Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bonus ni hii TU que Kuna ingineBONUS EPISODE
Hello Boys & Girls, members wa Jf, Mr X6 is back with full energy, this mwezi May has been really tough for me thanks to God I’m bounced back with the Grace
After this bounce back nimejifunza kitu, When your intentions are pure, you don't loose people, people loose you, na sio hicho tu nilichojifunza, nimejifunza mambo mengi sana kupitia hii story yangu, Pengine ningekuwa sijaandika hii story nisingepata nafasi ya kujifunza haya yote, Nikikaa chini na kupitia maandishi yangu naona kabisa sehemu nilizofanya mistake na sehemu nilizopatia
So after this Bonus Episode nitakuja na Summary ya mambo niliyojifunza kupitia hii story yangu, yani kila aliyehusika kwenye hii story yangu na kila niliyemtaja amenifundisha jambo kwenye maisha
Basi bhana kama nilivyosema hapo awali, mwezi huu wa tano nilipitia kipindi kigumu sana hadi kufikia hatua ya kutaka kupoteza watu wangu wa karibu ila kwasababu dhamira yangu haikuwa mbaya basi mimi nisingewapoteza wao bali wao ndio wangenipoteza Mimi
Basi wakaamua (Caryn) kunipoteza ili kubaki na mteja, Kiukweli iliniuma sana, na kilichoniuma sio kuwekwa Benchi na Kampuni bali ni kuwekwa Benchi kwa kosa ambalo nilijitahidi kulifukia despite all my best efforts lakini nayo ilionekana kazi bure
Nikamuambia Caryn "Unajua unaweza ukawa na mapenzi ya dhati kwa mtu lakini ukavunjwa moyo kwa vitendo unavyofanyiwa na huyo mtu"
Caryn: "Mimi najua nini nafanya, sometimes inabidi ucheze na akili za watu, and If you claim to love someone you don't stop loving them even when their decision is not in your favor"
Speaking of Claim to love someone, unajua Mwanamke anayekupenda atakuonesha signs zote ili umtongoze na hilo nililiona kwa Caryn, ili nisionekane Domo zege ikabidi nisipuuzie Green light iliyokuwa inanipiga usoni, nikachapa verses zangu lakini majibu ya Caryn Sasa naweza kusema hayakuwa mabaya na wala hayakuwa mazuri
Ilikuwa hivi, mnakumbuka ile siku tulienda kwa Michelle? nakumbuka hicho kipande nilikihadithia hapa, Sasa tulivyorudi nyumbani kwangu kutokana na maongezi tuliongea kule kwa Michelle ikabidi nijaribu kutupa ndoana ili nione kama itaibuka na Samaki, sikupindisha pindisha nilienda straight to the point
BM: "Caryn, nahisi upendo nilionao kwako ni zaidi ya urafiki"
Wakati namueleza hayo tulikuwa tumekaa sitting room, yeye alikuwa amekaa chini kwenye zuria na mimi nimekaa kwenye kochi, nikanyoosha maelezo kwamba nampenda kimapenzi
Caryn: "You're joking, right?"
BM: "Nop, I'm serious, very serious"
Caryn: "Kama unamaanisha sidhani kama ni idea nzuri mimi na wewe kuwa wapenzi"
BM: "Kwanini?"
Caryn: "Okay, I used to love you, I mean i developed feelings for you lakini for Dad's sake I had to let it die"
Nilivyosikia for Dad's sake nikajua tayari Mzee kuna venye ameongea na Mwanae, nikamuuliza Caryn "Kwahiyo hapa hofu ni Mzee sio?"
Caryn: "Hofu sio Mzee, hofu ni kukupoteza wewe"
BM: "Mmh! Aje sasa? kwa hatua tuliyofikia nayo sidhani kama tunaweza kuwa separated labda uwe Mpango wa Sir God"
Caryn: "Nimemaanisha kukupoteza as a friend, unajua we lose people who are potential and important to us and in our careers sababu ya mapenzi
.....Dad aliniambia kuna watu ni muhimu sana ambao we don't deserve to date them kwasababu tunaweza kuwapoteza pindi mapenzi yatakapoisha"
Kumbuka haya maongezi yanafanyika kabla ya Mzee kuja kwangu, Sasa baada ya Mzee kuja kwangu kama mnakumbuka aliniuliza kuwa nina Mpango gani na Mwanae kabla sijamjibu ndipo akaniambia kwamba[emoji1484]
"kwenye hii Dunia ukitambua wenye manufaa maishani mwako usiwape umuhimu, HAWATAKUUMIZA. Wenye umuhimu maishani mwako usiwafanye wenye manufaa, UTAUMIA"
Sasa hii siku jioni yake kuna kitu nilimuuliza Càryn ambacho sikukisimulia last episode
kutokana na lile swali kutoka kwa Mzee "Una Mpango gani na Caryn" nilimuuliza Caryn kama amemshirikisha Mzee kuhusiana na Mimi kumtaka kimapenzi, akaniambia hakumshirikisha"
BM: "Kuna swali ameniuliza ndio maana nataka kujua, so kama ulimshirikisha we niambie tu"
Caryn: "Swali gani kwani amekuuliza?"
