Ilikuwa ni missed call ya Mzee,

Nikampigia akapokea vipi Mzee ulifika salama "yeah Nilifika muda kidogo, nilikuwa nataka kukuuliza Kuna Kitu chochote ulisahau huku au Kuna Kitu umepoteza?" hapana mzee sidhani kama Kuna Kitu nimesahau au kupoteza "Inaonekana una shida kwenye swala la kumbukumbu, Kuna bahasha hapa niliiona tangu jana, leo nimefungua ndani nimekuta Documents za TRA na nimejua ni ya kwako kwasababu nimeona Jina la Kampuni yenu" Dah kweli Mzee nilisahau kabisa nilitakiwa kumpatia Accountant ile Ijumaa lakini hakuwepo......tulimaliza kuongea na Mzee akanambia nizifuate nikipata muda sababu wiki hii yote hatokuja town wala Ofisini kwake

Nikamcheki tena Demu wangu (anaitwa Annie, really name, hii code haina madhara nikiifungua) kupiga simu bado inatumika, nikaona hii ni too much Sasa, Dakika 30 zimepita mtu bado anaongea na simu tu, nikaona nikiendelea kumuwaza nitajipa stress tu nikawasha zangu Tv nikaweka Series ya Kings of Jo'Burg Wakati na naendelea ku watch katikati ya series huko Demu ndio anapiga eti, makasiriko kama yote na ananijua akaanza kuomba msamaha, kabla hajaongea sana nikaanza kumpa lecture uzuri wa Demu wangu nikiongea yeye huwa anakaa kimya kunisikiliza hadi nimalize

Nikaanza kumsomea>>>Nimeenda kuoga nimemaliza naweza movie naangalia karibia inaisha na wewe ndio unamaliza huo mkutano wako au siku hizi umekuwa Customer care na huniambii, kama umekua Customer Care inabidi uwe special phone wenzako hawatumii hizi simu za kawaida, Simu ya mkononi ilimaanishwa kuongea 'less than 10 minutes' kwasababu 'microwave' zinazosafirishwa na simu yako ukiongea zaidi ya dakika 10 una increase level yao inakuwa troublesome kwa brain yako kwasababu hizi simu tunazotumia zipo wireless.

Akajibu kwa upole "Sawa umeeleweka Boss lakini mimi nilikuwa nakuomba msamaha kwa kuchelewa kuja huko, aliyekuwa anaongea na simu sio Mimi ni rafiki yangu alikuwa anaongea na bwana ake ndio nilikuwa namsubiria amalize ili nikupigie" Okay mambo yasiwe mengi wewe kama unakuja we njoo ila hakikisha umebeba chakula Cha Supper kabisa (mida hiyo ilikuwa around 6:+PM)

Kweli bhana mchuchu kwenye saa mbili mbili hivi akawasili, tukapiga misosi watu wakashiba, Sasa Demu wangu nikiwaga nae ni lazima ashike simu yangu huwaga siwekagi password Sasa akiwa nayo yeye moja kwa moja anaenda kwenye messages kuangalia Jina la H....Accountant kuangalia kama kuna chats zote akikosa anaenda kwenye Call Logs anaangalia kama nilimpia au alinipigia akikuta vyovyote vile anaangalia muda tuliotumia kuzungumza akikuta zimezidi dakika 3 tu, basi anajua hayo maongezi hayakuwa ya kawaida, Sasa Leo katika kupekua akakuta nimeongeza na H.....Accountant kwa dakika 11 kesi ikaanzia hapo "kweli hizi Dakika zote mlikuwa mnazungumzia kazi tu au ndio hivyo tena nijihesabie Sina changu" Nikaona huyu kashaanza kesi zimeanza kufufuliwa upya

Iko hivi, kwenye hii Kampuni ninayofanya kazi sasa hivi nilipata kazi kupitia huyu H...Accountant ambaye nilisoma naye na nilikuwa namsaidia mambo kadhaa yanayohusiana na taaluma, Sasa huyu Demu bana tangu tupo chuo ananipendaga sema alikuwa anashindwa kunichana Sababu ya misimo yangu, ila mm simuelewi (kipindi hiki ndio nilianza Mahusiano na Annie) Sasa tulivyomaliza chuo Mimi nilivyoona ramani hazisomeki nikajikataa zangu nikaibukia Nairobi, hustle sana huko ngoma bila bila,

