Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Unashauriwa utumie network yako kuanzisha huduma ya kijamii kwa Watanzania kama vile chuo au hospitali kusudi uwe mfano wa kuigwa
Nan...
Lakini mbona mjadala wetu hauna uhusiano wowote na haya usemayo ya huduma za jamii?
 
Ukiishiwa point ndiyo kawaìda yako kujibu ovyo

Ukiishiwa point ndiyo kawaìda yako kujibu ovyo
Stux...
Mimi naitambua hidaya niliyopewa na Allah kitu ambacho si wengi wamejaaliwa.

Allah kanipa kalamu na ulimi wa kuzungumza.

Huwezi wewe kushindana na mimi ukanishinda hata kama utakuja na wenzako 20 kukusaidia.

Wala sisemi haya kwa kibri na kujigamba.
Nasema haya kwa kumshukuru Allah kwa kunipa kipaji hiki.

Wewe mara nyingi unaandka hapa umeghadhibika na mimi najua kuwa umeghadhibika na unanikejeli.

Sijapata kukurejeshea kejeli.
Nitakujibu kistaaraba.

Huwa nikiingia katika mjadala navutia wasomaji wengi sana.
Angalia hapa sasa hivi tuko wangapi?

Haiwezi ikatokea mimi nikaishiwa na la kusema.
Alhamdullilah.
 
Huu uwongo wako kadanganye wajukuu zako au wenzio kwenye mchezo wa dhumna
Stux...
Umeghadhibika.
Kwanza mimi sijui kucheza dhumna na sijpata hata kutamani kucheza.

Mimi sisemi uongo labda wewe unashindwa kukubali ukweli kwa kuwa ukweli huu una athari mbaya kwa wale waliohusika katika kuivunja EAMWS kuwazuia Waislam wasijenge Chuo Kikuu.

Unaona tabu kukubali kuwa historia hii imevunja, ''legacy.''

Historia hii inafahamika na hakuna uongo wowote niliosema.

Mwaka wa 2011 nilikuwa New York, nikitokea Northwestern University, Evanston, Chicago nilikoalikwa na Idara ya African History kufanya mhadhara.

Mwenyeji wangu pale New York akaniambia kuwa kuna Mmisri anafanya kazi Umoja wa Mataifa na huyu Mmisri aliwahi kufanya kazi Ubalozi wa Misri Tanzania katika miaka ya 1960.

Kitabu changu, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,’’ kilipotoka mwaka wa 1998 huyu Mmisri, jina lake Rigal alikisoma na alikipenda sana khasa kwa kuwa kilieleza historia ya Chuo Kikuu Cha Waislam kilichokuwa kijengwe na serikali ya Misri.

Rigal yeye akiwa ofisa katika Ubalozi wa Misri, Dar es Salaam alihusika sana na mradi ule na alisikitika kuwa chuo kile hakikujengwa.

Mwenyeji wangu alipomwambia kuwa niko mjini alimuomba amkutanishe na mimi.

Siku ya Ijumaa baada ya kuswali sala ya Ijumaa msikiti ulio jirani na ofisi za Umoja wa Mataifa Rigal alitualika chakula cha mchana kwenye mgahawa si mbali na msikiti ule.

Rigal alitaka kusikia kutoka kinywani kwangu nini khasa ilikuwa sababu ya serikali ya Nyerere kuipiga marufuku EAMWS wakati ilikuwa na maradi muhimu wa kujenga Chuo Kikuu.

Nilimweleza kila kitu nilichokijua.

Rigal akaniuliza hali ya Waislam ikoje hivi sasa katika elimu.
Nilimweleza.

Rigal aliniuliza kama nitakuwa tayari kwenda Misri na kufanya mihadhara kueleza uhusiano mzuri uliokuwapo kati ya Gamal Abdel Nasser na Julius Nyerere kiasi cha Nasser kuamua kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam mradi ambao kwa wakati ule ulikuwa mkubwa wa elimu Misri hawajapata kutekeleza nje ya nchi yao.

Picha hiyo hapo chini siku Julius Nyerere alipoweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Cha Waislam.



Rigal​
 
Maneno kuntu, hicho chuo cha morogoro kama hakiruhusu secularism hata waislam wenyewe wataogopa kusoma hapo. Watakuwa na wanafunzi kiduchu daima.
Taasisi za wakristo hazibagui waislamu na ndio siri ya mafanikio yao
 
Maneno kuntu, hicho chuo cha morogoro kama hakiruhusu secularism hata waislam wenyewe wataogopa kusoma hapo. Watakuwa na wanafunzi kiduchu daima.
Taasisi za wakristo hazibagui waislamu na ndio siri ya mafanikio yao
Imagine chuo kikuu hakiruhusu kujichanganya wanaume na wanawake,kila jinsia inakaa upande wao¡!¡ Wanawake lazima wavae kidini😓,ndiyo maana kinakosa wanafunzi wengi hata wa kiislam . Karne ya 21 Tanzania wanaleta mtindo wa Saudia, Afghanistan nk,inasikitisha sana .
 
Maneno kuntu, hicho chuo cha morogoro kama hakiruhusu secularism hata waislam wenyewe wataogopa kusoma hapo. Watakuwa na wanafunzi kiduchu daima.
Taasisi za wakristo hazibagui waislamu na ndio siri ya mafanikio yao
Jabulani,
Kuruhusu unachokiita ''secularism,'' MUM huo ni muhali mkubwa.

