Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Ilipoishia

Tukafikà kwenye gari Caryn akaona jinsi gari ilivyo haribika, nikamuona tu anatoa simu halafu akanipa funguo

BM: "Mimi funguo ya nini sasa?"

Caryn: "Unauliza funguo ya nini? we huoni Ulichokifanya?"

BM: "Naona, ila sasa una maana gani mm kunipa funguo?"

Caryn: "Maana yangu ni kwamba unirudishie hio funguo gari likiwa kama nilivyokukabidhi....

BM: "Sasa wewe unarudije nyumbani?"

Caryn: "Mimi nitajua narudi vipi, hata ku request nita-request"

BM: "Ebu acha utoto bhana, uta-request vipi Wakati Gari hili linaendesheka kabisa"
(Nikamshikisha funguo yake mkononi)

Caryn: "BM tunapimana akili sio? for your own good chukua hii funguo na kesho muda kama huu naitaka hii gari iwe imeshakamilika"

Muendelezo

(Episode 15 SEASON 2)

Nikachukua funguo nikajua huyu tayari kashamaindi nikaenda kukaa kwenye gari ndani kusikilizia labda anaweza badilisha mawazo, hakupita muda mrefu kupitia side mirror nikaona IST imekuja ikamchukua, Eeh ndio nikajua kumbe yupo serious na alichokuwa akikiongea

Ikabidi na mimi niwashe mzigo wangu niondoke maana sio gari tena naona kama ni mzigo, nikafika nayo hadi mtaani mida ya saa mbili kasoro usiku nikamcheki mshkaji wangu kumjulisha kwamba nimesusiwa gari, sikutegemea jibu alilonipa mshkaji

Eti "Kama vipi ibuka nalo mtaani twende tukale nalo bata viwanja" nilimjibu tu "kutoka tena itakuwa ngumu nina uchovu wa kutosha'

Ila mshkaji niliona kama ananiletea miyeyusho, Yani gari lina majanga anataka tukale nalo bata kwa mfano likitokea janga lingine? si ndio nitaambiwa nilinunue kabisa gari lenyewe

Kesho yake mida ya saa tatu asubuhi nikamcheki mshkaji akanambia nimuibukie mtaani, nikamuibukia mshkaji sijapita hata ofisini, Nilivyofika mtaani kwa jamaa gari lenyewe nikalipaki nje sikutaka mambo mengi

Mshkaji: "Ivi sijakuambia...yule jamaa wa kuirekebisha taa Jana alinicheki alienda Morogoro msibani ila anageuza leo masaa ya mchana mchana atakuwa kashafika town"

BM: "Dah! Oya kama vipi tukaanze na rangi tuokoe muda, kitambo hadi huyo jamaa ako afie tutakuwa tushamalizana na kipengele kimoja"

Mshkaji: "Lakini kwa ushauri wangu tungeanza na taa ila kwasababu ww ndio unaamua fresh"

MB: "Hizi heka heka za magari kwa huku bongo sijawahi kudili nazo, ni wapi wanafanya panel beating na kupiga rangi vizuri"

Mshkaji: "Sehemu ziko nyingi ila kidogo mfuko wako inabidi uwe umechangamka"

BM: "We twende bhana ila usinipeleke sehemu expensive sana"

Mshkaji akanipeleka Garage flani maeneo ya Mikocheni tumefika garage picha linaanza tukaambiwa tukabidhi gari halafu sisi tuende ofisini kuna viti vya wageni full kipupwe kama tupo njombe, sasa ili kubalance kipupwe na joto la mwili tukaletewa Kahawa ya motooo

Masaa kadhaa kupita tukapewa taarifa kwamba chuma ipo tayari, nikapewa invoice nikalipia, huduma ilikuwa nzuri lakini kibunda nacho kilinitoka

Tukakabidhiwa Gari kwenye majira ya saa nane mchana, Kilibaki kipengele Cha Headlight na uzuri jamaa nae alikuwa kashafika town tukampelekea gari, akacheza nayo chuma ikarudi kwenye ubora wake....siku hadi inaenda kuisha sikuwasiliana na Caryn