Nakumbuka Siku moja nimetoka Bypass ya Ruai naelekea Utawala kwa Chief (Quick mart) nimepanda matatu (Daladala) Ile matatu ilikuwa na wi-fi password wameandia chini ya screen, nikatumia fursa ili pesa ya Bando ikafanye mambo mengine, Sasa ile nimeconnect tu message ya kwanza Whatsapp ni ya huyo H....Accountant (wakati huo nilimsave tu H.....hiyo 'Accountant' haikuwepo) Ile msg ilikuwa inasema "BM Kuna nafasi ya kazi ya ***** kama itakufaa nambie nikulindie nafasi" Sasa wakati tunafanya Conversation ilibidi nisishuke stage (kituo) niliyokuwa nashuka kwasababu ya Wi-fi, nilienda kushukia Shutazi (Shooters) ikabidi nitembee kutoka Shutazi hadi mahali nilikuwa naenda kwa Chief

Sasa katika Yale mazungumzo kwakifupi tu ni kwamba nilikubali Offer nikamwambia Accountant najianda siku mbili tatu wiki ijayo Niko Dar es salaam, Hapo ndio nilipoachana na jiji la Stress, ule mji acha tu ningekua muandishi ningetoa kitabu kabisa

Mtu mzima nikaingia Daslam kubadilisha upepo, nilijoin kwenye Kampuni fresh na Kazi ikachapwa ikachapika, nikamuona huyu Demu (Accountant) kabadilika kabadilika Yani zile Fujo za chuoni kule simuoni nazo tena nikajua kakua maana wanasema vitu vingine vinasababishwa na utoto, kumbe Binti ananivutia Kasi ananizoom tu hakutaka papara, unajua hii Kampuni ni yao yeye ndio Muhasibu nahisi alikuwa anacheza na timing

Kuna siku hiyo bhana sitoisahau aliniita Ofisini kwake, nikaketi "naona siku hizi unanawili tu kijana jiji linakupenda hili lakini wewe hulitaki unajifanya kupenda nchi za watu, hivi ni Kwanini wanaokupenda huwapendi?" nikamuuliza unamaanisha nini? "Ukiwa Dar uHandsome wako ndio unakuwa kwenye ubora wake tofauti na ulivyokuwa Nairobi pengine hili ulikuwa hulijui, lakini nina uhakika unajua kwamba Mimi nakupenda. ndio maana nikasema wanaokupenda unawapuuzia!" nikaona huyu kumbe hajaacha mambo yake tu, Nikamwambia swala Dar sijui Nairobi hilo lipo kimaisha zaidi Sababu Nairobi sijaenda kama mtalii nikimaanisha kwamba sijaenda kwa kupenda bali kutafuta maisha, Sasa nilivyomjibu hivyo nikawa ndio nimeharibu kabisa[emoji1544]

"Kwahiyo Mimi kukupenda sio swala la kimaisha, hivi nikuulize unadai kwamba ulienda huko Nairobi kutafuta maisha, hayo maisha uliyapata? badala yake maisha umekuja kuyapatia Dar na hiyo yote ni kwasababu ya Upendo wangu kwako, Yani kama sio Upendo usingekua hapa Upendo wangu unaoudharau ndio unakupa maisha, hivi unajua kwamba Mtu anaweza kukusaidia viatu na bado akakukata Miguu. tunaishi kwenye Dunia yenye Unafki Sasa mm sijataka kuwa mnafki kwako nimekuambia ukweli" hii kauli yake ikazidi kunichanganya, kwanza huu ujasiri ameutolea wapi huyu, nikajisemea tu moyoni Leo ndio Ile siku, mara akaingia mama yake ambaye kwa hapa Tanzania yeye ndio anaiongoza Kampuni, ilibidi maongezi yaishie pale, na huyu Mama ananikubali sana nitakuja kueleza huko mbele ni kwasababu gani

"Tutaongea badae BM" alinambia hivyo yule Demu Mimi nikaondoka zangu....