BM: "Nina Mpango gani na wewe?"
Caryn: "Hapana, sijaongea na Mzee chochote kuhusu hayo mambo"
Siku zikapita, majanga yakatokea na kazi nikasimamishwa, nikawa sina budi ku move on lakini na-move on huku nikisikilizia Mpango wa Caryn huku nikitafuta Plan B ya kuni backup endapo mchongo wa Caryn uta-Bounce
Mpango wa Caryn ni gani sasa? ....ni huu hapa>>>kabla ya Mzee kumshirikisha Caryn kuhusu mimi kwenda China, Caryn nae alikuwa na Mpango wa kufungua Kampuni ya Air Cargo kama ile ya Baba yake, Sasa kabla hajanichana ndio Mzee akaja na Safari ya China na yeye ndio akaleta Proposal yake mezani
Mpango nikauona umenyooka kabisa na Caryn alikuwa serious na hilo kiasi kwamba aliachana na Mpango wake wa kununua Gari mpya kama alivyojiwekea ahadi,
Basi tulivyo sketch kila kitu kuhusu hiyo Kampuni ambayo mimi ndio nitakuwa nikiisimamia, kwasababu ya uchanga wa Kampuni tulipanga Mkurugenzi niwe Mimi na Logistic Manager niwe mimi na huku kwenye Kampuni ya Mzee pia nabaki na position yangu Ile Ile as a Logistic Manager Yani kwa kifupi nipige miguu yote yote
Hapa ndipo niliporudi kwa Mzee na kumchomolea Ile safari ya China, But guess what? Mchongo ukawa mchongoma na Deal halijakua done kama nilivyotegemea bali Dili limekuwa Dilisha, Wanasema mtaka yote hukosa yote...Yes, ila kwangu imekuwa tofauti kidogo, Mimi sikutaka yote na bado nikakosa yote
Nili think twice kwenye mchongo ambao ni wa uhakika na sikutakiwa hata kupoteza muda, I mean the deal was good and i wasn't supposed to think twice, Lakini sio mbaya Uzuri ni kwamba mtu aliye kwenda China badala yangu nammudu na tunaelewana vizuri basi naimani tutafanya makubwa zaidi
Lakini ubaya wa Binadamu huwa wanabadilika sana, so hutakiwi kuwategemea kabisa, ila sidhani kama Mchina atani disappoint kama alivyoni disappoint Kijana wa Buguruni, Kijanaa bhana alianza Ukola, nilianza kusikia makesi zake kutoka kwa sister mara "ooh huyu mtu leo hajarudi" mara "karudi lakini hakulala kabadilisha tu nguo na kuondoka"
Kabla ya kuongea nae nikaanza kumfuatilia, nilienda kule kijiweni kwake nikaambiwa ana kama wiki hivi hajaenda, lakini hiyo haikuwa kesi kwasababu jamaa kaniambia huwenda kuna kazi anafanya sehemu maana almost vifaa vyake vyote amebeba, moyoni nikajiuliza ni kazi gani hiyo inayomfanya mtu asirudi nyumbani
Nikaendelea na shughuli zangu hadi hivi unavyosoma hii story sijamtia machoni yule Kijana, nilienda tena kule anakofanyia kazi yule blaza aliniambia siku ile nilivyoenda kumuulizia baada ya siku kadhaa Kijana alienda na akachukua vifaa vyake vyote alivyoviacha huku madai yake yakiwa ni yale yale kwamba kuna kazi anaenda kuifanya,
Blanda niliyoifanya ni kutokumuambia yule blaza azuie vile vifaa vilivyobaki kama akivirudia lakini by that time sikuwaza nilichokuwa nakiwaza sasa hivi
Anyway, I have bad feelings kuhusu Kijanaa lakini mimi huwa mzito sana ku judge, nilichokifanya nilimjulisha Mzee tu, kilichobaki nikusubiria muda uniambie jambo (time will tell)
Back to BM & Caryn Nothing is working according to plan anymore, Caryn alirudi kwao lakini hakuondoka na nguo zake alienda yeye kama yeye hata Gari yake aliiacha akawa anatumia Jeep Wrangler ya Mzee, hiki kipindi Caryn alichoacha gari yake ndio kilikuwa kile kipindi kigumu, cos nilikuwa naenda misele na Gari naiacha nyumbani, si mnajua magari hayatumii Maji eeh, tena hii Engine Capacity yake si kubwa kihivyo, ni 2.5 tu
Hadi leo karibia mwezi sasa Gari bado imepark kwangu lakini siku niliyotoka nayo hazizidi 4, Hizo mara tatu ilikuwa ni misele yangu Binafsi mara moja nilitoka nayo kwenda kuonana na Càryn, tena ni juzi hapa hata week haijaisha nadhani
Hii ilikuwa Bonus Episode tu ya matukio ambayo sikuyasimulia lakini Wacha niunge na matukio yaliyotokea recently
Siku ya Jumatatu asubuhi najiandaa kwenda job kwasababu Jana yake Caryn aliniambia niende, Mimi bila hiyana nikachomoka hadi ofisini, kufika ofisini nilivyoonana na Caryn akaanza kunihoji kuhusu Ile Kampuni niliopoteza mzigo wao kama nipo sawa nao au kuna kabifu ka chini chini kanaendelea kati yetu
Nikashangaa Caryn kuniuliza vile kwasababu Mimi BM naanzaje kuwa na Bifu na likampuni linaloingiza mamilioni ya Pesa, nikamuambia Caryn hakuna Bifu na wala halitakuja litokee, labda nifungue Kampuni kama yao hapo ndio ita make sense mimi kuwa na bifu nao
Caryn: "Ooh! now I see nilichoambiwa kinaweza Kuwa na ukweli"
BM: "Umeambiwa nini na nani?"