Nikamcheki kwenye simu wakati naelekea ofisini ilikuwa saa kumi na moja jioni na dakika zake, simu haikupokelewa kufika ofisini nikakuta wamefunga

Nikasema ngoja nimpigie Michelle pengine yupo nae, Michelle akanijibu kwamba alikuwa nae muda sio mrefu ila ametangulia nyumbani walikuwa waondoke wote ila ni kama Michelle Bado ana viporo vya kazi ofisini

Halmashauri ya kichwa ikanambia hili gari kama lipo sawa halina tatizo nisilale nalo tena, nilirudishe kwa mwenyewe hata kama nimemcheleweshea, wanasema heri nusu shari kuliko shari kamili

Nikatia Gear kuelekea kwa Mzee, nimefika kwa kina Caryn na Caryn mwenyewe hayupo nimemkuta Mzee na Bi Mkubwa, nikasalimiana nao

Mzee: "Gari imeshafaa?"

Ka moyo kakafanya Pah! nikashtuka, (nikajua hapa Caryn kashamchana Mzee)

BM: "Yeah, ilikuwa ni sehemu ndogo tu"

Mzee: "Sasa na yeye amegonga gongaje! mbona ameanza kuwa mzembe, Gari mpya ameanza kuitia viraka"

(Nikagundua hapa kuna venye Caryn kachanganya ukweli na uongo, hiki anachokiongea Mzee ni kama vile amemuambia Gari ameligonga yeye)

Ikabidi na mimi nitambae na beat, alipoishia na mimi niendeleze

BM: "Ilikuwa bahati mbaya tu Mzee haikupata damage kubwa hivyo"

Mzee: "Nilishangaa Jana mtu anarudi bila gari namuuliza akasema kakuachia ili umpelekee garage"

BM: "Yeah, ni kweli na hata hivyo garage kwenyewe nimechelewa kutoka nilivyopita ofisini sikumkuta nikaona nimletee tu huku nyumbani"

Mzee: "Umefanya vizuri"

Sikukaa sana, muda ule ule ikabidi nimuage Mzee maana ningeendelea kukaa pengine ningejichanganya kwenye maelezo na sijui Caryn kamuambia vitu gani Baba ake

Nikarudi zangu kwangu, kesho yake Asubuhi nikatimba ofisini, nikakuta Storekeeper pamoja na Secretary wameshafika Caryn alikuwa bado hajafika na Accountant, nikashuka chini kushtua utumbo na chai ya moto

Kabla hata sijaletewa chai maana ilikuwa Bado ipo jikoni nikaona Bimmer ya Caryn inaingia, akashuka akaelekea ofisini, nilivyoshtua utumbo nikarudi ofisini nikaingia kwa Caryn

BM: "Madam, vipi uko poa?"

Caryn: "Yeah, I'm good"

BM: "Gari umeionaje? Iko sawa?"

Caryn: "Nilikuachia gari ofisini kwanini uliamua kuileta nyumbani? why?"

BM: "Sasa nakupigia simu hupokei na wewe ulisema gari yako unaitaka jana, unadhani mimi ningefanyaje? maana nilikuja ofisini nikakuta mshafunga"

Caryn: "Lakini sikukuambia ulipeleke nyumbani ww ungebaki nalo tu, haya ulivyofika nyumbani Mzee akasemaje?"

BM: "Mimi hata sikukaa nilimkabidhi funguo nikaondoka"

Caryn: "Hajakuuliza chochote?"

BM: "Hapana, aliniuliza tu kwamba gari lipo sawa? nikamjibu lipo sawa"

Caryn: "Sasa nikuulize na wewe ilikuwa ukagonga gari?"

BM: "Ooh, kwasababu gari limeshatengenezwa ndio unataka kujua ilikuaje ila Jana hukutaka kujua hayo mambo"

Caryn: "Ningekupa hiyo nafasi jana ningekuonea huruma though nilikuonea huruma hata hivyo, maana najua umetoboka hapo ulipo, ivi Headlight umenunua bei gani?"

