Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Lakini Mzee Said, kama issue ni kwa Baraza la Mitihani kuongozwa na watu wa dini moja mbona hili lilishatekelezwa

Maana kumbukumbu zangu za hivi Karibuni zinanionesha Kaimu Mtendaji wa NECTA alikuwa Athuman Amas, kabla ya Rais hivi karibuni Kumteua Dkt. Said Mohammed kuwa mtendaji mkuu wa NECTA

Je uteuzi huu umejibu kile mlichokuwa mnadai au bado mpaka ufanyike utafiti mwengine
 
Just..
Yote haya ya nini?
 
Mzee Mohamed Said kagoma kujibu swali lako karudi na swali kwako🤣 🤣 🤣 🤣
 
Tanbihi....Wakati Rais Benjamin Mkapa anwapa Waislamu Chuo cha Tanesco wakigeuze kuwa chuo chao kikuu, Wakristo walishapewa Chuo cha Benki Iringa walichokifanya kuwa Chuo chao Kikuu... Ben alikuwa anaweka sawa mizania, hakuwapendelea Waislamu.
 
Roman Catholic Church hawakupewa NBC College Iringa bure. Kiukweli ni kwamba walinunua kupitia NBC Holding Corporation ikuyokuwa inafuatilia mali na madeni ya iliyokuwa NBC baada ya kugawanyika kuwa NMB na NBC 1997.

Nendeni mukasome au pelekeni watoto wenu wakasome, acheni UFIADINI ni UJINGA
 
Stux...
Soma post #254.
Ghadhabu ziko juu mjadala umekuwa wa kutukanana.

Basi tuishie hapo tumebadilishana fikra kiasi tulichojaaliwa.
 
Hii napinga sababu hata leo hii tukianza kuangalia shule zilizojengwa kuanzia mwaka 2000 tu na kuja juu, utakuta shule zinazofuata misingi ya kikristo ni nyingi zaidi kuliko za kiislamu, vipi vyuo vya kati na vikuu??

Haya tutoke huko twende kwenye hizo taasisi za elimu utakuta hata idadi ya waislamu ni kubwa kwenye shule za Kikristo je na hili ni la kulaumu?? Sidhani sababu wazazi waliowapeleka wanafahamu umuhimu wa elimu na ndio wakafanya hivyo
 
Stux...
Soma post #254.
Ghadhabu ziko juu mjadala umekuwa wa kutukanana.

Basi tuishie hapo tumebadilishana fikra kiasi tulichojaaliwa.
Kubali umeshindwa HOJA ndiyo UUNGWANA
 
Kubali umeshindwa HOJA ndiyo UUNGWANA
Stux...
Unanifurahisha sana.

Ukiwa unapenda kuchukua "credit" kuwa umenishinda sawa sina tatizo na hilo.

Mimi siko hapa kushinda.

Mimi niko hapa kusomesha yale ambayo wengi hamkuwa mnafahamu.

Mlikuwa mnajua kuwa serikali mara mbili ilizuia Waislam kujenga Chuo Kikuu?
 
Kwa hiyo hiko chuo kikuu mngesoma waislamu tu? Mbona SAUT, tumaini n.k
Havina ubaguzi kwa mf saut waislamu wamepewa eneo la kuswalia msikiti mdogo..
Je, pale MUM wakatoliki wanaweza pewa eneo la chapel
 
Kwa hiyo hiko chuo kikuu mngesoma waislamu tu? Mbona SAUT, tumaini n.k
Havina ubaguzi kwa mf saut waislamu wamepewa eneo la kuswalia msikiti mdogo..
Je, pale MUM wakatoliki wanaweza pewa eneo la chapel
Inside10,
Chuo hakikusudiwa wasome Waislam peke yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…