Caryn: "Unajua nilienda kule nilikuwa na kikao nao, walikuwa na Agenda zao za kuzungumza ila na mimi nilikuwa na Agenda zangu, moja ya agenda inakuhusu wewe"
BM: "Mimi! how?"
Kwa kifupi Caryn alitaka kujua kama kuna makosa mengine nishawahi kufanya hapo nyuma au ni hili la juzi tu, maana Caryn anakuambia kwa namna Ile Kampuni ilivyoreact kuhusu upotevu wa mzigo alijua tu kuna something else, si ndipo wakamfungukia sasa
Iko hivi, kuna siku nilipeleka mizigo yao kule ofisini kwao, sasa wakati mizigo inashushwa kuna mzigo mwingine ulikuwa mzigo sana, kule Bandarini tuliupakia kwa Forklift na huku kwenye Kampuni pia tuliushusha na forklift, so you can imagine huo mzigo ni mzito kiasi gani, Sasa Mimi si nikaropota nikasema Hawa wateja ningewajua ningewaiba nikawa link moja kwa moja kwenye Kampuni yetu ningekuwa napata Commission ya kueleweka kwa aina hii mizigo (Hapo sasa ndipo nilipo halibu)
Kwasababu unajua wateja wa Ile Kampuni wao hawajui kama mizigo tunawasafirishia sisi wao wanajua ni Ile Kampuni ndio inafanya Kila kitu which is not true, Mimi nawaona ni kama mtu kati, ma broker flani ivi, ukiacha na hao pia kuna hawa watu wengine ambao wanakula pesa ya bure kabisa ambao huwa wanagiza mzigo china na kuwauzia wafanyabiashara wa mikoani, na unakuta yule mfanyabiashara wa mkoani nae anapata faida yake vizuri tu licha ya pesa yake kupita kwa mtu wa kati, sasa je kama angekuwa anaagiza yeye mwenyewe moja kwa moja kutoka china si angekuwa ana double profits,
Anyway ndio Biashara ilivyo lakini, kitendo Cha mimi kuongea Ile kauli kumbe yule jamaa aliibeba kama ilivyo akaenda kumuambia Boss wake, bwana weeh! wakawa wananisubiri niingie kwenye 18 zao na mimi si nikajaa[emoji2305] wakanila kichwa, Aisee sikufikiria Ile kauli yangu kama ingekuja kuni cost pakubwa hivi
Unajua nilianza kumfikiria vibaya Opportunist kama wengi walivyokuwa wanadhania humu, kuna wengine humu waliniogopesha zaidi kwa kusema Hilo ni game nachezewa na Mzee kwamba hata Caryn anaweza akawa anajua kinachoendelea sema amekausha tu, Aysee nyie[emoji1430] mliniogopesha sana
Sasa Caryn kaniambia kule kamalizana nao so nirudi mzigoni ila nikakataa, Caryn aliniruhusu niondoke badae au kesho atakuja mjengoni tuongee vizuri, nilitoka pale ofisini mida ya saa tano tano hivi asubuhi ndio nikaja humu kuandika I think we should forget a day to remember
Hamuwezi amini hii siku nilipata amani ya moyo maana siku zote nilihisi kama kuna kitu kinanikereketa, Hii siku Caryn hakuja nikabaki kuongea na Annie kwenye simu, Annie anawaza ujio wake wa kuja Dar na Bus anadai hataki kuja na ndege (Annie anakuja tarehe 4 mwezi wa 6)
Mimi nikawa namng'ang'aniza atumie ndege ili afike mapema, kwasababu akitumie Bus tutapeana heka heka za kwenda kupokeana saa sita za usiku, Mwisho wa siku nikamuambia atumie usafiri anaouona yeye unafaa
Zilipita kama siku 2 Caryn akaja home akanikuta na msimamo wangu ule ule, nikamuambia Caryn kuna ulazima gani wa mimi kurudi kufanya kazi ikiwa watu wengine wapo na wanafanya kazi vizuri tu, Caryn akaniambia Opportunist anafanya kazi vizuri lakini bado ana pwaya,
Caryn anadai Opportunist anatumia gharama kubwa kwenye kutoa mzigo, Mimi nikawa nishajua ni wapi anapokosea Opportunist, unajua kwenye haya maisha hutakiwi kuonesha mbinu zako zote za kivita, ukionesha siraha zako zote ujue wakulungwa watachukua Points 3 muhimu, inabidi ukiondoka sehemu uache pengo kwasababu siku hizi mapengo yanazibika vizuri tu
Nikamuambia Caryn amvumilie tu jamaa mwisho wa siku atajua, Mimi mwenyewe nilikuwa sijui chochote
Caryn: "BM bado una Grudge?"