BM: "Na nimetoboka kweli, taa Ile nimenunua milioni moja na laki nne"(Uongo)

Caryn: "Duh! pole mwaya, ndio ukome hata hivyo"

BM: "Gari yako siendeshi tena"

Caryn: "Wewe kwa unavyopenda magari, utaendesha tu na ukiharibu unalipa"

Muda wa kazi ukaisha, jioni Wakati nipo nyumbani napunga punga upepo kwenye balcony uzaramoni wanaita kibaraza Michelle akanipigia simu

Michelle: [emoji338] "Hello"

BM: "Yes"

Michelle: "Vipi uko poa?"

BM: "Yeah niko poa"

Michelle:. "Upo na Caryn?"

BM: "Hapana, niliachana nae ofisini"

Michelle: "Ooh, nikajua upo nae, vipi kazi yangu imefikia wapi?"

BM: "Kazi yako bhana nisha-play part yangu, so wewe msikilizie Caryn mwenyewe"

Michelle: "Majibu ya hivi ndio siyataki, wewe yule unammudu unajua, sema hujajua tu"

BM: "Sasa yeye ndio mwenye maamuzi unataka Mimi nifanyaje?"

Michelle: "Hujam convince vya kutosha, wewe kama mtu kosa lako analifanya lake atasokaje kukusikiliza"

BM: "Una maanisha nini unaposema kosa langu akalifanya lake"

Michelle: "Ooh unadhani mimi sijui kama mmemuongopea Mzee kuhusu gari, Mimi najua wewe ndio umegonga gari lakini Caryn kamuambia Baba ni yeye ndio amegonga"

BM: "Sasa kwani kuna shida gani? si ilitokea tu bahati mbaya kama ni gari nishalitengeneza"

Michelle: "Hapa shida sio gari tena, shida ni uongo mlioutengeneza ukijakugundulika ni uongo, kama ulikuwa hujui uongo ni adui namba moja wa Mzee na Mzee akija kugundua wewe na uongo ni marafiki automatically na wewe unakua Àdui kwa Mzee...Mimi nimemaliza

Akakata simu....hii sasa sio kawaida hawa mabinti wa Mzee ni kama kuna mchezo wananichezea, inawezekanaje Michelle kupata taarifa ninazojadili Mimi na Caryn tu kama sio Caryn mwenyewe anayemwambia hizi habari

Kupoteza mawazo nikampigia Annie nikaongea nae kama nusu saa ivi, eti ananiambia "Sasa hivi najua huyo Accountant atakuwa kashamia kwako kabisa" angejua tu huyo mtu haniambii kitu sasa hivi, basi tutaagana na kutakiana usiku mwema

Kesho yake jioni tumeshafunga ofisi wafanyakazi wote wameshaondoka nipo mimi na Caryn tu tumebaki ofisini, nikamuuliza Caryn issue ya gari

BM: "Caryn ivi Michelle anajua kama gari lako liliharibika?"

Caryn: "Yeah anajua"

BM: "Amejuaje?"

Caryn: "Si nilimuambia"

BM: "Lini?"

Caryn: "Bro! too much questions! what's wrong?"

BM: "Nataka tu kujua"

Caryn: "Aah achana na hizo mambo tuondoke"

BM: "Hapana Caryn Nipo Serious nataka kujua"

Caryn: "Kujua nini sasa"

BM: "Ulimuambia lini?"

Caryn: "Anyway, nilimuambia juzi siku ambayo ulitakiwa uniletee gari hapa ukachelewa nilipita ofisini kwake aliniona sina gari alivyoniuliza nikamuambia tena nikamdanganya sasa"

BM: "Aje?"

Caryn: "Nilimuambia nimechubua rangi so gari nimeiacha garage"

BM: "Sasa mbona yeye anajua mimi ndio nimeigonga"

Caryn: "Mmh! kajuaje? kwasababu unajua Hadi Mzee nimemdanganya anajua ni mimi ndio nimegonga that's why nilikuwa na wasiwasi juzi ulivyoenda isije ikawa umeropoka mambo tofauti na niliyoongea"

BM: "Mm nilivyosikia maelezo ya Mzee nilijua kabisa umemdanganya so na mimi nilipita mule mule ulipopita japokuwa sikujua kwanini ulimdanganya"

Caryn: "Aah achana nao bhana issues ndogo tu hiyo isikuwazishe"

BM: "Caryn ivi ulisema unatumiaga pombe eeh?"

