Huu uwongo wako kadanganye wajukuu zako au wenzio kwenye mchezo wa dhumna
Stux...
Umeghadhibika.
Kwanza mimi sijui kucheza dhumna na sijpata hata kutamani kucheza.
Mimi sisemi uongo labda wewe unashindwa kukubali ukweli kwa kuwa ukweli huu una athari mbaya kwa wale waliohusika katika kuivunja EAMWS kuwazuia Waislam wasijenge Chuo Kikuu.
Unaona tabu kukubali kuwa historia hii imevunja, ''legacy.''
Historia hii inafahamika na hakuna uongo wowote niliosema.
Mwaka wa 2011 nilikuwa New York, nikitokea Northwestern University, Evanston, Chicago nilikoalikwa na Idara ya African History kufanya mhadhara.
Mwenyeji wangu pale New York akaniambia kuwa kuna Mmisri anafanya kazi Umoja wa Mataifa na huyu Mmisri aliwahi kufanya kazi Ubalozi wa Misri Tanzania katika miaka ya 1960.
Kitabu changu, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,’’ kilipotoka mwaka wa 1998 huyu Mmisri, jina lake Rigal alikisoma na alikipenda sana khasa kwa kuwa kilieleza historia ya Chuo Kikuu Cha Waislam kilichokuwa kijengwe na serikali ya Misri.
Rigal yeye akiwa ofisa katika Ubalozi wa Misri, Dar es Salaam alihusika sana na mradi ule na alisikitika kuwa chuo kile hakikujengwa.
Mwenyeji wangu alipomwambia kuwa niko mjini alimuomba amkutanishe na mimi.
Siku ya Ijumaa baada ya kuswali sala ya Ijumaa msikiti ulio jirani na ofisi za Umoja wa Mataifa Rigal alitualika chakula cha mchana kwenye mgahawa si mbali na msikiti ule.
Rigal alitaka kusikia kutoka kinywani kwangu nini khasa ilikuwa sababu ya serikali ya Nyerere kuipiga marufuku EAMWS wakati ilikuwa na maradi muhimu wa kujenga Chuo Kikuu.
Nilimweleza kila kitu nilichokijua.
Rigal akaniuliza hali ya Waislam ikoje hivi sasa katika elimu.
Nilimweleza.
Rigal aliniuliza kama nitakuwa tayari kwenda Misri na kufanya mihadhara kueleza uhusiano mzuri uliokuwapo kati ya Gamal Abdel Nasser na Julius Nyerere kiasi cha Nasser kuamua kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam mradi ambao kwa wakati ule ulikuwa mkubwa wa elimu Misri hawajapata kutekeleza nje ya nchi yao.
Picha hiyo hapo chini siku Julius Nyerere alipoweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Cha Waislam.