BM: "Hapana! wala sina kinyongo, ila hizi nenda rudi nenda rudi kwangu hazinikalii poa"
Caryn: "Kama ni hivyo basi kulikuwa hakuna sababu za mimi kukukatalia wewe kuwa na mimi"
BM: "Unamaanisha nini?"
BM: "Daddy alinitahadharisha kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wewe"
Dah! Mzee bhana....eniwei, According to Caryn Mzee alipenda sana urafiki pamoja na bond iliyopo kati yangu mimi na Caryn, (Hapo ni Mzee Sasa anamuambia Caryn) Mzee ananichukulia mimi (BM) kijana wa tofauti sana, kwasababu kuna mambo Caryn anaweza kuyafanya na mimi nikayachukulia poa kwasababu ya urafiki sasa kama tutaingia kwenye Mapenzi na kwa Caryn jinsi alivyo akafanya mambo au maamuzi Fulani ambayo hapo awali nilikuwa nayachukulia poa lakini huku kwenye Mapenzi nisiyachukulie poa tena (Perspectives za Mzee hizo)
So Mzee akamuambia Caryn kama ataingia kwenye mahusiano na mimi, kwanza akubali kumpoteza rafiki na workmate na hata Business Partner kwa hapo badae
Mzee alimuambia Caryn kwamba anaweza kuniona mimi muhimu kama Rafiki lakini umuhimu huo asiuone pindi atakapokuwa na mimi katika Mahusiano ya kimapenzi
BM: "Lakini watu wanaweza wakawa wapenzi na bado wakawa marafiki"
Caryn: "Hata mimi nilimuambia hivyo hivyo"
BM: "Akasemaje?"
Caryn: "Kasema ina depend na Character ya mtu"
Caryn akasema kwamba kwa mujibu wa Mzee, anadai Michelle ndio ana sifa hiyo lakini Caryn hana so kama atafanya kinyume na kuwa kimapenzi na mimi basi kuna mawili yatatokea, either Mimi nimvumilie sana Caryn na nikishindwa kumvumilia basi tutaachana na tukiacha pia kuna mawili, urafiki utakufa au utabaki na hata kama utabaki hautakuwa kama ule wa mwanzo, Mzee akadai maamuzi ya kiakili yanahitajika zaidi kuliko maamuzi ya kihisia
BM: "Wow, nimemuelewa Mzee Kwa kiasi chake"
Caryn: "Mimi nipo tayari kukuvumilia wewe BM"
BM: "Una maanisha kwamba?"
Caryn: "Kama kuna tabia zangu ambazo huzipendi niambie nipo tayari kuziacha"
MWISHO WA SEASON 2, Maybe to be continued
Sawa, nimekuelewa lakini mm nikichagua nimechagua, Yani nitakayemchagua Sasa hivi basi huyo ndio atakuwa chaguo langu la maisha. Sitaki kufanya maamuzi nusu nusu Vinginevyo labda Mungu awe hajabariki hilo chaguoBraza hujasimama bado. Baki na Anna. Ukienda kwa mtoto wa bosi una vingi vya kupoteza. Nishikize ndani humo kwanza mpaka uwe hakuna namna ya kukureplace ndo uanzishe mahusiano na Carryn. Vinginevyo utachemka vibaya.
Huu Uzi ni mtamu, kinachotafutwa ni business ideas,,EPISODE 01, SEASON 01
Wakuu nahitaji ushauri wenu ili niweze kufaulu katika huu mtihani, nimepewa kazi kubwa ambayo nikifaulu basi milango mingi itafunguka huko mbeleni.