Caryn: "Yeah, but only wines na sinywi kulewa vipi unataka kunitoa out?"

BM: "Now I got you, kuna venye unakunywa ukiwa Michelle hadi unaongea ambayo hukupaswa kuongea"

Caryn: "Yani wewe bado uko na hizo mada! nikajua tushafunga chapter, ebu twende watu wasije wakatufikiria vibaya"

Tukafunga ofisini kigiza kilikuwa kishaanza kuingia kila mtu akashika njia yake, jumamosi yake huwa ni nusu siku wakati tunakaribia kufunga Ofisi Caryn akanambia hana pa kwenda so anataka akapaone kwangu

Kweli tulivyofunga ofisi tukasepa wote, mara nyingi kwenye safari ambazo nipo na Caryn huwa ana prefer mimi niendeshe lakini kwa mara ya kwanza hiyo siku nilimkatalia, akakaa kwenye Steering mwenyewe kazi yangu ilikuwa tu kuelekeza njia hadi tukafika

Kitu kimoja kuhusu Caryn huwa hapitishi vitu kirahisi, Yani Mfano umenunua saa atakuponda atakuambia "saa gani sasa hiyo" nakumbuka trip niliyoenda nae Zanzibar ile siku nilitinga shati langu flani ivi mwenyewe naliaminia akanambia "huongozani na mimi ukiwa umevaa hilo shati" hamuezi amini nilibadilisha pesa alitoa yeye lakini ya kununua shati jingine

Hata kule nilipokuwa nakaa zamani alikuwa hapakubali lakini nilivyofika nae makazi mapya mwenyewe alipakubali hadi nikashangaa....tulivyofika tu

Caryn: "Sasa hapa nakupa nyota zako bro, pazuri sana"

BM: "Aah basi kweli hapa pazuri hadi wewe umepakubali!"

Caryn: "Halafu sio kuzuri tu, kumetulia pia....hizi nyumba zote zina watu?"

BM: "Yeah zote zina watu"

Caryn: "Lazima watu wapakimbilie, nyumba moja ingekuwa vacant ningechukua"

BM: "Usiongee sana ebu twende ndani"

Tukaingia ndani bhana Disappointment zikaanza kama kawaida yake

Caryn: "Dah! nyumba nzuri unaweka mapazia ya kichaga"

BM: "Ushaanza, ebu sema unakunywa nini nikuhudumie mgeni"

Akanambia anachokunywa nikamletea story zikaanza, katikati ya story akauliza

Caryn: "BM unajua wewe ni Gentleman and you're handsome, nahisi una Mwanamke lakini hujawahi kunitambulisha, labda nikuulize una Mwanamke? I mean fiance or something"

Dah! Hili swali limekuwa la ghafla mno halafu anauliza huku ananiangalia machoni, hiyo ni kumaanisha nini...kwamba mdomo unaweza kuongopa lakini macho hayaongopi...

Itaendelea
Huyo mrembo anakuelewa ila we una delay sana .
 
Una uhakika gani kama mwezi wa 12 story itakuwa imeisha, kwasababu mm mwenyewe ninaendika sijajua mwisho wake

Yani nilichowazidi nyie ni mimi kujua matukio ya mwezi huu ambayo Bado sijayaandika lakini matukio ya kuanzia kesho na kuendelea wote hatuyajui, kwa maana hiyo ni ngumu kutabiri mwisho wa story
Hajui hii ni Isidingo the need
 
We BM huna shukran,ungemuoa huyo accountant ,maana ndo Mungu kamtumia akutoe mavumbin,..huyo Annie cjui Carren wangekujulia wap ,km siyo huyo accountant kukuita kazin,ukaanza kushika pesa ukamuona hafai.looh kuwa na fadhila kijana
 
Back
Top Bottom