Mzee wangu wewe kila siku unajinasibisha na tafiti za namna waislam walivyoonewa hapa nchini.Naamini kule ambako Nyerere hakuifuta EAMWS kuna maendeleo makubwa sana ya taasisi za huduma za kijamii za kiislamUkifuatilia kwa umakini taasisi nyingi zimeanzishwa na Bakwata na Tanzañia kuna ustawi wa uislam kuliko Kenya na Uganda.
Nan...
Bahati mbaya umeshindwa kuelewa uzito wa Nyerere kuipiga marufuku EAMWS kuzuia Waislam kujenga Chuo Kikuu.
Huu ulikuwa mgogoro mkubwa sana uliodumu takriban miezi mitatu kuanzia October hadi December 1968.
Mgogoro huu uliingiza TANU, Polisi na Usalama wa Taifa katika kupambana na Waislam na baadhi ya viongozi wao kama Tewa Said Tewa na Bibi Titi Mohamed na masheikh maarufu katika mji wa Dar es Salaam mfano wa Sheikh Hassan bin Ameir.
Baadhi ya masheikh wakawa wanafatwa majumbani kwao usiku kukamatwa na kuwekwa kizuizini Jela ya Ukonga.
Katika mgogoro huu ndipo Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa usiku nyumbani kwake Magomeni na usiku huo huo akapelekwa Uwanja wa Ndege akatiwa katika ndege na kurudishwa kwao Zanzibar kwa kuelezwa kuwa haruhisiwi kuingia Tanganyika.
Kilichofuatia ikawa kuvunjwa kwa EAMWS kuundwa kwa BAKWATA na mali zote za EAMWS kukabidhiwa BAKWATA.
Huu ndiyo ukawa mwisho wa ujenzi wa shule na Chuko Kikuu uliokuwa ukifanywa na EAMWS.
Haya hayakuwa mambo madogo ukichukulia kuwa hawa ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wakitegmea kuleta haki na usawa.
Nini ilikuwa sababu ya haya yote?
Mgogoro huu na yaliyofuatia kuanzia hapo yamechafua historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wema na hisani vilivyokuwapo vyote vimeingia doa na hapajakuwapo na juhudi za kutengeneza hali hii.
Wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika wakafutwa katika historia mpaka nilipokuja kuandika maisha ya Abdul Sykes na kuwarejesha.
Wengi wa hawa wazalendo wamekufa na kuzikwa wakiwa na kinyongo moyoni mwao.
Huu ndiyo urithi uliopo na utapokelewa kutoka kizazi kwenda kizazi kuwa Waislam ijaza yao ya kupigania uhuru haikuwa shukurani bali nuksani.
Hili si jambo jepesi, halikutakiwa kuwepo kabisa na wala halipendezi.
Hili ni jambo zito linalohitaji busara si kejeli kama hizi zinazotolewa hapa.