Kuna Mzee flani huwa tunashirikiana kikazi na mara nyingi mizigo yake huwa anaiagiza kupitia Kampuni yetu, ni Mfanyabiashara na ameanza Biashara miaka ya 90s alivyomaliza tu O level, Sasa huyu Mzee kijana (1971) huwa tunaongeaga mambo mengi kuhusu Biashara huku nikitaka anipe miongozo ili na mimi nielekeze nguvu na akili huko
Huyu Mzee akijaga Ofisini ni lazima nionane nae japokuwa muda mwingi Mimi huwa nakuwa nje ya ofisi kutokana na majukumu yangu mengi si ya kufanyia Ofisini nimesema ni lazima nionane nae ni kwasababu zangu Binafsi na si za kiofisi, Huyu Mzee ndio ameni inspire mm kutaka kufanya Biashara si kimafanikio tu bali hata lifestyle yake, Yani kifupi ana enjoy mafanikio yake anafanya kazi huku amerelax nyakati za kujituma usiku na mchana kwake zilishapita, sio kama wazee wengine wenye Utajiri lakini Bado anajitesa siku nzima kama yeye ndio kaajiriwa jambo ambalo ni tofauti kwa huyu mzee, huwezi kujua ratiba yake muda wowote yupo Ofisini na muda wowote pia anaweza akawa nyumbani, Ni siku ya Ijumaa tu ndio Najua kwamba haendagi ofisini kwake labda kuwe na jambo muhimu sana ambalo linahitaji uwepo wake.
Sio mtu wa mitandao sana hasa kama hii Jf pengine hata haijui, Kuna siku nilimuuliza kuhusu mitandao akanambia anatumia Twitter na Whatsapp tu, so hii story Najua itakua ngumu kwake kuiona, maana hata kwa codes nitakazoweka kama akiiona atajua tu ni Mimi na ndio mchongo mzima utaishia hapo
Sasa nikibahatikaga kukaa na huyu Mzee mtu mbili huwa namuonesha shauku ya mimi kutaka kufanya biashara lakini kila nikimgusia swala hilo ni kama anaona sipo serious, anahisi nataka kufanya biashara kwa kufuata mkumbo tu, Kwasababu nakumbuka aliniuliza nataka kufanya Biashara gani mimi nikamwambia nataka kufanya Biashara kama ya kwake, aliishia kucheka tu
Nakumbuka siku moja nimetoka Zanzibar kupokea mizigo ya ofisi ya wateja, nimefika Dar Huyu Mzee akanipigia simu kuniomba kwamba mzigo wake nisiupeleke store Bali niende nao Ofisini kwetu ili nikitoka kazi nimpitishie kwake, na ndio ilikuwa mara ya kwanza kufika kwa huyu Mzee, Asee vile nilivyokuwa namdhania ni robo yake, Kuna watu wanaishi acheni nyie
Basi Mzee alinikaribisha vizuri sana mjengoni mjengo mjengo kweli! Wakati naingia kwenye Parking sijaona Gari yake niliozoea kumuona nayo siku zote (Land Cruiser ZX V8) nilimkabidhi vitu vyake Mzee akapanda juu Nadhani ni Bedroom kwake alivyorudi akanipeleka Backyard tukakaa, Sasa tulivyokuwa mule ndani sikuona mtu mwingine yeyote ikabidi nimuulize Mzee nyumba yote hii unaishi peke yako? akanambia "hapana mabinti zangu na Mama yao wameenda Kibaha watarudi Jumapili" (Siku hiyo ilikuwa Ijumaa)
Story zikaendelea pale Mzee akanambia "Kijana wangu nilikuambia uniletee mzigo kwa makusudi, mm kila Ijumaa huwa na utaratibu wa kupata chakula Cha jioni na familia yangu ya ndani na ya nje hivyo nilitaka na wewe uwepo" alivyosema familia ya nje niliwaza mbali, nikamuuliza kwani Mzee wewe una wake wa ngapi? kabla hajajibu alitabasamu "mmoja tu na Najua umeuliza hivyo kwasababu gani, nilivyosema familia ya nje nilimaanisha watoto wa mitaani ambao hawana makazi maalum, kwahiyo badae tutatoka kwenda kuwachukua" nikasema sawa ni jambo zuri Mzee
Wakati tumekaa na kuendelea na story Mzee akanambia kama nitataka kunywa chochote niende kwenye fridge nijihudumie, Nikamwambia haina shida, Mara ghafla Mzee akapokea simu Wakati anazidi kuongea akachange ni kama kapokea Taarifa mbaya, yule Mzee aliinuka pale alipokuwa amekaa akiwa bado anaongea na simu huku akiingia ndani, alivyotoka alikuwa kashika funguo mkononi akanambia "Kijana wangu nimepata dharula itabidi nikuache kidogo ila nitajitahidi niwahi kurudi ili tufanye lile jambo nililokuambia, in case of anything utanipigia simu" Nikamwambia sawa Mzee
Tukatoka kule backyard hadi Parking pale kulikuwa na Magari mawili ambayo sikuwahi kumuona nayo akaingia kwenye Jeep, Yale majeep yenye muundo kama wa Benz G Wagon, Mzee alifungua geti na Remote control akasepa, Mtu mzima nikachoma ndani, nikajiachia kwenye Sofa huku nikiperuzi, Giza likaanza kuingia na saa Ile Mzee anaondoka ilikuwa ni around saa kumi jioni.
