Mkuu BM nafikiri hapo nimeelewa sasa. Unapoteza muda kujiweka kwa mtu asie na umuhimu kwako Caryn.
Nafikiri bora uende sambamba na mzee tu,achana kumsikilizia huyo binti.
Kwanza alikufanya ukaachana na Acauntant,na ukaacha na nafasi ya wazi aliyokuandalia Accountant.
Maana mpaka sasa ungekuwa ndio boss wa hapo. Angalau hata ungekuwa na maamuzi yako mpaka sasa. Ungemsikiliza tu yeye halafu usitekeleze anachohitaji. Mbona kwa Caryn unamfuata anachotaka,japo nia yake Caryn anakuandaa uwe wake,japo sina uhakika wewe uko tayari,japo nimehisi na wewe unajaribu kuzitengeneza hisia zako kwa Caryn.
Pili alikuambia uache kazi ukamsikiliza bila hata kumshirikisha mzee hilo swala ksbb ya Caryn. Lakini limekuletea shida kwa mtu ambaye ni muhimu kwako kuliko yoyote (mzee).
Tatu. Kakakudanganya kaje kulala kwako. Hata wewe bila kuwa wazi kwa mzee. Kama ulivyoanza na mzee na kumuelewa misimamo ya mzee. Ungeendekea kuwa upande wa mzee. Vinginevyo ungekataa kabisa,ungemhofu kum-disapoint mzee. Kumbuka pamoja na kwamba Caryn ni mtu mzima ana maamuzi yake,lakini ni mtoto wa mzee. Mzee yoyote atatamani mtoto wake awe kwenye mahusiano au ndoa isiyo yumbishwa na upepo wowote. (Ndio maana akakuuliza wewe ulisema una mwenzi wako. Pia akauliza una mipango gani na Caryn?. Uwe makini anza kujisahihisha).
Nne. Huyo huyo Caryn bado amekudanganya usiende China na wewe ukamuelewa sijui alichokuahidi. Lakini bado hakakupi umuhimu wowote. Hapa usitegemee ya kubahatisha ya mbele,fanya ya sasa ya muhimu kwako bila kusubiri usichokijua mbele.
Nafikiri sasa japo unaweza ukawa umechelewa ama la. Fanya maamuzi nenda kwa mzee kamuombe msamaha kwa kum-disapoint. Mueleze mambo yote yalivyoenda. Usimueleze kila kitu Caryn alichokudanganya,ila mgusie nguvu ya Caryn ilivyochukua nafasi fulani ktk maamuzi yako. Usimwambie kila hatua ya jinsi Caryn alivyocheza huo mchezo,ksbb mzee atakuona mzembe.
Pili chagua kuendelea kukaza kwa mzee huku ukimtarajia Caryn,japo huko iko wazi mpaka sasa ujue utachelewa sana. Na usipomuoa ndio ujue hutapata kabisa,msome.
Naona kabisa bado hujacheza vizuri huu mchezo. Umejiegesha kwa mtu anaetaka akutumie vile anavyotaka. Umechezea nafasi zote za mzee alizokuandalia.