Turudi Leo,>>>hiyo Sasa ndio sababu ya huyu Demu wangu kuwa na wivu sana sasa Visa vyote nilimuhadithia yani amefikia hatua ananiambia niache kazi[emoji849] ni kama hajiamini anajua muda wowote meza inapinduliwa na Accountant ila kiukweli kabisa Demu wangu ni PISI KALI nyie acheni tu, nampenda sana japokuwa hata Accountant ni Pisi lakini hajamfikia Mama lao,

Nikamwambia Annie kama umechoka nenda kalale hatuwezi kujadili jambo moja kila siku, akaniangalia machoni kwa sekunde kadhaa akaenda Bedroom kinyonge sana, Asee nilibaki naiangalia Ile series lakini haipandi nahisi kama nimemjibu kimkato sana manzi angu, nilizima Tv nikaingia chumbani, nikamkuta wifi yenu amelala lakini yupo macho kama ana waza kitu nikawa najiuliza huyu anawaza ya kwake au ni Yale Yale ya Sebuleni? nikajidai kuzuga nikamuuliza hivi umekuja na funguo zako au itabidi kesho nikuachie za kwangu nikitoka?.....kimya!!![emoji849] nikaona hapa vinyongo vishaanza wale wenye vipaji vya kubembeleza hapa ndio wanahitajika, Nikamwambia Annie unanijua kabisa Mimi upande wa kubembeleza sipo vizuri, naomba niambie tu wewe mwenyewe kama nimekukwaza nijue kama nilikuwa sahihi kukukwaza au nimekuonea "na sitaki unibembeleze ndio maana nilikuacha sitting room" nikamwambia sawa lakini mimi sitaki vinyongo kama Kuna sehemu hujapenda nilivyokuongelesha we nambie, Annie akanipiga jicho flani nikawa nishagundua Kitu

Mimi nipo hivi nikafanya kosa (hasa katika Mahusiano ya kimapenzi) siwezi kukiri tu mwenyewe kwamba nimekosea, hadi uniambie mwenyewe, Sasa lile jicho la Annie ni kama alikuwa anasema ("Yani wewe sijui ukoje") Mwanaume nikakaza nikazima taa nikalala

Asubuhi ikafika mida ya kwenda kazi ikafika ila nikajidai kupitiwa na usingizi kuna nilikuwa nataka kujua, Annie akilala kwangu Asubuhi ni lazima aniamshe hata kama sio siku ya kazi ila kama hajaniamsha Najua Kuna jambo, na kawaida yake huwa anaamka mapema sana, hata kama hana kazi utamkuta anaangalia Movie, halafu aina za Movie au Series anazoangaliaga sasa ni zile za ki Gangster kama Ile Kings of Jo'Burg yeye ndio kaileta,

Sasa zimepita kama Dakika 10 naona siamshwi, nikajua tu huyu mwanamke yale ya Jana bado hayajaisha ninachokipima hakipimiki, nikajiamsha mwenyewe chooni hamna mtu naenda sebuleni sikuti mtu mazingira yakaonesha kwamba huyu mtu hayupo hiyo ni saa moja kasoro Asubuhi, nikaenda zangu kuoga nimeshajianda nachukua simu nitoke kucheki Kuna Messages 2 moja ya Annie nyingine ni ya Mzee,

Ya Annie ilikuwa inasema "Naweza nisiwe mwema leo lakini isikufanye usahau wema wangu wa jana, tumia wema wangu wa jana kunirekebisha ili niwe mwema zaidi, Najua makosa ni ya kwako lakini naomba msamaha Mimi, Naomba nisamehe kama nilikukwaza jana".

Na meseji ya Mzee ndio ikanivuruga zaidi, ilibidi kwanza nikae chini aliandka "kila unapocheka hakikisha unaandaa mazingira ya utakapolilia"

INAENDELEA
Ulisema thready Mbili tu. Sasa mbona haiishi?
 