Simu ikaita, kucheki ni Mzee, akanambia "Kijana wangu ni kama nitachelewa kurudi Sasa wewe Fanya hivi, umeiona hiyo gari hapo parking?" nikamjibu ndio "Sasa panda juu mkono wa kulia chumba Cha mwisho fungua mlango ingia ndani nenda hadi kwenye dressing table utakuta funguo ya Gari ichukue, si unajua kuendesha gari?" nikamwambia ndio lakini Sina leseni Mzee "Wachana na mambo ya leseni, kwani Driving licence ndio inaendesha gari? Sasa si umesema unajua ku drive, nenda jikoni kachukue hicho chakula pakia kwenye gari wapelekee wenye uhitaji sababu ninaweza nisirudi halafu hicho chakula kikaharibika" nikamjibu sawa Mzee akakata simu
Nikawa najiuliza pa kwenda kuwapata hao watoto, Basi bhana Mimi nikapanda juu kuchukua funguo ya Gari, nikazama hadi chumbani asee ni noma, Chumba kama sebule nikawa sielewi dressing table Iko wapi, kilichonisaidia ni kioo, nilivyoona kioo nikajua tu hii ndio yenyewe hadi kesho sijaelewa Ile dressing table imetengenezwaje, kweli nikakuta funguo pale juu Ile kupiga jicho pembeni nikakuta maburungutu ya pesa elfu tano tano, hata sijayagusa maana nilijua nyumba kama Ile haiwezi kukosa CCTV camera, me nikabeba funguo kikashuka chini hadi jikoni nikakuta mahotpot yana msosi wa kutosha (Wali njegere maini) nikayabeba hadi kwenye Gari (Alphard) nikarudi jikoni kucheck sahani zote za dongo nikaachana nazo nikarudi kwenye Gari nikafungua Geti nikasepa ila sasa nimetoka na sijui naelekea wapi nikicheki saa ni saa moja kasoro, nikaenda hadi Mwenge, nikapark kando ya Barabara nikawa nawaza hao watoto nitawapata wapi, mawazo yakaja niende kwa sister angu flani anakaa uswahilini huko ndiko nikagawe hiki chakula, nikapiga mahesabu ya masaa nitakayo tumia hadi kufika huko muda utakuwa umeenda hata hivyo nitakuta watoto wengi wapo majumbani mwao na watakuwa washakula nikaona nikifosi kufanya hivyo nitaendelea kuipa nguvu ile kauli ya "mwenye nacho huongezewa"
Nikatoka pale Mwenge nikaenda Buguruni, nimepitia Ile footbridge na Mataa nikaingia Barabara ya kama naelekea Ilala, sijafika hata mbali nikapark pembeni kusikilizia, sijakaa sana nikaona madogo wawili nikawasimamisha Nikawauliza wanapoishi hawakunijibu, nilivyoona hivyo sikutaka story nyingi tena niwaambia ninachakula nataka niwapatie lakini nyie wawili hamtakimaliza mnaweza kuwaita na wenzenu? mmoja akaniuliza "kiko wapi hiko chakula chenyewe?" nyie kawaiteni wenzenu mkija mtakiona chakula, nitawaambia hivyo wakaondoka nikakaa kama Dakika 8 nikaona wale madogo wanakuja na rundo la madogo wenzao nikajisemea Leo kazi ipo maana kwa Ile idadi niliyoiona ya wale watoto na nikipiga mahesabu ya kile chakula nilichobeba ni kama hakitatosha kabisa halafu saa hiyo hiyo nikakumbuka nilibeba tu chakula na sikubeba sahani nilipanga nipitie supermarket ninunue zile sahani za karatasi nikasahau
Madogo wakafika hadi kwenye gari, nikawauliza mgahawa wa karibu uko wapi?wakanionesha lengo nikwenda kununua chakula ili niongezee na hapo hapo nitapata sahani za kutumia kwasababu kwa kile chakula kilichopo kinatoshea kwa watu kama 9 ivi na kile kikosi Cha madogo 15 wamefika, nikalock gari nikawaacha madogo pale kwenye gari nikavuka Barabara hadi upande wa pili nikaulizia chakula nikaambiwa kipo, saa hyo ni saa 2 usiku na madakika yake, Nikwambia Mama ntilie nataka chakula Cha watu kama kumi, Yani sahani kumi za wali, akanipakulia akaniwekea kwenye ndoo, nikatumia ujanja wa kumwambia kila sahani ifunike ili chakula kisipoe ili nipate sahani excess, alivyomaliza nikampatia 20k Nikamwambia siendi mbali sana sahani nitakuletea mwenyewe, akakubali bila wasi na sijui kwanini aliniamini kiwepesi vile