Ikiwa Muislam anaogopa kusoma MUM kwa kuwa yeye angependa uhuru wa kufanya alitakalo hata kama linakwenda kinyume na mafunzo ya Uislam hili ni bahati mbaya kwake anaweza kwenda chuo cheye kuruhusu hayo.

MUM haibagui lakini lakini mwanafunzi lazima afate sheria na maadili ya chuo.

Sina taarifa kuwa MUM hakina mafanikio.

Wala sijasikia popote duniani kuwa chuo kinapata mafanikio kwa kuruhusu mchanganyiko wa wasichana na wavulana.
 
Ipyax,
Kutoruhusu wanaume na wanawake kuchanganyikana si mtindo wa Saudia au Afghastan.

Hii ni amri katika Uislam.

Ikiwa kuna nchi za Kiislam na hawafuati sheria hii huko ni kuasi tu si kuwa wako sawa.
 
Ipyax,
Kutoruhusu wanaume na wanawake kuchanganyikana si mtindo wa Saudia au Afghastan.

Hii ni amri katika Uislam.

Ikiwa kuna nchi za Kiislam na hawafuati sheria hii huko ni kuasi tu si kuwa wako sawa.
Hiyo ni moja ya sababu inayofanya vijana waikimbie Muslim university of Morogoro.
 
Mzee Mohamed naomba nikuulize. Wewe waislam unaosema walionewa ni wa dhehebu gani? Ni Ahmadiyya, Sunni, Ibadi, Shia, Ismail, Bohora au ni wepi hao.

Maana hapa ni kama unataka kutuaminisha Waislam hapa Tanzania ni
homogenize group walioonewa sana na Serikali ya Tanzania/CCM.

Hebu leo utuambie ni Waislam wepi wali/wanao newa na Serikali?
 
Ipyax,
Kutoruhusu wanaume na wanawake kuchanganyikana si mtindo wa Saudia au Afghastan.

Hii ni amri katika Uislam.

Ikiwa kuna nchi za Kiislam na hawafuati sheria hii huko ni kuasi tu si kuwa wako sawa.
Amri hiyo hata kama ni ya kidini basi ni ya HOVYO
 
Hiyo ni moja ya sababu inayofanya vijana waikimbie Muslim university of Morogoro.
Ipyas,
Hilo si tatizo kama wanaikimbia MUM kisa ni kuwa hairuhusu kuchanganyika wanawake na wanaume hapana neno.

Wako wanaopenda kuchunga mipaka.
Hawa wataabiki.
 
Kinyungu,
Umetumia neno ''kuonewa.''
Mimi sijapata kutumia neno hilo popote katika maandishi yangu.

Mimi hueleza historia ya Waislam kwa upana wake.

Nimeeleza hapa kuwa mwaka wa 1968 EAMWS ilipokuwa inajenga Chuo Kikuu serikali iliivunja na kuunda BAKWATA.

Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa na kurejeshwa kwao Zanzibar.

Naeleza kuwa katika miaka ya 1970 OIC walitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania serikali ikakataa kutoa kibali.

Hii ndiyo namna yangu ya uandishi.

Wewe unaniuliza habari ya madhheb ya Waislam na ni dhehebu gani linaonewa.

Mimi sijazungumza hilo.

Lakini nimeandika paper: ''Islam and Politics in Tanzania,'' ikiwa unataka kujua tatizo hili nakuwekea link hapo chini:

 
Mmeuza Mali zenu wenyeweeee
Nyie

Ova
 
Bakwata ilirithi Mali za East Africa
Muslim,alharamain,kiboyoye moshi,dodoma shile jamhuri,bukoba mlikuwa na shule
Nyumba mlikuwa nazo upanga, nyumbabya sheikh mkuu msasani peninsula, mkauziana kiujanja akanunua hemed
Ukienda magomeni mikumi mlikuwa
Tena alikaaga sheikh nasri pale
Unataka data zenu .....
Mlikuwa na mabasi,malori mlikuwa na hospitali pia
Tatizo la nyie baadhi yavwaislam hamkubali makosa mnajiona sawa
Nyie mnashindwa kusimamia mambo
Serikali ya tz hampendelei yyt
Mali mnauza wenyewe mnawasikingizia wakina John

Ova
 
Hicho chuo kilitakiwa kujengwa kibaha kwa mfipa mlikuwa na eneo,wakati wa mwinyi hela ilitolewa
Lakini nyie mlikulaaaaa
Mnawasingizia wakina John

Ova
 
Toka like Shamba la Waislamu la Chang'ombe Maduka mawili liuzwe kwa bei Chee kwa tajiri flani, mimi sina cha kuwaambia hawa watu.

Raslimali kubwa namna hii liko mjini linauzwa kwa bei ya kutupwa sina hamu nao.
Halafu utawasikia
"tunaonewa na Mazayuni"
 
Huyu mzee said analalamika tu na kulialia
Wakati tatizo liko ndani mwao wenyewe,ile shule ya alharAmain na eneo lote wamempa mwekezaji
Na akibisha hata huyo mwekezaji tunaweza mtajiaaaa
Tatizo hawapendi kukubali ukweli

Ova
 
Kwa hiyo changombe aliuza John
Tena hilo eneo la changombe nyerere alitaifisha na akawapa waislam ilikuwa 1966
Mzee said analalamika nn

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…