EPISODE 04, SEASON 1

ILIPOISHIAA

Meseji ya Mzee ndio ikanivuruga zaidi, ilibidi kwanza nikae chini aliandka "kila unapocheka hakikisha unaandaa mazingira ya utakapolilia"

MUENDELEZO

Nikawa natafakari huyu Mzee amewaza Nini hadi kuniandikia msg kama hii. kuhusu Annie hata sikuwaza sana najua kwanini ameandika hivyo, nikaelekea zangu kazini, sasa nimefika kazini nimemkuta Accountant kashafika na si kawaida yake, sijakaa hata kwenye kitu mlango ukafunguliwa kuangalia ni Accountant

"Documents na risiti za mizigo ulizo ziko wapi? I mean mizigo iliyowasili last Friday na Ethiopian Airways"

(Kabla sijamjibu nikajiuliza Leo siku gani?) Leo ni 'Tuesday' eeh? ndio maana! hii siku inakuwa ndefu sana kwangu "siku iwe ndefu iwe fupi naomba hivyo vitu nivipate kabla ya muda wa kazi haujaisha" hata sijamjibu akaondoka

Nikaendelea kuchapa kazi japokuwa Mood haipo kabisa, Imefika Lunch time sijatoka nje Accountant akaja "BM kwani Leo huli?"

Nikamwambia mm nishashiba mbona

"umeshiba? umekula saa ngapi?"

Si mkwara wako wa Asubuhi ulivyotoka tu nikaushushia na Kahawa,

"Ebu nambie ww ulitaka nikuongeleshaje? Pamoja na huo unaouita mkwara lakini hadi sasa hujanipa hizo Documents, hizi ni kazi za watu ujue"

Unajua shida sio huo mkwara wako...japo ungesalimia basi najaribu ku apply politeness katika maongezi yako

"Ooh kumbe tatizo ni hilo! sasa kitu kidogo hivyo ndio umechukua?"

Tuheshimiane tafadhali siwezi kuchukia kwa upumbavu huo, nilikasirika tu kuniletea ma attitude yako asubuhi asubuhi

"Sasa si ndio kuchukia kwenyewe huko"

Siwezi kuhifadhi chuki kwa mambo madogo kama hayo, kwanza tangu lini Mwanaume akachukia? anayeweza kuchukia ni Mwanamke kama wewe, Mwanaume anakasirika tu. Mwanaume ana hasira lakini mwenye chuki ni Mwanamke, Chuki ni muendelezo wa hasira kwani Mwanamke hasahau, Mwanaume ana sahau

"Sasa kama mnasahau mbona mambo ya Asubuhi ameyakumbushia Sasa hivi?"

Madam inaonesha Leo ulijiandaa eeh? tufanye umeshinda, na marisiti yako nitakuletea kesho asubuhi.

Ilibidi tu nimpe ushindi ili aondoke lasivyo tungekesha, Mwanamke anapenda ligi kama kitu gani, hapa ndipo Annie anapochukulia points 3. Sifa ya mwanamke ni upole

Nilikaa kama nusu saa after lunch time nikampigia Mzee, [emoji338]Hello mzee shikamoo

"Marhaba, habari ya Leo"

Nzuri tu Mzee nauliza kama upo nyumbani nataka kuja badae kuchukua ule mzigo

"Nimesafiri kidogo ila unaweza tu ukaenda utamkuta Mama"

Sawa[emoji3513]

Ilivyofika saa kumi na nusu nikachukua kilicho changu nikaitafuta njia ya kuelekea kwa Mzee safari ya 1 hour nikafika nikapress [emoji348] nikafunguliwa Geti, asee bi mkubwa yupo sawa Mzee alijua kuchagua au sijui ni pesa ndio imechangia, Shikamoo Mama

"Marhaba kijana nikusaidie Nini?"

Kuna mzigo nilisahau Nimekuja kuuchukua "Ooh! you are BM right?"

Yeah ndio Mimi, nilivyosema tu ndio Mimi nilikaribishwa hadi ndani usivue viatu zilikuwa nyingi sana

"Karibu sana, sijui utapenda kunywa Nini?"