Nikafika kwa madogo nikafungua gari nikatoa Yale mahotpot ujinga mwingine ambao niliufanya sikubeba vijiko vya kupakulia na kule kwa Mama ntilie sikuchukua Maji ya kunawa, Sasa ule msosi wa Kwenye hotspots nikaupakua kwa kutumia sahani nikakigawa kile chakula wengine ilibidi wale wali wa mama ntilie na baadhi yao wakala ule niliokuja nao ila ngegere na maini nilizigawanya katika Kila sahani, sasa nikawa nawauliza madogo mtanawa wapi mikono?, dogo mmoja akasema blaza haina haja mikono yetu misafi[emoji3] basi nikawaruhusu wafinye msosi na mm nikichukia sahani moja, walivyomaliza Nikaingiza mahotpot kwenye gari nikalock nikamchukua dogo mmoja Nikamwambia abebe ndoo yenye sahani anifuate wale wengine niliwaambia watusubiri, tukaenda hadi kwa mama ntilie nikampatia sahani zake akanirudishia balance yangu elfu 5, nikamuomba chenchi ya elfu 10 buku buku, akanipatia, tukarudi hadi kwenye gari na yule dogo, Nikawaambia Sasa Mimi na nyie tushamaliza nikampatia Kila mmoja buku buku angalau kesho Asubuhi wawe na uhakika nikaagana nao pale nikasepa, Wakati nipo Njiani nikampigia Mzee kumjulisha kwamba nishafanya kile alichoniagiza akanambia "sawa Sasa wewe unaweza kwenda na hilo gari kesho utalileta nyumbani, si ulifunga vizuri nyumba?" aliniuliza Nikamwambia ndio na funguo Niko nazo, "Haina shida ww unaweza kwenda kupumzika Sasa" okay Mzee, Sasa wakati huo naongea nae kwenye simu Mimi nilikuwa nishapita Ubungo Interchange naitafuta Mwenge, nikielenda nyumbani kwake, ilibidi nigeuze gari nilirudi nilikotoka sababu mm naishi Tabata, Yani kama ningewahi kumpigia simu basi nisingejisumbua kufika mbali kote huko
Kwa mara ya kwanza nafika mtaani kwangu na Gari, siku zote Mimi niwakufungua kale kageti kadogo Leo nafungua Geti lote kubwa ili kuingiza ndinga, maana nilipopanga tunakaa watu 3 nyumba zinajitegemea ila tunashea Compaund, nikapark gari nikaingia ndani kulala, kukakucha, Jumamosi mara nyingi huwa siendagi ofisini labda itokee naenda Zanzibar, so nikawa Sina ratiba ndefu nikafua nguo kadhaa nikaingia mtaani kupiga chai, nilivyomaliza nikarudi home direct nikakuta missed call ya Mzee maana nilivyotoka simu niliiacha, nikampigia akanipa maelekezo fulani pale ya kwamba atarudi Jumapili Pamoja na familia yake hivyo kama Nina muda nilipeleke Gari kule nyumbani au nibaki nalo hadi Jumatatu aje alichukulie Ofisini, nikamjibu sawa yote yanawezekana ila acha niangalie lipi litakuwa rahisi zaidi
Baada ya kukata simu nikapiga hesabu kurudisha hili Gari hadi kule mwisho wa mji, nikaona uvivu isitoshe gari lenyewe lilikuwa rafu mavombo machafu humo ndani, Yani ukifungua mlango wa gari Gari lote linanuka wali, nikatoa vyombo vyote, nikajikaza kuviosha hakuna Kitu kinanikera kama kuosha vyombo ndio maana huwa sipikagi mara kwa mara. nilivyomalizana na hiyo Kero nikalipeleka Gari Car Wash nikalirudisha kulipark home, hamuwezi amini nilishinda ndani hiyo weekend yote hadi inaisha na Gari limepark tu uwani
Jumatatu hii hapa, Asubuhi na mapema nikawa najianda kwenda kazini, Nikaingiza vile vyombo kwenye gari ila Sasa nikawa nawaza hao police huko Barabara kwasababu Sina Driving licence, nikasema potelea mbali nikatekenya mchuma hadi kazini nikalipark kimya kimya kama sio Mimi nikaingia Ofisini kwaajili ya kuchapa kazi
Imefika Lunch time najiandaa kwenda kupiga Menu yule Mzee nikamuona anaingia Ofisini halafu ana hasira amekunja sura, nikajisemea hapa kimeshanuka nikaanza ku recall matukio ili nijue ni wapi nimekosea hasa kule nyumbani kwake, kote nilicheza safe na mara ya mwisho kuongea na huyu Mzee ilikuwa ni Ile Jumamosi akinipa mabadiliko ya ratiba yake huku akinipatia option mbili za yeye kupata gari yake, na Mimi nilivyochagua kubaki na Gari hadi Jumatatu sikumpigia tena simu kumjulisha uamuzi niliouchukua....nikapata majibu kwamba inawezekana hapo ndipo nilipo haribu, alikuja kwenye desk langu na kuniambia "nipatie funguo ya Gari na ukimaliza kazi nitafute" hata hakunisalimia akatoka nje ya ofisi akaondoka....