Juice mama Inatosha (nilitaka kuagiza Maji nikasema hapana, last time nipo kwenye hii nyumba nilifungua fridge nilikuta juice za kila rangi) nikaulizwa ya flavor gan? nikasema Any flavor.

Akaitwa Caryn (code) sijui ndio mdada wakazi Caryn akaja alikuwa Upstairs aisee sidhani kama ni beki tatu, Yani Caryn na Annie Baba alitakiwa awe mmoja,

Basi bhana Caryn (Karen ukitaka kutamka kiBuza) akaambiwa mletee Kaka Juice ya Passion (Mama kalenga mule mule, Passion ndio my favorite) Juice ikaja ikisindikizwa na straw, Mama akapanda upstairs akarudi na bahasha akanikabidhi sikukaa sana nikamuaga Mama, mama akaleta zile za nisubirie hata chakula nile, Nikamwambia mama siku nyingine Kuna sehemu nawahi, mimi huyoo

Sasa nimefika kwa nyumba nikasema nimtafute Annie,

Calling...[emoji338]"Yani nimeamini kweli hunipendi"

Nikamuuliza kwanini

"Kuanzia Asubuhi ndio unanitafita Sasa hivi, hata message yangu hujaijibu"

Wanawake sijui huwa mnashida gani, Yani unanirudisha tena kule kule, Sasa skia ukiwa sawa utanipigia[emoji3513]

Jumatano, Alhamisi Ijumaa, Jumamosi nipo kazini nakaribia kutoka simu inaita kucheki ni Mzee ndio anapiga nikapokea akanambia ndio Yuko Njiani anarudi mjini ila akaniomba nimtafutie 'Land Cruiser Rear Chrome' with LED Light, nilivyotoka kazi nilifanya hivyo ila ila bei sasa duh! kale kadubwana kanauzwa laki 3 aisee. Sasa wakati nipo pale Dukani yule jamaa akaniuliza

"Hiyo Gari yenyewe inayowekewa Iko wapi?"

Nikamwambia sipo nayo mimi nimetumwa tu,

Muujazi akaniuliza "kwahiyo mtaenda ku install wenyewe?",

Nikamwambia ebu ngoja kwanza nimpigie mwenyewe, nilivyomjulisha Mzee Akasema kuhusu installation haina shida itafanyikia nyumbani.

Mzee akatuma pesa laki 3 na 20 ila Nikamwambia jamaa (muhindi flani ivi) itabidi unipunguzie kwasababu mwanzo alinambia hiyo kitu inauzwa laki 3 Pamoja na Installation

Muhindi alichojibu sasa "I can't go lesser than that".

Isiwe kesi nikampatia chake nikachukua mzigo then nikamjulisha Mzee akanambia yeye atafika usiku sana so hii kitu niende nayo kesho

Masaa yakaenda siku ikaisha, Jumapili hii hapa, nilivyomaliza kupata lunch nikajiandaa kwaajili ya kwenda kwa mzee. Nikafika mjengo Safari hii nilifunguliwa gate na Caryn nikakaribishwa kama kawaida Juice Passion ikaletwa,

Mzee saa hiyo alikuwa Upstairs Mama ni kama alitoka maana sikumuona siku hiyo, akashuka nikampatia mzigo wake, kama kawaida tukaenda Backyard tukaketi huko

Mzee akaniuliza Habari za kazi pale nikamjibu hapo hapo nikamuuliza kuhusu Ile msg yake alikuwa anamaanisha Nini?

"Ndio uhalisia wa maisha, utacheka lakini Kuna wakati Utalia, Kuna wakati kusheherekea na Kuna wakati wa kuomboleza &. vise versa"

Wakati tunaendelea na mazungumzo alichukua simu nakumpigia mtu wakaongea Dakika chache wakamaliza ila katika mazungumzo nimemsikia Mzee akimuomba huyo mtu wheelbarrows, hicho kitendo kilinifikirisha kidogo kwa uwezo wa alionao Mzee wheelbarrows ni zakukuta stop, ilibidi nimuulize Mzee wheelbarrows za kazi gani?

"Wheelbarrows zakutumia mafundi nataka kujenga nyumba ya mlinzi pembeni ya Geti"

Nikamwambia Mzee hizo hata Mimi naweza kukuletea

"Wala usijali kijana wangu, labda nikwambie kitu pengine ndio utanielewa zaidi Mungu akikubaliki ukiwa na Utajiri tafuta cha kuomba kwa ndugu zako wanaokutegemea kwa kila kitu ili wajisikie kumbe na wao ni wa thamani mbele yako, itaongeza upendo na mshikamano"

Ooh sasa nimekuelewa ila inaonekana ndugu zako Mzee wanajivunia kuwa na wewe, Matajiri wengi wanapesa za kutosha lakini ndugu zao wanakufa njaa

"Hapana BM usitupe lawama kwa watu wenye pesa tu, hata hao masikini wanakosea sana, unajua unapo waomba Watu Pesa Kisha Wakakunyima utawasema Kuwa Wamebadilika Kumbe wewe ndiyo umebadilika sababu Zamani haukuwa na tabia ya Kuwaomba, Ila Sasa hivi umebadilika na Kuanza Kuwaomba, mfno mzuri ni Mimi mwenyewe wakati naanza maisha Sina kitu, jambo jema ni kwamba nilipa mke Bora ila kwa upande wa ndugu hakuna iliyenijulia hali hata kwa bahati mbaya na nikisema niwatafute mimi niwasalimie sikupata mapokeo mazuri"

Wow kwahiyo mzee unataka kunambia huyu mke wako wa Sasa hivi ndiye uliyeanza naye maisha? hili swali kabla hajanijibu Mzee akaniuliza kama nna Girlfriend/mchumba mawazo yote yakaenda kwa Annie, nikamjibu ndio ninae

"Okay vizuri ila unatakiwa kuwa Makini katika kupata mtu sahihi, Mimi pamoja na mafanikio yangu yote mchango mkubwa unatoka kwa mke wangu, unajua kila mtu anahitaji mtu wa kumtia moyo na kusimama naye katika nyakati zake, Wakati mwingine kwenye maisha si vile ulivyonavyo, ila uko na nani? Vitu haviwezi kutupa tumaini au kutuhurumia"

Ni kweli Lakini Mzee kwasasa kumpata mtu kama huyo ni ngumu sana, zamani ilikuwa rahisi ndio maana haikuwa ngumu kwenu kupata mtu wa design hiyo (Mzee hapa alitabasamu)

Akanambia "Hakuna Cha urahisi Wala ugumu kijana wangu, Binadamu ni wale wale sisi hatujaishi na malaika, Iko hivi, Sehemu zozote katika mwili ambapo unapata Utamu ndizo sehemu zinazotoa Uchafu, watu wengi hawaelewi kwamba utamu unaambatana na uchafu. Vijana inabidi muelewe mtu yeyote unaeishi naye sio malaika inabidi pia awe na Kasoro na Dosari"

Sasa wakati tunaendelea na mazungumzo na Mzee, Caryn akaja ila hakufika tulipokaa alisema "Dad your coffee is ready can I bring there?" Mzee akaitikia pale akamwambia alete 2 cups, Caryn akaenda akaleta Kahawa,

Kumbe Caryn ni mtoto pili wa mzee, firstborn yupo Kibaha nae ni wakike.

Katika siku nimeongea na Mzee kwa muda mrefu ni Leo, wakati kawaha zimeletwa hapo hapo nikabadilisha topic nikamwambia Mzee kwa miaka ya hivi karibuni nimepata Idea ya kufanya Biashara **** (naomba nisiitaje kwa sababu maalum)

Akanambia "It's good idea but it just sounds too easy"