Inaendelea badae acha nipate msosi.....story yangu ina episode 6 tu, episode ya kwanza na ya mwisho (1 & 6) ndio muhimu zaidi Sababu ushauri wako ndio unahitajika hapo
1. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
2. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
3. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
4. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
5. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
6. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
Yesterday your comment was most interesting ila hii ya leo [emoji1430][emoji1430][emoji1430]My vote biasennes;;
Kama wewe Ni mwanaume I mean if you're really real a man inatakiwa umuoe Annie.
Mana suala la hela Ni ishu ya mental skills. Unaweza ukarithi miradi ya hundreds of billions Ila usipokuwa how to produce money haitazaa. Na mwingine akaanza from minus or zero na akafikia hizo level za 100s of billions. If you're real man who you aren't afraid to go to zero and stand up go with Annie.
Wengi hapa wanaelekea kwa carryn kisa tu Kuna unafuu.
A real man must be proud with his hustles and stand up from rock bottom.
Ila ukiwa huko kwa Caren Ile your manhood ,or manly huwezi ionyesha kwa mwanaume aliyeanza zero na mko naye level moja utakuwa unaywea mbele yake tu kuwa wewe Ni ke fulani.
Naona watu wanatoa Theory kuwa hela inatakiwa Mana mtu anaumwa ghafula Kuna mdau kaleta theory utadhani Kama ukiwa na pesa na guarantee ya uhai.
By nature we love pleasure,luxury and lavish life and we hate/repel pains ndio Mana wengi wanamuwazia mno Caren Ila mie napenda niwe na mtu ambaye nitakuwa naye na sauti.
Otherwise nikiwa na huyo siku nikimzaba kibao akijisahau tu aseme kwanza tumekupiga tafu kimaisha usingekuwa ivyo Kama usingeoa ukoo wetu wenye pesa ,shukuru una bahati Ila bado haushukuru unaninyanyasa ndio mwisho.
Pia kumbuka mapenzi ama kila kitu hapa duniani huwa kina fade with time.
Hapana bro sijavote tena japo baada ya kusoma na kukuta ulikata utepe kwa Carryn nikawa dilema. Sema risk ya Carryn ni kubwa. Mapenzi ni risk. Be ready to face the consequencies. Anna kuwa mbali ni kikwazo tena kikubwa. Wanawake kukaa muda bila kusaliti ni changamoto. Leo nimekaa sehemu namsikia shemeji yangu amepigiwa simu ambayo sikuilewa elewa. Huyu ni mtu mwenye ndoa changa inaonekana dear x kamkumbuka. Excitement aliyopokea nayo mpaka njmeshtuka ndo hivo inabidi bro awe ameweka ulinzi wa kumtrace mtu wake. So kwa hapo Annie alikupenda ila umbali ni tatizo tena kubwa.Sawa, nimekuelewa lakini mm nikichagua nimechagua, Yani nitakayemchagua Sasa hivi basi huyo ndio atakuwa chaguo langu la maisha. Sitaki kufanya maamuzi nusu nusu Vinginevyo labda Mungu awe hajabariki hilo chaguo
Halafu hii I'd nahisi kama ni mara ya pili kuvote au ni mimi ndio nachanganya? Or you just wrote a comment to advise me and not a vote?
Double vote hairuhusiwi jamani
Eniwei! Nitahakiki badae
Naomba muendelezo wa Kama kuna tabia zangu ambazo huzipendi niambie nipo tayari kuziacha"Nimependa ulivyomalizia
Kama kuna tabia zangu ambazo huzipendi niambie nipo tayari kuziacha"
Watu mna akili sana ,best commentKama nakumbuka mwanzoni kabisa ulisema
Annie alikuwa na wewe kipindi huna kitu na aliwahi kukubustisha Enzi unasoma......mpaka sasa sijaona kosa ka Annie...ni either upendo umeisha au distance....as wanaume huwa hamuwezi kuvumilia umbali....unless Kuna issue umeficha kuhusu mahusiano yako na Annie....Familia ya Carren Ina nguvu sana ila hautaweza kuitawala kwasababu huna mabavu....utakuwa submissive kwao till your last breath...simaanishi Carren Ana akili kukuzidi ila she can twist you whatever she want...in short usiache mbachao kwa msala upitao
Sawasawa mkuu!Nadhani unaweza ukatukuta hapa hapa tulipoishia, Muendelezo Bado sana. Cos hadi niishi kwanza ndio niandike
I mean ni Live Story
Mkuu,kamwendo Sijaona vote yako