Sasa Mzee unanishauri nini kwasababu Sasa hivi natamani kufanya Biashara

"Ndio maana nikakuambia nitakupatia mtihani, na inahitaji umakini ili uuvuke, unajua kuna majaribio 3 watu wengi wanakwamishwa nayo ambayo ni Njaa, Upuuzi na Tamaa katika haya majaribio matatu hili la tamaa wewe huna, na watu wengi Bado wapo katika jaribio la kwanza la njaa, ili ufaulu yote jitahidi kuwa kama State House, majaribu 3 hayo yasisomeke kwako, ukiingia Ikulu utagundua ww ndio una njaa pale njaa hakuna, ww ndio mpuuzi pale Upuuzi hakuna, ww ndio mwenye tamaa, pale Tamaa hakuna, Watu wanao Excel katika maisha ni wafanyabiashara, sio wapuuzi, hawapuuzii hata sent 5. Upuuzi ni kushinda Tamaa na Njaa. Sasa ukiwa Mfanyabiashara na Bado hujashinda tamaa na njaa huwezi kufanikiwa kama unakumbuka last Monday tukiwa hotelini nilikuambia wafanyabiashara wengi wanafelishwa na mambo ambayo pengine wanayajua ila wanayapuuza huo ndio upuuzi"

Dah Mzee natamani kuendelea kusikilizia lakini ndio hivyo tena muda unaenda nisije nikakosa Daladala

Ilibidi nimuage Mzee pale tukatoka backyard tukaingia ndani Mzee akapanda juu Bedroom kwake, Sasa wakati Mimi nipo Sebuleni pale kwenye TV kulikuwa Kuna documentary flani Inaendelea (Jina limenitoka)

Wakati nashangaa nikasikia "Please excuse me, you're obstructing my view"

Kugeuka kumbe Caryn nilikuwa sijamuona, alikuwa kakaa kwa Dinning table, nikataka kumuongeresha Mzee akawa anashuka ngazi, nikakausha

Nikamuaga Caryn pale nikatoka nje na Mzee

"BM hii funguo utampatia **** nitampigia simu aje kuichukua ofisini kwenu Mimi kesho nasafiri tena nitarudi siku ya Ijumaa Asubuhi, nataka niwahi kurudi siku hiyo ili niweze kujumuika na familia yangu ya nje kama unavyojua ni Ijumaa mbili sasa zimepita sijafanya hivyo"

Okay! kwahiyo kumbe Hilo Zoezi hufanyikia hapa hapa nyumbani?

"Ndio, unajua Ile siku nisingeweza kukwambia ukakusanye watoto mtaani ambao huwajui halafu uje nao hapa nyumbani isitoshe Mimi mwenyeji sikuwepo, Mimi huwa nachukua watoto kwenye vituo maalum lakini Safari hii ningependa ukawachukue wale wale wa kule Buguruni"

Sawa Mzee hamna shida

"Okay uwe na usiku mwema "

Nikaachana na Mzee, mimi huyoo

Nikalala zangu mapema, kesho Jumatatu muhimu kuwahi kwenye maofisi ya watu

*******

Fresh Monday with sadness information

ITAENDELEA

Muendelezo soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
 
Wakati nashangaa nikasikia "Please excuse me, you're obstructing my view" kugeuka kumbe Caryn nilikuwa sijamuona, nikataka kumuongeresha Mzee akawa anashuka ngazi, nikakausha

Nikamuaga Caryn pale nikatoka nje na Mzee

"BM hii funguo utampatia **** nitampigia simu aje kuichukua ofisini kwenu Mimi kesho nasafiri tena nitarudi siku ya Ijumaa Asubuhi, nataka niwahi kurudi siku hiyo ili niweze kujumuika na familia yangu ya nje kama unavyojua ni Ijumaa mbili sasa zimepita sijafanya hivyo"

Okay! kwahiyo kumbe Hilo Zoezi hufanyikia hapa hapa nyumbani?

"Ndio, unajua Ile siku nisingeweza kukwambia ukakusanye watoto mtaani ambao huwajui halafu uje nao hapa nyumbani isitoshe Mimi mwenyeji sikuwepo, Mimi huwa nachukua watoto kwenye vituo maalum lakini Safari hii ningependa ukawachukue wale wale wa kule Buguruni"

Sawa Mzee hamna shida

"Okay uwe na usiku mwema "

Mimi huyoo nikaachana na Mzee

Nikalala zangu mapema, kesho Jumatatu muhimu kuwahi kwenye maofisi ya watu

*******

Fresh Monday with sadness information

ITAENDELEA
🔥
 
Back
Top Bottom